April 17, 2013

UHARIBIFU: MAFURIKO YALIYOTOKEA MAENEO MBALIMBALI WILAYANI NYASA

Hoops Kamanga, Mbamba Bay
Wiki iliyopita wilaya ya Nyasa ilikumbwa na simanzi kubwa kutokana na mvua kubwa iliyonyesha kisha kusababisha maafa kwa wakazi wake. Katika maeneo mbambali ya wilaya hiyo yalikumbwa na mafuriko kutokana na mvua kubwa iliyonyesha kwa muda mrefu na kusababisha maeneo mbalimbali kujaa maji na hivyo kusababisha uharibifu mkubwa.
Moja ya mifereji iliyoharibika
Maeneo kama Mbamba Bay, Lundo, na vijiji vya jirani kulitokea maafa makubwa. Watu walipoteza mali, zana za kazi, majengo kuharibiwa, barabara kuharibika zaidi, huku madaraja yakivunjika hivyo kusababisha usumbufu wa mawasiliano kati ya vijiji mbalimbali wilayani hapa. 

Nilipita maeneo mbalimbali wilayani hapa yaliyokumbwa na mafuriko kwa hakika hali ni mbaya, na ukweli ni kwambahali sio nzuri mashamba yameharibika mifugo imekufa wananchi wamerudishwa hatua nyingi nyuma. 

Kwa hakika maeneo mbalimbali yameharibika sana, wamekufa mamba na ilikuwa balaa mamba wa mtoni wamesombwa wotkuna mamba mmoja aliamua kukimbilia kwenye makazi ya watu yupo pale kwa akina jairos kama unae mizoga tu imejaa ziwani.  

Pamoja na hayo yako mambo yaliyoshangaza sana maji yalikuwa kasi sana, mfano maeneo ya Fisheries kwenye yale mashamba ya mpunga....yaani yupo live niliacha wanafanya utaratibu wa kumrudisha mtoni lakini maji bado yapo kasi na vile vichaka vyote pembeni ya mto hakuna kwa hiyo hana pa kukaa niliwashauri waombe kibali wamuue atakula watoto.

Baadhi ya Mpunga ulioharibiwa.

  

Ni daraja lililokuwa linaunganisha kijiji Mbamba  Bay na Ndesule.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako