NA KIZITO MPANGALA
PICHANI ni duka la dawa za binadamu. Unaona limefungwa.
Limefungwa kwa sababu maalumu kisheria. Tazama jinsi lilivyo, kwa nje hata
utambulisho ya kwamba hili ndilo duka mojawapo miongoni mwa maduka ya dawa za
binadamu lifahamikalo katika mtaa husika.
Hatupo kwa ajili ya kuharibiana wasifu. Hatupo kwa ajili ya
kubaniana michongo na madili. Hatupo kwa ajili ya kukatishana tamaa. Wakati ule
nilipokuwa Mseminari tulikuwa tukifimdishwa kitu kinachoitwa
"DHAMIRA". Tuwe na dhamira zenye kujali uwepo wa wengine.
Duka hili lililofungwa liwe funzo kwa wengine ambao bado
hamkuguswa kwa maana unyoya bado unapepea na utakuja kukuguseni popote mlipo.
Ninaheshimu wasifu wenu nyote, ila uwe wasifu wenye nia nkema na kuachana na
dunia ya michongo na madili.
Aliyekuwa anasimamia duka hili na ambaye ndiye mhusika mkuu
wa umiliki wa bidhaa zilizokuwemo dukani humu HANA UJUZI WOWOTE UNAOHUSU
FAMASIA. Hivyo, alikuwa akiuza dawa na kuandika maelekezo ya matumizi ya dawa
kwa mgonjwa kwa kutumia UJANJA. Alikuwa ANABASHIRI tu. Ukihitaji Magnesium (Mg)
anakutazama kwa makini na kukuambia POLE SANA, UNA MINYOO. Huu ni mchongo wa
kibedui kabisa! Duka limefungwa.
Ifahamike kuwa dawa ya minyoo nfani yake lazima ihusishe
chembe za dutu Silver (Ag), hivyo ni niambata vya "pergertives" Duka
limefungwa.
Wale wenye maduka ya dawa za binadamu hata mifugo kuweni
makini. Kuuza dawa iliyokwisha muda wake ni kosa na ni uharamia dhini ya uhai
wa binadamu na mifugo. Faida ya fedha haikatazwi lakini tazama yule
anayekuletea faida mjengee uwezo ili akufae kwa faida wakati mwingine tena.
Duka limefungwa!
Siyo maduka ya dawa tu, yako maduka ua namna mbalimbali.
Hata wauzaji wa simu wapo wanaouza simu zilizotumika mida mrefu lakini huvikwa
vifaa vipya ili zionekane murua. Duka limefungwa!
Leo tumakinike na masuala ya dawa kwanza. Maana inawezekana
mtu akakuambia anauza "Morphine" tena kwa bei kubwa lakini huenda
ikawa imekwusha muda. Kama anadai kuitengeneza yeye mwenyewe huenda akawa
amezidisha viambatanisho au ameweka pungufu. Ni biashara safi, lakini CHEZA
KARATA YAKO VIZURI. Duka limefungwa!
© Kizito Mpangala
No comments:
Post a Comment
Maoni yako