Kwa hisani ya blogu ya MAISHA NA MAFANIKIOHospitali ya Ludewa iliyoko wialaya hapo katika mkoa wa Iringa.
Akina mama ambao wanawauguza ndugu zao katika hosptali ya Wilaya ya Ludewe wakisonga Ugali nje ya wodi ya akina mama wanaosubiri kujifungua, kati ya akina mama 100,000.wajawaito 200 hupoteza maisha katika Wilaya hiyo kutokana na ukosekanaji wa miundombinu.Wanawake wajawazito toka katika vijiji 76 vinavyo zunguka Wilaya ya Ludewa wakiwa wamelala na wengine wakila chakula huku wakiwa wamesubilia siku zao za kujifungua katika hospitali ya Wilaya ya Ludewa Mkoa wa Iringa kati ya akina mama 100,000 wajawazito 200 hufariki kutokana na ukosefu wa huduma.
Inasikitisha: Baadhi ya akina mama wajawazito wakiwa nje ya wodi ya wazazi katika hospitali ya Wilaya ya Ludewa ambapo jengo hilo lina vitanda 6 na kila kitanda hutumiwa na akina mama wajawazito wawili. Wengine hulazimika kulala chini. (picha na Albart Jackson).
Na: Yasinta Ngonyani
Nimefurahi kuona wengi wameguswa na habari hii.
ReplyDeleteYasinta na Marcus Mpangala, acheni hizo. Hii si hospitali, wala watu wanaoonekana si wagonjwa. Hili ni jengo ambalo ndugi wa wagonjwa wanaotoka mbali hufikia hapa kwaajili ya kuuguza wagonjwa wao. Nilitegemea mngeusifia uongozi wa hospitali kwa kuendeleza sera za kijamaa. Kitu kama hiki kinakosekana sehemu nyingi sana.
ReplyDeleteNaamini hampajui mahali hapa, hamjawahi kufika, na picha hii mmeiba sehemu bila kulipia wala kutaja haki za msingi za mpiga picha hii.
Hii picha ni yangu mimi. mmetoa wapi? Ninyi watu wa Mbinga, mnajihusishaje na mambo msiyoyajua ya Ludewa? Andikeni mapungufu ya taasisi zenu. naamini hizo mnazijua vema.Hospitali ya Ludewa ni ya kisasa na ina huduma nzuri sana za mama na mtoto. Kama mnabishia, tembeleeni muone.
Tubuni na kuacha uongo huu.Laasivyo tutawaadhibu kwa makosa ya kihafidhina ambayo babu zenu waliwafanyia babu zetu. naamini tutawarudisha Afrika kusini mkachomwe moto na ndugu zenu 'The Ngunis'