Showing posts with label Kesi. Show all posts
Showing posts with label Kesi. Show all posts

December 09, 2017

SIKU YA UHURU DESEMBA 9: PAPII KOCHA NA NGUZA VIKING WAACHILIWA HURU.

NA MWANDISHI WETU, DODOMA
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli amewasamehe wafungwa zaidi ya 8000 na kuagiza wengine takribani 1000 waachiliwe huru leo. Hatua hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa sherehe za uhuru wa Tanganyika (Tanzania Bara) ambapo kila mwaka rais anatoa msamaha kwa wafungwa kulingana na taratibu zilizowekwa. 
 BONYEZA HAPA KUTAZAMA VIDEO YA WIMBO WA SEA
Miongoni mwa wafungwa ni wanamuziki mashuhuri, Nguza Viking au maarufu kwa jina la ‘Babu Seya’, na Johnson Nguza maarufu kwa jina la ‘Papii Kocha’ wameachiliwa huru kwa msamaha wa rais. Wanamuziki hao walikuwa wanatumikia kifungo cha maisha jela kutokana na kuhukumiwa kwa makosa ya kuwadhalilisha kijinsia watoto. Msamaha huo ni sehemu ya maadhimisho ya sherehe za uhuru wa Tanzania Bara iliyopata uhuru wake mnamo Desemba 9 mwaka 1961.

November 08, 2017

WAAMUZI WETU NA MITIHANI YA SIMBA NA YANGA



NA HONORIUS MPANGALA

TANZANIA ni miongoni mwa nchi zinazotajwa kuwa na amani na hii ni kutokana na muingiliano wa mambo manne.  Yako makundi yaliyojikita katika masuala ya dini, siasa, ushabiki wa soka na mwisho hali ya kuoleana.

Kupitia makundi hayo manne kunapelekea jamii ya watanzania kuishi pamoja. Makundi hayo hukutanisha watu tofauti kutokana na ufuasi wake. Haitakuwa ajabu unapomuona Waziri wa Mambo ya Ndani na kada wa CCM Mwigulu Nchemba akikaa jukwaa moja na kiongozi wa upinzani Freeman Mbowe na kuipa hamasa klabu wanayoipenda ya Yanga. Pia haitashangaza kwa kiongozi mkuu wa chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe kukaa pamoja na Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa na kuipa hamasa klabu yao pendwa ya Simba. Hayo yote hufanyika bila kujali itikadi za kisiasa walizonazo.

September 21, 2017

SERIKALI IMEKATA RUFAA KATIKA KESI ILIYOSHINDWA YA UMRI WA MTOTO WA KIKE KUOELEWA



DAR: Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kupitia ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imekata rufaa kesi iliyoshindwa mwaka Jana Baada ya Rebecca Gyumi Mkurugenzi wa Taasisi ya Msichana Initiative kufungua kesi ya Kupinga Ndoa za umri mdogo.

Sheria ya Ndoa ya Mwaka 1971 inaruhusu mtoto wa kike kuelewa akiwa na miaka 14. Rebecca Gyumi alifungua kesi hiyo Mwaka Jana kupiga sheria hii Kandamizi dhidi ya watoto wa kike walio chini ya umri wa miaka 18 kuolewa kwani wanakosa fursa ya kupata elimu

Mwaka jana Mahakama Kuu ilitoa amri Kwamba Serikali ipeleke mswaada Bungeni kuondoa sheria hiyo, Kinyume chake Serikali imefungua rufaa kupinga Uamuzi huo ikitaka sheria hiyo iendelee kuwepo ili watoto wenye umri chini ya miaka 18 waolewe kama wenye zaidi ya miaka 18

Ndimi,
Ndahani N. Mwenda