July 08, 2008

Siyo Ukali Bali Anafurahia Nyasa

Kuna swali dadangu Ruhuwiko bloguni aliniuliza kuhusu huyu mnyama,nilikwepa kulijibu shauri nilikuwa natafuta kwanza picha yake na sasa nimeibamba.Ilikuwa adhuhuri fulani watu wakakusanyika kushangaa huyu mnyama wengine wakajiuliza ni Mamba gani huyu asiyejificha?Lakini ukweli ni kwamba dadangu alikuja nyasa toka ughaibuni lakini akaogopa kuogelea kisa mamba.Kimsingi huyu ni mnyama ambaye anaogopwa sana na Binadamu.Pale Liuli mzungu mmoja aliitwa Rainer alishikwa kwenye jicho na mamba mpaka kifo kikamkuta ikadaiwa ni sayansi ya kiafrika.Mimi sijui ila kwa hakika mambo wapo lakini kusema ndiyo hatari katika ziwa letu ni hapana,hawa ni wanyama ambao kila mmoja anatamani kuwaona,niambie kama unaogopa nikupe mbinu za kupuuza na kukupa nyakati za kuibuka kwa mamba ziwa nyasa.Kwa faida ya wasomaji ni kwamba nyakati za masika ni rahisi sana,hususani mwezi desemba na machi.Pia kiangazi hasa mwezi oktoba jua kali na joto kali,mamba hutokea sana vipindi hivi lakini siyo kuhatarisha maisha....hivi nimejitahidi kujibu au sijaweza?.....

July 07, 2008

Nashindwa kusema Labda nitakosea

Hivi unajifunza nini unapotazama picha kama hii.Kuna lolote unalojifunza?Niambie wewe unayeiangalia mimi sijui.Lakini jiulize wale wezi walioongozwa na yule jamaa anamvi anatoka mondulini...au monduli nini sijui.Jikomboe sasa

Mahaba Ni Raha na Faraja.....

Kuna raha,utamu,faraja,nidhamu na ukakasi.Au kuna ile hali ya kuona kwamba unaishi halafu hufurahii maisha yenyewe,unabisha?...Jamani samahani usije ukadhani kwamba nimechanganyikiwa.Lakini mahaba,raha na mafunzo ya kuyasaka yapo. hakika.Unajua kwanini.Nakumbuka wakati fulani nikiwa hapa nyasa maisha yanakwenda chini ya amri za wazazi{jambo ambalo hadi sasa nafuata amri za wazazi hao} lakini huku pembeni unastawisha gumzo,watu wanafurahia wanaona gumzo limenawiri utafikiri limewekwa mbolea kumbe mnyasa anaongoza gumzo.Gumzo lenyewe nimelikumbuka wakati ule tunatafuta ujiko mitaani si unajua mambo ya kinyasa?Basi hayo mahaba tunawaona watu yameshamiri ni raha tupu,kila mtu anaona hii ni raha na faraja.Kuona hivyo jamani mbona sisi hatuna gumzo la kustawisha mahaba na raha.Jamaa akaibuka kwamba inawezekana katika nafsi zetu hakuna maana ya mahaba..lakini tukamuuliza tutafute vipi?Eeeh jamaa akaanza ukitaka mahaba lazima uyatafute hakika hivi au ukitegemea kuwa yanakuja hilo umekosea.Basi suala lenyewe ni hili kuna rafiki yangu mnyasa hapa ana mambo ya ajabu kila siku yeye analalamikia kukosa mahaba na faraja za mahaba yenyewe.Kumbe nimegundua anaogopa kutafuta,akiona akina dada anatamani kuyasaka mahaba lakini anaogopa kuanza hata kuongea neno japo kusalimia...lakini ananilazimisha nimfundishe kuyatafuta mahaba shauri ni faraja.Nimeshindwa sababu mimi nimezoea kuvua na kutengeneza nyavu zangu shauri yake....jamani anayeweza popote ulimwenguni amsaidie au awasiliane nami hapa bloguni nimsaidie lakini tafadhali hakikasha unaweza kumtimizia maana ameniambia kuna zawadi nono kwa atakayemfundisha kuyasaka...au labda ajifunze katika blogu ya kaka Mbilinyi...ngoja nitamwambia ili anipunguzie mzigo kwani nimechoka kelele zake...lakini rafiki yangu mmmhh siwezi kuacha kumsaidia....ngoja nikomee hapa kwanza..

July 06, 2008

Mwalimu wangu Ndesanjo

Nimemkumbuka mwalimu wangu ndesanjo,Nimemkosa sana kila nikifikiria namna ninavyoringa katika blogu hii najikuta nataka kumwuliza mengine mwalimu wangu kwani bado yananipiga chenga.Njoo mwalimu wangu mwanafunzi wako nimekukumbuka sana....kuna teknolojia zingine zinanishinda....nifanyeje...ebu mwangali hapa alikuwa kwenye warsha ya mambo ya teknolojia India

July 05, 2008

Muwe Makini Usafiri wa Meli Mwezi Julai

Nimekwisha kusema kwamba mwezi Julai kuna dhoruba sana hivyo kama siyo wazoefu wa kusafiri kutumia meli basi nashauri kuacha.Wakati huu dhoruba kali watu wanatapika hovyo,hali ya hewa mbovu yaani mawimbi sana.Huu ni msimu wa dhoruba toka julai mpaka mwezi agosti mwishoni inategemea mabadiliko ya hali ya hewa maana inaweza kupitiliza hadi Septemba.Kuweni makini au tumieni usafiri wa magari toka Ng'ombo,Mbamba Bay,Liuli na mwambo wotewa ziwa nyasa usafiri upo Lundu, Lituhi na maeneo mengine

Kimya Kimya Leo Mawazo Sana

July 04, 2008

Kiangazi Mambo Huwa Bomba Sana

Kipindi hiki ziwa nyasa huamabatana na dhoruba kali sana,wakati mwingine inategemea hali ikoje maana dhoruba inaweza kuvuka hata mwezi septemba kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa.Lakini matajaio kuanzia septemba mambo huwa bomba sana hali inamkuna kila mmoja,watu huogelea sana ndiyo msimu wa wanyasa kupumzika kidogo.Ni kipindi safi sana ambacho kila mmoja anakifurahia,iwapo hakuna mabadiliko ya hali ya hewa.Hakika ni kipindi chetu hicho ndipo tunapoona mambo bomba sana.Inakuwa kama hivi...

Yasinta Watajie Jina...Anaitwaje Huyu...

Nimesahau jina nimejaribu hadi nikataka kupiga ngumi ukuta.Lakini kuna jamaa anapenda sana kujificha mapangoni kama wale jamaa wa al Qaida,amenikumbusha eti saizi nimesahau.Haya dada Yasinta wasaidie kuwatajia jina la huyu mnyama.....halafu pale Liuli karibu na hospitali wamejazana sana kama ndiyo kambi yao

Sina Neno Hapa kazi tu

July 03, 2008

Kazi kwenu Mganda ndiyo huo,hapo vipi?Hapo sawa? acheni wivu

Ndani Ya Meli Ya Mv Songea

kwa utulivu na safari yenye uhakika.Lakini tafadhali mwezi julai siyo mzuri kwa wale wasiozoea usafiri wa meli kuna dhoruba sana mwezi huu mpaka agosti mwishoni.Karibuni nyasa utamu kolea

Utulivu Wa Ziwa Nyasa

Kwa wale wanaopenda usafiri wa meli kipindi hiki siyo kizuri kwao iwapo tu siyo wavumilivu.Mwezi julai huambatana na dhoruba kali sana hivyo wale wasiozoea safari za meli hutapika sana.kwa hiyo tujihadhari kama hatujazoea mawimbi makali.Hapo ni Mbamba Bay,ukiwa mtaa wa zambia upande wa magharibi ya mji kutazama mashariki.

Bandarini Mbamba Bay Utamu Kolea

Hapa ndipo Mv Songea inapotia nanga.Tazama kwa umakini ujione uzuri hata kama ni kidogo acha tujivunie.Unajua nini?Kuna jamaa anapenda sana kuja hapa kutazama shughuli zinavyokwenda.Mara kwa mara ukimuuliza anakwamba anaenda kumpumzika Bandarini kutazama kazi na vituko vya wanyasa visivyo na shari.Mv Iringa nayo hutia nanga hapa ila lile meli la Malawi kubwa kama nini sijui linabaki kilindini na kutumia maboti.Jamani meli kubwa hilo utafikiri za wale jamaa walioenda kuvamia uarabuni.

July 02, 2008

Karibuni Tena Mbamba Bay

Ukitazama mbele kabisa unaona kama kuna majengo fulani-hapo ni karibu na Hoteli ya Neema.Yaani mahali pale ni pazuri sana kuna barabara toka uwanja wa hoteli hiyo mpaka ziwani yaani unabarizi tu taratibu siyo kwa usafiri bali matembezi.Kwa wapendanao wanajua matembezi lakini mnyasa hata sijui mimi kuvua samaki tu.Hili eneo lenye mawe pana uwazi mzurisana ambao hutumika kwa kujipumzisha nyakati za mchana.Hii ndiyo Mbamba Bay ndugu yangu karibu tena mmm lakini dadangu pale Ruhuwiko bloguni anaumia shauri amekosa sana utamu wa nyasa....ngoja nitakutumia basi la ungo uje kwa kasi kisha kurejea ughaibuni.

Mnyasa Nimetua Mbinga Leo Unasemaje.......

Angalia picha hii kwa umakini halafu niambie inakupa fikra kidogo?Mmhh hapa ni barabara kuu ya Mbinga mjini pale,ukingalia kwa mbali kidogo kuna jengo au mnara fulani-hapo ni jimboni au makao makuu ya jimbo la mbinga.Sasa itazame barabara hii halafu jiulize ni mara ngapi unapenda hali hiyo,ni namna gani unaweza kuwa na ustadi wa mazingira bora au maisha bora kwa kila raia.Lakini sitaki ulaumu ila nimependa sana hii picha nilipoipiga kwa mara ya kwanza kwani inaonyesha njia kuu ya mjini na maduka pembeni.Ukiwa upande wa juu pale karibu na hoteli ya Madina njia panda ya benki ya NMB na barabara ya kwenda kiwanda cha kahawa ndipo barabara hii ilipo.Ni barabara kuu katikati ya mji.Habari ndiyo hiyooo wabunge wa jimbo la Mbinga magharibi na mashariki.