Na Kizito Mpangala
Wanawake wanayo nafasi ya kufikia malengo ambayo wanakusudia, ni kwa juhudi na maarifa wataweza kufikia malengo hayo. Suala la kipaumbele kwa wanawake duniani kote limepitia hatua kadhaa za ushawishi na changamoto kadhaa ambazo hasa huwakabili wanawake wenyewe. Katika uga wa sayansi na teknolojia, ni wanawake wachache ambao wamefikia malengo yao ugani humo. Hata sasa uhamasishaji bado unaendelea duniani kote.
Baada ya kuweka juhudi zaidi katika elimu hiyo ya sayansi, mwaka 1732 Laura aliandika kazi yake ya kwanza ambayo aliitetea mbele ya hadhira katika mihadhara mbalimbali katika ukumbi wa Pazzalo. Hiyo ilikuwa dira yake ya mafanikio ya elimu aliyokuwa akiitafuta zaidi.
Wanawake wanayo nafasi ya kufikia malengo ambayo wanakusudia, ni kwa juhudi na maarifa wataweza kufikia malengo hayo. Suala la kipaumbele kwa wanawake duniani kote limepitia hatua kadhaa za ushawishi na changamoto kadhaa ambazo hasa huwakabili wanawake wenyewe. Katika uga wa sayansi na teknolojia, ni wanawake wachache ambao wamefikia malengo yao ugani humo. Hata sasa uhamasishaji bado unaendelea duniani kote.
Haikuwa kazi rahisi kwa
mwanafizikia Laura Caterina Bassi kufikia kiwango cha profesa wa Fizikia katika
chuo kikuu cha Bologna nchini Italia.
Laura Bassi alizaliwa mwaka
1711 mjini Bologna nchini Italia ambapo baba yake alikuwa mwanasheria. Laura Bassi
alifundishwa nyumbani na mwalimu aliyeajiriwa na familia yake kwa muda wa miaka
saba. Alianza kufundishwa akiwa na umri wa miaka 13. Mwalimu wake, Gaetano
Tacconi, alimwelekeza zaidi katika sayansi na hisabati ndipo Laura alipoingiwa
na hamu ya kutaka kujua zaidi yaliyomo katika sayansi.
Kutokana na msukumo aliokuwa
nao katika sayansi, Laura alivutiwa zaidi na somo la Fizikia ambapo alijifunza
zaidi kuhusu Sayansi ya Newton (Newtonian Science) ingawa mwalimu wake alitarajia
kwamba Laura atajikita zaodi katika hisabati, lakini haikuwa hivyo.
Laura Bassi, katika juhudi zake
za masomo alilazimika kusoma pia hisabati ili kujiimarisha katika Fizikia. Hapa
Laura alimuomba binamu yake, Padre Lolenzo Stegani, amfundishe hisabati. Padre Lolenzo
Stegani alikuwa akijua hisabati na lugha ya kilatini. Kwa kuwa vitabu vingi
viliandikwa kwa lugha ya Kilatini, Laura alipaswa kujifunza sarufi ya lugha
hiyo na baadae akafundishwa hisabati kwa lugha ya Kilatini.Baada ya kuweka juhudi zaidi katika elimu hiyo ya sayansi, mwaka 1732 Laura aliandika kazi yake ya kwanza ambayo aliitetea mbele ya hadhira katika mihadhara mbalimbali katika ukumbi wa Pazzalo. Hiyo ilikuwa dira yake ya mafanikio ya elimu aliyokuwa akiitafuta zaidi.