December 22, 2012

PhD YA KWANZA KUANDIKWA KWA LUGHA YA KISWAHILI UDSM

Na Honorius Ngachipanda, Mbeya

Katika hali ambayo inaleta matumaini makubwa kwa wapenzi wa lugha ya Kiswahili, taarifa wkamba Dk. Metho Samweli amefanikiwa kuandika Thesis yake ya PhD ya somo la Kiswahili kwa lugha ya Kiswahili ni za kusisimua.
Kwa mujibu wa gazeti la THE HILL OBSERVER la Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Dk Method Samweli amekuwa mhitimu wa kwanza wa Chuo hicho kuandika Thesis ya PhD kwa lugha ya Kiswahili. The Hill Observer limeeeleza kuwa kwa muda mrefu sana wahitimu wote walikuwa wakiandika thesis zao lwa lugha ya kiingereza. 
Lakini Dk Method Samweli mwenye miaka 32 ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu kishiriki cha Elimu (UDSM-DUCE) ametunukiwa PhD hivi karibuni wakati wa sherehe za 42 zilizofanyika kwenye ukumbi wa MCCC (Mlimani City Conference Center).
Mkuu wa Idaya ta fasihi, Mawasiliano na Uchapishaji katika Idara ya Kiswahili ya Chuo kikuu cha Dar es salaam, Dk. Shani Omari alisema kuwa kabla ya thesis ya Dk method Samweli, hapakuwahi kutokea Thesis yoyote iliyoandikwa kwa lugha ya Kiswahili Chuoni hapo. 
Aidha, Chuo Kikuu cha Dar es salaam kinafuata nyayo za Chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) ambacho tayari wapo wanafunzi kadhaa walioandika thesis zao lugha ya Kiswahili. Miongoni mwa wahitimu wa PhD waliofanikiwa kuandika Thesis zao kwa lugha ya kiswahili, ni Mohamed Seif Khatibu ambaye ni waziri mwandamizi na kiongozi wa siku nyingi ndani ya CCM.

WASIFU WA DK. METHOD SAMWELI
Alijiunga sekondari ya Ndanda, kisha akajiunga na UDSM mwaka 2002 hadi mwaka 2006 alipomaliza masomo yake ya B.A with Education na kuwa mhadhiri msaidizi wa UDSM-DUCE. Kati ya mwaka 2006 na 2008 alimaliza masters katika masomo ya Linguistic hapo hapo UDSM. 

NAFASI YA KAZI ICT TECHNICIAN; MWISHO JANUARI 14, 2013

Anahitajika ICT TECHNICIAN, mwenye uzoefu, ujuzi na uwezo wa kusimamia masuala yote ya IT katika mtandao, servers, software development, maintenance and trouble shooting, and hardware maintenance.
Kama unazo sifa hizo hapo juu basi unakaribishwa kuomba nafasi ya kazi hiyo ukiambatanisha WASIFU WAKO (CV) na kuzipeleka kwenye ofisi zetu zilizopo ghorofa ya 9 katika jengo la NSSR HIFADHI HOUSE makutano ya mitaa ya Samora Avunue/Azikiwe Street Dar es salaam. Tuma kwa njia ya P.O BOX 3209 Dar es salaam.
Tarehe ya mwisho kupokea maombi hayo ni januari 14, 2013.
WAHI SASA.

December 21, 2012

WAZIRI MKUU AAHIDI KUCHANGIA SH. 25M/- ZA JENERETA

WAZIRI MKUU Mizengo Pinda ameahidi kuchangia gharama za ununuzi wa jenereta kwa ajili ya kata ya Majimoto wilayani Mlele mkoani Katavi ili waweze kuwa na umeme wa uhakika.
Alitoa ahadi hiyo jana mchana (Jumatano, Desemba 19, 2012) wakati akizungumza na wakazi wa kata ya Majimoto kwenye uwanja wa mpira akiwa katika siku ya saba ya ziara yake jimboni kwake Katavi wilayani Mlele, mkoani Katavi.
“Kuna wafanyabiashara wa hapa Majimoto ambao walikuja kuniona na wakasema wako tayari kuchangia ununuzi wa jenereta lenye uwezo wa kutoa kilovoti 60 za umeme kwa nyumba kama 300. Wao watoe milioni 25 wakiwa tayari na mimi nitatoa milioni 25... jaribuni mkae na kupanga namna ya kuchangia gharama.”
“Baada ya muda fulani mtakuta mmemaliza kuchangia, tuwarudishie wafanyabiashara hela yao ili hilo jenereta liwe la kijiji. Mkilipata, nitawasiliana na TANESCO ili watupatie nguzo za umeme,” alisema.
Akijibu hoja kuhusu viwanja, Waziri Mkuu ambaye ni mbunge wa jimbo la Katavi alisema upimaji wa viwanja ulifanyika miaka miwili iliyopita na vikapatikana viwanja 270 lakini hadi sasa havijagawiwa kwa wananchi. Aliwataka viongozi wa kata na wilaya wasimamie zoezi hilo.
Hata hivyo, Waziri Mkuu alitumia fursa hiyo kuwaonya juu ya ujenzi wa nyumba za makazi na biashara kando ya barabara kuu. ” Ninawasihi sana mheshimu sheria za barabara... msijenge nyumba zenu ndani ya hifadhi ya barabara.
Kesho (Ijumaa, Desemba 21, 2012) Waziri Mkuu atakwenda kata ya Usevya ambako atazindua mradi wa umemejua (solar power) kwenye sekondari ya kata ya Usevya na kuhutubia wananchi.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
ALHAMISI, DESEMBA 20, 2012.

NAFASI ZA KAZI DESEMBA HII MPAKA MWEZI JANUARI MWAKA 2013

WADAU: kwa wale wanaoendelea kutafuta kazi mbalimbali kwenye amshirika na taasisi za umma yaani serikalini, kuna nafasi za kazi zimetolewa ambazo nanyi wadau mnatakiwa kuzifuatilia.
Kwahiyo hapa naweka tanagzo hili ambali lionyesha nafasi za kazi katika sekta binafsi na umma.

BONYEZA HAPA KUSOMA ZAIDI

December 20, 2012

MAKAA YA NGAKA KUIMARISHA UZALISHAJI VIWANDANI


Mitaa ya mbinga mjini.
picha kwa hisani ya Prof Joseph Mbele

Uzalishaji wa makaa ya mawe unatarajiwa kuongezeka baada ya mradi wa uchambiaji wa makaa ya mawe mjini NGAKA wilayani MBINGA katika mkoa wa Ruvuma kufanza kufanyiwa kazi na kampuni ya uchimbaji makaa hayo wilanai humo.
KWA TAARIFA ZAIDI BONYEZA HAPA KUSOMA HABARI NZIMA

SERIKALI YATENGA SH. BILIONI MOJA KUJENGA DARAJA LA KAVUU

mbunge wa jimbo la Mbinga Magharibi.

SERIKALI imetenga kiasi cha sh. bilioni moja kwa ajili ya kazi za awali za ujenzi wa daraja la mto Kavuu linalounganisha kata za Mamba, Kasansa, Majimoto, na kijiji cha Inyonga yalipo makao makuu ya wilaya mpya ya Mlele. 

Hayo yamesemwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda jana jioni (Jumatano, Desemba 19, 2012) wakati akizungumza na wakazi wa kata ya Mamba kwenye uwanja wa mpira akiwa katika siku ya saba ya ziara yake jimboni kwake Katavi wilayani Mlele, mkoani Katavi. 
Waziri Mkuu alisema Serikali ina nia ya kufungua mawasiliano kati ya bonde la Rukwa na mikoa ya kaskazini ambako kuna uhaba wa chakula. “Bonde hili linasifika kwa uzalishaji mkubwa wa nafaka kwa hiyo kujengwa kwa daraja hilo ni ukombozi mkubwa wa kufungua soko kwa mazao mnayozalisha huku,” alisema. 
Alisema katika mwaka huu wa fedha, barabara ya kutoka Sitalike kupitia Kibaoni, Majimoto, Mamba hadi Kasansa yenye urefu wa kilomita 33.5 imetengewa sh. milioni 837/- na kwamba wakandarasi wawili wamekwishapatikana ili kuifanyia ukarabati barabara hiyo.
Kuhusu barabara ya Majimoto hadi Inyonga yenye urefu wa kilometa 135, Waziri Mkuu alisema zimetengwa sh. milioni 943/- kwa ajili ya ujenzi wa madaraja katika barabara hiyo. 
Alipoulizwa kuhusu kuwepo kwa fedha hizo, Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS) Mkoa wa Katavi, Mhandisi Isaack Kamwelwe alimthibitishia Waziri Mkuu kuwepo kwa fedha hizo. 
“Fedha zimeshatengwa na leo nimepokea kibali cha kutangaza zabuni za ujenzi wa daraja hilo. Zabuni zitatangazwa kuanzia Januari 2013,” alisema. 
Kutokuwepo kwa daraja la Kavuu kunawafanya wakazi waishia bonde la Rukwa (maeneo ya Majimoto na Mamba) kila wanapotaka kwenda Inyonga, walazimike kupitia Mpanda yaliko makao makuu ya wilaya yao ambako ni zaidi ya kilometa 350. 
Kesho (Ijumaa, Desemba 21, 2012) Waziri Mkuu atakwenda kata ya Usevya ambako atazindua mradi wa umemejua kwenye sekondari ya kata ya Usevya na kuhutubia wananchi.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
ALHAMISI, DESEMBA 20, 2012.

December 19, 2012

HALI YA WAVUVI NA UVUVI KATIKA ZIWA NYASA WILAYANI NYASA

Mvuvi akiwa na zana zake za kazi. 
PICHA: kwa hisani ya kaka Francis Godwin

UHABA wa samaki ziwa Nyasa upande wa Tanzania unaochangiwa na vifaa duni vya uvuvi umepelekea baadhi ya wanaume wa tarafa ya Mwambao wilaya ya Ludewa mkoani Iringa kutelekeza familia na kwenda nchini Malawi kufanya shughuli za uvuvi kama njia ya kukwepa changamoto za uchumi zinazoendelea kuwa kikwazo katika wilaya hiyo.
Uchumi wa wananchi wa tarafa yaMwambao ambao ulikuwa ukitokana na ajira ya uvuvi kwenye ziwa Nyasa nao umezidi kuporomoka kwa kasi kubwa na kupelekea hata biashara za wananchi wa maeneo hayo ambazo zilianzishwa kutokana na wingi wa wageni waliokuwa wakifika kujumua samaki kwenye ziwa hilo pia kuathirika kwa kiasi kikubwa.
Kama inavyofahamika kuwa uvuvi wa samaki kwa wananchi wa tarafa ya Mwambao wilayani Ludewa ndio shughuli kubwa ya kiuchumi ambayo imekuwa ikitegemewa na karibu robo tatu ya wakazi wa tarafa hii ya Mwambao na ndio shughuli iliyopelekea tarafa hiyo kuwa na mzunguko mkubwa wa fedha hasa kipindi cha nyuma japo kwa sasa imeanza kubaki historia pekee. 
Bonyeza kiungo;    SOMA ZAIDI HAPA

WAKAZI WA WILAYA YA NYASA WATAMUDU KULIPIA GHARAMA ZA KUUNGANISHWA UMEME?


Na John Chitanya, Nyasa

Wilaya ya Nyasa ni miongoni mwa wilaya mpya zilizoanzishwa mwaka huu kwa mujibu wa sheria za TAMISEMI chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu. Juhudi za kuanzishwa kwa wilaya mpya, sote tunajua linalenga kusogeza huduma kwa wananchi ili kukabiliana na matatizo mbalimbali na kuweza kujiletea maendeleo.. Wakala wa Nishati Vijijini kwa mujibu wa sheria Na.8 ya Bunge ya mwaka 2005 inaeleza kuhamisha, kusimamia na kuruzuku miradi ya Nishati vijijini ili kuongeza wigo wa upatikanaji wa nishati bora vijijini kwa ajili ya shughuli za uzalishaji,  mali na kijamii.
Wakala wa Umeme vijijini umeandaa mpango wa kusambaza umeme uitwao Underline Transformers na unatarajiwa kuunganisha vijiji zaidi ya 726 katika mikoa yote ya Tanzania Bara. Kwahiyo jukumu la wakala wa umeme katika maeneo ya vijiji kwa maana ya kujenga ‘Backbone Transmission Line’ inatakiwa wananchi kulipigia gharama za kuunganishwa kwenye ofisi za TANESCO zilizopo karibu na eneo la kijiji chao.


Wanafunzi wakienda shuleni katika shule ya Kata wilayani Nyasa.
Picha kwa hisani ya jaizmelaleo blog.


Miongoni mwa vijiji vitakavyopitishwa nyaya za umeme ni vijiji vya wilaya Nyasa. Kutokana na hali hiyo, nikiangalia hali ya uchumi ya watu wa vijiji vya Nyasa hakika najikuta nabaki na swali, ni namna gani wataweza kumudu gharama za kuunganishiwa umeme katikati yamiundombinu mibovu iliyopo wilaya hiyo? 
Kwa sasa harakati za kutengeneza miundombinu inafanyika. Ujenzi wa Barabara kutoka Mbamba Bay hadi Liuli, kisha kutoka Liuli hadi Lituhi, ikiwa na lengo la kurahisisha usafiri kwa wakazi wake. Mpango wa serikali ni mzuri, lakini ni vema tukaangalia namna ya kuhakikisha gharama za kuunganishiwa umeme zinatozwa kulingana na eneo husika.
Kusema hivi sina maana kwamba wakazi wa wilaya ya Nyasa wapate upendeleo, la hasha ila kwa hali ya uchumi wa wilaya hiyo naelewa ugumu wao kuweza kulipigia gharama za kuunganishiwa umeme. Wilaya Nyasa ni changa, na wakazi wake wanategemea shughuli za kilimo na uvuvi.
Kilimo cha mpunga, kahawa, mahindi, mtama, uwele, ulezi, zinaweza kuwakwamua ikiwa watajengewa miundombinu mizuri. Lakini suala la nishati ya umeme licha ya kuwa muhimu katika maisha yao, bado naona taswira ngumu kwa wakazi wa wilaya hiyo.
Miji muhimu kama Lituhi, Lundu, Kihagara/Njambe, Liuli, Mkali, Lundo, Mbamba Bay,na Kilosa inaweza kujipatia huduma za umeme kwa baadhi ya wananchi. 855 ya wakazi wa wilaya Nyasa hawatakuwa na uwezo wa kulipigia gharama za kuunganishiwa umeme.
Hiki ndicho kitendawili ninachoona hapa. Wakala wa umeme kwa kushirikiana na TANESCO wanatakiwa kufanya tathmini juu ya mazingira ya wakazi wa vijijini kuunganishiwa umeme.
Ni rahisi kuunganisha umeme katika mji wa Mbinga ambapo shughuli za kiuchumi ni kubwa na zimekuwa zikifanyika kwa muda mrefu. Lakini kwa wakazi wa wilaya mpya kama Nyasa, hakika ni mtihani mkubwa kwa wakazi wake.
Nadhani tunao wajibu sio wa kuwaelimisha juu ya matumizi ya nishati ya umeme, bali umuhimu wa kuwawekea mazingira mazuri ya kufanikisha upatikanaji nwa umeme. Ni vyema kabisa wahusika wakaelewa hili kuwa suala la wakazi wa wilaya ya Nyasa kulipia kuunganishiwa umeme ni kitendawili.

December 18, 2012

AIBU NA KASHFA KWA TANZANIA NA KENYA

Kuna taarifa huko Hong Kong kukamatwa kwa meno ya tembo kutoka Tanzania na Kenya.
Katika hali inayoshangaza juu ya idara zetu za uhamiaji, pamoja na ulinzi wa rasilimali zetu, ni wazi tunahitajika kufanya mapinduzi makubwa juu ya kulinda mali zetu.
Hii ni moja ya jambo linalosumbua akili za wananchi kwani haiwezekani tukakosa uadilifu kiasi cha ksuhindwa kulinda mali zetu.   Najiuliza tu, tuombe ile kesi ya wahusika ifike mahali pazuri kwa kuwatia hatiani.

SOMA HAPA ZAIDI KUJIKUMBUSHA

SASA UNA HAKI YA KUMILIKI GARI!




Je, unahitaji kununua gari la kutembelea, gari la abiria ama la mizigo? Nyaluke Motors, biashara tanzu ya Anesa Co.,Ltd; tunakupa jibu zuri la hitaji lako. Sasa tunaagiza na kuuza magari aina mbalimbali (used cars) kutoka Japan. Tuna utaratibu na mfumo ambao haujawahi kuwepo Tanzania. Unachohitaji kufanya ni kuchagua gari ulipendalo ama kutuarifu; kisha sisi tutaliagiza na kukuletea mahali popote ulipo Tanzania.
Gharama zote utatulipa baada ya kukabidhiwa gari lako. Kwa kununua gari kupitia Nyaluke Motors utaweza kupata unafuu wa hadi milioni 5 ukilinganisha na bei zilizopo katika showrooms zote nchini. Chagua gari lolote; Nissan Serena, Nadia, Xtrail, Prado, Scania, Fuso, n.k: kisha sisi tutatimiza ndoto yako kwa bei nafuu sana na utaratibu rahisi.
Pia kwa kupitia mpango rafiki ambapo mteja anaweza kulipia gari kwa awamu; akiwa anaendesha gari lake. Tunapatikana: Iringa-Mjini na Kilombero-Morogoro.
Wasiliana nasi kupitia: stepwiseexpert@gmail.com. Haijawahi kutokea Tanzania; ununuzi wa magari kurahisishwa namna hii. Changamka sasa ununue na kumiliki gari lako mapema. Nyaluke Motors: tunaamini kuwa; "KUMILIKI GARI NI DEMOKRASIA YA KILA MTANZANIA".

December 17, 2012

BEATRICE MPANGALA ASAJILIWA RASMI KUWA WAKILI

Wakili mpya, Ms Beatrice Makelele, anayeongea na Kilongalonga ambaye pia ni mdogo wa kaka Nathan Mpangala, akikata hatua huku akiwa na tabasamu tele mara baada ya kukubaliwa na kusajiliwa kuwa wakili katika sherehe zilizofanyika katika viwanja vya Law School of Tanzania, jijini Dar es Salaam, mapema Dec. 17, 2012. Hongera Salaam

Picha kwa hisani ya NATHAN MPANGALA, na hongera sana BEATRICE MPANGALA (Ms Makelele)