December 17, 2009

MWANAFALSAFA CHRISTIANI BWAYA

MWANAZUONI BWAYA
Nimekuwa mfauatilaji mkubwa wa blogu ya kaka Christiani Bwaya. Mara nyingi unaweza kukutana na sentensi chache sana na ambazio zinakupatia maswali mazito. N amoja ya amaswali hayo nimekwisha kumwuliza, maadamu ameniahdi kulitoa jawabu..basi nasubiri jawabu lake.

Hata hivyo leo katika kupitia blogu mbalimbali kama ilivyoada, nimekiuta blogu ya mwisho kama kawaida yangu ni bwana Bawaya ili kujifikirisha zaidi. Wakati nasoma mada yake hii ambayo nimeambatanaisha hapo chini nilijiuliza maswali menghi sana. Ni maswali ya kifalsafa, na majibu yake yanahitaji utundu sana.

Pamoja na hayo, naona baadhi ya blogu zinatumia huduma nyingi za zamani, jamani huduma mpya za blogu ziko nyingi tu zitazameni ili kuboresha blogu zenu. Tuache hilo ambalo siyo mda kuu hapa. Nimelazimika kuikwapua mda hiyo na kuiweka hapa ili labda tuisafirishe zaidi na kuwa mda pana.

ISOME ALIVYOANDIKA MWENYEWE, HII HAPA;

Je, tunafikiri kwa kutumia lugha?
Kuna changamoto zimejitokeza kwenye ule mjadala wa tasnifu ya msomi wetu ambayo kwa maoni yaliyotolewa huenda ingekuwa bora kama ingekuwa katika kiswahili.Changamoto kubwa zaidi ni ile iliyoletwa na msomaji Godwin Habib Meghji akihoji ikiwa mwanadamu hufikiri kwa kutumia lugha.Hapa anasema: "Mimi sina uhakika kama binadamu anafikiria kwa kutumia lugha fulani. Viziwi na bubu pia hufikiri". Hii ni changamoto nyingine. Una maoni gani katika hili?Je, tunawezaje kufikiri? Fikra zinauhusiano wowote na lugha?Je, bubu ama kiziwi hana lugha kwa sababu tu hawezi kutamka ama kusikia?

No comments:

Post a Comment

Maoni yako