January 04, 2018

NYASA YAKAMILISHA UJENZI WA BWENI YA WANAFUNZI

NA MWANDISHI WETU, NYASA
HALMASHAURI ya Wilaya Nyasa inamilisha ujenzi wa Mabweni ya Wasichana katika Shule ya Sekondari ya Mbamba bay (Mbamba Bay High School) iliyopo mjini Mbamba ikiwa ni njia ya kukamilisha mpango wa elimu bora kwa wakazi wa wilaya hiyo.

Bweni hilo ambalo linaonekana picha linatarajiwa kuchukua idadi ya wanafunzi Wanafunzi 312 hivyo kuondokana na tatizo la makazi ya wanafunzi katika wilaya hiyo. Ujenzi wa Bweni hilo umetokana na juhudi za ushirikiano na Mbunge wa Jimbo la Nyasa ambaye pia ni Naibu waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Stella Manyanya pamoja na wadau mbalimbali. 


Akizungumzia juhudi hizo, Diwani wa Kata ya Kihagara, George Ndimbo amsema, “Watu binasfi wamekuwa wakijitolea katika shughuli mbalimbali za kuboresha hali ya Nyasa, wakiwemo Mama Salome Nkondola na wengineo wengi sana siwezi kuwataja wote wanaunga mkono jitihada za Mheshimiwa Mbunge wetu. Kuna Familia ya Mzee Ndembeka, Kuna akina Madenge na wengineo wengi sana,”
Aliongeza kwa kusema, “Na sasa inajengwa Wodi First Class pale Mbamba Bay, Kituo cha Afya, kwa fedha kutoka kwa Wanyasa wenyewe na wahisani wengine ambao Mheshimiwa Mbunge amewatafuta. Tutafika tu ikiwa kila mmoja atawajibika katika nafasi yake. Kesho tarehe 05/01/2018 kutakuwa na hafla ya chakula cha usiku pamoja na waziri mkuu,Kassim Majaliwa kitafanyika ndani ya Meli yetu Mpya, na kila mwananchi anayo nafasi ya kushiriki chakula hicho kitaambatana na harambee ya kuchangia wodi hiyo ya daraja la kwanza. Mwananchi mwenye nafasi ya kuchangia kuanzia sh..5000/= atapata nafasi ya kuungana na waziri mkuu kwenye chakula hicho,”


No comments:

Post a Comment

Maoni yako