Na
Amon Mtega, Songea
JOPO
la makocha kutoka timu ya Arsenal
ya Uingereza wamewasili Songea
mkoani Ruvuma kwa ajili ya kutoa mafunzo ya ukocha ya siku tano ya mpira wa
miguu kwa walimu wa shule 40.
Akizungumza
jana na waandishi wa habari, Mratibu wa mafunzo hayo Selwin Ngonyani alisema makocha hao kutoka timu ya
Arsenal Uingereza wamefika mkoani hapa
kutoa mafunzo kwa lengo la kuibua vipaji kwenye shule hizo.
Alisema
mafunzo hayo yanafanyika kutokana na ushirikiano uliyopo kati ya Shule ya Sekondari
ya wasichana ya Peramiho na Mtakatifu Arouse
ya Uingereza ambayo ina urafiki na timu ya Arsenal.
“Mafunzo
hayo yatatusaidia kuwafundisha vijana wetu
shuleni kwa kuibua vipaji vyao
ili na sisi kwa siku za baadae tuwe na wachezaji wazuri wenye viwango vya hali
ya juu,” alisema.
Kwa
upande wake mmoja wa makocha hao, Tony David
alisema Tanzania ni nchi yenye vijana wenye vipaji vya michezo hasa
mpira wa miguu kwa kuwa wanafundishika na kuelewa haraka.
No comments:
Post a Comment
Maoni yako