November 18, 2009

KICHWA CHINI, MIKONO NYUMA

Fredy Macha namhusudu sana, kama ilivyo kwa Ndesanjo Macha ambaye ni kiini cha mimi kuanza kublogu. Nakumbuka nilikuwa nasoma sana kazi zake katika gazeti la Mwananchi, nikawa nakata ile sehemu ya safu yake na kuihifadhi-hadi leo ninazo sehemu hizo katika makataba yangu ya kijijini na hapa mjini. Nakumbuka mengi kwani wakati nataka nilimjulisha ananiambia ukitaka kublogu usifikirie mbali sana, bali tafakari kawaida tu kwamba una kitu gani ambacho wenzako wanaweza kujifunza toka kwako.

Maneno haya ya Ndesanjo ndiyo ikawa msingi wa mimi kuanza kublogu ingawaje nilianzia katika programu za Wordpress. Nakumbuka alinihimiza ni lini nitakuwa tayari kublogu. Jawabu langu likawa muda nikiwa tayari nitakuhabarisha. Ikawa mchana ikawaq usiku hadi leo nablogu na kuandika mambo yanahusu nyasa ambayo mimi ni sehemu yake, na inabidi kuyaeleza. Alisema blogu siyo upepo wa kupita ni zama nyingine hii usipitwe. Somo likaingia, likakolea nikaanza kublogu kuhusu mkoa, lakini dhamira ilikuwa kuhusu nyasa yetu tamu.

Nashukuru moyo wake wa kujitolea kunijuza, nashukuru pia rafiki yangu Simon Regis kwa mwongozo, nikawa katika uimara ninaoutaka ingawa sijaridhika. Nikasema blogu yangu ni kujitolea.

Sasa kwa Fredy Macha kuna kitu kimoja anazungumzia mara nyingi. Na alipokuja mwezi mei mwaka huu alirejea neno lilelile pale Soma Cafe(mgawahawa wa vitabu-mikocheni). Nilimweleza maendeleo ua utunzi wa vitabu, nikajaribu kumdodosa dhana ya maendeleo. Jibu lake kwangu ndilo linalonifanya niweke picha za aina hiyo kuhusu nyasa, yaani zile zenye kuonyesha uduni,ulalahoi n.k lakini naelewa nianza kufagilia mambo ya nyasa hapa hapatatosha. Ningeweza kuandika mambo mengi kuhusu jamii za Wajerumani wakiwa LUNDU na hususani wialaya ya Mbinga kwa uzoefu wangu. Ningeandika mengi kwani ni sehemu ya maisha yangu.

Ndiyo maana nakumbuka maneno ya Fredy Macha kwamba UKITAKA KUPATA MAENDELEO LAZIMA UJITAMBUE,UJIJUE. UJUE WAPI ULIKOTOKA, WAPI WAZAZI WAKO WALIZALIWA. THAMINI UTAMADUNI WAKO. KUWA NA NIDHAMU ILI UPATE HESHIMA. USIONE AIBU KUHUSU UTAMADUNI WAKO. UNA THAMANI SANA KWAKO.

Nikikumbuikamaneno hayo halafu ukitazama picha hiyo unaweza kudhani ninachofikiria unakifahamu. Hakuna kitu kikubwa kwangu kama AMANI YA MOYO. Nadhamini sana jambo hili bila kujali kitu chochote nilichonacho nje ya mwili wangu. SIWEZI KUTHAMINI KITU CHOCHOTE KILICHONJE YA MWILI WANGU, lakini suala ya utamdauni lipo kati yangu ndani mwangu nakihusudu sana.

Kwa bahati nzuri nimetembelea mwambao wa ziwa nyasa wote kwa upande wa Tanzania, na kwa upande wa Malawi kuna baadhi ya meneo ambayo nimeyatembelea, NAYAHUSUDU SANA KAMA VILE BANDARI YA CHILUMBA. Sasa thamni ya utamaduni wako ni kubwa hata kama watu wanaishi katika mazingira kama hayo. Unaweza kumtazama mtoto huyo halafu ukajifikiria ndiyo wewe unajijua sasa upo katika gali hiyo. Je utafanyaje? Ingawa kuna jambo la kufanya lakini jaribu kufikiria kama upo wewe.

Nadhani kuna jambo ambalo katika blogu yangu yanautofauti na maisha ya mjini. Kwanza mie siyo mtoto wa mjini, nimekulia kijijini na hata nilipokuwa nasoma nilipendelea kwenda kijijini, nimezoea misoto hata nikilosti mkwanja leo, sina maneno kwani nimefundishwa kuwa huru kifikra. Sasa wakati fulani nilimwuliza diwanmi wetu hivi unaonaje watoto wana[poshindwa kwenda shule shauri ya karo, ukachukua jukumu la kuwalipia? Alijibu UJAMAA UMEPITA. Nikamwambia mzee umekulia katika ujamaa mbona unabeza au maumivu sasa? Akasema ndiyo taabu ya wasomi.

Jawabu langu likawa kuwa mimi siyo msomi, mimi ni mwanenu mliyenilea hapa kabla sijahamia Mbinga pale shule ya smingi Kiwanjani. Naijua nyasa naelewa nyasa ninapenda sana kuliko chochote. Najua maisha hayao ya mtoto kama huyo pengine anamakamasi. Lakini ndivyo ilivyo, kwani wote hawakuumbwa na macho ya goroli, ndiyo maana wengine wanachongo.

Thamani ya utamaduni wako ni muhimu sana. Na naiona jamii za mijini kama zile alizozungumzia karl Marx kwamba jamii ambazo hazina utamaduni, na sifa moja kuu ni kwamba waafrika tamdauni zetu zinafanana. Kwakuwa Ndesanjo aliniasa unaweza kuandika kile ambacho wenzako hawakijui, na yale maneno ya mzee wangu Fredy Macha ni thawabu kwangu.

Nikiwatazama binadamu kama huyu aliyepichani ndipo ninapopata raha ya kuutibu moyo wangu kwamba ninapenda kuzungukwa na watu wenye hali hiyo ili tusonge mbele na kuiona dunia angavu ya ukwasi. Naweza kutembea KICHWA CHINI, MIKONO NYUMA, nikiwaza binadamu hawa. Mungu awe nanyi daima, awabariki wanaopigani hali zao na kuwalinda daima. MOYO KABLA YA SILAHA

2 comments:

  1. asema mshairi mmoja;


    utamaduni ni sauti
    ya mtu na mazingira
    tuipende tanzania
    nchi tuliyozaliwa

    ReplyDelete
  2. kamala umenena
    thawabu imejaa
    kwetu raha
    uhuru staha
    utamu sambaa
    karibu nyasa

    ReplyDelete

Maoni yako