Showing posts with label utulivu. Show all posts
Showing posts with label utulivu. Show all posts

March 07, 2018

KITABU KIPYA KUTOKA KWA MWANDISHI BEKA MFAUME

March 05, 2018

MAMBO 10 USIYOYAJUA KUHUSU BUSTANI YA MUNGU- HIFADHI YA KITULO.

1.Hifadhi ya Taifa Kitulo ndiyo eneo pekee Tanzania lenye ndege aina ya tandawala machaka (Denhams Bustard) wenye uwezo wa kuruka kutoka bara moja hadi jingine.
2.Hifadhi hiyo inayopita katika mikoa ya Mbeya na Njombe ilitangazwa rasmi kuwa hifadhi ya Taifa mwaka 2005 ikijumuisha sehemu ya eneo la shamba la mifugo, msitu wa Livingstone na bonde la Numbi.
3.Kitulo ina ukubwa wa kilometa za mraba 442. Awali ilijulikana kama Elton Plateau baada ya Mvumbuzi Fredirick Elton kupita eneo hilo mwaka 1870. Mwaka 1960 Shirika la Chakula na Kilimo (FAO) lilichukua eneo hilo kwa ajili ya ukulima wa ngano na ufugaji wa kondoo.
4. Ndege aina ya tandawili machaka hawapatikani sehemu nyingine yoyote hapa Tanzania zaidi ya Kitulo.
5.hifadhi hiyo ndiyo eneo pekee ambalo ndege hao hutaga mayai na kuzaliana kwa wingi kabla ya kusafiri kwenda mabara mengine.

January 06, 2018

JIMBO LA NYASA: KWANINI WANANCHI WAISHI BILA HUDUMA ZA POLISI?

NA MARKUS MPANGALA, August 24, 2017 
JESHI la Polisi limepata Kiongozi mpya, Kamanda Simon Sirro. Kiubindamu Kamanda Sirro si mtu mpya kwakuwa anafahamika tangu makuzi yake. Kiuongozi Sirro anafahamika tangu akiwa askari wa cheo cha chini, Mkuu wa Operesheni na Mafunzo na baadaye Kamishna wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam.
Nikiwa nazungumza na Msemaji wa Jeshi la Polisi, Barnabas Mwakalukwa.

Hii ni sehemu ndogo tu kumhusu Sirro ndani ya Jeshi la Polisi. Kwa maana hiyo kiongozi huyo mpya aliyechukua nafasi ya Ernest Jumbe Mangu anao wajibu wa kuendeleza na kuleta ufanisi wa utendaji wa Jeshi la polisi nchini.
Pamoja na hayo ninalo jambo linaloniogopesha mno kwenye jamii zetu. Nimechunguza kwa muda mrefu na baadaye kuchora picha ya miaka ijayo, kwamba ni kwa namna gani tutaendelea kuishi katika jamii ambayo haina vituo vya Polisi?

Ni kwa vipi wananchi wawe mbali na walinda usalama na mali zao? Ni kwanini wananchi washindwe kupata huduma za Jeshi la polisi nchini kwenye baadhi ya maeneo? Chukulia mfano maeneo yaliyoko mipakani, lakini hayana vituo vya jeshi la Polisi. 

Takwimu za Jeshi la Polisi zilizoko kwenye tovuti yao (www.policeforce.go.tz) zinaonyesha kuwa matukio ya uhalifu na ajali zilizoripotiwa kati ya Januari hadi Desemba 2015 ni 1,909,685.

November 09, 2017

WILAYA YA NYASA INAO UTAJIRI WA VIVUTIO VYA UTALII

Mwonekano wa fukwe za Ziwa Nyasa.

MAMBO 50 YA KISAIKOLOJIA YATAKAYOKUACHA KINYWA WAZI

NA VITUS MATEMBO, MBAMBA BAY 
Mwonekano wa ufukwe wa Mkwakwa katika Ziwa Nyasa.
Hii ni kweli hata kama ulikua hujui kubali tu, maana ndio ukweli uliopo.
 
1. Mtu hufanya ishara nyingi za mikono akiwa anazungumza ukweli. Azungumzae uongo mikono yake huwa imetulia zaidi.
2. Sikiliza kwa makini namna mtu anavyozungumzia watu wengine akiwa na wewe, na ndivyo atakavyokuzungumzia wewe akiwa na watu wengine.
3. Ndoto zako zinabeba ujumbe mhimu sana. Asilimia 70 ya ndoto zako zina ujumbe wa siri.
4. Kwa kawaida watu huwa waaminifu na wakweli mwili ukiwa umechoka, na ndio sababu hutubu na kutoa siri zao kwenye mazungumzo yatekeayo usiku wa manane,

October 17, 2017

MANDHARI YA KIGOMA

Kigoma Tanzania, Barabara ya kuelekea Makumbusho ya Dr. David Livingstone Ujiji.

October 16, 2017

CHUO CHAANZISHA SHAHADA YA WADUDU

NAIROBI, KENYA

KITUO cha Elimu na Utafiti kinachofadhiliwa na Benki ya Dunia kimeasisiwa katika Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Jaramogo Oginga Odinga na kinasubiri ruhusa ya kuanzishwa kwa programu za Uzamifu na Uzamili kuhusu wadudu wanaoweza kuliwa.

Taasisi hiyo inapania kubuni njia za kuzalisha wadudu hao kwa wingi bila ya kuharibu mazingira ili kukidhi utashi mara baada ya wazo hilo likifanywa kuwa biashara.Wadudu wanaoliwa sana maeneo ya Magharibi mwa Kenya, ambao wana wingi wa madini ya protini na Zinki watafanywa kuwa biashara ili kuimarisha uwepo wa chakula cha kutosha, na kuondoa dhana mbaya katika kula wadudu. 

October 14, 2017

WATU WASIOJULIKANA WATAIKIMBIZA AFCON U-17 2019

NA HONORIUS MPANGALA 
 
MWANDISHI maafuru wa fasihi kutoka Nigeria,marehemu Chinua Achebe katika kitabu cha 'Things Fall Apart' alisema kukimbia matatizo sio njia sahihi ya kutatua hayo matatizo. Wakati msomaji wa fasihi hiyo akiona kama burudani kusoma vibweka vya Okonkwo lakini kuna mafundisho katika kitabu kile. Nyakati zote huwezi kuona ugumu wa jambo kama halijakutokea.
Chinua ananifanya nihusianishe matukio ya watu wasiojulikana na hatima ya Nchi katika nafasi ya kuandaa fainali za mataifa ya Afrika kwa vijana wa chini ya miaka 17.
Serengeti Boys wakifurahia katika moja ya mabao waliyofunga katika mechi za kimataifa
Ukimya wetu katika kuchukulia kila jambo ni kitu kinachofanyika na tukashindwa kutambua tatizo au kuwabaini wahusika linaweza kutuondolea mwonekano wetu nje ya mipaka ya nchi.

Matatizo yanatakiwa kutatuliwa kwa kufahamu chanzo na kuchukua hatua ya kuyamaliza. Sisi kama Taifa tuna hamu kubwa na kuona tukifanikisha Michezo inafanyika vyema hapa nchini kwa kuhusisha sekta zote kushiriki vyema.
Labda nikumbushe jambo moja baada ya Afrika kusini kutangazwa kama waandaaji wa fainali za kombe la dunia mwaka 2010. 

September 30, 2017

UTUNZI WA VITABU NA KISWAHILI CHA PROFESA SHAOPING

NA KIZITO MPANGALA

KESI YA ALMASI ni kitabu kilichoandikwa na Profesa Rao Shaoping wa China. Kitaaluma yeye ni mhandisi. Alijifunza Kiswahili nchini Tanzania kwa muda wa mwaka mmoja na ushee, mwalimu aliyemfundisha aliitwa Ali Omari Mzee.
Profesa Shaoping ndiye msimamizi wa kazi za TAZARA wakati inajengwa. Alikuwa akimtafsiria Mwalimu Nyerere mazungumzo aliyokuwa akijadiliana na wenzake. Pia alikuwa mkaliamani kwa Mh. Salim Ahmed Salim, Mh. Rashid Kawawa, Spika Adam Sapi kwa mazungumzo aliyokuwa akijadiliana na Wachina wenzake. Na mwaka 2013 Profesa Shaoping alikuja tena nchini Tanzania kumtembela Mzee Ali Hassan Mwinyi.

Profesa Shaoping anasema hivi "ninaipenda Tanzania. Ninawapenda watu wa Tanzania". Profesa Shaoping anayafahamu maeneo mengi nchini Tanzania ambayo amewahi kutembelea, maeneo hayo ni kama vile Kisuwa cha Saa Nane, Arusha, Ifakara, Iringa, Kimbwe, Kidatu, Mikumi, Makambako, Mbarali, Tunduma, Zanzibar, Moshi, Dodoma na kadhalika.

Profesa Shaoping ameandika kitabu hiki kwa bidii mno. Anasema tangu tuwe Koloni la Mjerumani na baadae Mwingereza, wageni hao hawakuwa na morali ya kutunga riwaya za Kiswahili lakini yeye kama mgeni alipenda sana kuacha kitabu kwa Kiswahili, naam, ndicho hiki hapa pichani.

September 29, 2017

UFUKWE WA BANDARI YA MBAMBA BAY


September 27, 2017

UHONDO WA KITABU

Wahenga wanasema kitabu ni sila. Mwanamke huyu alikutwa akisoma kitabu ndani ya Basi la Mwendokasi kati ya Mbezi-Posta kupitia barabara ya Morogoro jijini Dar es salaam. 
Usomaji wa vitabu huongeza maarifa.

Mwanamke huyu alikutwa akichagua kitabu cha kujisomea katika eneo la Mbezi jijini Dar es salaam.

Huyu alitafuta eneo zuri kwake linalomwezesha kusoma kitabu kwa utuvuli.

PICHA ZOTE NA KIZITO MPANGALA
 

September 21, 2017

UJENZI WA UKUTA MKOANI MANYARA

PICHANI:  Meja Jenerali Michael Isamuyo atua Mererani, Mkoani Manyara kukagua maeneo ambayo ukuta utajengwa kwa ajili ya ulinzi wa madini.


Wananchi wakiangalia Helikopta ya JWTZ iliyomleta meja jenerali Michael Isamuhyo kusimamia ujenzi ukuta wa eneo la vitalu A hadi D katika machimbo ya Tanzanite ,Mirerani.

PICHA KWA HISANI YA; Innocent Vitalis Inno

May 30, 2013

MANDHARI YA FUKWE ZA ZIWA NYASA KATIKA WILAYA YA NYASA

 
Ardhi yenye rutuba wilaya ya Nyasa

Beach ya BioCamp-kijiji cha Ndengere wilaya ya Nyasa

Kilimo cha Maksai katika kijiji cha Lundo wilaya ya Nyasa

Ufukwe wa Mbamba Bay upand wa kaskazini kuanzia bandarini

Ufukwe wa Mbamba Bay upande wa kaskazini kuanzia bandarini.

Zabibu Nyasa


PICHA ZOTE NA HOOPS KAMANGA, Mbamba Bay

October 27, 2012

NYUMBANI LUNDU

Picha hii inaonyesha maeneo ya kijiji cha Lundu. Maeneo hayo ni mtaa wa Maliwa au Missionari, na wka upande wa magharibi kushoto unaonekana mlima ambao unaitwa Chipyaghela. Kisha maji ya ziwa Nyasa yanaonekana. Huu ndio mji ulionikuza na kunilea, katika mitaa yangu ya Maliwa, au missionari.
Picha hii imepigwa na kaka Egbert Jeremy aliyeko wilaya ya Nyasa katika shughuli za ujenzi wa miundo mbinu. Lundu ni miongoni mwa vijiji ambavyo anaendelea kujenga miundombinu ya wilaya hiyo. Karibuni kuwekeza wilaya ya Nyasa ambayo imeanza kutoa fursa mbalimbali. KARIBUNI NYASA

October 17, 2012

HARAKATI ZA MAENDELEO WILAYA YA NYASA, KARIBU KUWEKEZA


Wilaya ya Nyasa ni miongoni mwa Wilaya mpya zilizoanzishwa na serikali ya awamu ya nne. Habari za kuundwa wilaya ya Nyasa nilianza kuzisikia mwaka 1993 nikiwa shule ya msingi. Lakini mwaka huu Wilaya ya Nyasa imezinduliwa rasmi na shughuli za maendeleo zinaendelea ili kukidhi mahitaji ya wananchi. Katika harakati hizo ni pamoja na huduma ya Maji ambayo ni muhimu sana kwa wananchi wa Wilaya hiyo. Hapa ni picha mbalimbali ambazo zinaonyesha suala la upatikanaji wa maji katika vijiji mbalimbali wilayani humu.  Bila shaka wageni na wenyeji watavutiwa kuwekeza katika wilaya mpya ambayo fursa mbalimbali zinajitokeza. karibuni. Picha zote na Hoops Kamanga
 Chanzo cha Mradi wa maji kikifanyiwa ukaguzi.
 Tenki la Maji katika mradi wa maji katika kijiji cha Ng'ombo wilaya ya Nyasa
 Mradi wa Maji katika kijiji cha Kindimba Juu ambao umekamilika na wananchi wanategemea kutumia siku chache zijazo. Hapo fundi anamalizia marekebisho katika tenki.

June 03, 2010

NIKUPE NINI??

Moja ya wasanii wa Mukirikiri, ila samahani nimeshindwa kutamka kwa ufasaha jina lao. Jamani ugonjwa wangu wa utamaduni ulinifanya nitulize 'boli' hapa kwa kujinufaisha na kujipendelea kutazama tu aina ya mvao wa kitamaduni.
Angalia na hapa chini kidogo iko vipi kadiri utazamazpo?
Mimi naona vizuri a.k.a African Bantu hadi nimemkumbuka Bambuu, yule mwanamuziki wa Kenya. Mwenye namba yake ya simu au anuani pepe naomba tafadhali..............Lol

April 09, 2010

HERI WAZAZI WANAOKULEA CAMILLA T.K!

CAMILLA T.K
Umekaa umetuliya,
kazi zako jifanyiya,
mafunzo shikiliya,
Camilla nakushangliya,
mwana kujifuniya
baba na mama fikiriya,
malezi kushikiliya,
mema kujivuniya,
makuzi yasikurabiya.

Heri baba alinaekulea na heri mama anayekulea

Camilla, bado kazi moja ya kulima maana sijui (?) kama umeshaanza. Ila usilalamike sana, ungekuwa kipindi hiki Bongo kuna kiubaridi ambacho kingekufanya uache kushinda ndani ya maji kama samaki...Lol..
Heri wazazi wanaokulea, heri kwao kukupatia malezi bora,kazi kujifunzia na mengineyo mema. Love you Baby Gal

May 15, 2009

"HAPPY BIRTHDAY MARKUS"


Hongera MARKUS HONORIUS MPANGALA, mwana wa nyasa umpendaye MALCOM X kila leo au JENERALI ULIMWENGU na JULIUS NYERERE, amani kwao watu hawa!
UPENDO UWE NANYI
Nashukuru baba na mama
Kwa kunileta hapa duniani
Nami najivunia kuishi ndani
Nashukuru sana wangu maanani
Kwani yupo nami kwa shida na raha
Kama machozi na majonzi naamini yanapita
Nashukuru ndugu waliopo hai
Na wale wasiohai, nawapenda kikweli
Upendo wangu, zaidi ya mshumaa
Nitawaangzia kwa uwezo wangu daima
Ningali nawajali, upendo usiopimika
Kwani ni tunu yake maulana
nawashukuru marafiki zangu nyote
Bila ninyi nikiri siyo mwenyewe
Najua imani yangu nimejaza kibaba
Naamini mola yupo nasi daima
Anajali,kutulinda na kutuhusudu
Ndiyo maana avumilia wetu utundu
Nawashukuru enyi wapenzi mlokuwa nami
Nawapenda kama amri ya mola
Kwani ni agizo la thamani daima
Nipo nanyi kwa mapenzi ya maulana
Nawashukuru maadui wote
Kwani mnanifanya niwe kama nilivyo
Bila ninyi sitokamilika, nawapa upendo
Mungu mkubwa.
Ni siku yangu ya kufurahia kuzaliwa kwangu, nashukuru wanablogu wote mliopo karibu nami. kwa pamoja tuseme waweke upanga au shoka au kufa ama kupona-mtaani tutabanana kwa pamoja tutafanikiwa kile kinachotakiwa kufanikiwa.
Na kwa yule mke/mchumba/mpenzi/demu n.k, ingawa nanua hujui kama wewqe ndiwe ninayekuhitaji. Labda hujui kama wewe ndiwe ninayependa uwqe demu/mchumba/mke wangu, lakini leo ujue ni siku yangu ya kuzaliwa.
Ingawa leo malaria yamenibana lakini nashukuru manesi ingawa wameshika matako yangu na kunidunga sindano. Najua kwa nia njema nitapona ndiyo maana ukichomwa sindano takoni unaambiwa poleeeeeee, ingawa nilisahau kumjambia ili nimwambia nami poleeeeee.
Najua kila mmoja anayozawadi yake lakini Koero Mkundi sijaona zawadi yako, unabifu na mimi au? Nashukuru Yasinta Ngonyani, zawadi yako nimeipenda sana1 daima tupo pamoja! OOOOhhh kwa wazee wangu nawaambia mjue mtoto wenu ni mwingi wa utani, mnivumilie ninaposema nesi amechezea TAKO langu. nadhani mnajua mambo ya kutaka uzima
LAKINI
atakayeweza anitunuku kitabu cha THE WORLD IS FLAT cha Thomas Friedman, nimtafuta hadi najamba. Mwenyewe ninacho mknoni JULIUS KAIZARI na CRYSTAL RAPTURE pia nakwenda duku la vitabu sasa kujinunulia zawadi. Bwaya, Kaluse,Kamala, na wengine naweka ..................................... ili ujaze jina lako kama nimesahau.
upendo daima, salama kwa mchumbangu usiyejijua kama ni wewe, naweka ........ andika jina lako

November 26, 2008

ndizi ndizi KAPOLOTA karibu sana

wale walaji wa ndizi KAPOLOTA karibuni. Dada Yasinta huko ughaibuni unazikumbuka hizi

October 31, 2008

tunaweza kutunza mazingira yetu siyo samaki tu