Na Vitus Matembo,
Ndengele
Ukanda wa ziwa Nyasa
huvutia sana hasa kutokana na mandhari yake kuwa ya kustaajabisha machoni kwa
wageni. Hali ambayo inatarajiwa kuongezeka zaidi miaka ijayo kutokana na kasi
iliyopo.
Lakini jambo kubwa
zaidi ni ujio wa wageni hususani wazungu umeleta chachu ya uwekezezaji na
maendeleo ya kijamii na uchumi.
Hoteli ya Mbunge wa Jimbo la Mbinga Magharibi(Nyasa), John Komba. |
Nyumba iliyojengwa juu ya Jiwe katika kijiji cha Ndengele. |
Katika suala la ujenzi
wa nyumba, kwa muda sasa nimeshuhudia mzungu mmoja akijitahidi kujenga Nyumba
ya Ghorofa Juu ya jiwe. Alianza muda mrefu ila
mwaka huu ameikamilisha Kwakweli inavutia sana. Nyumba hiyo ipo katika kijiji cha Ndengele,
Wilayani Nyasa, kando kando ya barabara itokayo MBAMBA BAY kwenda LIULI.
Wengi wameshangazwa na
ujenzi huo kuwa kwanini ajenge juu ya jiwe. Ila kwangu binafsi naona haina
tatizo na nyumba ni nzuri sana.
Natamani nipate nafasi
ya kuishi kwenye nyumba kama hiyo kwani Mandhari ya ziwa Nyasa huonekana vyema
sana hususani fukwe ya Mbamba bay na Ghuba yake yote.
Aidha, Mbunge wetu, Mh.
JOHN KOMBA naye ameamua kujenga hoteli yake pembezoni mwa ziwa hapa mjini Mbamba
bay, wilayani Nyasa. Huu ni mwanzo tu wa
kupeperusha utalii wa Nyasa. Mengi yatawajia, Usikose kutembelea mara kwa mara
blog yetu upate uhondo.
KARIBUNI NYASA WAPENDWA
WETU
Ndengele ...ninekumbuka mbali sana ..ni kijiji cha kwanza toka Lundo...lwika au ni Chinula?.....
ReplyDelete