Showing posts with label soga. Show all posts
Showing posts with label soga. Show all posts

October 21, 2017

MBUNGE WA CHEMBA AONDOA HOJA YA KUONGEZA MUDA WA UBUNGE

NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM

MBUNGE  wa Chemba Juma Nkamia (CCM)amesema ameondoa kwa muda kusudio lake la kutaka kuwasilisha muswada binafsi wa mabadiliko ya Katiba unaohusu kuongeza ukomo wa Bunge. 
JUMA NKAMIA
Nkamia ambaye aliwasilisha kusudio hilo  katikati ya mwezi uliopita mjini Dodoma kwa mujibu wa kanuni ya 81(2) ya kanuni za Bunge toleo la 2016,kupitia barua yake aliyoisaini Septemba 12  iliyokuwa ikipendekeza kuongeza muda wa bunge kutoka miaka mitano hadi saba na kupunguza wa uongozi wa vijiji kutoka miaka mitano hadi minne.

Kupitia ujumbe mfupi aliouandika katika mtandao wa kijamii wa WhatsApp,alisema ameamua kuondoa kusudio hilo  baada ya mashauriano  na maelekezo kutoka kwa viongozi wa juu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM).

“Ndugu viongozi wenzangu naomba kuwataarifu kuwa baada ya mashauriano na maelekezo  ya viongozi wa juu wa chama(CCM) na hali ya kisiasa  katika nchi kadhaa za Afrika  Mashariki  nimelazimika kuondoa kwa muda hoja yangu binafsi ya ukomo wa Bunge niliyokusudia kuiwasilisha katika bunge lijalo,”aliandika Nkamia.

Mbali na andiko hilo gazeti hili pia lilimtafuta Nkamia kupitia simu yake ya kiganjani ili kumuuliza kama  na sababu nyingine zaidi ya alizozitaja kupitia ujumbe  huo mfupi na lini atakuwa teyari kuwasilisha tena muswada huo alisema.

“Naomba ibaki hivyo hivyo kama ilivyo kwenye meseji  sina cha kuongeza,kuhusu ni lini nitapeleka tena nayo subiri kwa sababu nimesema nimesitisha kwa muda maana yake nitawasilisha tena nitakapokuwa teyari,”alisema Nkamia.

Hoja ya  Nkamia ambayo ilianzia  katika Bunge lililopita ilikuw aikipingwa na wanazuoni pamoja na wanasiasa wakongwe akiwemo Spika Mstaafu wa Bunge Pius Msekwa.

Msekwa ambaye alikuwa akiongea na televisheni ya Azam  mwishoni wa wiki hii alisema  chama cha CCM hakiwezi kukubaliana na maoni au mpango wa kuongeza muda wa kiongozi yeyote kutoka kipindi cha miaka mitano kilichopo kikatiba kwa sasa.

Msekwa alisema kwa uzoefu wake bungeni tayari anaona kuna tafakari nyingi zilizofanywa kabla ya Taifa kuamua kipindi cha utawala kuwa miaka mitano na si vinginevyo.

Alisema hoja hiyo inabidi iangaliwe kwa umakini mkubwa kutokana na ukweli kuwa, iwapo kiongozi atakuwa mbaya, maisha yanaweza kuwa ya mateso kupitia kiongozi huyo na kuongeza kuwa hilo hata Hayati Baba wa Taifa, Julius Nyerere aliliona hilo.

“Ni kwamba miaka kumi tu inatosha, ili kama mtu ni mbaya tuvumilie kwa hiyo miaka kumi, na siyo kwamba haikufikiriwa. .na sidhani kama CCM itakuwa na nafasi ya kujadili hilo kwa sasa” alisema Msekwa. Mbali na Msekwa wasomi wakiwemo Dk.Benson Bana nao walimpinga huku akisema kuwa lengo lake lilikuwa ni kujipendekeza kwa Rais Dk. John Magufuli ili ampe uwaziri.

March 24, 2010

CHEMSHA BONGO, SHINDANO, ZAWADI NONO

KAMA KWELI UNA 'MIAKILI', nataka uanze kusumbua kichwa kwa neno hili.
Hivi karibuni kumezuka neno fulani hivi lenye kumaanisha jambo fulani. Neno lenyewe linaitwa 'MKUU WA POSTA'.

Limeene neno hili, linazidi kukua, lakini usifikirie lina maanisha kazi ya ofisi za Posta, bali ni jina la mtu mwenye tabia fulani hivi.

Mwenye tabia hiyo ndiyo huitwa 'MKUU WA POSTA' ili kumtaja hadharani kutokana na tabia yake hiyo.

JE UNAWEZA KUNG'AMUA NENO HILI LINA MAANISHA NINI KATIKA TABIA?

December 17, 2009

TABASAMU HLIJUI; UCHEKE UNA MWANYA WEWEEEE??

Kama ni tabasamu basi hilo ndilo linaloqweza kukufanya ukasahahu kuwa kuna watu wenye matatizo duniani. kama ni raha basi hapa nadhani raha utaipa vema biloa kukosa sana. Nina uhakika kila utazamapo unajiuliza kitu inakuwaje hii....inakuwaje hawa vimbe wengineni

Ndiyo dunia hiyo wapo wenye vituko na mikogo mingi. Wapo wenye mambo ambayo unaweza kushangaa kwamba ni kwavipi wanastahimili kuishi katika dimbwi la kuchekwa kama hilo.

Lakini sote tunapaswa kujikubali kwamba ndivyo ilivyo na ndivyo inavykuwa. Na labda inategemea na mtu alivyo kama unavyoona hayo mapozi. Vipi imetulia ama



Wakati mwingine huwa nawa sana kuwa unapocheka na kujidai unatbasamu unamwanya wewe au? Sasa tazama wenzio wenye mwanya wanavyolina nao angalia wanavyojidai kwa mbwembwe. N labda inategemea na mtu usije ukamdharau kwakuwa yuko hivi...lakini ujue anajambo la kukufurahisha asana kama ambavyo mimi nafurahi msomaji wangu. Ungekuwa pembeni hapa ungeona furaha yangu ni kuwaona watu wenye jkukabiliana na changamoto kadhaa duniani. Imetulia au imakaa vibaya?



Mwanya huna halafu unataka kulingana huyu? Aisehee mimi nashindwa hata kuongeza zaidi jamani ebu oneni alivyopendeza kijana wa watu, tazama meno yalivyojipanga kwa raha zake jamani. Kma unadhani wewe unaweza kuwarusha roho watu yaani kuwachekesha hadi wakakuona ndiyo tiba yao, nadhani kwa hilo hapo unaweza kujifunza kuwarusha zaidi. lete mambo
Ushawahi kukutana na kijana mtanashati kama huyu? Ni wapi niambie kwanza nikushushue?
Lione hata haloina aibu eti anajilinganisha na kakangu huyu alivyojipamba kwa pamba kali.
Wewew unacheka una mwanya?
Unakumbuka mwanamuziki King G.K aliimba katika vibao vyake vya AMA ZANGU AMA ZAO na ile ya ITIKADI? Jamaa nawahususudu sana watoto wa EASTCOAST ARMY. wanakunja ndita hadi spika zinagoma kuendelea na midundo, jamani zile kujikunjia ndita nikajiuliuza unacheki hilo lilivyokali kuzidi lile la vijana wa Upanda east na upanga west? Tazama kwanza mkunjo wa sur unaweza kuona kabisa kuna hali tulivu kuliko ugomvi jamani
mpeni alama zake jamani au?
Nasikia kuna bingwa wa kutabasamu lakini hapa naona anafunga breki kabisaaaaa...angali mwenyewe

Wakati nazzitazama picha hizo nilijiuliza swali moja muhimu. Je kuna mkono wa kompyuta katika picha hizo? Nilijiuliza je kuna Photoshop iliyofanyuika ama Illustrator au CorewDraw yoyote hapo? Nikajua jamani kuna watu wapo hivyo siyo mikogo ya kompyuta








































































































November 24, 2009

KATIKATI YA MAELEZO, KUNA SWALI

Sina cha kuandika leo ingawaje naandika. Lakini ninachoanadika ndicho nisichokifikiria lakini naona tu maneno yanatiririka kama maji mtoni. Nakumbuka nilipoanza kuwaza sikupata jawabu kama nawaza lakini sijui nakumbuka nini.

Nasikiliza maenelezo mengi tu, nayaona na kuyasoma mengi lakini naongea machache sana yenye mkondo mmoja tu ambayo ni mahusiano ya sisi wanadamu. Sasa wakati maelezo yanatoka nikajikuta nina ninaswali ambalo linatakiwa kujibiwa mwishono na nikajua sitajibiwa katikati ya ya maelezo.... duh! sijachanganyikiwa ila najikuta naandika tu sijui nawaza nini...hebu msomaji nisaidie katikati ya maelezo yangu kuna swali...na pengine kuhusu utashi wangi wangu.

Acha bwana mawazo mengine hata hayana huruma eti yanakuja tu na kujiwazisha yenyewe kama yalivyo. Na nadhani nawaza kwasababu tu ninakichwa chenye kiwazua mambo lakini sifuri kabisa hakina ustaarabu. Na inatosha tu kusema sijui nawaza nini.....

Nimekumbuka msimu wa kuogelea unavyoshamiri nyasa sasa, watu wanajiandaa mwisho wa mwka kwenda kujiburudisha huko jamani sijui vipi wasijua kuogelea aibu yao ........nina uhakika hata wewe msomaji hujui kuogelea, njoo nimeanza kufundisha namna ya kuogelea vizuri lakini usije na masharti nisikushike popote aiseh..... SINA KITU leo ndiyo maana napumzika tu kwa kuandika hivi......

Ngoja nimsikilize kipenzi changu King Gk anipoze na mistari ya kiHIP HOP yenye majigambo kinamna au siyo msomaji wangu.... nachagua kibao bomba sana SAUTI YA MANKA. haya anza .....

November 11, 2009

VITUKO VYA WANYASA NA SANAMU LA ASKARI DAR ES SALAAM


Nakumbuka nikiwa mdogo, simulizi za snamu la skari huyu zilinitihs akuona mji huu siyo wa kuishi. Nakumbuka waliowahi kufika huko Dar es alaam wakisifia na kutisha kuhusu mji wenyewe. Nakumbuka wengine waliwahi kusimulia kuwa hapo zamani kulikuwa na mzee fulani MNYASA aliwahi kukaa hapo kwa kuombeleza asamehewe makosa yake kwani hakujua kama anavunja kanuni za mji.
Na kosa lenyewe lilikuwa kushangaa ghorofa zilizojipanga katikati ya mji tangu alipokuwa akiishi Upanga. Na kwakua alikuwa mgeni basi aliamua kujipa jukumu la kuyajua mazingira kwakuwa alizowea mji kiasi chake. Basi akaijikuta maefika katika sanamu la askari huyu, mzee wa watu akapiga magoti kuomba msamaha sana kwa makosa ya kushangaa majumba makubwa watu wanaishi angani kama FIDEGE tena wale mbayuwayu...nawapenda sana hawa ndege.
Mzee huyo inasemekana alilia kwa nguvu zote kwa kudhani atasamehewa kosa la kushangaa majumba makubwa, yenye watu wasiotosheleza ubongo hadi wakawa walarushwa wakubwa na kuita TAKRIMA. Basi mzee huyo akaangua kilio hapo lakini hakuna aliyejali sana kuhusu hilo kwani alidhaniwa kua ni kichaa tu.
Lakini kama ujuavyo wabongo kwa kunusanusa udaku wakamsogelea mzee wa kinyasa na kumhoji inakuwaje anaongea na sanamu kwani amekuwa kichaa? Lakini mzee akasisitiza kuwa askari yule amemweleza atamdhuru kwanini ameshangaa maghorofa wakati anajua yanalipiwa? watu wakacheka inasadikika hivyo, wakamweleza huyo askari ni samanu tu hivyo kumtaka arejee nyumbani, ndipo mzee alikubalina lakini kwa sharti la kusindikizwa.
Alipotoa rai hiyo basi waungwana wakafanya hivyo hadi mtaa wa Undali na akaonyesha anapoishi kisha wenyeji wakajitokeza. Ndipo ikaulizwa kulikoni? Mzee akasimulia kisa na kudai jamaa wamemwokoa.... hee wenyeji wakaangua kicheko ikawa usiku ikawa mchana ......simulizi zimeendelea vizazi hadi vizazi vya mzee wa Lundunyasa alisimuliwa.....na hapo kale alikuwa akikataa kuja mji huu sababu hiyo ingawaje baadaye alikubali tu shauri ya elimu siyo sababu ya askari sanamu. Na akitimiza agano mzee wa Lundunyasa lazima arejee agano lake la nyasa. Vituko vya wanyasa na sanamu hilo jamani nilikuweo enzi hizo wakitusimulia yatokanayo

February 11, 2009

Hakuna kulala hapa

Vipi, unaonaje ukijiunga nao! Unaweza kweli mauno ya viuno kama Fifimoto wa Enomizizi au wewe ni laini yaani nyororo! Utaweza wewe mtoto wa geti kali mambo haya? Mtoto umekulia wapi kama siyo ndani kutazama kideo na propaganda za seleka za walami ughaibuni.
Nakumbusha umuhimuwa kunengua mitindo ya kwetu, hakuna kulala aiseh

February 06, 2009

ndiyo maana nakupenda sana

Daima nawaza, nakumbuka enzi za uvuvi bwana,kabla sijajua kubonyeza niandikacho. Mmmmhh Koero aliagiza samaki, akadai anahitaji Kamongo, DUH! Pengine sijui hawa samaki wapo wapi lakini sijui kama ziwa letu lina Kamongo. Mmmhh labda nimesahau mambo yetu. Haya weeeeee tayarisha ugali mimi naandaa mboga, wala usilete kitu tofauti na ugali tena wa muhogo.

January 17, 2009

Mseto,Teknolojia na Yasinta+Klayson

Gumzo lilikolea si haba, tukajiburudisha kwa utani wa hapa na pale. Lakini jambo la msingi ni matumizi ya blogu katika kuelemisha na kuwa na marafiki zaidi. Sasa gumzo lilipokolea ilibidi mambo ya teknolojia yaanze kujadiliwa. Mosi ilikuwa huduma poa ya NeoWORX Widgets.
Huduma hii inakuwezesha mambo mengi ikiwemo kujua idadi ya watembeleaji, hali ya hewa, picha na mambo mengine. Hii inamaana pamoja na Free NeoCounter (wageni wanaoitembelea blogu yako), NeoBoard, NeoEarth (hali ya hewa ya mahali unapotaka), NeoPod, NeoFlags( ukipenda bendera mbalimbali ziwepo katika blogu yako), NeoPlanet (mambo ya sayari) na NeoKube.
Huduma hizo ni pamoja na zile za malipo na za bure, sasa kama tunavyojua kwamba blogu zetu zinazidi kupewa kipaumbele kwani zote hizi nia yao ni kuboresha zaidi. Sasa gumzo na mseto wa mazungumzo ilikuwa huduma hizi, lakini binafsi bado najifunza hazijakaa kwenye medulla sawasawa ndiyo maana kuna NeoCounter pekee. Basi bwana Klayson akahoji huduma za bure huzipendi, ikabidi nimweleze mimi bado najifunza hizo kwahiyo polepole.

Mambo ya blogu zetu siku hizi ni mengi huduma ni nyingi mno ambazo Wanablogu inabidi tuzitumie, pia ipo ya Feedbliz , hii ni huduma ambayo kila unachoandika unawatumia wasomaji katika akaunti zao, hivyo wao huingia moja kwa moja kukuta mjadala uliowasilishwa au habari/picha. Hata hivyo ahadi zetu ni kwamba huduma hizi tutaweza kuzitumia iwapo tutajipa muda kuzielewa umuhimu wake. Blogu ni mambo yanayokwenda na mabadiliko sana kwani tayari wataalamu wamebaini siyo upepo wa kupita. Kivumbi cha Gaza blogu zimeweka video, picha na habari motomoto ambazo hutumiwa na mashirika kama BBC, DW, AP, Skynews n.k jamani blogu ni teknolojia ambayo sijui magazeti itakuwaje tuendako maana Thomas Friedman anasemaje katika kitabu chake 'The World is Flat', yanawezekana, AMKA anza WEWE ili tuibadili jamii. Gumzo lilikuwa tamu sana aiseh

December 09, 2008

heee!!! warina asali nao !!!!!

TAMU ni yenye ladha ya sukari ambayo huridhisha kinywani. Ingawa vipo vitu vitamu vya kuhisia ambavyo havihitaji vipitie KINYWANI. Vitu VITAMU vipo vingi sana duniani. Havina hesabu. Vipo vinavyokolea UTAMU wake kwa kupikwa ama kuchemshwa au hata kukaangwa. Navyo huwa VITAMU, vipo vya kukorogwa kuchanganywa na kughushiwa ili UTAMU unoge. Kazi hiyo hufanywa na sisi binadamu wenye akili na busara. Lakini viumbe wengine wakiwemo wanyama, ndege, na wadudu husaidia kuifanya kazi hiyo adhimu wakati mwingine bila wao kujua.
VITAMU huwa VITAMU.
Lakini VITAMU viongozavyo na ambavyo huvivumilia vinaporishai katika GEGO na FIZI za kinywa ni asali. Lo masalaleee!! Huu ni UTAMU ulioje wa asali? Sijui unatoka wapi?. Sio wa kukaangwa wa kughushiwa. UTAMU wa maumbile. UTAMU huo wa asali si bure, umefanyiwa kazi kubwa. Haushuki duniani kama mvua Wapo wenyewe ambao wanatengeneza. Ni viumbe kama sisi waitwao NYUKI. Hivi huo UTAMU WA MAUMBILE Upoje??? mbona NYUKI wanatupatia UTAMU mpaka WARINA ASALI wasitake kujua mtengenezaji??

November 13, 2008

kipindupindu kiingie ikulu


sikujua uchungu, sononeko la moyo
akili yagota kwangu, moyoni harijojo
ghadhabu yanisibu,adhuhuri si kikomo
dibaji ya nini,uchafu mitaani?

kila leo twaumwa,vichomi na kuhara
miili yatuuma,akili nayo yagoma
maji haba salama, twanywa ya visima
dibaji ya nini uchafu mitaani?

kipindupindu chapindua,kinyesi kuwa maji
mwili kukongoroka,acheni dhihaka jamani
kila leo twanya uharo, ikulu vipi?
dibaji ya nini,uchafu mitaani

kipindupindu ikulu,napenda kitinge
waharishe wakuu,nasi tupumzike
aghalabu isiwe vigumu, wanye uharo preeee
wakome na kuona mashudu,wanune au wacheke?
dibaji ya nini,uchafu mitaani

ngoja kipindupindu kiingie ikulu
ooooh alamsiki waungwana wema

October 25, 2008

vijana wapya Jamani wapeni moyo.

Inaonekana kama nimekuwa mvivu kuhusu blogu siku hizi, lakini amini nawaambia siyo ila mambo ya hapa na pale kuvua samaki kuogelea sana mpaka machp yawe mekundu kama wale mabibi wa shinyanga halafu mseme uchawi.
Kuna vijana wapya nawasaka wamekuja katika blogu jamani. Kazi yangu nyingine sasa ni kuhamasisha kuanza blogu kwahiyo msione kimya. He waangalieni hawa vijana ambao nimefanikiwa kuendeleza kazi za Ndesanjo Macha

www.kambilisports.blogspot.com
www.shamakala.blogspot.com

wapeni moyo, nafanya juhudi kubwa kuhamasisha kuhusu blogu

October 22, 2008

mabusu + mabusu mpaka jela !!!!!!!!!!!

ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha jamani mambo juu ya mambo, kilichonifanya niblogu leo ni hiki ninachoandika achana na picha hizo hapo chini. hizo ni changamoto tu.nilikuwa mapumzikoni kwa juma moja lakini utamu wa kublogu bwana!!!!! wanaoacha na kupuuza shauri yao. basi nitawapatia ile santuri ya ETAT MAJOR ya wale vijana wa EXTRA MUSICA, nawapenda mno, au Kwaito ya MANDOZA ya zamani ile ya M DO or DIE. ha ha ha aha ha kazi kwenu mnaoacha kublogu.

DUBAI
Ingawa DUBAI imekuwa ikifanya juhudi kubwa katika biashara yake ya utalii, ikiwa ni pamoja na kujenga hoteli za kadhaa za kitalii, imetuma ujumbe kote duniani kwamba pamoja na hamu yake ya kuongeza idadi ya watalii wanaotembelea lakini haiko tayari kutelekeza utamaduni wake na sheria zake.
Ujumbe huo umetumwa kupitia kwa raia wawili wa Uingereza kwa kuhukumu kwenda jela miaka mitatu kwa kosa la kufanya mapenzi ufukweni. Michelle Palmer(36) na kidume chake Vince Acors(34) ambao siyo wanandoa. wali-BANJUKA huko ufukweni DUBAI, lakini kwa mujibu wa sheria za nchi hilo ni kosa. Jamaa walikuwa wakipigana MABUSU na inasemekana wali-BANJUKA ingawa wamekanusha KUBANJUANA huko wanatakiwa kwenda jela kosa lao kupigana mabusu.

CHANZO: gazeti makini la Raiamwema

tamu+tamu= lakini chungu

harakati za kupiga vita ukimwi ndiyo hizo, sasa msifikirie hapa nyasa hatufanyi hivyo. Lakini swali kweny tuta utamu nao una ukakasi? mmm utamu utaliwa kwa maganda? ebo mnyasa vipi miye? oooh najiuliza tu

October 09, 2008

habari ndiyo hiyo

hapa hakuna la mnadi swala wala sauti za kanisa, mchezo ni kujiburudisha, mchezo kufurahi yanini kujibana wakati muda wenyewe robo eti tutakwenda peponi mmmm

October 08, 2008

Labda leteni huku nyasa

sijaomba picha hii, lakini poa tu. Kuna jamaa walevi wanapenda sana hivi vitu. wengine wakunywa eti kupoteza mawazo. ebo nani kakwambieni mawazo yanapotezwa? mnajidanganya,mkipoteza mtapata wapi mengine. ndiyo nimechukua hapo bloguni Ruhuwiko kwa wanywa ulanzi na chimpunu(natania). jamani ukitaka kuwa na urafiki bora nami ni vema ukatofautisha haya makopo na nami. kama unasema unataka kupiga gumzo nami hakikisha pembeni hakuna makopo kama hayo. hata kama iwe mnasema 'mtoko' au 'matembezini' nakwambia nakuachia mtoko wako ukiniletea hayo makopo kama vipi kunywa kwa muda wako kisha harufu yako usilete kwangu au vipi waungwana. Unajua nini hapa nyasa hakuna, kwahiyo washamba tumekuwa wengi nasikia ukinywa tu unakufa. Kuna daktari mmoja alipogundua kwamba nina damu nyingi aliniuliza eti kama nakunywa pombe nusura nimzabe kibao, nikamwambia akome na akomae au vipi. karibuni nyasa lakini ONYO usije na hayo makopo ni haramu

maswali magumu

Mwanablogu Yasinta Ngonyani aliandika kuhusu yeye katika blogu yake. Ilikuwa Agosti 23, 2008 kwamba udadisi kwake ni sehemu ya maisha, akaongeza kwamba katika hali hiyo amejikuta amepoteza baadhi ya marafiki hasa wale wasiopenda maswali yake yaani walikuwa wakikerwa na maswali yake. Mimi sijui walikerwa kwasababu gani, wao wanajua. Sasa mimi namfahamu kiasi dadangu Yasinta, jamani hapo ni kiboko ya maswali yaani jamaa anauliza maswali mpaka unaona hee huyu vipi? Ukweli mmoja ya waathirika ya maswali yake ni Mnyasa hapa lakini kawaida ya Mnyasa ni uvumilivu na utulivu ndiyo uliobaini kwamba uulizwaji kwake maswali ni njia yake ya uwasilishwaji wa urafiki tofauti na wengine walivyokuwa wakidhani. Jamani dadangu anamaswali mpaka unaweza kuungua utadhaniumeunguzwa na moto. Sasa huwa najiuliza vipi mjomba wangu Erik na Camilla watakuwaje? nikajikuta nimegota,nimeishiwa maneno ya kuwatabilia. Lakini maswali yake yanakufanya muda wote uwe unafanya kazi ya kujibu na usipojibu heee umemkimbia au la. Jamani mimi nilivumilia na nimekubali kwamba kama alivyoandika ni kawaida yake kwahiyo naona poa tu. Habari ndiyo hiyo, kublogu/kuandika unachopenda

October 07, 2008

weweeee mambo iko ukuuuuuu

jamani eti watu wa mjini nao wanabanjuka baharini. waone kwanza wanaogelea maji ya chumvi wakati kwetu maji salama kabisa

September 26, 2008

kwa wanaotaka kwenda majuu - II

Awali nilikuwa sielewi kwanini hawa watu wangu wanataka kuondoka nchini mwetu, lakini baadaye nilipokuwa Uchina na bwana Mao rais wa pale nilielewa sababu zao kwani nilikutana nao wataalamu wetu walioondoka Tanzania. Walinieleza sababu zao zenye maana kabisa,nikaelewa kwamba wanamipango mizuri. ...hata hivyo nikawaambia msisahau nyumbani jamani si mnajua kule mmewaacha ndugu zenu. kumbukeni hata sisi tulisomeshwa na mkoloni halafu tukapambana naye kwahiyo hata ninyi mnaweza kupambana nami kama sifanyi yale yanayowapendeza,huo ni utumiaji wa elimu. Sasa mkiondoka hawa wasiojua kitu watapambana vipi,watanitikisa vipi wakati siwaogopi. Lakini vijana wetu wakifundishwa kwenda mahala bila mipango,kuondoka kinyemela kwa ahadi za watu wasiowajua wala utamaduni wao,nadhani taifa litaaibika sana. Mnamwachia Mwl.NYERERE kupamba na umasikini kwani yeye ndiye aliwaletea? Haaa(kicheko). Lakini ninyi watu lazima mfikiri siyo kuhubiri tu maghorofa ya ulaya na amerika hapa..hayakuja bure shauri yenu....na...na ....na elimu yenu bado mnawapatia kila jambo hawa ndugu zetu...(wazungu).Msidhani kwamba mnyasa ninaandika mambo gani..kwani naona ile kasi ya kutaka kuishi majuu kwa kusingizia kusoma na wengine kutafuta kazi imezidi sana.Wabongo hayo maneno ni ya huyu mzee pichani JULIUS KAMBARAGE NYERERE.kama siku ya mwisho kuwepo duniani ningelikuwa naye,ningelimuomba kichwa chake yaani ubongo wake tu basi. Lakini kama kweli tunadhani elimu bora iko huko ughaibuni,elimu yetu airekebishe nani? tukisha soma huko basi tunaomba kazi hukohuko tena kufagia n.k baada ya hapo unarudi bongo unalalamika mbona hali haibadiliki? eboo! huna adabu akubadilishie nani wakati ulipomaliza shule hukurudi kuibadilisha si ulikwenda kuishi na yule Mwenyekiti wa Marais waongo duniani Joji Kichaka? Natumia lugha kali bila kutumia tafsida ili mpate ghadhabu na kuongeza juhudi. Mungu akupe hekima Ndesanjo Macha, Fred Macha nipo nanyi daima.Jikomboe. Uhuru daima

September 21, 2008

haaa haaa haaaa sicheki nafurahia ngoma

angalia uone utamu wa kupenda utamaduni wako, si unaona ilivyo na raha? kazi kweu msiopenda utamaduni mtamu kama wa kiafrika.

September 14, 2008

nakupenda nyasa yangu.....upendo wa dhati

karibuni nyasa, unajua wakati mwingine naishiwa maneno ya kusfia labda mna wivu mno hata nashindwa kusifia. kazi kwenu