October 27, 2012

ELIMU: SEKONDARI ZA WILAYA YA NYASA ZAENDELEA KUBORESHWA

Wengi wanafahamu kuwa Wilaya ya Nyasa ni miongoni mwa Wilaya zilizoundwa na kuzinduliwa mwaka huu. Kila wilaya inapoundwa basi masuala mengi yanahitaji kufanyiwa kazi. Moja ya masuala hayo ni elimu. Wilaya Nyasa kwa sasa kuna mengi yanafanyika yenye lengo la kuongeza maendeleo na kuboresha zaidi. Shule zinajengwa au kuboreshwa ili kuweka mazingira mazuri ya kusomea. Kufuatia suala hilo, Nyasa inaelekea kuhimiza ujenzi wa shule mpya na zile za zamani kurekebishwa kwa manufaa wa wananchi wote. Hapa ni baadhi ya shule ambazo zinafanyiwa marekebisho na zilizokamilika. Elimu ni Uhai, kama Misitu ni Uhai.
Picha ya juu inaonyesha sehemu ya majengo la shule ya Sekondari ya Mkwaya baada ya kukamilika kwa ujenzi wake na kuboresha mazingira ya shule hiyo.
Picha ya pili inaonyesha nyumba ya Mwalimu katika shule ya Sekondari ya Mkwaya. Hii ni moja ya mikakati ya kuweka mazingira mazuri kwa walimu wa sekondari katika wilaya ya Nyasa.

Picha inaonyesha majengo mawili ya madarasa katika Sekondari ya Kipololo. Ujenzi wa Sekondari hiyo unatokana na fedha za mradi wa serikali kuboresha Elimu ya Sekondari(MMES) kwa kushirikiana na LGCDG kwa mwaka wa fedha 2006/2007 
Picha ya mwisho inaonyesha jengo la shule ya Sekondari ya Ruanda. Jengo hilo ni miongoni mwa majengo yanayotakiwa kukarabatiwa ili kuboresha hali yake na kuweka mazingira mazuri ya kusomea.

PICHA ZOTE na Hoops Kamanga, Nyasa

2 comments:

  1. Asante sana kwa taarifa hizi za kutia moyo. Mimi kama mwalimu naguswa sana na taarifa hizi. Katika kupanga mikakati ya safari zangu za Tanzania, itabidi nipitilize hadi Nyasa tena. Nimeshafika Mbamba Bay mara tatu katika miaka ya karibuni, lakini itabidi nifanye juu chini kuzitembelea angalau baadhi ya hizi shule.

    Mimi hupenda kutembelea shule na vyuo katika mkakati wa kujionea kinachoendelea, na kuongea na walimu kuhusu mikakati ya kushirikiana. Kwa upande wangu, nazingatia zaidi suala la kuchangia vitabu, kwani huku ughaibuni niliko ni chimbuko zuri la vitabu. Mtihani huwa ni namna ya kulipia gharama ya kuvisafirisha. Huwa najikongoja na kupeleka kidogo kidogo.

    ReplyDelete
  2. nakuunga mkono prof. mbele hata mimi natamani sana kufiki huko ingawa nimezaliwa nyasa lakini itabidi nifike na kuona hii Wilaya...Ahsante sana kwa taarifa za Nyasa

    ReplyDelete

Maoni yako