June 12, 2008

Mnyasa,Mwanakijiji na Markus X

Kuna tofauti kubwa kati ya wivu na usongo,vivyo hivyo wivu humuua mtu mjinga,na huwezi kumchukia mtu unayemuona halafu ukampenda mungu usiyemuona yani itachekesha sana.Unajua kwanini?Kuna jamaa anapenda sana kupongezwa basi jana nikamwambia haniwezi mimi mtoto wa kijijini,mnyasa na mwana wa Malcom X.kilichofuata ni kicheko,halafu akagundua kuwa nimekasirika kisa kabeza majina yangu,nikasema hana jipya mimi ni mwanakijiji,myasa mpaka kufa halafu nikaongeza Markus X.Ndiyo mimi ni mnyasa wala hilo halina ubishi,kwani hiyo ni fahari yangu wala haina maneno.Pili Mwanakijiji,ni kweli kwani mimi nimezaliwa kijijini Lundu hivyo napenda kuitwa Mwanakijiji yaani toka huko nyasa kwenyewe.Sasa unajua kisa cha kujiita Markus X?Nimeamua kujita hivyo labda nitaridhika maana kila ninapoona sura yake Malcom X na kusoma hoja zake basi nahisi navaa ushujaa na ukombozi wa watu wa nyasa lakini sina maana kwamba wanamatatizo bali napenda nikimaliza ujuzi wangu ninaoutafuta sasa nataka nikawe mwenyekiti wa kijiji chetu cha Lundu.Napenda falsafa za Malcom X mpaka napata wazimu{natania usije ukadhani kichaa kweli}.Ni kweli nimeamua kujiita Markus X ili mjue kwamba nina utajiri wa akili lakini nimekuwa fukara wa kipato lakini ni mimi Markus X,Mwanakijiji na Mnyasa asilia.

June 10, 2008

TANGAZO; Nafasi Ya Kazi Nyasa

Kuna nafasi ya kazi hapa nyasa.Ni kazi nzuriikiwa unasifa hakuna haja ya kulemaa njoo haraka.Hakuna masharti magumu bali ni afya njema isiwe na migogoro.Kazi yenyewe ni kuwa TARISHI kwani wanyasa tunampango wa kuwatumia samaki na vyakula vya nyasa kwa wote wazaliwa wa nyasa waliopo mbali hususani wale wa ughaibuni.Msingi wa kazi yenyewe ni kwamba tunataka kutuma vyakula vya huku nyasa kwani tumeona ndugu yetu hapati samaki kwa uhakika.Pale Ruhuwiko kuna hamu ya vyakula vya nyasa hivyo usipoteze nafasi hii kwani malipo ni kujitolea wala hakuna sumuni au shilingi bali ni moyo wa upendo.Kama unataka kazi hiyo tuma wasifu wako ukiambatana na uzoefu wako wa vyakula vya nyasa na uwezo wa kufanya kazi.Tazama mfano wa vyakula vya nyasa hapo juu

June 09, 2008

Hapa Kazi tu Hakuna Kuremba

Nakumbuka niliweka picha ya aina hii hapa bloguni.Lakini naona huu ni mwendelezo wa Wanyasa katika shughuli za kuinua uchumi wetu.Sifa ya kwanza ya wanyasa ni kazi,huwezi kuolewa kama mwanamke hujui kazi,mwanaume anakamilika kwa kuonyesha uwezo wa kufanya kazi.Wamo au unasemaje?

June 08, 2008

Hatujashindwa Tunasonga Mbele kama Hivi...

Ni kweli Timu yetu ya Taifa imefungwa jana na Timu ya Cape Verde bao moja, lakini haimaanishi kwamba tumeshindwa,tutashangilia na kujionea fahari ya timu yetu yaTaifa 'TAIFASTARS' kama hivi,tena kwa moyo mmoja,upendo mmoja,amani moja na juhudi Moja wala siyo The Philosophy Of loser.Tunaimanai na Maximo Wetu tuna imani na kila mchezaji kwani hao ndiyo mtaji wetu wa kuelekea kuwa na kina Zidane wetu,saa zaja,wakati waja twende pamoja jumamosi tukawashangilie kaka zetu vijana wenzetu dhidi ya kina Eto'o wa Kameruni.....Twende pamojaaaa iwe kwa upendooooo .....marafiki zaidiiiiiii..

Janeti na Hamu ya Njika kusoma Blogu

Kuna jamaa hapa ananitazmasana sijui anashangaa nini.Labda tokana na kasi yangu ya kundika hapa bloguni.Lakini namfahamu sana huyu jamaa unajua jina lake nani?nimemkumbuka umeona jina la mtu mwenye hamu ya kublogu hapo juu?Ndiye huyo anaitwa Njika Clara ni ndugu yangu,basi leo nimemnogesha kublogu nakwambia amebaki kutola mate tu jinsi anavyonogea mmm halafu ananiudhi amshika shavu sijui anamanaa gani.Najua hapa akitoka hapa nyasa anahamu ya kwenda kumtembelea shangazi yake mtaa fulani najua anafuata samaki tu si unajua wanyasa kitoweo chao.uache hilo,kuna mwingine tazama jina lake mwanzo "Janeti" basi jana kasoma blogu ya nyasa hii mpaka akakasirika kisa wivu eti wanyasa wanajidai na blogu yao.Haa nikammwambia mbona nawe mnyasa?akaniambia haijalishi ila wanyasa tunaringia kublogu.Lakini akamaliza kwamba hata yeye Blogu hii inamhusu shauri ye mnyasa.Basi huyu Njika anasoma blogu hii naona mpaka njaa inamuuma sijui hajala..ebu mtazama huyo hapo pembeni anakunja ndita sababu gani?.Mmmmm timu yetu ya taifaimefungwa na CapeVerde bao moja jana mmmm inauma sana

June 06, 2008

Wanyasa Tumuombe mungu Tushinde

Huyu ndiye Mrisho Ngasa (mwenye jezi ya bluu)ambaye tutamkosa katika mechi ya Jumamosi hii tarehe7/6/2008 nchini Cape Verde katika mechi ya kuwania kufuzu kwa kombe la dunia.Tutamkosa sana kwani mechi iliyopita hakuacheza baadaya kuumia nyonga mazoezini.ni mchezaji mahiri na mwenye msaada mkubwa kwa timu licha ya umri mdogo alionao.Tuloge na kuwanga kichawi kinyasanyasa

Timu Ya Taifa Imeondoka Leo

Timu ya taifa imeondoka leo kwenda nchini Cape Verde kwa mechi ya kuwania kufuzu kwa kombe la dunia.Hapa ni sehemu ya mashabiki wakishangilia timu ya taifa katika mechi dhidi ya Malawi iliyofanika hivi karibuni