Showing posts with label Uchumi. Show all posts
Showing posts with label Uchumi. Show all posts

March 07, 2018

JOSEPH BOIMANDA: MTAJI WA MILIONI HAMSINI SERIKALI HAWANA MUDA WA KUKUFUATILIA

NA.HONORIUS MPANGALA
MAISHA popote unaweza kusema hivyo kwani waliofikiria katika hoja hii walikuwa na sababu za msingi zilizokuwa na maana kiuhalisia. Wakati kipato ndio sababu hasa zilizopelekea kukawa na maneno kama haya ambayo yanasadifu uhalisia wa maisha. Katika mazungumzo yangu na mmoja ya watanzania waishio nchini Afrika kusini ilinifanya nistaajabu kile anachonieleza ambacho ndio uhalisisa wa maisha ya huko.

Ni rafiki yangu na ndugu yangu Joseph Boimanda alinifanya nistaajabu pale aliposema mtaji wa milioni hamsini za kitanzania ukiwa Afrika Kusini sio lolote kwa serikali ya huko. Maisha yamekuwa yenye uhuru na amani ya kutosha kwa raia.
Wakati nataka kuyajua haya ananieleza kuwa mamlaka ya mapato ya huko haina muda wa kufuatilia mfanyabiashara wa kati.Kama inatokea mtu anataka kulipa mapato serikalini basi ni hiari yake,hii ni kwa wale wafanyabiashara wadogo na wa kati amabao mtaji yao ni kitu kidigo kwa serikali yao. 

February 28, 2018

SERIKALI IMESIKIA KILIO CHA WENGI

NA GABRIEL MWANG’ONDA
HATIMAYE serikali imesikia kilio chetu kuhusu Single Customs Territory (SCT), wakati mfumo huu ukianzishwa na kutumika hapa kwetu Tanzania, binafsi nilipinga sana japo yalikuwa ni maazimio ya jumuiya za uchumi za Afrika Mashariki na SDC countries walikuwa ndio wanaanza kuipigia chapuo.
Mfumo huu unahusisha maafisa wa Forodha kutoka nchi jirani kuja kuweka kambi katika bandari yetu ili mtu akisema anaingiza bidhaa na zinaelekea DRC kisha aende kwenye deski la DRC lililopo hapahapa bandarini kwetu na kulipa kodi zote pale Bandari ya Dar es salaam. Kifupi ni kwamba sisi tulikuwa tunasaidia nchi jirani kudhibiti ukusanyaji kodi.
Mfumo huu ulilenga pamoja na mambo mengine kudhubiti wizi mkubwa wa bidhaa zinazokuwa zinanasinishwa kwamba ziko in transit wakati si kweli kwamba ni transit, mara nyingi huishia mikoa ya karibu na Dar es salaam na kurudi sokoni hapa nchini. 

February 26, 2018

WAMACHINGA WA KIZUNGU NDANI YA MJI WA MOROGORO

Nimewanasa mwenyeeeeewee kwa kamera yangu. Msamvu Morogoro,wanauzia bidhaa abiria Wa kwenye magari. Jana nilimnasa mmoja katika mgahawa uliopo maeneo Stand ya daladala ya mjini kati moro nami nikawa mmoja wa wateja wake. Wakati sisi tukiwashangaa wenzetu wanapiga hela wanaondoka. Vyuma vimepata grisi ya kizungu.
 PICHA; Honorius Mpangala

February 23, 2018

SEKTA BINAFSI KWA MAENDELEO YA UCHUMI WA AFRIKA YA MASHARIKI

AJENDA: Afrika ya Mashariki.
WENYEJI; Uganda
WAHUSIKA: Ndugu Rais Yoweri Museveni, ndugu Rais John Magufuli na ndugu Rais Uhuru Kenyatta
MADA: Sekta binafsi kwa maendeleo ya nchi za Afrika mashariki.
MAONI: Sekta binafsi ina lengo la kutafuta faida. Haitatokea kuwa utoaji wao wa huduma kuwa kigezo cha kutotafuta faida. Ni jukumu la serikali kusimamia kupata haki zake kutoka kwa wadau wa sekta binafsi kwa njia zinazofaa. Tukitaka kuilazimisha sekta binafsi isilenge faida tutarudi kwenye "Mashirika/viwanda vilivyobinafsishwa" enzi hizo na baadhi yao kuwa "ghala za popo".

--MARKUS MPANGALA

January 01, 2018

SALAM ZA MWAKA MPYA 2018; KOROSHO MTWARA

NA GABRIEL MWANG’ONDA
 
KAMA ilivyo kwenye korosho kule Mtwara, basi kwa wale wahenga wenzangu wa mji wa Tukuyu mtakuwa mnajua zile karanga za mitini kwa watu wa mjini na sehemu zinginezo wanaweza kudhani nadanganya, lakini la hasha ni kweli kuna karanga humea mitini na ni miti mikubwa kabisa, kwa kinyakyusa zinaitwa (Macadamia). Hizi zina vinasaba vya korosho kwa mbali, ni very delicious and healthy vilevile. 

Wakati bei ya korosho ikipanda mpaka kufikia elfu nne kwa kilo kule Nangwanda Sijaona kunako Mtwara, watani wetu wa jadi hapo Kenya wameamua kuachana na mashamba ya Chai na kukazania kilimo cha Karanga za mtini ambazo zimefikia kilo moja Tshs 21,000.00 nakuendelea. 


November 22, 2017

MAONI YA MHARIRI: ‘Nani atalinda samaki wa Ziwa Nyasa?


Naanza katika maliasili zetu. Sisi kama Tanzania tuna maliasili nyingi sana na watu wengi hawajui kabisa hilo na pia tuna wataalamu wangeweza kuwafumbua watu macho. Tukianza kwa kusafirisha nje ya nchi, Samaki hai wa maji baridi yaani Tanzania ndio ina samaki wa bei kubwa kuliko wote duniani. 

November 16, 2017

MV NJOMBE INAVYOFUNGUA FURSA KWA WAKAZI ZIWA NYASA.


Honorius Mpangala, 0628994409

NA. HONORIUS MPANGALA
AKIWA katika kampeni za urais mwaka 2005 Rais mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete katika ardhi ya Kyela Mkoani Mbeya alihaidi meli. Alirudia tena kauli hiyo alipokuwa katika ardhi ya Mbamba Bay Mkoani Ruvuma. Baada ya kipindi cha utawala wake hatimaye meli alizoahidi tayari zimeonwa na Wanyasa. 

MV Njombe imekamilika na kufanikiwa safari moja ya majaribio kutoka Bandari ya Itungi hadi Mbamba Bay.  Yapo mambo ambayo ni fursa kwa wakazi wa Nyasa kutokana Meli hii. Kama inavyoitwa ni meli ya mizigo ni chombo kitakachoweza kuwainua kiuchumi wakaza wa Nyasa kama watakitumika ipasavyo. Kuinuka kiuchumi kutatokana na kujikita katika shughuli ambazo wakazi wake watajishughulisha na shughuli kama ilivyo kilimo biashara na hata ufugaji wa kisasa na wenye tija katika maisha ya leo.
Kilimo cha biashara ni moja ya ujasiriamali ambao watu wengi wamekuwa wakijishughulisha nao. Katika mwambao wa Ziwa Nyasa hususani wilaya Nyasa yapo mabonde ambayo yanaweza kufanyika kilimo cha mazao ya muda mfupi na kwa mfumo wa kilimo cha umwagiliaji, na kile cha kutegema mvua na kuleta tija.


October 23, 2017

URUSI, CHINA KUTAWALA BIASHARA DUNIANI



 
MOSCOW, URUSI

MIKAKATI ya serikali ya Urusi kuifanya China kama mshirika thabiti na muhimu kiuchumi umechochea kukuza sekta ya biashara na kufikisha asilimia 22 katika mapato yake.

Gazeti la The Moscow Times limesema kuwa ushirikiana wa karibu baina ya Urusi na China umechangia kuimarisha mapato katika biashara na kufikia kiasi cha dola bilioni 80 mwaka huu huku matarajio yakiwa ni kufikiwa dola bilioni 200. 

October 16, 2017

“RAIS ANA MIAKA 31”


Sebastian Kurz
JUMAMOSI nilikuwa nasoma makala ya James Masters kwenye tovuti ya CNN. Sentesi yake ya kwanza ilinivutia sana, “Ulikuwa unafanya nini ulipokuwa na umri wa miaka 31? Ingawa aliendelea na mengine lakini staili pekee haikuwa kivutio bali mtu aliyekuwa akizungumzwa alivutia zaidi.
James Masters alikuwa anamzungumzia Sebastian Kurz ambaye amewahi kuwa waziri wa  Ushirikiano wa Kimataigfa tangu mwaka 2013 akiwa na miaka 27.  Sebastian  Kurz ambaye amekuwa Kansela wa Austria mwenye umri mdogo zaidi kwani sasa hivi ana miaka 31 tu. 

Ni mwenyekiti wa chama cha  OVP. Sebastian kuanzia jana jumapili aanaongoza serikali ya Austria ( kama vile Rais hapa kwetu) baada ya chama chake kushinda viti vingi vya bunge. 

September 27, 2017

MAKAZI DUNI

Hii sehemu mojawapo iliyopo jijini Dar es salaam. Ni eneo la makazi duni yaliyopo katika jiji hilo.

September 23, 2017

TANZANIA IS RAPIDLY CLOSING ITS ECONOMIC GAP WITH KENYA



BY GABRIEL MWANG’ONDA

Kenya’s status as East Africa’s economic powerhouse is at stake as Tanzania races closely behind, with a higher growth rate that is increasingly narrowing the gap between the two economies.
Tanzania has added impetus to its economic firepower, growing by an impressive seven per cent over the past five years compared to Kenya’s growth of just above five per cent.

The latest International Monetary Fund (IMF) data shows that Tanzania’s economy expanded seven times in the past 20 years while Kenya’s output grew five times since 1997 with the trend expected in coming years, weakening Nairobi’s future dominance. The same data shows that there were times in the past when Kenya’s economy would be as many as four times as large as that of Uganda.
However, such a big gap has not been reached in many years and is has remained mostly below three times.

September 16, 2017

WANAFUNGA SHUGHULI ZAO?



Sherehe ya kuwaaga wawejezaji huko mgodini.

September 30, 2014

WHY CAPITALISM CAN’T BE A SOLUTION FOR AFRICA



By Waheed Nsubuga, South Africa

To understand capitalism better first we have to look at its origin, nature and its connection with brutal history such as slavery...

Africans, Africa and its economical, cultural and social values are all based on the African concept of “UBUNTU”. This has been the fundamental challenge to Africans and for Africa to adapt and progress under capitalism since Ubuntu and capitalism do not have a harmonious match.

Apart from a very marvelous picture painted about capitalism; the ugly side of it hence; Selfishness, heartlessness, discrimination, murder, racism, apartheid, segregation and all other crimes against humanity need to be brought to the fore.

When we look at African values; it’s just opposite of all those! Our values are based on unity among families, villages and beyond…Not forgetting welcoming visitors in our homes and helping those in a need.

Having said all that, capitalism has been very successful in Europe and America due to the nature of the people there (the Europeans). It is not a secret that capitalism has molded white people into becoming heartless, selfish and self-centered. This has enabled them to accumulate capital from all over the world, leaving many in abject poverty and killing millions.

In Africa; it’s a shame if not a crime not to know your neighbor’s name while very normal with the Europeans.
In Africa; all the village elderly are regarded as parents to all the village children which is not the case with Europeans where the notion “everybody for himself/herself” reigns. This is also further emphasized by the fact that in Africa extended families are highly valued, whilst the west looks at family as husband, wife, sons and children.

In Africa; it’s against cultural values to get rid of your parents just because they’re old since parents must pass away in our hands no matter the conditions whilst in the west elderly have to be pushed somewhere far away from their own homes to old age homes something which to Africans may be looked at as “burial before their actual death”.

In Africa; you cannot let anyone to go hungry for the reason we’re all responsible for one another as sharing is in our blood, whilst the west again embraces the everybody for himself or herself !!!

Capitalistic elements have had a good hand in destroying the continent, creating confusion, wars, poverty and diseases.

History has it that the selfishness, heartlessness, self-centeredness nature of capitalism have led to oppression, racism, apartheid to all races more so those that have always been at the bottom of the ladder; “the non whites”.

Even today in the 21 century, living in any territory/country which is control by the majority Europeans has always made non-whites second class citizens. As longer as you don’t look European, you shall always remain a half citizen in countries such as; America, Canada, Australia and European countries. On the other hand Europeans living in African controlled territories have always enjoyed the African receptive nature deeply rooted in the Ubuntu African spirit.
 
One of the main tools of capitalism is centralized system of governance which gives the capitalists or neo colonialist’s easy access to resources, a system that contradicts the African way of life and governance. The centralized system empowers the leadership with the right to sell without consulting the masses as history has it regarding Africa and the Middle East. This has led to discontent and eventually rebellion in many places in Africa and beyond.
Unfortunately neocolonialists have now been favored with a new term which is used for those who stand and expose their exploitative system; the term is “terrorists”.

Decentralized governance system, a potential replacement for centralization, had been the model used by the Africans for centuries before colonization which suited their way of life, economical, beliefs, culture and other social values. This system gives trusted people/individuals from different communities, positions of responsibilities to work hand in hand with their communities along with the Government to ensure fair distribution of resources.

Unlike decentralization, centralization has even failed in the place where it had started that is United Kingdom as the Scottish vote recently revealed the need to grant more autonomy to the four members of the union.

Decentralization can thus be a solution to many war torn countries in Africa and the Middle East such as Nigeria, Congo, Libya, Southern Sudan, Central African republic, Kenya, Libya and Uganda to mention a few. The same system can be used against capitalism and neocolonialism helping to give more powers back to the local populations….


January 29, 2014

MBINGA ANGAVU SASA, UCHUMI KUNG'AA

Na Mwandishi Wetu, Mbinga

Huo ni mwonekano wa barabara itokayo Songea kuelea wilayani Mbinga kama inavyoonekana picha.Barabara hii kwa miaka mingi ilikuwa imetengenezwa kwa kiwango cha kawaida, lakini sasa imefikia kiwango cha Lami. 

Kutengenezwa bara hii ni ishara kuwa mabadiliko ya kiuchumi yanatarajiwa kutokea zaidi wilani Mbinga ikiwa ni sehemu ya mpango wa ujenzi wa barabara ya kutoka Songea hadi Mbamba Bay. 

Shughuli za uchumi hukua kutokana na ujenzi wa miundo mbinu kama barabara ambayo zamani ilisababisha mji wa Mbinga kuwa nyuma kimaendeleo na pia maendeleo yalikuwa yanakua polepol. 

Sasa tunaweza kusema Mbainga ni angavu na mwelekeo wake ni mpana zaidi kiuchumi, ikukumbukwa kuna viwanda vya KAHAWA ambavyo husaidia kuajiri watu mbalimbali na kukuza vipato vyao.

KARIBUNI SANA MBINGA
Picha kwa hisani ya Maggid Mjengwa/Mjengwablog, 2014. 

December 10, 2013

JE MAPATO YA DAR PORI YANADHIBITIWAJE NA HALMASHAURI YA WILAYA YA NYASA?



Na Vitus Matembo, Mbamba Bay
 
Leo kilio changu kipo katika kijiji cha Dar Pori au jina jingine Runyeli. Ambako ni maarufu sana kwa machimbo ya madini. Hali ya maisha huko ni ya juu sana ukilinganisha na maeneo mengne wilayani Nyasa. 

Maisha yapo juu ila huduma muhimu hakuna HOSPITALI, Usafiri  na Kituo cha POLISI. Kijiji kipo kilomita 8 kuingia Msumbiji, sasa wakazi wa Dar Pori wanalindwaje?


 Wakiumwa hupelekwa Zahanati ya Mpepo iliyopo kilomita 20 toka kijiji cha Dar Pori. Kijiji hicho kina takribani watu 6000 wengi kuliko hata wakazi wa Mbamba Bay na Liuli, ila watoto wanaokwenda shule ya msingi ni wachache sana, kwa mfano waliofanya mtihani wa darasa la 7 mwaka huu ni 11 tu.
 
Sambamba na hayo yote,hebu tujiulize WANYASA wenzangu mapato yanayopatikana katka machimbo ya kijiji cha Dar Pori yakwenda wapi?,
Mpaka sasa hakuna geti lolote la ukaguzi wa bidhaa na malighafi zinazoingia na kutoka katika eneo hilo? Pia wakazi wa maeneo ya Tingi, Kingerikiti na Dar Pori kila kitu hutegemea kutoka Mbinga na si wilaya ya Nyasa, Je tutapata chochote ?
Halmashauri yetu itafute namna ya kukusanya mapato yatokanayo na machimbo yaliyopo kijiji cha Dar Pori.
"PAMOJA TUIJENGE NYASA"

September 20, 2013

KARIBU UMEME WA GRID YA TAIFA NYASA



Na Vitus Matembo, Mbamba Bay

Leo Tanesco wameanza kutoa semina na elimu kuhusiana na uzinduzi wa umeme, matumizi, malipo na gharama za kujiunga. Pia wamealikwa wananchi wote wahudhurie bila kukosa. Ni semina endelevu kwa vijiji vyote wilayani Nyasa. Ila sasa wapo stand ya mjini Mbamba bay wakifanya mkutano.