October 13, 2007

CHIMATE;Nyasa,Safi na Watu

Kma ilivyoada naendelea na simulizi ambazo ni habari za nyasa na leo nimetinga katika kijiji cha CHIMATE.hapa ni pana utamaduni na ufanano na vijiji vingine kama nilivyosema awali kuwa vijiji hivi havitofautiani sana kimazinginra.Lakini kijiji hiki kina eneo kubwa za maraba na ni eneo lenye mchanganyiko wa ardhi;kuna ule wenye rangi nyekundu{ngunja} na ule ufananao na mazingira ya mchanga ingawa si kwa kiasi kikubwa.Shughuli kubwa katika kijiji hiki uvuvi,kilimo,ufugaji na biashara ambayo hufanyika baina ya wakazi wa nchi jirani ya Malawi na Msumbiji.Lakini pia kwa kiasi kikubwa kijiji hiki kinategemea sana shughuli za kilimo kwani ni uti wa mgongo wa maeneo haya.Pia eneo hili ndilo ambalo shule ya sekondari ya kata imejengwa kwani ule mpango wa sekondari kila kata umefika pia katika eneo hili.Jambo kubwa ba la kujivunia ni kwamba hiki ni kijiji alichozaliwa jaji mstaafu Barnabas Samatta.Hivyo wakazi wake wanajivunia kijana wao ambaye amestaafu hivi karibuni mwaka huu 2007.Hali ya hewa ya eneo hili ni joto la wastani na baridi pia ni ya wastani inayowezesha wakazi wake kuwa na hali ya afya njema.Tukutane katika kijiji kingine.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako