November 25, 2017

JINA LA WILAYA YA NYASA LINAPOPATIKANA NDANI YA JIJINI DAR ES SALAAM

Mtaani huu unapatikana katika makutano ya Mitaa ya Lumumba na Mafia jijini Dar es salaam

UCHU WA MADARAKA DHIDI YA UZALENDO

KITABU: ZIMBABWE: STRUGGLES-WITHIN-THE-STRUGGLE (1957-1980)”
MWANDISHI: PROFESA MASIPULA SITHOLE
MCHAMBUZI: MARKUS MPANGALA
JESHI la Zimbabwe limetangaza wiki iliyopita kuchukua madaraka nchini humo na kumwondoa Rais Robert Mugabe ambaye ametawala nchi hiyo kwa kipindi cha miaka 38 hadi sasa. Kutokana na hali hiyo tunalaizmika kukumbuka namna mwanazuoni Profesa Masipula Sithole alivyobainisha matatizo ya Zimbabwe kupitia kitabu chake cha “Zimbabwe: Struggles-within-the-struggle (1957-1980)”

November 24, 2017

JIWE LA POMONDA NA FORODHANI PANAWEZA KUTUPATIA WATU WA 'DIVING' KATIKA MASHINDANO YA OLIMPIKI.

NA HONORIUS MPANGALA

LICHA ya kuwa mazingira mazuri na yenye kila aina ya vivutio lakini wafrika tunashindwa kuwa wabunifu wa katika kuyafanya kama fursa.Mungu aliiumba Afrika hivi ilivyo na kuweka jiografia ambayo nyakati zote watu Wa mataifa ya ulaya wamekuwa wakivutiwa nayo.
Mmmoja wa Warukaji katika Jiwe la Pomonda, Ziwa Nyasa
Iko michezo mingi inayochezwa Ulaya na Amerika inatokana na jinsi wenzetu walivyo makini katika kutumia mazingira yao katika kujipatia fursa ya maisha yao. Nyakati zote mataifa ya wazungu yamekuwa na michezo mingi ambayo ina mashabiki na wanafanya vyema,hakuna michezo ambao unakosa mashabiki Amerika na Ulaya.

TANZIA: MBUNGE WA SONGEA MJINI AFARIKI DUNIA



NA MWANDISHI WETU, SONGEA
MBUNGE wa Jimbo la Songea Mjini kupitia chama cha CCM ndugu Leonidas Tutubert Gama amefariki dunia usiku wa kuamkia leo hii katika Hospitali ya Peramiho ambapo alilazwa kwa saa chache kabla ya kifo chake.

November 23, 2017

ABDI BANDA AMETUONYESHA MAANA YA “SOKA LA KULIPWA”

Abdi Banda
NA HONORIUS MPANGALA
KATIKA pambano la kirafiki kati ya Tanzania na Benin pale mjini Porto Novo nilimshangaa Abdi Banda. Kama tumjuavyo Banda ni kiraka katika kucheza soka anauwezo wa kucheza nafasi za ulinzi kama mlinzi wa kushoto, beki ya kati na kiungo wa ulinzi kwa usahihi mkubwa. 

Sasa alichokuwa akikifanya pale Benin alikuwa anatuonyesha utulivu wa akili yake katika maeneo hayo mawili yaani kumudu hulka yake na kuwa mzuri katika kucheza soka lenyewe. Banda alikuwa mtu aliyewatuliza wachezaji wenzake waliokuwa wamepatwa na hasira kwa maamuzi ya mwamuzi wa mchezo ule. Kwa penati iliyotolewa na mwamuzi ambayo mpira ulionekana wazi kuguswa na mchezaji wa Benin lakini pigo likawa kuelekea katika goli la Tanzania. 

FREDDY MACHA ALIVYOLIZUNGUMZIA JUKWAA LA KISWAHILI SOCIETY

NA MARKUS MPANGALA 
SWALI: Naam, shikamoo Mzee Macha?
FREDDY MACHA; Marahaba. Habari zako bwana! uko wapi wewe siku hizi? Maana tangu tuliposalimiana pale Soma Café,Mikocheni na baadaye Nyumba ya Sanaa, Dar es Salaam wakati wa warsha nilizoendesha huko.
SWALI; Nipo hapa Bongo naendelea vema tu. Ni kweli, kitambo hatujawasiliana, pia nilifaidika sana na warsha zako hata hivyo si neno, tutaongea kidogo leo.
Freddy Macha
 FREDDY MACHA; Asante. Nadhani leo unalo la kuongea zaidi. Karibu.
SWALI; Ni kweli, nahitaji mengi kutoka kwako mzee wangu. Kiu yangu ni huu mradi wa Kiswahili Society, kwani umeeleza mahala fulani nikasoma nami nimevutiwa ili niwaarifu wasomaji. Je mradi huu ulianza lini na wapi?
FREDDY MACHA; Umeanzishwa na wanafunzi na Wahadhiri wa Kiswahili pale chuo cha lugha cha SOAS (School of Oriental and African Studies) hapa London,Uingereza.
SWALI: Nini dhumuni la kuanzishwa kwa Kiswahili Society?
FREDDY MACHA; Kuunganisha Wazungumzaji wa Kiswahili duniani lakini hasa hapa Uingereza.
SWALI: Nashukuru sana. Ndugu Macha, wewe ni Mwanamuziki,Mwanafasihi,na Mwandishi mkongwe. Katika fani hizi kuna mambo mengi umejifunza kutoka bara letu la Afrika,Latin Amerika,Marekani na sasa Ulaya. Unadhani jamii za watu wa Ulaya hususani Uingereza zinaweza kuhamasika kukiendeleza Kiswahili?