December 03, 2008

nawapenda Kingoli na Litumbandyosi, lakini poleni

Mvua kubwa iliyoambatana na upepo makali imeleta maafa makubwa katika kijiji cha KINGOLI kata ya LITUMBANDYOSI iliyopo wilaya ya MBINGA. Upepo huo umeezua mapaa ya nyumba TISA. Akizungumza kwa masikitiko Afisa mtendaji wa kijiji hicho Aloyce Nchimbi alisema mvua hiyo ilinyesha kwa zaidi ya saa moja na kusababisha baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi KINGOLIkutokuwa na mahali pa kusomea.
Mvua hiyo iliambatana na upepo mkali imeezua MADARASA MAWILI ya shule ya KINGOLI na NYUMBA mbili za WALIMU pamoja na majengo mawili ya ZAHANATI ya kijiji hicho
Mkuu wa wilaya ya MBINGA Amina Masenza amesema kamati ya kushughulikia tukio hilo imeundwa na itafanya kazi mara moja

NB; waungwana poleni watani zangu na watu wangu wa mkoa wetu PAMOJA DAIMA

2 comments:

  1. Mungu wangu Kijiji cha kingoli nimeishi pale tangu nilipokuwa darasa la tano mpaka la saba. Shule yangu imeezuka na nadhani pia nyumba yetu tuliokuwa tunaishi. Yaani nasikitika sana kiasi kwamba mchozi unanitoka. Kwani mnajua ile sehemu ni ya mchanga mwingi sana kwa hiyo kama sikosei inaweza kutokoa mmomonyoko mkubwa sana. Natumaini huduma ziende mara moja. Asante sana kwa taarifa, kwani unajua bado nina Ndugu na marafiki wanaishi kule. Roho inaniuma sana.

    ReplyDelete
  2. Usijali kwani mujibu wa RIPOTI niliyoipata leo hii ni kwamba hakuna vifo na hakuna maafa makubwa kiasi cha kutishia uhai, ila hili la kuezuka nyumba na shule vilevile mashamba yamepata mushkeli kidogo kwani inatokana na kasi ya upepo ingawa hatuna vipimo kamili

    ReplyDelete

Maoni yako