Na Vitus Matembo,
Mbamba Bay
Nyasa ndio Nyumbani
halisi, nimezaliwa na kukulia katika mji wa Mbamba bay. Pia nimewahi kuishi
vijiji vingi ukanda wa ziwa Nyasa kama vile Mkali, Ndengele, Mtipwili, Lundo,
Kilosa na Ndesule kutokana na kuhamishwa kikazi kwa Mzazi wangu ambaye ni
mwalimu.
Nimewahi kutembelea
vijiji vingne kama vile Mango, Tumbi, Kihagara na Ng'ombo Ila kwakweli
Jiografia ya Nyasa ni nzuri ukiitafakari kwa kina. Kwa wageni huwa ni lulu
wafikapo Nyasa. Kwa muda wote huo bado
nimeendelea kuipenda Nyasa yangu ila toka utotoni kitu UCHAWI imekuwa kero sana
katika masikioni mwangu.
Uchawi ndio changamoto
inayoleta kuoneana wivu katika maendeleo na ndicho kinachorudisha maendeleo hapa
kwetu Nyasa. Mtu akisoma sana/ akiwa
na akili sana lazima achezewe au kufanyiwa mambo ya kichawi. Kwa mfano mimi
napata tabu sana kwa kupigwa chale karibu kila wiki. Hakika naumia sana, japo
sina namna kwani ndiyo Nyumbani.
Wengne huwa hawaji
Nyasa kabisa hata kama ni kwao, ila kwangu nitavumilia tu na nimebakia kumuomba
Mungu ili aniepushe ni hao waovu. Kwa mfano toka nimalize
chuo mwezi june mwaka huu. Nilipofika Nyasa nimesikia na kuona matukio mengi ya
kutatanisha kama vile kukuta nyama ya binadamu sebuleni huko kijijini Chiulu.
Pia babu kumlazimisha mwanae aende ziwani na kusababsha kifo. Vilevile askari
waliotoka Depo kufa maji kiholela. Matumizi ya radi kuuana.
Kubwa kabisa na la
kustaajabisha ni uwepo wa mamba wa watu ziwani. Kwa mfano mwezi uliopita kuna
mamba aliuawa alipopasuliwa tumbni watu hawakuona Nyongo, si kwamba ilipasuka
LAHASHA, ila haikuwepo.(ona pichani).
HAKIKA KWA MATUKIO YA
UTATA KAMA HAYA YANANIPA CHANGAMOTO KUBWA.
Ila haina maana ya
kukukimbia Nyasa ndo suluhisho, hapana ila kinachotakiwa ni kuzidi kutoa elimu
kwa jamii ili kutokomeza imani za kishirikina.
MABADILIKO DAIMA HUANZA
NA WEWE.
"PAMOJA TUIJENGE
NYASA"
No comments:
Post a Comment
Maoni yako