Showing posts with label Teknolojia. Show all posts
Showing posts with label Teknolojia. Show all posts
October 21, 2017
TABASAMU NA KITABU
Madhumuni
afya,
amani na upendo,
malezi,
mawazoni,
Nyasa,
Teknolojia,
urafiki,
utalii,
utamaduni,
uzuri,
vicheko,
Vitabu,
wageni,
wazo
October 16, 2017
CHUO CHAANZISHA SHAHADA YA WADUDU
NAIROBI, KENYA
KITUO cha Elimu na Utafiti kinachofadhiliwa na Benki ya Dunia kimeasisiwa katika Chuo Kikuu cha
Sayansi na Teknolojia cha Jaramogo Oginga Odinga na kinasubiri ruhusa ya
kuanzishwa kwa programu za Uzamifu na Uzamili kuhusu wadudu wanaoweza kuliwa.
Taasisi hiyo inapania kubuni njia za kuzalisha wadudu hao
kwa wingi bila ya kuharibu mazingira ili kukidhi utashi mara baada ya wazo hilo
likifanywa kuwa biashara.Wadudu wanaoliwa sana maeneo ya Magharibi mwa Kenya, ambao
wana wingi wa madini ya protini na Zinki watafanywa kuwa biashara ili
kuimarisha uwepo wa chakula cha kutosha, na kuondoa dhana mbaya katika kula
wadudu.
Madhumuni
habari,
Mafanikio,
maisha,
Sayansi na Teknolojia,
Teknolojia,
uhai,
Utafiti,
utulivu,
Vitabu
October 11, 2017
SOMO LA LEO
“Mheshimiwa Kakunda (Joseph –Naibu Waziri Tamisemi)
nakuagiza kuanzia leo maana wewe ndiyo nimekukabidhi jukumu la elimu, nataka
mtihani wa 2019 shule za vipaji zote 22 ziongoze mtihani wa Taifa na shule
binafsi ziwe nyuma, lakini tuongoze kwa halali si ubabaishaji hapo ndipo shule
binafsi za makanjanja zitajifuta zenyewe,”
-Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi, Selemani Jafo.
Madhumuni
Mazingira,
Teknolojia,
Vitabu,
wazo
September 30, 2017
UTUNZI WA VITABU NA KISWAHILI CHA PROFESA SHAOPING
NA KIZITO MPANGALA
KESI YA ALMASI
ni kitabu kilichoandikwa na Profesa Rao Shaoping wa China. Kitaaluma yeye ni
mhandisi. Alijifunza Kiswahili nchini Tanzania kwa muda wa mwaka mmoja na
ushee, mwalimu aliyemfundisha aliitwa Ali Omari Mzee.
Profesa
Shaoping ndiye msimamizi wa kazi za TAZARA wakati inajengwa. Alikuwa
akimtafsiria Mwalimu Nyerere mazungumzo aliyokuwa akijadiliana na wenzake. Pia
alikuwa mkaliamani kwa Mh. Salim Ahmed Salim, Mh. Rashid Kawawa, Spika Adam
Sapi kwa mazungumzo aliyokuwa akijadiliana na Wachina wenzake. Na mwaka 2013
Profesa Shaoping alikuja tena nchini Tanzania kumtembela Mzee Ali Hassan
Mwinyi.
Profesa
Shaoping anasema hivi "ninaipenda Tanzania. Ninawapenda watu wa
Tanzania". Profesa
Shaoping anayafahamu maeneo mengi nchini Tanzania ambayo amewahi kutembelea,
maeneo hayo ni kama vile Kisuwa cha Saa Nane, Arusha, Ifakara, Iringa, Kimbwe,
Kidatu, Mikumi, Makambako, Mbarali, Tunduma, Zanzibar, Moshi, Dodoma na
kadhalika.
Profesa
Shaoping ameandika kitabu hiki kwa bidii mno. Anasema tangu tuwe Koloni la
Mjerumani na baadae Mwingereza, wageni hao hawakuwa na morali ya kutunga riwaya
za Kiswahili lakini yeye kama mgeni alipenda sana kuacha kitabu kwa Kiswahili,
naam, ndicho hiki hapa pichani.
Madhumuni
diplomasia,
elimu,
falsafa,
Teknolojia,
utulivu
June 16, 2013
MADE IN TANZANIA: HATIMAYE, HAYAWI HAYAWI SASA YAMEKUWA
Mwanafunzi wa Chuo kikuuu cha Dodoma, ndugu Justice
Donatus amefanikiwa kutengeneza mtandao wake wa kijamii JUST LIKE FACEBOOK
IS,uitwao MAYOCOO ambao utasaidia kuiunganisha jamii ya kitanzania na kimataifa....Mtandao huu
umezinduliwa Jumamosi iliyopita tu....Watanzania tunaweza jamani,haya mambo sio
tu Mark Zuckerberg aliweza,hata sisi tumeweza...Nampongeza sana dogo,ndo yuko
mwaka wa 3 pale UDOM...Namuombea asiache chuo kama alivyofanya Mark,Warren
Buffet na Bill Gates...WATANZANIA WENZANGU TUSAPOTI KILICHO CHETU....Mimi
Nimeshajiunga na MAYOCOO, Follow me kwa jina la GIOVANNI
Habari hii kwa hisani ya SETH DE JESUS GIOVANNI
Habari hii kwa hisani ya SETH DE JESUS GIOVANNI
Madhumuni
Taarifa,
Teknolojia
January 02, 2013
TOKA ANALOJIA HADI DIGITALI: NINI MAONI YETU?
![]() |
| John Mnyika, MB |
Na John Mnyika, Dar es salaam
Naomba majibu yenu kwa kuzingatia kuwa kazi ya wabunge ni
kuishauri na kuisimamia Serikali: baada ya kutekelezwa kwa uamuzi wa kuhama
kutoka analojia kwenda digiti kwa mkoa wa Dar es salaam; kwa watumiaji, nini
faida na athari mlioanza kuzipata kwa wenye ving’amuzi? Na nini kikwazo kwa wengine ambao hamjahamia mpaka sasa? Na
nini mnataka watoa huduma na mamlaka zingine kuzingatia? Katika hatua ya sasa,
ni muhimu Tanzania Consumer Advocacy Society (TCAS) ifanye tathmini ya kina kwa
niaba ya watumiaji kwa ajili ya hatua zake.
Ikumbukwe kwamba Consumer Federation of Kenya ilikwenda
mahakamani na kuzuia mitambo kuzimwa watumiaji tarehe 31 Disemba 2012, na
mahakama imesitisha mpaka itakapofanya uamuzi wake wa msingi.
Kwa upande mwingine, Baraza la Ushauri la Watumiaji wa
Huduma za Mawasiliano Tanzania (TCRA-CCC) litumie mamlaka yake kwa mujibu wa
kifungu cha 37 cha Sheria ya Mamlaka ya Mawasiliano namba 12 ya mwaka 2003 na
vifungu vingine vinavyohusika kushughulikia malalamiko yaliyotolewa kwa nyakati
mbalimbali kwa kuzingatia tahadhari tuliyotoa kwa serikali bungeni miezi mingi
iliyopita kuhusu athari zitazojitokeza kwa kutozingatiwa kwa maandalizi muhimu.
NB: John Mnyika ni mbunge wa jimbo la Ubungo
Madhumuni
Digitali,
Teknolojia
Subscribe to:
Posts (Atom)


