Showing posts with label Mbaha. Show all posts
Showing posts with label Mbaha. Show all posts
March 26, 2018
MWONEKANO WA ZIWA NYASA KATIKA KIJIJI CHA MBAHA WILAYA YA NYASA
November 16, 2017
MV NJOMBE INAVYOFUNGUA FURSA KWA WAKAZI ZIWA NYASA.
![]() |
| Honorius Mpangala, 0628994409 |
AKIWA katika kampeni za urais mwaka 2005 Rais mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete katika ardhi ya Kyela Mkoani Mbeya alihaidi meli. Alirudia tena kauli hiyo alipokuwa katika ardhi ya Mbamba Bay Mkoani Ruvuma. Baada ya kipindi cha utawala wake hatimaye meli alizoahidi tayari zimeonwa na Wanyasa.
MV Njombe imekamilika na kufanikiwa safari moja ya majaribio kutoka Bandari ya Itungi
hadi Mbamba Bay. Yapo mambo ambayo ni
fursa kwa wakazi wa Nyasa kutokana Meli hii. Kama inavyoitwa ni meli ya mizigo
ni chombo kitakachoweza kuwainua kiuchumi wakaza wa Nyasa kama watakitumika
ipasavyo. Kuinuka kiuchumi kutatokana na kujikita katika shughuli ambazo wakazi
wake watajishughulisha na shughuli kama ilivyo kilimo biashara na hata ufugaji
wa kisasa na wenye tija katika maisha ya leo.
Kilimo
cha biashara ni moja ya ujasiriamali ambao watu wengi wamekuwa
wakijishughulisha nao. Katika mwambao wa Ziwa Nyasa hususani wilaya Nyasa yapo
mabonde ambayo yanaweza kufanyika kilimo cha mazao ya muda mfupi na kwa mfumo
wa kilimo cha umwagiliaji, na kile cha kutegema mvua na kuleta tija.
Madhumuni
ajira,
Biashara,
habari,
Imani,
Kilimo,
Linda,
liuli,
Matenje,
Mbaha,
mbamba bay,
Nyasa,
Uchumi
October 27, 2017
KWANINI WILAYA YA NYASA IMESHIKA MKIA KATIKA MATOKEO YA DARASA LA SABA?
![]() | |
| RAYMOND NDOMBA, SONGEA |
Mawazo yangu
ni haya; Pamoja na sababu nyingi zilizosababisha matokeo hayo ya aibu kubwa.
Wazazi wanapaswa kubeba lawama kubwa. Wengi wao hawafuatilii maendeleo ya
watoto wao, pia makuzi na malezi mabaya.
Miaka
ya hivi karibuni (kuanzia mwaka 2000), Wazazi wengi katika wilaya ya Nyasa
hawajali elimu, hawajigusi katika ufuatiliaji wa watoto wao kielimu na hata
kitabia (Angalia matokeo ya mitihani ya Taifa ya shule za msingi na sekondari
kunzia miaka hiyo ya 2000 kwa shule kongwe ndani ya wilaya).
Madhumuni
elimu,
habari,
Linda,
liuli,
lundu,
Maarifa,
Mbaha,
mbamba bay,
Mgodi Unaotembea,
na Uchumi,
Nyasa,
Nyumbani,
Ruvuma,
Songea,
uchambuzi
October 17, 2017
TAKWIMU MUHIMU ZA WILAYA YA NYASA HADI OKTOBA 2017
1. Total Number of
Hamlets in the District = 4252. Total Number of Households for Nyasa dc = 31,146
3. Total Female Population for Nyasa dc = 74,768.
4.Total Male Population for Nyasa dc = 71,392.
5. Total Population for Nyasa dc = 146,160.
6. Total Number of Secondary school = 14
7. Total Number of Primary School = 106
Total Number of Villages = 84
8. Total Number of Ward = 20
9. Total Number of Division = 3
CHANZO: Nyasa dc statistics
September 29, 2014
MBAHA KUNA UFUKWE MZURI KUVUTIA WATALII
Picha imepigwa na mdau wetu Hoops Kamanga. Eneo la Picha hii ni kijiji cha Mbaha katika tarafa ya Ruhuhu wiliya ya Nyasa.
Kiji cha Mbaha ni moja ya miji iliyojaliwa fukwe nzuri sana wilayani Nyasa. Ni maeneo ambayo bila shaka yanavutia watalii.
Karibuni wenyeji na wageni.
February 07, 2013
MVUA KUBWA YANG'OA MADARAJA BARABARA YA LITUHI-MBAMBA BAY
Na Egbart Jeremy, Nyasa
Mvua mkubwa iliyonyesha mapema mwezi huu imesababisha baadhi
ya miundombinu kuharibiwa. Miongoni mwa maeneo yaliyoharibiwa kabisa ni Daraja
la Mbaha, na barabaraba ya Lituhi kwenda Mbamba kwa ujumla, ambapo imejifunga
kutokana na kukosekana kwa vivuko vingine.
![]() |
| Moja ya maeneo yaliyoharibiwa kutokana na mvua kubwa iliyonyesha wilayani Nyasa |
Mvua hiyo imechangia kwa kiasi
kikubwa ukosefu wa mawasiliano baadhi ya vijiji hadi vijiji katika mwambao wa
ziwa Nyasa. Sio madaraja pekee, bali ukuna uharibifu mkubwa sana vyanzo vya
miradi ya maji hususani katika kijiji cha Lundu.
Hadi sasa hali haijatengemaa
kiasi amabcho wakazi wa maeneo yaliyokumbwa na uharifu wanakosa huduma muhimu
kutokana na ukosefu wa usafiri kutoka eneo moja kwenda jingine. Ikumbukwe
miradi ya maji katika kijiji cha Lundu ni moja ya miradi mipya iliyokamilishwa
mapema mwishoni mwa mwaka jana hivyo kuleta nafuu kwa wakazi wake. Lakini kutokana
na uharibifu uliotokana na mvua kubwa kunyesha utalazimisha miradi hiyo kuanza
kukarabatiwa upya.
Subscribe to:
Posts (Atom)





