September 27, 2007

Chiwindi Mpakani!!

CHIWINDI-hiki ni kijiji kilichopo katika mpakani mpakani mwa Tanzania kama unaelekea Msumbiji kupitia mwambao wa ziwa nyasas.kijiji hiki kinapokea nakukaribisha wageni wa aina mbalimbali ambao wengine huwa katika taifit mbalimbali juu ya maeneo haya au nchi kwa ujumla.Ni kijiji kinachotegemea uvuvi,biashara ambayo si kubwa sana,kilimo ambacho ni nguzo za maisha ya raia wake.Eneo hili lina barabara ambayo huwasasidia wakazi wake kusafiri umbali mfupi kwani linamatatizo ya kijiografia tokana na milima na mawe yanayozunguka kijiji hicho lakini ni kijiji chenye utulivu naraia wake wanamahusiano mazuri na jirani zao Msumbiji,hujaribu kushirikiana kimichezo,kitamaduni nakiuchumi kwani wanakaribiana sana.Lugha inatumika ni kiswahili na kinyanja(kinyasa) ambacho huzungumzwa pia nchini Malawi amabayo ianapakanana kiji hiki kupitia ziwa nyasa.Wakaazi wake pia hufanya safari mara kwa mara kwenda Malawi kani ni muda wa saa 1 kwa boti.Hapa ni mpakani kabisa hivyo pana shughuli za hapana pale na pana walinzi na usalama ka pande zote mbili yani Msumbiji na Tanznia.wakaazi wake wanapendana sanalicha ya kuwa nchi tofauti na wanashirikiana.

2 comments:

  1. Eneo lakijiji hiki lipo upande wa kusini.Hivyo kinachofanyika hapa ni kueleza kutoka uapande huo kwenda kaskazini.

    ReplyDelete
  2. Ni furaha sana kuipata simulizi za aiana hii kwa wakazi ambao hatujaenda huko lakini kupitia shajara yako naamini tutafanikiwa

    ReplyDelete

Maoni yako