Showing posts with label Biashara. Show all posts
Showing posts with label Biashara. Show all posts

February 28, 2018

SERIKALI IMESIKIA KILIO CHA WENGI

NA GABRIEL MWANG’ONDA
HATIMAYE serikali imesikia kilio chetu kuhusu Single Customs Territory (SCT), wakati mfumo huu ukianzishwa na kutumika hapa kwetu Tanzania, binafsi nilipinga sana japo yalikuwa ni maazimio ya jumuiya za uchumi za Afrika Mashariki na SDC countries walikuwa ndio wanaanza kuipigia chapuo.
Mfumo huu unahusisha maafisa wa Forodha kutoka nchi jirani kuja kuweka kambi katika bandari yetu ili mtu akisema anaingiza bidhaa na zinaelekea DRC kisha aende kwenye deski la DRC lililopo hapahapa bandarini kwetu na kulipa kodi zote pale Bandari ya Dar es salaam. Kifupi ni kwamba sisi tulikuwa tunasaidia nchi jirani kudhibiti ukusanyaji kodi.
Mfumo huu ulilenga pamoja na mambo mengine kudhubiti wizi mkubwa wa bidhaa zinazokuwa zinanasinishwa kwamba ziko in transit wakati si kweli kwamba ni transit, mara nyingi huishia mikoa ya karibu na Dar es salaam na kurudi sokoni hapa nchini. 

February 23, 2018

SEKTA BINAFSI KWA MAENDELEO YA UCHUMI WA AFRIKA YA MASHARIKI

AJENDA: Afrika ya Mashariki.
WENYEJI; Uganda
WAHUSIKA: Ndugu Rais Yoweri Museveni, ndugu Rais John Magufuli na ndugu Rais Uhuru Kenyatta
MADA: Sekta binafsi kwa maendeleo ya nchi za Afrika mashariki.
MAONI: Sekta binafsi ina lengo la kutafuta faida. Haitatokea kuwa utoaji wao wa huduma kuwa kigezo cha kutotafuta faida. Ni jukumu la serikali kusimamia kupata haki zake kutoka kwa wadau wa sekta binafsi kwa njia zinazofaa. Tukitaka kuilazimisha sekta binafsi isilenge faida tutarudi kwenye "Mashirika/viwanda vilivyobinafsishwa" enzi hizo na baadhi yao kuwa "ghala za popo".

--MARKUS MPANGALA

January 11, 2018

KUFUNGWA KWA BENKI TANZANIA.

NA LAMECK KUMBUKA, USWISI
BENKI zinafungwa sio ishara njema kwa ucuhumi, lakini tufikirie pia sababu nyingine mbali na lile tunaloshabikia sana la “kuporomoka kwa uchumi”. Unajua kuwa idadi ya watu wenye simu na idadi ya watu wanaotumia huduma ya pesa kwa simu imepita zaidi sana idadi ya watu walio na Account benki?
Benki nyingi zilikuwa zinategemea wateja wa kawaida, amabao ndio idad kubwa ya watanzania. Bahati mbaya  Benki nyingi zilishindwa kujibu matakwa ya watu wa kijijini ambao ndo hufanya idadi kubwa ya watanzania wengi (hata wale wanaoishi mjini, wako Connected sana na ndugu jamaa marafiki, na miradi yao vijijin. Kile kilichoshindwa kufanywa na benki hizo, kinafanywa na huduma za simu, Mzunguko wa pesa umehamia kwenye simu sio tena katika mabenki.

January 01, 2018

SALAM ZA MWAKA MPYA 2018; KOROSHO MTWARA

NA GABRIEL MWANG’ONDA
 
KAMA ilivyo kwenye korosho kule Mtwara, basi kwa wale wahenga wenzangu wa mji wa Tukuyu mtakuwa mnajua zile karanga za mitini kwa watu wa mjini na sehemu zinginezo wanaweza kudhani nadanganya, lakini la hasha ni kweli kuna karanga humea mitini na ni miti mikubwa kabisa, kwa kinyakyusa zinaitwa (Macadamia). Hizi zina vinasaba vya korosho kwa mbali, ni very delicious and healthy vilevile. 

Wakati bei ya korosho ikipanda mpaka kufikia elfu nne kwa kilo kule Nangwanda Sijaona kunako Mtwara, watani wetu wa jadi hapo Kenya wameamua kuachana na mashamba ya Chai na kukazania kilimo cha Karanga za mtini ambazo zimefikia kilo moja Tshs 21,000.00 nakuendelea. 


November 16, 2017

MV NJOMBE INAVYOFUNGUA FURSA KWA WAKAZI ZIWA NYASA.


Honorius Mpangala, 0628994409

NA. HONORIUS MPANGALA
AKIWA katika kampeni za urais mwaka 2005 Rais mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete katika ardhi ya Kyela Mkoani Mbeya alihaidi meli. Alirudia tena kauli hiyo alipokuwa katika ardhi ya Mbamba Bay Mkoani Ruvuma. Baada ya kipindi cha utawala wake hatimaye meli alizoahidi tayari zimeonwa na Wanyasa. 

MV Njombe imekamilika na kufanikiwa safari moja ya majaribio kutoka Bandari ya Itungi hadi Mbamba Bay.  Yapo mambo ambayo ni fursa kwa wakazi wa Nyasa kutokana Meli hii. Kama inavyoitwa ni meli ya mizigo ni chombo kitakachoweza kuwainua kiuchumi wakaza wa Nyasa kama watakitumika ipasavyo. Kuinuka kiuchumi kutatokana na kujikita katika shughuli ambazo wakazi wake watajishughulisha na shughuli kama ilivyo kilimo biashara na hata ufugaji wa kisasa na wenye tija katika maisha ya leo.
Kilimo cha biashara ni moja ya ujasiriamali ambao watu wengi wamekuwa wakijishughulisha nao. Katika mwambao wa Ziwa Nyasa hususani wilaya Nyasa yapo mabonde ambayo yanaweza kufanyika kilimo cha mazao ya muda mfupi na kwa mfumo wa kilimo cha umwagiliaji, na kile cha kutegema mvua na kuleta tija.


October 23, 2017

URUSI, CHINA KUTAWALA BIASHARA DUNIANI



 
MOSCOW, URUSI

MIKAKATI ya serikali ya Urusi kuifanya China kama mshirika thabiti na muhimu kiuchumi umechochea kukuza sekta ya biashara na kufikisha asilimia 22 katika mapato yake.

Gazeti la The Moscow Times limesema kuwa ushirikiana wa karibu baina ya Urusi na China umechangia kuimarisha mapato katika biashara na kufikia kiasi cha dola bilioni 80 mwaka huu huku matarajio yakiwa ni kufikiwa dola bilioni 200. 

October 18, 2017

SABUNI ZA MAWESE MWANGA, KIGOMA

Wachuuzi wa sabuni maarufu Kigoma ambazo hutengenezwa kwa malighafi ya Mawese. Sabuni zina wateja sana. Mfano maeneo ya Dar es salaam kama mtu atabahatika kuwa na mtaji halafu akasambaza hata kwa wale wenye maduka ya jumla atapata fedha. Hii bidhaa nzuri sana.
 

October 04, 2017

KITAI NI ENEO ZURI KWA UWEKEZAJI

Pichani ni sehemu ya mji wa KITAI. Mahali hapo ni makutano ya barabara za Songea-Mbinga, Mbinga-Lituhi, Songea-Lituhi, mkoani Ruvuma ambapo kunajengwa Kituo cha usambazaji wa umeme vijijini (REA). Hilo eneo kushoto, na upande wa kusini ni tambarare na ambalo halikumbwi na mafurikio. Panafaa sana kufungua mradi wa uwekezaji hapa ni kiunganishi cha wilaya tatu za Mbinga, Songea na Nyasa. Sifa yake kubwa ni kuzikutanisha wilaya hizo na kuwa eneo la katikati katika kupata huduma za kibiashara n.k

June 27, 2014

RADIO CONSULT LIMITED



RADIO CONSULT LTD

Ni kampuni inayotoa huduma za ushauri wa kitalaamu kwa masuala ya radio. Moja ya huduma tunazotoa ni kama ifuatvyo:-
Tunatoa huduma zifuatazo:-
1. Wanaotaka kuanzisha kituo cha radio, tunatoa huduma zote ikiwemo kuandika maandiko ya uombaji wa leseni TCRA.
2. Tunauza vifaa vya radio kwa order (Transmitter, mixer, microphones, Hybrid Telephones, antenna, STL n.k)
3. Tunadesign studio za mazoezi kwenye vyuo vya unadishi wa habari kwa bei nafuu. 4. Kuandaa ratiba za vipindi vya radio (scheduling&Planning)
5. Media Research
6. Kuandika maandiko (Business Plan, Strategic Plan, Editorial Policy, Feasibility Study n.k)
7. Tunatoa mafunzo mbalimbali (Uandaaji wa vipindi, Management, Marketing, ICT for radio, Internet Radio, Journalism n.k)
8. Tunachuo cha media pia www.dmctanzania.org. Kwa huduma zaidi fika ofisini kwetu Nanenane Mbeya, jengo la Chai (RSTGA) au tupigie simu namba 0768188429 au 0759307280 au tuandikie email: consultancy@radiotz.com zaidi tembelea www.radiotz.com Facebook: www.facebook.com/radiotz

September 20, 2013

KARIBU UMEME WA GRID YA TAIFA NYASA



Na Vitus Matembo, Mbamba Bay

Leo Tanesco wameanza kutoa semina na elimu kuhusiana na uzinduzi wa umeme, matumizi, malipo na gharama za kujiunga. Pia wamealikwa wananchi wote wahudhurie bila kukosa. Ni semina endelevu kwa vijiji vyote wilayani Nyasa. Ila sasa wapo stand ya mjini Mbamba bay wakifanya mkutano.

September 10, 2013

WATANZANIA TUKAZANE KUWEKEZA KWENYE ARDHI



Na, Albert Sanga, Iringa
 
Leo ni mwaka mmoja kamili umepita tangu nilipoandika makala hapa safuni iliyokuwa na kichwa, “Njooni shambani mtajirike”. Ilikuwa ni makala iliyotoa shime kwa watanzania kuchangamkia fursa ya uwekezaji kwenye kilimo cha miti.

Katika makala ile niliwaeleza watanzania upana wa faida ya kuwekeza katika miti aina mbalimbali huku nikijikita katika miti ya mbao, karatasi na nguzo.  Nilichambua kwa kina sana gharama za upandaji wa miti hiyo, muda wa kuvuna, soko lake lilivyo na matarajio ya biashara hiyo kwa miaka ya baadae.

Leo ninaandika tena makala hii huku nikiwa na furaha tele moyoni mwangu kwa sababu makumi ya watanzania waliuitikia mwito wangu na wakachangamkia fursa hii. Kama ambavyo nilitamani iwe, ndivyo ilivyokuwa kwani wengi wamenijulisha kuwa hawakulazia damu, walichangamka na kuanza kuwekeza.
Ingawa mimi ni mmoja ya watanzania ambao wanajishughulisha na uwekezaji katika mashamba ya miti mkoani Iringa, kiu yangu ilikuwa ni kuona watu wakichangamkia fursa hii mahali kokote inakopatikana. Mikoa ya Tanga, Njombe, Mtwara, Tabora, Mbeya, Bukoba na kwingine kwingi kunastawi miti ya aina mbalimbali.

Kwa hakika wengi wameendelea kufanya hivyo kwani wamekuwa wakinijulisha. Wapo makumi waliosafiri hadi hapa Iringa kujifunza na kujionea fursa hii inavyowanufaisha na kuwatajirisha watu; kati yao wapo walioamua kuanza kuwekeza na wapo ambao walirudi makwao ili kujipanga kwa ajili ya kuwekeza wakati ujao. 

Furaha yangu ilikuwa kubwa zaidi pale ambapo wapo waliofika kujifunza hapa Iringa kasha wakaenda katika maeneo yao na kuanza kuwekeza. Wapo mamia ambao walizungumza nami kwa simu kutoka maeneo mbalimbali wakiwa wamevutiwa na habari zile.  

Nami kwa moyo mkunjufu nilishirikishana nao uzoefu wangu na kuwahamasisha waanze hata kama ni kidogo kidogo mahali popote wanapoona inafaa. Ni jambo la kujivunia na la fahari kutamka kwamba makala ile imekuwa na ‘impact’ kubwa mno kwa mamia ya watanzania ambao walihamasika kuanza kuwekeza katika miti kule Tanga, Tabora, Mbeya, Mtwara, Morogoro na wengine wengi hapa Iringa.

Kama ambavyo nimekuwa nikisema mara kwa mara katika makala zangu; ni kwamba muda wa kulalamika lalamika umekwisha. Mazoea na utamaduni wa watanzania wengi kudhani kwamba tunaonewa wakati wote haujatusaidia mpaka hapa kwa jinsi hii hakuna sababu ya kuendelea nao. 

Mtindo wa kuishi maisha ya kutaka kuhurumiwa yanatupotezea muda wenye thamani. Tumekuwa tukilalamika kuwa wageni (wanaokuja kwa jina la wawekezaji) wanatupora ardhi; lakini tusichokitafakari ni hiki, “Mimi kama mtanzania kwa nafsi yangu na kwa uwezo wangu nimefanya nini cha maana katika ardhi ninayoweza kuipata hapa nchini ama ninayomiliki?”.

Bahati nzuri ni kwamba idadi kubwa ya watanzania tunafahamu kuwa ardhi ni utajiri; lakini hatufanyi juhudi za makusudi kuuvumbua na kuutumia utajiri huo. Tunayo mamilioni ya hekta za ardhi zenye rutuba na zinazofaa kwa kilimo cha aina mbalimbali lakini bidii zetu hazijatosha hata tufike mahali tuseme ardhi haitutoshi.

Itakumbukwa kuwa wakati nikiandika makala ile mwaka jana pia nilizindua kampeni ya kimazingira niliyoibatiza jina la “Green The World And Become Rich”.  Kimsingi kampeni hii nililenga kuwahamasisha watanzania washiriki kikamilifu katika utunzaji wa mazingira na wakati huo huo wakitengeneza utajiri. 

Unapochukua fedha yako na kuwekeza kwenye shamba la miti moja kwa moja unakuwa umetunza mazingira kupitia miti uliyopanda lakini pia usiku na mchana kadiri miti inavyoendelea kukua unakuwa ukitengeneza mamilioni. 

Na hii ni namna moja nzuri ambayo watanzania tunaweza kuwekeza kwenye ardhi. Leo unapanda miti inakaa miaka saba ama kumi unavuna halafu baada ya hapo ardhi yako unaitafutia matumizi mengine. Si hivyo tu, lakini katika hiki hiki kilimo cha miti; ndani ya shamba lako unaweza kufuga nyuki, ukawa unavuna asali hukuku ukisubiri kuvuna miti yako.
Msukumo wa kuanzisha kampeni hii ya “Green The World And Become Rich” niliupata baada ya kutafakari nafasi walizonazo watu wengi wenye nia ya kuwekeza katika kilimo cha miti na katika ardhi kwa ujumla. Nilifahamu kuwa sio rahisi sana kwa mtu kutumia fedha zake na kupanda miti kwa faida moja tu ya kutunza mazingira. 

Nilijaribu kufikiri namna ya kuongeza thamani; hivyo ilinibidi nifanye kazi ya kuwaelimisha watu mbalimbali mambo mengi kuhusu miti, biashara yake na namna inavyolipa. Ninafahamu kuwa mamia ya wanaoendelea kuwekeza kwenye miti sehemu mbalimbali Tanzania, kufuatia kampeni yangu; wanawezekeza kwa mtazamo wa kupata faida kifedha huko mbeleni. 

Hilo ni jema sana lakini wakati huo huo mimi na wadau wengine wa mazingira tunashangilia kwa sababu mazingira yanaimarika huku watu wakitajirika. Vile vile Nilitambua kuwa wengi wanaweza wasiwe na taarifa sahihi kuhusu kilimo hiki, kwa maana ya maeneo kinakostawi, taratibu za upataji maeneo, lakini kubwa kuliko yote ni namna ya usimamiaji pindi wakiwa mbali. 

Nilifahamu mtu angeweza kujiuliza maswali mengi yakiwemo; “Nitawezaje kumiliki shamba Tabora wakati mimi kikazi nipo DaresSalaam?”, “Nitawezaje kufahamu biashara ya mbao, magogo, pindi ukifika muda wa kuvuna?”, “ Mbali na faida nitajuaje gharama za uendeshaji na je nitazimudu?”.  

Katika kampeni hii kulikuwa na majibu yote ambao kwa wale waliovutiwa kuwekeza Iringa katika maeneo inakowekeza kampuni yangu, nilijitolea kuwapa usaidizi wa kuwatunzia na kuyahudumia mashamba yao. Fursa bado zipo nyingi, watanzania wenzangu tusilale.
Ninapoandika makala haya leo ninatumia wasaa huu kuwakumbusha wale jamaa zangu wa kule Tanga, Tabora, Mbeya na kwingine ambao waliniahidi kuwa wataanza kuwekeza katika maeneo yao mwakani (yaani mwaka huu). 

Msimu ndio umeanza, kuandaa mashamba, kuaandaa miche na maandalizi mengine. Hapo hapo mlipo fanyeni kitu katika ardhi zenu, wekezeni kwa manufaa yenu na ya watoto wenu, isaidieni dunia kwa kuboresha mazingira yake.

Wale waliofika Iringa wengi wao nilikuwa ninawapa zawadi ya nakala ya sheria ya ardhi ya mwaka 1999. Na wengine waliokuwa wakiwasiliana nami nilikuwa ninawapa semina fupi kuhusu sheria ya ardhi. Kiujumla sheria hii inatupendelea mno wazawa tofauti na malalamiko mengi ambayo huwa ninayasikia.

Pengine Watanzania tuna tatizo katika ubunifu na inapotokea wengine wamebuni tunakuwa wepesi wa kudhani wametuibia. Mathalani, tunaishi na ardhi tusiyoifanyia kazi miaka nenda rudi, akitokea mwekezaji akabuni mradi Fulani katika ardhi hiyo; tunaanza kuja juu! Hatujiulizi tulikuwa wapi na kwa nini hatukuchangamkia?

Kingine kinachotumaliza Watanzania wengi ni ile dhana ya kudhani kuwa kilimo ni utumwa, shamba tunaona ni kwa ajili ya waganga njaa na waliokosa nafasi ya kupata ajira nzuri. Hii ni dhana mbaya na inachangia sana watanzania kutokuwa na mikakati ya kuitumia ardhi kikamilifu. 

Hata hivyo nikiri kuwa wapo watanzania ambao wanatambua thamani ya ardhi na wanaitumia ardhi vizuri kwa uzalishaji na uwekezaji wenye tija. Lakini idadi hiyo haitoshi ukilinganisha na idadi ya wasiotambua nguvu na utajiri wa ardhi ambao wanaendelea kulalamika ugumu wa maisha na waliopoteza tumaini.

Jambo jingine linalotumaliza watanzania ni kutokuwa na maono ya muda mrefu. Wengi wetu tunataka mambo ya papo kwa papo, hatupendi kuangalia mambo ya vipindi virefu mbele. Mfano mzuri ni katika hili la uwekezaji katika ardhi. 

Mtu anaona ni kupoteza fedha kununua shamba leo ambalo pengine linaweza kuja kutumika miaka ishirini huko baadae. Mtu anaona ni kama kupoteza fedha kupanda miti leo ambayo atakuja kuivuna miaka saba ama miaka kumi ijayo. 

Wasichokumbuka wengi ni kuwa unachopuuza kufanya leo kwa gharama ndogo miaka ishirini ama kumi ijayo hutakuwa na uwezo wa kukifanya hata kama ukitamani. Mzee wangu mmoja hapa Iringa alinisimulia namna alivyopuuza kununua kiwanja kimoja hapa mjini Iringa mtaa wa Miyomboni mwaka 1994. 

Wakati huo anasema kiwanja hicho kilikuwa kikiuzwa kwa shilingi laki nne; lakini mwaka jana, 2012 kimeuzwa kwa milioni 320! Mzee wangu huyu anasema mwaka huo 1994 laki nne kwake zilikuwa ni hela ndogo sana lakini akapuuza. Leo hii miaka 20 baadae kiwanja kile kile kimeuzwa mara mia nane ya bei aliyoipuuza ilhali yeye (mzee wangu huyu) leo hana hata ujanja wa kupata milioni kumi! 

Kwa maneno yake anasema, “Ningekuwa na mipango ya muda mrefu katika kuwekeza kwenye viwanja, ardhi na mashamba, leo mimi ningekuwa milionea hapa mjini” Anachofanya mzee wangu huyu ni utekelezaji wa ule msemo, “Majuto ni mjukuu”!
Watanzania tusilale, ushindi wetu kiuchumi umo ardhini!
stepwiseexpert@gmail.com +255 719 127 901

August 24, 2013

BOTI HUTUMIKA KAMA SEHEMU YA UVIVU


HATA KAMA HAWATAKI TUNUNUE MABOTI YA KWENDA MALAWI, BADO TUNAYO KAMA HAYA ZIWA NYASA.