June 01, 2008

Watunza Afya Zetu Hao,Wapeni Malipo Mazuri

Wauguzi ni watu muhimu sana katika ulinzi wa afya za wananchi katika taifa lolote.Hebu waone hapo walijipumzisha wakisiliza mawaidha ya kuboreshwa kwa malipo na kuiomba serikali iwasomeshe kwa kiwango kikubwa au mnasemaje?Najua wanafunzi wa vyuo vikuu watasema wanataka kuwabania "mshahara wao" wanaolipwa na ile bodi,au watasema ufisadi!hapana hawa ni watu muhimu sana hao.

1 comment:

  1. Kweli kabisa wauguzi ni watu muhimu sana. Kwani hata huku ughaibuni kumekuwa na mgomo wa kazi kwa muda wa wiki sita kwa sababu watu wengi wanaona wauguzi si kazi ya kulipwa malipo mazuri kwa hiyo kwa jambo hili limesababisha wagonjwa wengi hasa opereshen kuto fanyika. Unajua nimeshangaa kuona ni wakati mmoja hili jambo linatokea.Sasa cha kushangaza ni kwamba wiki ilijopita kulikuwa na kikao lakini hata hivyo WAUGUZI wamekataliwa kuongezwa mshahara. Kwa kweli inasikitisha sana.

    ReplyDelete

Maoni yako