December 22, 2007
Likwilu,Kilosa,Mtipwili na mengineyo
Naam kamanilivosema inabidi kuangali kwa uchache baadhi ya maeneo nyeti ya ukanda waziwa nyasa lakini nimeona kilasehemu ipewe nafasi yake.Likwilu na Kilosa ni vijiji vinavyopakana au tunaweza kusema kwa Likwilu ni mtaa mkubwa ndani ya kijiji cha Kilosa kwani umekuwa maarufu katika maeneo hayo huku ukikiacha nyuma kijiji halisi cha Kilosa.Maeno haya kama ilivyo mengine yanatawaliwa na mashamaba makubwa ya kilimocha mpunga ambacho ndiyo uti wamgongo wa maeneo hayo.Hata hivyo kijiji cha kilosa kinapakana kwa kiasi kikubwa na mji mdogo wa Mbamba Bay ambako ndiyo kama makazi makuu ya watuwa maeneo hayo.Shughuli kubwa ni kilimo,uvuvi,biashara na maeneo ya historia.Kilosa ni mahali ambapo miaka ya kale ilikuwa kituo kikuucha kufundishia vijana JANDO na UNYAGO ambapo hadi leo kuna majengo na maeneo yaliyowazi ambayo yalikuwa yakifanyika shughuli hiyo.Watu wengi wamekuja kujionea historia hiyoya mababu wa kale katika kijiji cha kilosa na vitongoji vyake kwani pamekuwa mahali muhimu katika kazi ya kumbukumbu za watu wa kale.Eneo kubwa la kijiji hiki ni tambarare hali inyowafanya watu wake kuishi kwa amani bila kuwapo na hofu ya wanyama wa porini ambaoni hatari wapendao kuishi karibu na milimani.Usafiri hupatikana kwa uhakika.Pia watu wa maeneo haya huwa na mawasiliano makubwa na watu wa nchini MALAWI kama nilivyoainisha mwanzo.Mawasiliano ya karibu yapo katika miji ya NKATA BAY,MZUZU,LIKOMA NSISI na mengineyo ambayo hufikiwa na wakazi hawa.
Madhumuni
habari,
kumbukumbu,
mapumziko,
Nyasa
WASIFU: Mwandishi wa Habari,Tawasifu,Mhariri na Mchambuzi wa Vitabu,Siasa, Utamaduni, Michezo,Afrika, Kimataifa,Mshauri wa Habari na Mikakati. TUWASILIANE: mawazoni15@gmail.com, lundunyasa@yahoo.com. WHATSAPP; +255 719226293/SMS; +255 764 936655
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment
Maoni yako