October 24, 2007
KWAMBE;nyasa,sifa na uzuri
Naam hiki ni kijiji kinachopakana na kijiji cha chiwanda.kwa asili kinashabihiana sana jirani yake huyo.Sifa kubwa ya kijiji hiki ni upepo mkali nyakati za kiangazi,upepo ambao huambatana na na kasi ya mimea kupukutisha majani yake.Ni kijiji ambacho sifa hiyo inakifanya kiwe tofauti na jirani zake kwani ingawa kipo katika ukanda mmoja kina tabia hiyo tofauti na vijiji vingine.Wakaazi wake wengi ni kama vijiji vingine kwani hutegemea sana uvuvi,kilimo,na ufugaji ambao kuna makundi makubwa ya ng'ombe na wanyama wengine.Pia kiji hiki kinategemea zao la Mpunga kama nguzo ya uchumi kwa kiasi fulani.Ardhi yake ni kama kilivyo kijiji cha chiwanda kwani ni ya mchanga na kuna mabonde makubwa ambayo hufanya watu kulima mpunga katika nyakati tofauti iwe masika au kilimo cha umwagiliaji.Umwagiliaji huu huwa katika mifereji iliyochimbwa katika mashamba hayo ili kupitisha maji kwa wingi kama zao lenyewe linavyotaka maji kwa wingi.Wakaazi hawa hupata maji safi na salama ya bomba yaliyopishwa hapo kwa miaka mingi hivyo kupunguza idadi ya magonjwa yanayoambatana na ukosefu wa maji salama.Ziwa nyasa limekuwa kama kiunganishi chao na wakaazi wa nchi jirani ya Malawi.Kuna mito ambayo husaidia wakaazi hawa kulima bustani nyingi kwani maji yanayotokea katika mito ni mengi sana hivyo hurahisisha kazi ya umwagiliaji wake.Naam kwa wakati huu kijiji hiki hulima kilimo cha mpunga kwa kumwagilia kwani hakitegemei masika pekee,hivyo huwa na vipindi viwili vya ulimaji wa zao hilo.Tukutane katika kijiji kingine nan kisha tutaenelea na masimulizi yenye ufasaha kwani tunawakaribisha sana kuogelea na kujiliwaza katika ukanda wa ziwa nyasa.
Madhumuni
habari,
kumbukumbu,
kwambe,
Nyasa
WASIFU: Mwandishi wa Habari,Tawasifu,Mhariri na Mchambuzi wa Vitabu,Siasa, Utamaduni, Michezo,Afrika, Kimataifa,Mshauri wa Habari na Mikakati. TUWASILIANE: mawazoni15@gmail.com, lundunyasa@yahoo.com. WHATSAPP; +255 719226293/SMS; +255 764 936655
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment
Maoni yako