September 30, 2007

Mtupale

MTUPALE; ni kijiji kinachopakana na kijiji cha mpakani cha CHIWINDI.Hiki ni kijiji ambacho hakitofautiani sana na vijiji vilivyopo nyasa kwani katika shughuli za kijamii na kiuchumi hutegemea pia uvuvi,kilimo,ufugaji n.k lakini hiki kina nyongeza zaidi kuliko chiwndi kwani kina mashamba mengi ya kilimo cha mpunga.Kwa kiasi kikubwa kilimo cha mpunga kina nafasi kubwa katika kijiji hiki kwani ardhi yake inakubali sana zao hilo,hivyo wakaazi wengi hujituma katika ulimaji wa zao hilo.Zao hilo huuzwa hata kwa majirani zao Malawi ambao ni umbali wa saa 1 na 30 kwa boti hivyo wengi hushirikiana nao wageni hao ili kujipatia kipato cha kila siku.Kwa asili kijiji hiki kina baadhi ya wakaazi ambao asili yao ni nchi za Msumbiji na Malawi,kwani waliingia Tanzania kabla ya uhuru hivyo wamekuwa raia kamili.Shughuli kubwa zifanywazo katika kijiji hiki hakuna tofauti na chiwindi isipokuwa hiki ni kijiji chenye wavuvi wengi wenye dhana za kawaida ambazo husaidia kupata samaki.Eneo lake ni tambarare kwa wastani na lina misitu ya kutosha kwa hali ya hewa nzuri,hupata mvua zake bila matatizo.Biashara nayo imekuwa sehemu ya wakaazi hao kwani hushirikiana na wale wa ng'ambo pia baadhi ya wakaazi wake hutumia biashara ya kubadilishana mazao kama zama za kale.maendeleo ni mazuri licha ya uduni wa hapa na pale.

3 comments:

 1. Kijiji hiki ndipo asili ya mama yangu,kwani wazazi wake waliishi hapo baada ya kutoka afrika kusini hasa mzee frank machusa huku mkewe(bibi) yangu alitokea Msumbiji ambako wazazi wake waliishi hivyo akawa raia wa Tanzania.eneo zuri lenye mito na vyanzo vingi vya maji.

  ReplyDelete
 2. Tuletee mambo ya kwetu bwana maana hatuwahi kukanyaga huko tunasikia tu,kumbe yapo mazuri ya kujifunza na naamini mengi yatakuja

  ReplyDelete
 3. Hi, Good Blog :)
  Look from Quebec Canada
  http://www.wwg1.com

  WWG :)

  ReplyDelete

Maoni yako