Showing posts with label utalii. Show all posts
Showing posts with label utalii. Show all posts

January 15, 2018

KARIBUNI RUVUMA. KARIBUNI KUTALII TUNDURU

Hili ni Jiwe kubwa sana ambalo linavutia watalii. Hili ni mojawapo tu, maana yapo zaidi ya haya. Mawe haya yanapatikana kilometa chache tu kutoka Tunduru Mjini mkoani Ruvuma.

December 28, 2017

UTAFITI: HISTORIA YA ENEO LA TINGITINGI ZIWA NYASA


...TULIPOFIKA hapa tukiwa tunatafakari sehemu ya kupita Mdogo wetu Thobias (mwenye tisheti nyekundu) akaniambia brother nimekumbuka movie moja inaitwa The Hard Way Is The Only Way. Akanielezea kidogo maana jamaa anapenda movie sana. 

Moja ya msitu ulioko eneo la jiwe maarufu Tingitingi. Karibu na ukuta wa mawe wa wampoto.Hapa ilikuwa tunasikiliza sauti za kanga pori tu na kuona kenge na mijusi wa rangi rangi.

UMENG’ATWA NA MANYIGU, LAKINI KIU BADO UNAYO.

NIKIWA njiani kurejea Dar es salaam, mdogo wangu Honorius Mpangala alinitumia ujumbe mfupi katika simu yangu, “Aisee tupo Tingitingi, lakini nimeng’atwa na manyigu. Vifaa tulibeba kama kawaida,”. 
  
Nikashangaa. Sikufikiria kama eneo lile laweza kuwa na manyigu au hatari zozote za wanyama wakali. Leo pichani anasema, “Nikiwa najikagua mkono na miguu baada ya kung'atwa na manyigu saba. Ilikuwa tarehe 25/12 saa saba mchana pori moja kando ya ziwa Nyasa.Pori lenye msitu unaogota katika maji ukiwa na mawe makubwa huko ndo maskani ya wanyama kama ngedere, nyoka, nungunungu, mijusi wa rangi rangi,ndege kama kanga pori na Kwale. Baada ya shambulizi nilijiziba uso na kuacha sehemu ya miguu kuwa wazi lakini ajabu niling'atwa hadi kwenye makalio,”.

December 11, 2017

MAREKEBISHO: UTEUZI WA WAJUMBE WA KAMATI YA KITAIFA YA UTALII


December 01, 2017

WAZIRI MKUU ATAMBUE NYASA IMEJAA UTAJIRI

Na MARKUS MPANGALA
 
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa wakati akifunga mkutano wa tisa wa Bunge la 11 Novemba 17 mwaka huu alibainisha jambo muhimu linalohusu ubora wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini ambayo inajumuisha mikoa ya Ruvuma, Mbeya, Lindi na Mtwara.
Makala haya yalichapishwa katika safu yangu ya MAWAZONI ndani ya gazeti la RAI linalotoka kila alhamis
Waziri mkuu katika hotuba yake alimwagiza Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamis Kigwangala kuanzisha Mamlaka ya Fukwe za Bahari na Maziwa ili kutangaza utalii na kuendeleza fukwe ambazo hazina shughuli.
 
Agizo la Majaliwa linaakisi mpango wa serikali wa kuendeleza utalii Nyanda za Juu Kusini kwani kuna vivutio vingi lakini pamekuwapo idadi ndogo ya watalii wanaotembelea ukanda huo, ukilinganisha na Kaskazini.

November 24, 2017

JIWE LA POMONDA NA FORODHANI PANAWEZA KUTUPATIA WATU WA 'DIVING' KATIKA MASHINDANO YA OLIMPIKI.

NA HONORIUS MPANGALA

LICHA ya kuwa mazingira mazuri na yenye kila aina ya vivutio lakini wafrika tunashindwa kuwa wabunifu wa katika kuyafanya kama fursa.Mungu aliiumba Afrika hivi ilivyo na kuweka jiografia ambayo nyakati zote watu Wa mataifa ya ulaya wamekuwa wakivutiwa nayo.
Mmmoja wa Warukaji katika Jiwe la Pomonda, Ziwa Nyasa
Iko michezo mingi inayochezwa Ulaya na Amerika inatokana na jinsi wenzetu walivyo makini katika kutumia mazingira yao katika kujipatia fursa ya maisha yao. Nyakati zote mataifa ya wazungu yamekuwa na michezo mingi ambayo ina mashabiki na wanafanya vyema,hakuna michezo ambao unakosa mashabiki Amerika na Ulaya.

November 22, 2017

FUKWE ZA LUNDU, KARIBUNI ZIWA NYASA

 Hapa ni Forodha ya Lundu. Eneo hili lina fukwe mzuri sana kama huu. Picha ya Juu ni upande wa Kusini mwa forodha. Picha ya chini ni upande wa kaskazini magharibi mwa forodha hiyo. Ufukwe huu umepokea wageni kutoka Ujerumani, Italia, na wengineo ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Karibuni sana Lundu. Karibuni Wilaya ya Nyasa.

November 16, 2017

MBAMBA HILL KUWA HIFADHI YA PILI YA ASILI TANZANIA KUWA MJINI

NA MWANDISHI WETU 
MKOA wa Ruvuma unatarajia kupata hifadhi ya wanyamapori ya pili ya asili inayoitwa Kilima Mbamba (Mbamba Hill) ambayo ipo mjini Mbamba Bay makao makuu ya wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma. 
Hifadhi pekee Tanzania ya kwanza ya asili iliyopo mjini inaitwa Luhira iliyopo kilometa saba toka mjini Songea mkoani Ruvuma iliyoanzishwa mwaka 1974. Mkoa wa Ruvuma unapata hifadhi ya pili ya asili mjini. 

November 15, 2017

KISIWA CHA MBAMBA BAY KIMEPENDEKEZWA KUWA HIFADHI

NYUMA yangu ni kisiwa cha Mbambabay wengine wanakiita kisiwa cha Zambia kilichopo Mbamba Bay wilayani Nyasa mkoani Ruvuma ambacho kimependekezwa kuwa Hifadhi ya wanyamapori. Kisiwa hicho kina ukubwa wa hekta 27.kisiwa hicho kimejaliwa kuwa na uoto unaovutia wa misitu ya miombo ambao ni maarufu duniani ambapo mawe yanayozunguka katika kisiwa hicho ni mazalia ya samaki wa mapambano aina zaidi ya 400 wanaopatikana katika ziwa Nyasa pekee.
Kutokana na udogo wa kisiwa cha Mbambabay Afisa Maliasili na Utalii wa Mkoa wa Ruvuma Afrikanus Challe anashauri katika kisiwa hicho kusijengwe makazi ya kudumu kwa ajili ya wafanyakazi wa kuhudumia watalii ili kuendelea kutunza uoto wa asili uliopo hivi sasa.
Albano Midelo

KIFAHAMU KISIWA CHA LUNDO KILICHOPO ZIWA NYASA


HISTORIA ya kivutio cha utalii, kisiwa cha Lundo kilichopo Ziwa Nyasa, inaonesha kuwa kisiwa hicho kina ukubwa za hekta 20 kimepewa jina la Lundo kwa sababu watu wa kwanza waliovuka kisiwa hicho kwenda ng’ambo ya pili walifikia kijiji cha Lundo.

Kisiwa hicho tangu zamani kilikuwa na manufaa makubwa kwa wananchi wa vijiji vya Lundo,Ngindo na Chinula kwa sababu wakati wa vita ya Majimaji vilivyotokea kati ya mwaka 1905 hadi 1907 watu walikuwa wanakimbilia katika kisiwa hicho ambacho kina maeneo ya maficho.

Baada ya vita ya Majimaji kuanzia mwaka 1908 kisiwa hiki kilitumika na wakoloni wa kijerumani kuwahifadhi watu waliopata ulemavu kutokana na ugonjwa wa ukoma ambao baada ya uhuru walihamishiwa katika makazi ya Ngehe wilayani Nyasa. Serikali imependekeza visiwa vya Lundo na Mbamba Bay kuwa hifadhi za wanyamapori.

Visiwa hivyo vitakuwa ni hifadhi ya pekee ya wanyamapori pamoja na samaki wa mapambo wanaozaliana katika visiwa hivyo ndani ya ziwa Nyasa hivyo kuvutia watalii kufika kusini na kutekeleza Sera ya nchi ya kufungua biashara ya utalii Kusini.

November 13, 2017

MILIMA NA MABONDE YA MATOGORO KIVUTO CHA UTALII


Katika eneo hilo lililopo kusini mwa mji wa Songea, kuna bonde kubwa kabla ya kuufikia mlima huo. Ni eneo ambalo linavutia watalii. Mtu yeyote akipanda mlima wa Matogoro anaweza kutazama mji wa Songea ukiwa chini yake. 

November 10, 2017

KINANDA: MAJI YA ZIWA NYASA YANAPUNGUA?

NA MARKUS MPANGALA

JIWE hili ni maarufu sana katika kijiji cha Lundu. Linaitwa Kinanda au kwa wenyeji tunaliita kienyeji “Chinanda”. Lipo katika forodha ya Chivanga. Picha hii ilipigwa mapema Mwezi Februari mwaka huu. 
Honorius Mpangala akiwa katika Jiwe la Kinanda, Februari mwaka huu.
 
Lipo jambo moja la kusikitisha ni kwamba kiasi cha Maji katika Ziwa Nyasa si kama kile kilichokuwa zamani. Katika miaka ya 1980 hadi miaka 90 jiwe hilo lilizungukwa na Maji. Lakini miaka mwanzoni mwa 200o kumekuwa na mabadiliko mengi katikam ziwa.

MAJINA YA MITAA HUFANANA

Mtaa wa Muhoro

Pichani ni mtaa mmojawapo ulipo jijini Dar es salaam. Ni mtaa wa Muhoro. Katika kumbukumbu zangu mtaa kama huu wenye jina hili upo katika Kijiji cha Lundu, kilichopo Kata ya Mbaya, Tarafa ya Ruhuhu, wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma. Lundu ni miongoni mwa vijiji vyenye historia kubwa na kipo mwambao wa ziwa Nyasa. 

Kumbukumbu hizo za kihistoria zinaonyesha uhusiano wa watu na namna wanavyoingilia au kuathiriwa na maisha ya eneo moja kwenda jingine.
Hakuna taarifa rasmi inayosema mtaa wa Muhoro wa Dar es salaam ulianzishwa kwasababu gani, sambamba na ule wa kijiji cha Lundu.  

MUHIMU: Kuanzia mwaka huu tutakuwa na habari kemukemu za kihistoria kuhusiana na ukoloni,wamisionari,wangoni na mengineyo katika mwambao wa Ziwa Nyasa (husuani Tarafa ya Ruhusu).
Endelea kubaki nasi…
Honorius Mpangala akiwa na Alfred Mpangala katika kibao chenye jina la Mtaa wa Muhoro jijini Dar es salaam

MAJIMAJI FC KUFANYA ZIARA NYASA

 Na Mwandishi Wetu
 
KLABU ya Majimaji ya mjini Songea inatarajia kufanya ziara ya kimichezo katika wilaya ya Nyasa. Katika ziara hiyo Majimaji wanatarajiwa kucheza 
mechi mbili za kirafiki, Novemba 11 na 12 wilayani hapa. 

November 09, 2017

WILAYA YA NYASA INAO UTAJIRI WA VIVUTIO VYA UTALII

Mwonekano wa fukwe za Ziwa Nyasa.

November 04, 2017

UTALII: UFUKWE WA KIJIJI CHA LUNDU

Wilaya ya Nyasa imebarikiwa kuwa na fukwa zuri zinazotokana na ziwa Nyasa. Huu mojawapo ya ufukwe wenye historia kubwa sana, kupokea wageni kutoka Ujerumani, Uingereza, Italia na nchi mbalimbali ambao wengi wao walikuja kupitia Shirika la Benedictine Fathers la Peramiho na wengine kwa njia zao binafsi. Ni ufukwe wenye kumbukumbu nzuri sana kwa wakazi na wageni.
KARIBUNI NYASA.

November 01, 2017

WAZIRI KAZINI

Waziri wa Maliasili na Utalii nchini, Hamis Kigwangallah, akiwa kwenye ziara ya mojawapo ya Mbuga za wanyama

October 21, 2017

TABASAMU NA KITABU


Ragin Mmbanga (kushoto) na Markus Mpangala (Kulia)
Huyu ni rafiki yangu. Anaitwa Ragin Mbaga, ila tuwapo farashani hupendelea kumwita "Mzee wa bustani ya usomaji". 

October 13, 2017

WATALII TOKA ULAYA WATEMBELEA HIFADHI YA LUHIRA

SONGEA, RUVUMA
Watalii toka nje ya nchi wameanza kutembelea hifadhi ya Asili ya Luhira iliyopo katika Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma. Takwimu za mwaka 2016/ 2017 zinaonesha kuwa hifadhi hiyo imepokea watalii toka nchi za Ujerumani,Afrika ya Kusini,India,Ufaransa,Italia, Uholanzi na wageni toka mikoa mbalimbali nchini ambao pia wanafanya utalii wa kuchunguza aina ya mimea na ndege katika hifadhi hiyo.

Msimamizi wa Hifadhi hiyo Msonda Simwanza anasema wanajiandaa kuweka mazingira ambayo yatawezesha wanyama kama tembo,simba na wanyama wengine adimu kuishi katika hifadhi hiyo bila kuleta athari kwa wanyama na binadamu.