Showing posts with label familia. Show all posts
Showing posts with label familia. Show all posts

January 18, 2018

HAKUNA CHAMA KINACHOENDESHA MAISHA YA MPIGA KURA.

NA HONORIUS MPANGALA, BAHI
NILIPOKUWA mdogo niliamini maisha ni jambo ambalo liko tofauti na la kuogofya sana katika jamii. Sababu kubwa ni pale nilipokuwa nayasikia maneno kama “Usicheze na maisha”. Fikra zangu zilinipeleka kuwa maisha ni jitu linalotisha sana katika jamii.

Baada ya makuzi nikapata misemo kama “Maisha yenyewe ndiyo haya haya” nikaanza kutambua kumbe mwenendo wa kuanzia asubuhi unaamka hadi usiku unaingia kulala hizi harakati zote ufanyazo ndiyo maisha yenyewe.

Katika vipindi ambavyo wapiga kura na wananchi wa kawaida toka vyama vya siasa wanajiona kama na wao ni wenyechama basi ni katika kampeni za uchaguzi. Kipindi hiki kila mwanachama anajiita ni mwenyechama. Ni kipindi ambacho watu hao hudiriki kunukuu maneno ya wagombea wao na kuiaminisha hadhira aliyonayo kuwa chama chetu kitatekeleza mambo kadha wa kadha.

November 02, 2017

SOMO LA LEO

“Nitashangaa sana kama patakuwepo wanafunzi waliopo kwenye orodha ya kupata mikopo na wawe hawajapata, nitashangaa sama lwa sababu mimi najua nimeshaidhinisha fedha hizo na zimeshatoka,”
 
RAIS JOHN MAGUFULI

October 30, 2017

SEBASTIAN KURZ; Kiongozi mbichi anayeugusa ulimwengu



NA MWANDISHI WETU

“ULIKUWA unafanya nini ulipokuwa na umri wa miaka 31? Hiyo ni sentensi ya kwanza iliyoandikwa na Mwanahabari wa Televisheni ya CNN, James Masters, kwenye tovuti ya CNN. Sentensi hiyo ilinivutia zaidi, ingawa aliendelea na mengine, lakini staili pekee haikuwa kivutio, bali mtu aliyekuwa akizungumzwa alivutia zaidi. 

Mwandishi James Masters alikuwa anamzungumzia kijana mmoja aitwaye Sebastian Kurz kutoka Austria. Ni kijana ambaye anazidi kuvutia duniani kutokana na siasa zake ambazo kwa namna moja au nyingine ziliibua nchi hiyo kwenye ramani ya kidiplomasia. 

Baada ya hapo nililazimika kufuatilia habari zaidi za Sebastian Kurz. Niliyokutana nayo ni somo, ingawa kwa Tanzania lilianza muda mrefu.
Nimekuandalia makala haya msomaji ili kujifunza jambo katika malezi ya familia na taifa kwa ujumla. Austria ipo tayari kwa kiongozi kijana? Fuatilia.

Sebastian Kurz ni nani?

October 11, 2017

MTAHINI ANAPOKUWA MTAHINIWA.

NA KIZITO MPANGALA
Nchini Nigeria zaidi ya walimu 20,000 kufutwa kazi kutokana na "hat trick" iliyofanywa na serikali ya nchi hiyo kwa kuwatahini walimu mitihani ile ile ambayo huwa wanawatungia wanafunzi wao.


 Walimu zaidi 20,000 wamafeli mtihani huo hali ilinayofikirisha wengi kuwa inakuwaje mtahini ashindwe utahiniwa? Hivyo, uamuzi wa serikali ya Nigeria ni kiwafuta kazi wale wote ambao wamefeli mtihani huo.

Hilo linanikumbusha mwaka 2011 ambapo mwalimu mmoja wa Seminari ya Likonde nchini Tanzania alitoa simulizi fupi kuhusu mchakato na manyanyaso waliyokuwa wakipata msimu wa kusahihisha mitihani ya kitaifa ambao ulikuwa ukifanyika jijini Dar es Salaam. 

Viongozi wa wizara ya Elimu pamoja na wale wa baraza la mitihani wakati huo walikuwa wakiwataka walimu wanaokuja lusahihisha mitihani hiyo watahiniwe kwanza ndipo wajue nani anafaa kusahihisha. 

Walimu wote kwa ujumla walitoa pendekezo kwamba wao waanzr kuwatahini viongozi wote wa wizara ya elimu na baraza la mitihani mtihani uleule uliofanywa na wanafunzi wao ndipo wajue kama wanafaa kusimamia Elimu nchino. Hapa hapakitosha kabisa! Hakuna aliyetaka kuaibika!

Hivyo basi, Nigeria wameua lufanya hivyo na wamewanasa waliowataka. Taifa la Nigeria lina watu wengi sana barani Afrika hivyo utoaji Elimu una changamoto kubwa. Hali hii imeilazimu serikali kuruhusu shule nyingi binafsi kianzishwa kwa ada elekezi.

RAI:
Lengo siyo kuwaaibisha walimu, lengo ni kujua nani ni nani katika nini. Hilo siyo mbafala wa vyeti feki. Hivyo, ingawa kuna maswali Mengi ya kuuliza kuhusu jambo hilo, ni vema walimu wawe na utamaduni wa kuperuzi vitabi mbalimbali kulingana na somo husika analofundisha ili kujiimarisha katika ufahamu na kuweza kiwapa wanafunzi kinachostahili. 

Pia serikali iongeze ubora vitabu na kuchapisha vingi na ikibidi hata vitabu vya ziada viruhusiwe kwa kuwa vipo vingo vizuri na bora. Na jambo la mwisho ni kuwajali walimu. Si tu yule anayeitwa profesa ndiye anastahili kujaliwa, bali yeyote aliye mwalimu anastahili hilo. Na walimu wenyewe wajielewe kuwa wao ni walimu.

©Kizito Mpangala

August 24, 2014

UZURI WA FUKWE ZA NYASA

Mnaysa mwenzetu kaka Jerome Maendaenda, kila mwaka huiepeleka familia yake nyumbani Nyasa kutoka Dar es salaam. Hapa wakiwa wanafurahia maji ya ziwa Nyasa katika ufukwe wa Mbamba Bay.
KARIBUNI NYASA

December 22, 2013

UHABA WA SAMAKI



Mwandishi wetu Vitus Matembo amezoea kula samaki huko Nyasa, lakini kwa sasa analalamika kuwa kuna uhaba wa Samaki. Katika hali ya kawaida miezi ya Septemba, Oktoba mpaka Novemba kunakuwa na uhaba wa samaki wa aina fulani. Kwa wanyasa kuna samaki wanawapenda sana, lakini wanapotoweka basi inakuwa tatizo. 

Hivyo kwa sasa samaki wanaopatikana zaidi ni maarufu kama MCHUKWA, lakini samaki aina ya Kambale upatikanaji wake ni mgumu kipindi hiki labda kuanzia januari. Na kwakuwa wanyasa wamezoea kula samaki wanono basi tusmishangae ndugu yetu Matmebo akilalamikia kukosekana kwa samaki anaowapenda.
Ndiyo Nyasa yetu, raha na changamoto.
Kwa sasa ununuzi wa Kambale unaweza kuuziwa kipande badala ya kambale mzima. Hapo ni kipande cha Kambale akiwa tayari kwa kuuzwa. KARIBUNI NYASA


December 27, 2012

MIKONO NA MOYO WA NATHAN MPANGALA KUWAFANYA WATOTO WENYE SARATANI KUTABASAMU

Nathan Mpangala akiwa anawafundisha watoto kuchora michoro mbalimbali. 
Nathan Mpangala ni miongoni mwa watanzania wanaogusa mioyo ya watu kutokana na kazi zao za sanaa. Wengi wanakumbuka michoro ya katuni za Kijastibikozi na mingine mingi sana. 
Yeye ndiye mwasisi wa michoro ya katuni za Daladala ambazo huchapishw ana gazeti la MAJIRA hapa nchini. Tasnia ya uchoraji imemfikisha katika nchi mbalimbali kuhudhuria mihadhara ya kuelimisha jamii akiwa miongoni mwa waandishi wa habari wanaotumia vipaji vyao kufikisha ujumbe kwa njia ya sanaa za michoro. Moja ya kazi zake kubwa zinazoonekana kote nchini kupitia Televisheni ya ITV ni kibonzo cha MTU KWAO. 
Kibonzo hivyo hubeba ujumbe mbalimbali wenye nia ya kuelimisha na kuburudisha jamii. Kutokana na kipaji chake, Nathan Mpangala anarudisha faida anayopata kwa kazi hiyo kwenda kwa jamii. 
Amekuwa akifanya hivyo kupitia programu ya WAFANYE WATABASAMU akiwa na lengo la kuwaliwaza watoto wote wanaougua saratani nchini. Juhudi hizo ni kutokana na mapenzi yake kwa jamii na nchi kwa ujumla. Kama anavyoonekana pichani akiwa na watoto hao, pamoja na mchoro mwingine upande wa kulia unavyoonyesha watu wasiofikiria jamii yao. 
Hakika Mikono na moyo wa NATHAN MPANGALA umekuwa faraja kwa wazazi wa watoto na watoto hao kwa ujumla. Nawe waweza kuchangia juhudi zake kwa kuungana naye katika WAFANYE WATABASAMU.


Anaelezea zaidi safari yake .............
UCHORAJI UMEPAMBA MOTO. Baadhi ya watoto wanaendelea na matibabu ya saratani katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, jijini Dar es Salaam, wakijimwayamwaya wakati wakichora. Kupitia Program ya Wafanye Watabasamu, nilitembelea watoto hao kuwapa zawadi kisha kuchora nao. 
Katika ziara hiyo niliyoambatana na baadhi ya wachoraji katuni na marafiki wa Wafanye Watabasamu tuliwazawadia watoto zawadi kisha kuchora nao. Kwa niaba ya watoto, nawashukuru ndugu na marafiki wa Programu ya Wafanye Watabasabu kwa zawadi mbalimbali walizochangia ambazo zimefanya ziara hiyo kuwa ya mafanikio. Pia nawashukuru sana marafiki na wachoraji wote waliojitokeza na kuungana nami Muhimbili. Picha na michoro mbalimbali iliyochorwa na watoto hayo iko njiani.

November 14, 2012

SHULE ZA AWALI NYASA ZINAKABILIWA NA CHANGAMOTO LUKUKI


Na Albano Midelo, Nyasa
SERIKALI kupitia wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi iliamua kuanzisha mfumo wa elimu ya awali katika shule za msingi kwa lengo la kuwaandaa watoto wenye umri kuanzia miaka mitano.
Wizara ya elimu imedhamiria kuhakikisha kuwa watoto wenye umri wa miaka mitano hadi sita wanasoma darasa la awali kabla ya kuanza kuingia shule ya msingi wanapokuwa na umri wa miaka saba.
Uchunguzi uliofanywa katika kata za Kihagara na Liuli umebaini kuwa madarasa ya awali katika shule hizo yanakabiliwa na changamoto mbalimbali hali ambayo inaathiri utoaji wa elimu hiyo muhimu kabla ya kuanzia shule za msingi.

Wanafunzi wa Darasa la Awali wapatao 90 katika Shule ya Msingi PUULU, Kata ya LIULI, wilayani Nyasa wakiwa katika darasa ambalo halina dawati hata moja.

Mwalimu wa taaluma katika shule ya msingi Ndonga kata ya Kihagara Amos Kilongo anasema shule hiyo ina darasa la awali lenye wanafunzi 37 ambao wanasomea kwenye mti kutokana na kukosekana kwa chumba cha darasa na kwamba mwalimu anayefundisha katika darasa hilo ni aliyemaliza kidato cha nne.
“Wanafunzi wa darasa la awali hawana darasa wanasomea chini ya mti,pia darasa halina madawati wa awali wanakaa  wakati wa mvua wanafunzi hao wanasome katika kanisa katoliki ambalo tumewaomba wamiliki wa kanisa hilo wamekubali kutusaidia’’,alisisitiza.
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Kihagara Anet Ngindo anasema shule hiyo ina darasa la awali lenye wanafunzi 52 ambao wanasomea chumba cha shule ya msingi wakifundishwa na mwalimu ambaye hajapata mafunzo ya ualimu na sio mwajiriwa analipwa posho kupitia michango inayochangwa na wazazi.
Mwalimu mkuu katika shule ya msingi Tumbi  Evaristo Ndiwu anasema katika shule yake kuna darasa la awali lenye watoto 45 ambalo halina chumba cha kusomea ambapo mwalimu wake hana taaluma ya ualimu ni mhitimu wa kidato cha nne analipwa posho kutokana na michango ya wazazi na walezi.
Katika shule ya msingi Mango,mkuu wa shule hiyo anasema katika shule yake kuna darasa ka awali lenye wanafunzi 60 ambao hawana chumba cha kusomea na  wanafundishwa na mwalimu ambaye hajapata mafunzo ya ualimu sio mwajiriwa badala yake analipwa posho na wazazi kati ya shilingi 30,000 hadi 50,000 kwa mwezi.
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Ngehe Silivanus Mbeya anasema katika shule yake kuna darasa la awali lenye watoto 36 ambalo halina chumba cha kusomea na linafundishwa na mwalimu ambaye amehitimu kidato cha nne hana mafunzo ya ualimu analipwa posho na wazazi ambayo haikidhi mahitaji ya mwalimu huyo.

Uvuvi ni shughuli inayoongeza kipato na ukuaji wa uchumi kwa wakazi wa wilaya ya nyasa. hapa wavuvi wakiwa kazini.

Katika shule ya msingi Puulu  mwalimu mkuu wa shule hiyo Cathibert Maluka anasema katika shule yake kuna darasa la awali lenye wanafunzi 90 na kwamba wanafunzi hao wanakabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwemo na ukosefu wa madawati ambapo wanafunzi wote wanasoma kwa kukaa chini.
“Darasa la awali katika shule yetu limebahatika kuwa na walimu wawili ambao wamepata mafunzo rasmi ya kufundisha wanafunzi wa darasa la awali hali ambayo inawawezesha kutoa elimu ya awali kulingana na malengo ya wizara ya elimu licha ya wanafunzi kusomea chini’’,alisema .
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Nkali Erasmus Haule  anasema shule hiyo yenye jumla ya wanafunzi 210 ina darasa la awali lenye wanafunzi 45 ambao hawana darasa badala yake wanasomea kwenye banda ambalo jioni linatumika kama klabu cha pombe na kwamba mwalimu anayefundisha hajasomea.
Katika shule ya msingi Hongi  kwa mujibu wa mwalimu mkuu Simon Ndunguru shule hiyo ina darasa la awali lenye wanafunzi 52 changamoto kubwa hakuna chumba maalum cha kusomea na kwamba mwalimu anayefundisha sio mwajiriwa na wala hajasomea kufundisha darasa la awali.
Katika shule ya msingi Mwongozo yenye wanafunzi 654 inakabiliwa na changamoto ya ubovu wa darasa la awali lenye watoto 81 halina sakafu lina mwalimu mmoja ambaye hana mafunzo ya ualimu ,hajaajiriwa analipwa posho na wazazi wenye watoto hao
Baadhi ya wadau wa elimu katika kata za Kihagara na Liuli ambao ni Neema Msumba,John Ndunguru,Joel Makelele,Melikion Mapunda na Victor Komba wametoa wito kwa serikali kuhakikisha kuwa kila shule ya msingi inajenga darasa rasmi kwa ajili ya elimu ya awali badala ya shule nyingi kutumia vyumba vya shule ya msingi.
Wameitaka wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi kuhakikisha kuwa kila darasa la awali inapeleka walimu waliopata mafunzo rasmi ya namna ya kufundisha watoto wa awali badala ya tabia ambayo inafanywa na shule nyingi kuwatumia vijana ambao wamehitimu kidato cha nne huku wakiwa hawajapata elimu ya ualimu.
Mratibu elimu kata ya Liuli Abrahamu Challe amesema kata yake imejipanga kuhakikisha kuwa changamoto zote zinazoikabili elimu ya awali katika kata yake yenye shule saba zinatafutiwa ufumbuzi haraka ikiwemo kuwa na chumba rasmi kwa ajili ya awali,walimu na madawati.
Challe ametoa wito kwa serikali kutumia mfumo wa uboreshaji wa elimu ya awali kama ilivyokuwa kwa uboreshaji wa elimu ya msingi na sekondari kwa kujenga  vyumba viwili vya madarasa kwa kila shule na kusisitiza kuwa vifaa vyote vya ujenzi vitolewe na serikali na wananchi waachie ujenzi.
Afisa elimu msingi katika Halmashauri ya wilaya ya Mbinga David Mkali ambaye anahusika na wilaya ya Nyasa anasema elimu ya awali ni sera ya wizara ya elimu kuhakikisha kila shule ya msingi inakuwa na darasa la awali kwa lengo la kuinua elimu hapa nchini.
Ameahidi kushirikiana na viongozi mbalimbali wakiwemo madiwani,watendaji wa vitongoji,vijiji,kata,tarafa pamoja na wenyeviti wa vijiji kuhakikisha wanahamasisha wananchi katika maeneo yao kusimamia ujenzi wa madarasa ya awali na kutengeneza madawati ili watoto hao waweze kusoma katika mazingira bora.
“Ni ukweli madarasa ya awali yaliyo mengi yanafundishwa na walimu wasiopata elimu ni kutokana na uhaba mkubwa wa walimu uliopo katika shule nyingi nchini,lengo ni kuhakikisha tunapata walimu wa kutosha ikibidi hata kuwatumia walimu wanaostaafu kufundisha katika madarasa ya awali’’.alisisitiza.

Unaweza kuwasiliana na mwnadishi kwa anuani ifuatayo: albano.midelo@gmail.com,simu 0766463129

UHARIBIFU WA MAZINGIRA KIJIJI CHA NDUMBI??

 Zipo taarifa kwamba kampuni ya uchimbaji ya makaa ya mawe, TANCOOL katika kijiji cha NDUMBI kilichopo wilaya ya Nyasa imesababisha uharibu wa mazingira ndani ya kijiji hicho. Taarifa hizi zimeifikia mtandao huu wa KARIBUNI NYASA kupitia kwa mdau wetu Egbert Jeremy, ambaye yupo kwenye wilaya hiyo katika shughuli za utengenezaji wa Barabara na mradi mkubwa wa mami safi na salama wilayani humo. 
Kutokana na suala hili, mtandao huu unafuatilia kwa karibu taarifa za kampuni ya TANCOOL ili kubaini ukweli, na ikiwezekana kuishauri njia na umuhimu wa kulinda mazingira mbali ya mradi wao wa uwekezaji. Tuna imani wataelewa na watasaidia ulindwaji wa mazingira ya kijiji cha NDUMBI ambacho kama kitaharibiwa bila shaka yoyote kinaweza kuwa Jangwa kutokana na hali yake ya hewa kukosa uoto wa asili.

November 01, 2012

AYUBU RIOBA ALIPOTOA NONDO ZA NGUVU CHUO KIKUU CHA TAMPERE, FINLAND

AYUBU RIOBA akiwa katika Chuo Kikuu cha Tampere, jijini Tampere nchini Finland, ambako anapata Shahada ya Udaktari wa Falsafa(Phd) katika Sayansi ya jamii.
Kabla ya kufanikiwa kutunikiwa shahada hiyo, alitumia muda wake zaidi saa mbili(masaa mawili) kutetea utafiti wake juu ya "Media Accountability in Tanzania's Multiparty Democracy: Does Self Regulation Work"?
Baada ya mjadala mzito wa kitaaluma na maswali mengi kutoka kwa Profesa Audrey Gadzekpo kutoka Chuo Kikuu cha Accra, Ghana, pamoja na jopo la Maprofesa walifikia hitimisho na kumtunukia Shahda ya Falsafa ya uDAKTARI(Phd) katika fani ya Sayansi ya Jamii. Bila shaka ni jambo la kujivunia kwa watanzania na kwake AYUBU RIOBA. Mwenyzi Mungu ampe afya njema na kumlinda.

October 27, 2012

NYUMBANI LUNDU

Picha hii inaonyesha maeneo ya kijiji cha Lundu. Maeneo hayo ni mtaa wa Maliwa au Missionari, na wka upande wa magharibi kushoto unaonekana mlima ambao unaitwa Chipyaghela. Kisha maji ya ziwa Nyasa yanaonekana. Huu ndio mji ulionikuza na kunilea, katika mitaa yangu ya Maliwa, au missionari.
Picha hii imepigwa na kaka Egbert Jeremy aliyeko wilaya ya Nyasa katika shughuli za ujenzi wa miundo mbinu. Lundu ni miongoni mwa vijiji ambavyo anaendelea kujenga miundombinu ya wilaya hiyo. Karibuni kuwekeza wilaya ya Nyasa ambayo imeanza kutoa fursa mbalimbali. KARIBUNI NYASA

October 22, 2012

KILIMO CHA KISASA CHA MPUNGA LWIKA KATIKA VIKUNDI VYA WAKULIMA

Bonde la mto Lwika lipo katika kijiji cha Lundo na linatengenisha vijji viwili, Lundo na Ngindo. Bonde la mto Lwika linafaa sana kwa kilimo cha Mpunga na Miwa. Katika kuboresha maisha ya wananchi kilimo cha miwa kimekuwa na nafasi kubwa kama ilivyo kwa kilimo cha Mpunga. kwa sasa wakulima wanaweza kutumia zana za kisasa ikiwemo Matreka. Pichani Trekta la Kikundi cha Umwagiliaji cha LWIKA. Treka hilo limenunuliwa kupitia Mpngo wa Uendelezaji wa Sekta ya Kilimo katika Wilaya ya Nyasa(DADPS). Kilimo ni uti wa mgongo kwa wakazi wengi wa Wilaya ya Nyasa ikiwemo Mahindi, Mtama, Ulezi, uvuvi na mengineyo. Kikundi cha wakulima wa eneo hilo kimepewa ekari 2200. 

Picha ya Hoops Kamanga idara ya maendeleo Wilaya ya Nyasa.

Huyu ni mzee Mputa, ambaye alikuwa afisa Uvuvi, kwa sasa ameshastaafu. Hapo alikuwa katika ukaguzi wa kilimo cha Mpunga katika bonde la mto Lwika.


April 30, 2010

NI MAISHA YAKO??

                                                               NIPO NAWAZA SANA
Kwanini ni maisha yako? Je marafiki zako hawana maisha yao? Kama ni Maisha yako, marafiki wa nini? Kwanini uwahitaji watu wengine endapo una maisha yako?

Kweli! Wewe ni wewe na hakuna anayefanana na wewe. Sasa kwanini useme ni maisha yako?

Ni maisha yako? Mume/mke wa nini kama unayo maisha yako? Jirani wa nini kama unayo maisha yako?
KUMBE ni maisha yako? Wengine je hawana maisha yao?

April 17, 2010

SIRI

HIVI KUNA SIRI YA WATU WAWILI? KWANINI?

January 28, 2010

PENDO BANDIA!


Niambie, Pendo Bandia,
Wapi Linapoanzia,
Moyoni au Kichwani?
Huzaliwa Jinsi Gani?
Hulelewa Jinsi Gani?
Nijibu Hima Nijibu!
Nalisubiri Jawabu,
Macho Ndivyo Hulizala
Na Chakula ni Kulola
Na Hufia Pendo Hilo
Pa Pale Penye Malalo
Sote Tupige Malalo
Kwa Kifo Cha Pendo Lile
Ninaanza, Ngoo Ngooo
Ngooo, Ngooo, Ngooo!

KIBWAGIZO
Nahitaji Mwanamke Halisi!
Ni Mwanamke Makini
Sitaki Mwanamke Feki
Nahitaji Mwanamke mimi
Atumie Muda kunifahamu mimi
Sihitaji Mwanamke wa Mahotelini
Ndiyo tiba ya kunipenda mimi.

MAWAZO YA PENDO LILE!
Ulizaliwa Peke Yako,
Kutoka kwa mama yako,
Ni wazi uko peke yako,
Unapaswa kuangalia yako,
Namna gani utaishi kivyako,
Hata kama uko Peke yako
Yote yanawezekana

Iwaze amani
tafakari furaha ni nini?

November 11, 2009

VITUKO VYA WANYASA NA SANAMU LA ASKARI DAR ES SALAAM


Nakumbuka nikiwa mdogo, simulizi za snamu la skari huyu zilinitihs akuona mji huu siyo wa kuishi. Nakumbuka waliowahi kufika huko Dar es alaam wakisifia na kutisha kuhusu mji wenyewe. Nakumbuka wengine waliwahi kusimulia kuwa hapo zamani kulikuwa na mzee fulani MNYASA aliwahi kukaa hapo kwa kuombeleza asamehewe makosa yake kwani hakujua kama anavunja kanuni za mji.
Na kosa lenyewe lilikuwa kushangaa ghorofa zilizojipanga katikati ya mji tangu alipokuwa akiishi Upanga. Na kwakua alikuwa mgeni basi aliamua kujipa jukumu la kuyajua mazingira kwakuwa alizowea mji kiasi chake. Basi akaijikuta maefika katika sanamu la askari huyu, mzee wa watu akapiga magoti kuomba msamaha sana kwa makosa ya kushangaa majumba makubwa watu wanaishi angani kama FIDEGE tena wale mbayuwayu...nawapenda sana hawa ndege.
Mzee huyo inasemekana alilia kwa nguvu zote kwa kudhani atasamehewa kosa la kushangaa majumba makubwa, yenye watu wasiotosheleza ubongo hadi wakawa walarushwa wakubwa na kuita TAKRIMA. Basi mzee huyo akaangua kilio hapo lakini hakuna aliyejali sana kuhusu hilo kwani alidhaniwa kua ni kichaa tu.
Lakini kama ujuavyo wabongo kwa kunusanusa udaku wakamsogelea mzee wa kinyasa na kumhoji inakuwaje anaongea na sanamu kwani amekuwa kichaa? Lakini mzee akasisitiza kuwa askari yule amemweleza atamdhuru kwanini ameshangaa maghorofa wakati anajua yanalipiwa? watu wakacheka inasadikika hivyo, wakamweleza huyo askari ni samanu tu hivyo kumtaka arejee nyumbani, ndipo mzee alikubalina lakini kwa sharti la kusindikizwa.
Alipotoa rai hiyo basi waungwana wakafanya hivyo hadi mtaa wa Undali na akaonyesha anapoishi kisha wenyeji wakajitokeza. Ndipo ikaulizwa kulikoni? Mzee akasimulia kisa na kudai jamaa wamemwokoa.... hee wenyeji wakaangua kicheko ikawa usiku ikawa mchana ......simulizi zimeendelea vizazi hadi vizazi vya mzee wa Lundunyasa alisimuliwa.....na hapo kale alikuwa akikataa kuja mji huu sababu hiyo ingawaje baadaye alikubali tu shauri ya elimu siyo sababu ya askari sanamu. Na akitimiza agano mzee wa Lundunyasa lazima arejee agano lake la nyasa. Vituko vya wanyasa na sanamu hilo jamani nilikuweo enzi hizo wakitusimulia yatokanayo

March 02, 2009

Nakumbuka Mengi sana

Nayakumbuka mengi niliyoyaona na kuishi. Nakumbuka enzi zile kuvaa kandambili tu bonge la utajiri. Nakumbuka mbali kwa kweli, nakumbuka bibi akiwa mfinyanga vyungu. Nakumbuka kwakuwa wazazi wangu walikuwa na ahueni ya maisha basi hali hii niliepuka kidogo sana. Na kwakuwa kila jambo lifanyikalo lilionekana basi kila mtu anajua kwanini nina uchungu pia na msimamo mkali. Weka mapenzi kando, nipe hoja msingi! Ni wangapi mtanipenda nikiwa sina SHILINGI?????

Nikumbuka sana maisha yale, kuvaa viatu tu tulichukiwa eti watoto wa matajiri, lakini nikiangalia hali nyumbani eti kwakuwa nilikuwa na viti vizuri kama vya ofisini. Nakumbuka niliwahi kupigwa kwa kuitwa :najivuna" kwa hali yetu nyumbani, lakini nakumbuka tulikuwa tunakunywa chai isiyo na sukari tena kwa mihogo jamani.
Nikikumbuka muundo ule ndiyo maana wazazi wangu walipiga sana kelele hoja yangu ya kutaka kucheza soka tu bila kusoma shule. Nakumbuka baba yangu anaposema 'huna kitu hapa nyumbani, tafuteni vyenu kwani hivi ni vyangu na mke wangu"

Nakumbuka sana, yaani unaona wengi wanakuchukia sababu wewe kwenu kuna wageni wanakuja toka mbali, au kwavile ndugu zako wanasoma mahali. Jamani, mazingira yangu yananikumbusha na kunitoa machozi, yananifanya nione hakuna ninayeweza kumwamini kama siyo mimi ingawa wakati mwingine simwamini hata mimi mwenyewe..
Lakini leo najua wapi nilipotoka, wapi nilipoanzia na wapi niliposimama kabla ya kutembea na vidole katika blogu tena kabla ya kugeuka mtundu wa teknolojia niliyojifunza kupitia maandishi kama hadithi ya sungura na fisi. Nisije nikalia zaidi, najua wenzangu hawa wanaweza wakasema mbona umepata nafuu, tuokoe na nasi. NAWAPENDA SANA, SIJAIONA KESHO!!!!

February 18, 2009

Jibu la Kitendawili, na pole kwa Yasinta

Wanazuoni, wapo hoi,wameomba jawabu limekuwa thawabu,hawanalo,wanataka ahueni lakini tuweke tu AFANALEKI ili tupaje jibu lake.
Pengine hongera SARA kwa kujaribu kuwa MANII ni jibu lako, lakini nilikupamaswali kadhaa ambayo unaweza kunipatia jibu la kitendawili changu. Jamani eeeeh hivi kweli mmeshindwa au mnanitega?
JIBU; nimehangaika na kitendawili hiki tangu mwishoni mwa mwezi Novemba mwaka 2008, nilipewa,nikashindwa kisha nikajua hakuna shemu ya kusemea tena kama Blogu zetu maana kuna kila wajuzi wa mambo mbalimbali yatuhusuyo kila leo. LAKINI binafsi sina JAWABU ndiyo maana niliweka hapa ili tusaidiane, na kwahakika mwenye jibu atusaidie.

Kuhusu Yasinta, pole sana rafiki yangu, najua ni mabadiliko ya mazingira ndiyo maana imekuwa hivyo. Ninakuombea zaidi kwani nimevumilia kutoandika hapa, lakini naona lazima wanablogu wenzetu wajue kuwa unaumwa, toka uje bongo ni homa na afya kidogo kuzorota. Lakini naamini unaweza kubadilika, unaweza kurejea katika uhalisia wako.

Tupo pamoja,tunakuombea mema,tunangojea Tanzaniaresan irejee hewani kwa moto na makusanyo ya uhakika. Ni mungu pekee anayeuongoza kwa imani lakini miongozo tunayo mikononi mwetu. Ugua Pole Yasinta utarudi kama kawaida na kuwakilisha maofisini mpaka kwenye mageto, afrika na ughaibuni. Na wenye nia tunakuombea
Mnyasa.

February 11, 2009

Shindano! KITENDAWILI........

KITENDAWILI........................................., "Ni CHEUPE kama barafu na ni CHEUSI kama giza, KULIWA ni HARAMU na kunywa ni HALALI, kina herufi 5 na kinaanza na herfi M.
Kinatumiwa na WANAWAKE mara moja katika UMRI wao, na kinatumiwa na WANAUME mara tatu kwa siku.
Je, ni kitu gani hicho? Ukipata jawabu lake.

NB: ZAWADI NONO kwa mshindi

January 19, 2009

naona upo karibu yangu

upo karibu au mbali, umewahi kufanya haya tufanyayo? Si mengine ni kuvua tu samaki na kuoposha vindongo hapa nyasa. Karibu nyasa, uwe nasi daima, unatuonaje sasa