February 05, 2014

KILICHOJIRI MKUTANONI LEO NA MBUNGE JOHN KOMBANa Vitus Matembo, Mbamba Bay

Mkandarasi ametambulishwa Rasmi toka Sri Lanka anaitwa MR.DIISA. Kazi inaanza kesho ya upimaji. KITUO Kikuu cha upokeaji umeme kiko KILOSA ila utaanza kupatikana hapa MBAMBA BAY baadae kwingine kote NYASA mwaka huu.

Gharama za kuchukua fomu ni sh.5700/= na kodi ya kuweka na kuingiza umeme ni Sh. 26000/=. Mchakato rasmi wa kuweka nguzo za umeme toka Mbinga mwisho ni mwezi Machi mwaka huu.

NIMEWAWAKILISHA VYEMA kwa kutoa hoja nzito nne: Hospitali kutokuwa na dawa wakat tunatozwa hela, Suala la Elimu, Uzuiaji maji kwa kujenga mifereji, pia Lini hasa umeme utafika Nyasa!.

Mengine ni Lami kuwekwa Mbamba bay kwa K.M 1, kufutwa mchango wa madawati kila mwaka, alama za X zifutwe kwa hapa Mjini MBAMBA BAY.

HALMASHAURI IMESEMA TUIPE MUDA KWANI INA MIEZI SITA TOKA IINGIE MADARAKANI!!. Mambo yote yatarekebishwa.

HAKIKA NIMESIFIWA SANA NA MBUNGE NA MKUU WA WILAYA KWA MASWALI YENYE AKILI!

ILA SUALA LA ELIMU NI KILIO KWA WILAYA YA NYASA!.

JAMANI TUWE KIOO KWA JAMII ZETU HUKU NYASA. Yaani fursa niliyoipata leo ni utambulisho tosha kwamba vijana tunaweza kuleta maendleo KWETU NYASA.

(PAMOJA TUIJENGE NYASA)

No comments:

Post a Comment

Maoni yako