Showing posts with label Utafiti. Show all posts
Showing posts with label Utafiti. Show all posts

December 28, 2017

UTAFITI: HISTORIA YA ENEO LA TINGITINGI ZIWA NYASA


...TULIPOFIKA hapa tukiwa tunatafakari sehemu ya kupita Mdogo wetu Thobias (mwenye tisheti nyekundu) akaniambia brother nimekumbuka movie moja inaitwa The Hard Way Is The Only Way. Akanielezea kidogo maana jamaa anapenda movie sana. 

Moja ya msitu ulioko eneo la jiwe maarufu Tingitingi. Karibu na ukuta wa mawe wa wampoto.Hapa ilikuwa tunasikiliza sauti za kanga pori tu na kuona kenge na mijusi wa rangi rangi.

November 15, 2017

KIFAHAMU KISIWA CHA LUNDO KILICHOPO ZIWA NYASA


HISTORIA ya kivutio cha utalii, kisiwa cha Lundo kilichopo Ziwa Nyasa, inaonesha kuwa kisiwa hicho kina ukubwa za hekta 20 kimepewa jina la Lundo kwa sababu watu wa kwanza waliovuka kisiwa hicho kwenda ng’ambo ya pili walifikia kijiji cha Lundo.

Kisiwa hicho tangu zamani kilikuwa na manufaa makubwa kwa wananchi wa vijiji vya Lundo,Ngindo na Chinula kwa sababu wakati wa vita ya Majimaji vilivyotokea kati ya mwaka 1905 hadi 1907 watu walikuwa wanakimbilia katika kisiwa hicho ambacho kina maeneo ya maficho.

Baada ya vita ya Majimaji kuanzia mwaka 1908 kisiwa hiki kilitumika na wakoloni wa kijerumani kuwahifadhi watu waliopata ulemavu kutokana na ugonjwa wa ukoma ambao baada ya uhuru walihamishiwa katika makazi ya Ngehe wilayani Nyasa. Serikali imependekeza visiwa vya Lundo na Mbamba Bay kuwa hifadhi za wanyamapori.

Visiwa hivyo vitakuwa ni hifadhi ya pekee ya wanyamapori pamoja na samaki wa mapambo wanaozaliana katika visiwa hivyo ndani ya ziwa Nyasa hivyo kuvutia watalii kufika kusini na kutekeleza Sera ya nchi ya kufungua biashara ya utalii Kusini.

November 10, 2017

MAJINA YA MITAA HUFANANA

Mtaa wa Muhoro

Pichani ni mtaa mmojawapo ulipo jijini Dar es salaam. Ni mtaa wa Muhoro. Katika kumbukumbu zangu mtaa kama huu wenye jina hili upo katika Kijiji cha Lundu, kilichopo Kata ya Mbaya, Tarafa ya Ruhuhu, wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma. Lundu ni miongoni mwa vijiji vyenye historia kubwa na kipo mwambao wa ziwa Nyasa. 

Kumbukumbu hizo za kihistoria zinaonyesha uhusiano wa watu na namna wanavyoingilia au kuathiriwa na maisha ya eneo moja kwenda jingine.
Hakuna taarifa rasmi inayosema mtaa wa Muhoro wa Dar es salaam ulianzishwa kwasababu gani, sambamba na ule wa kijiji cha Lundu.  

MUHIMU: Kuanzia mwaka huu tutakuwa na habari kemukemu za kihistoria kuhusiana na ukoloni,wamisionari,wangoni na mengineyo katika mwambao wa Ziwa Nyasa (husuani Tarafa ya Ruhusu).
Endelea kubaki nasi…
Honorius Mpangala akiwa na Alfred Mpangala katika kibao chenye jina la Mtaa wa Muhoro jijini Dar es salaam

October 16, 2017

CHUO CHAANZISHA SHAHADA YA WADUDU

NAIROBI, KENYA

KITUO cha Elimu na Utafiti kinachofadhiliwa na Benki ya Dunia kimeasisiwa katika Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Jaramogo Oginga Odinga na kinasubiri ruhusa ya kuanzishwa kwa programu za Uzamifu na Uzamili kuhusu wadudu wanaoweza kuliwa.

Taasisi hiyo inapania kubuni njia za kuzalisha wadudu hao kwa wingi bila ya kuharibu mazingira ili kukidhi utashi mara baada ya wazo hilo likifanywa kuwa biashara.Wadudu wanaoliwa sana maeneo ya Magharibi mwa Kenya, ambao wana wingi wa madini ya protini na Zinki watafanywa kuwa biashara ili kuimarisha uwepo wa chakula cha kutosha, na kuondoa dhana mbaya katika kula wadudu. 

October 13, 2017

WATALII TOKA ULAYA WATEMBELEA HIFADHI YA LUHIRA

SONGEA, RUVUMA
Watalii toka nje ya nchi wameanza kutembelea hifadhi ya Asili ya Luhira iliyopo katika Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma. Takwimu za mwaka 2016/ 2017 zinaonesha kuwa hifadhi hiyo imepokea watalii toka nchi za Ujerumani,Afrika ya Kusini,India,Ufaransa,Italia, Uholanzi na wageni toka mikoa mbalimbali nchini ambao pia wanafanya utalii wa kuchunguza aina ya mimea na ndege katika hifadhi hiyo.

Msimamizi wa Hifadhi hiyo Msonda Simwanza anasema wanajiandaa kuweka mazingira ambayo yatawezesha wanyama kama tembo,simba na wanyama wengine adimu kuishi katika hifadhi hiyo bila kuleta athari kwa wanyama na binadamu.

September 29, 2017

UTAFITI: UHANDISI NI FANI INAYOLIPA ZAIDI

WANAFUNZI wa elimu ya juu ambao husomea taaluma ya uhandishi au biashara katika wana nafasi kubwa kuwa mabilionea kuliko wanafunzi wanaosomea taaluma nyingine.

Aidha, wanafunzi wale ambao tayari wameingia katika soko la ajira katika kazi ya mauzo au biashara ya hisa ni miongoni mwa wenye fursa kubwa  kuwa katika sehemu watu matajiri duniani.

Kwa mujibu wa utafiti uliyofanywa hivi karibuni na shirika la ajira la Aaron Wallis, ambalo utafiti wake umeangalia watu matajiri duniani zaidi 100 ili kuona kama kuna uwiano au uhusiano wowote kati ya taaluma yao ya kwanza na jinsi walivyokuwa matajiri au kutengeneza utajiri.

Ripoti hiyo ilibaini  kwamba kazi yao ya kwanza, kati ya mabilionea wakubwa wa juu waliajiriwa kwa mara ya kwanza katika mashirika ambalo sio yao. Pia  kuna wajasiriamali ambao walianza kampuni zao wenyewe na wengine wale walioajiriwa katika biashara za kifamilia  katika nafasi masoko na mauzo.
Mabilionea 10 wa mwanzo kati ya 53 ambao waliajiriwa  katika shirika ambalo sio yao wakati mabilionea tisa tu walianza kazi yao kama mfanyabiashara wa hisa au mauzo.

Utafiti huo pia uligundua kuwa matajiri wakubwa duniani 75 kati ya watu 100 akiwemo Bill Gates, Warren Buffet, George Soros na Jeff Bezos wana elimu ya ngazi ya shahada tu.

Kati ya hao 75,  matajiri 22 walisomea shahada katika taaluma ya uhandisi (ikiwa ni pamoja na mwanzilishi wa mtandao wa Amazon, Jeff Bezos na  mwanzilishi wa Google Larry Page, aidha matajiri 16 walisomea masuala ya biashara ambapo 11 wamesoma taaluma ya fedha na uchumi.

Mabilionea 30 kati ya 100 wanautajiri wa kurithi au wanafanya kazi katika biashara ya kifamilia, wakati 17 walianza kampuni zao wenyewe. Mwezi Julai mwaka huu, muda mfupi tajiri Jeff Bezos alichukua nafasi ya Bill Gates kuwa mtu tajiri zaidi duniani baada ya kuongezeka kwa hisa katika mauzo ya mtandao kabla ya ripoti yake ya mapato, lakini hisa zilishuka tena na Gates alirejea katika nafasi ya kwanza.

Bill Gates ambaye ana utajiri wenye thamani ya dola za Marekani bilioni 87, na amekuwa mtu tajiri  zaidi duniani tangu mwaka 2013. Billionea huyu mwenye moyo wa kusiadia ametoa dola bilioni 31.1 ya utajiri wake katika kusaidia jamii kupitia taasisi mbalimbali, wakati Jeff Bezos ametoa dola milioni 100 kwa mujibu wa jarida la Forbes  la nchini Marekani.

Hata hivyo, ripoti imebaini kuwa matajiri wengi katika 100 wamesomea shahada ya kwanza ya uhandisi kama orodha ilivyoeleza. Matajiri wakubwa 22 duniani wanataaluma ya uhandisi, ambapo matajiri 16 wamesomea masuala ya biashara, katika fedha na uchumi (11) sheria (6) sayansi ya kompyuta (4) historia (3) Falsafa (2), Siasa (2), lugha ya Kiingereza (2), Historia (2), Hisabati (2) na masuala ya madawa (1).

©MTANZANIA