Showing posts with label sanaa. Show all posts
Showing posts with label sanaa. Show all posts

February 19, 2018

FEROUZ, BABA YAKO YUPO KIJIJI CHA MATIMBWA, BAGAMOYO

Na. HONORIUS MPANGALA
MAISHA kama yalivyo na tafsiri pana kwa binadamu tunaoishi katika hii dunia,inatufanya tusiwe na maana halisi.Ujana kwa jinsi zote mbili yaani ya kike na ile ya kiume una changamoto nyingi.  

Waswahili husema ujinga wa ujanani ndio umaskini wa uzeeni. Katika umri huo yatupasa kujiandalia kila aina ya mazingira ili tuweze kuwa na uwepesi katika kutimiza majukumu yetu uzeeni. Unamjua msanii wa bongo fleva aliyesifika kwa kutoa wimbo ambao ulikuwa na ujumbe mzito wa Starehe. Anaitwa Ferouz Mrisho kama watanzania wanavyomfahamu. Kabla ya hapo alikuwa kundi la Daz Nundaz pamoja na Daz Baba.

February 10, 2018

‘LOCATION’ YA WANAMUZIKI WA BONGOFLEVA ASLAY NA NANDY


Unaupata wimbo unaobamba sana katika vituo vya redio, kwenye magari ya abiria, bodaboda na Bajaj wa “SUBAKHERI MPENZI” ulioimbwa na wanamuziki wawili; ASLAY na NANDY?

Sasa hii pikipiki niliyokaa ambayo inamuundo wa aina yake imetumika katika video ya huo wimbo, maana ina usukani kama gari na makorombwezo ya mfumo Wa gari. Cratch inakanyagwa kama ya gari. Subiri kile ambacho wenye maeno yao wanavyosema pale inapotokea msanii anafanya video ya wimbo au kazi nyingine ya Sanaa kama filamu wao wanavyojisikia na namna gani wananufaika kupitia Location za hizo video zinazochukuliwa.

 Honorius Mpangala,

Matimbwa, Bagamoyo

November 13, 2017

WARAKA WA AFANDE SELE KWA KIFUNGO CHA MSANII LULU

Nakumbuka vizuri saana mwaka 2006 yaani miaka miwili tu baada ya mimi kushinda taji la ufalme wa rhymes Tz na kukabidhiwa ile gari maridadi sana ya zawadi aina ya toyota sera yenye milango ya kubinuka kama mabawa ya ndege anaejiandaa kuruka....
Lulu

Jumamosi moja ktk mwaka ule nikiwa kwenye ubora wangu wa hali ya juu na ushawishi mkuu kuliko msanii yeyote Tz nilialikwa kutumbuiza Tabata kwenye ukumbi wa Dar West uliokua maarufu sana nyakati zile...

Lkn wakati nikiwa back stage kabla sijapanda jukwaani huku usiku ukiwa umetamalaki yaani ule usiku wa manani au usiku wa manane kama wengi tulivyozoea kusema ingawa tunakosea nikashangaa nashikwa begani na mtu aliyekua nyuma yangu ambapo kulikua na watu wengi tu. 

August 24, 2013

MWIGIZAJI WA KIPINDI CHA VICHEKESHO CHA ITV ALIPOTEMBELEA OFISINI, TUKAPIGA GUMZO KIDOGO


Ilinibidi niwe nacheka sana maana kuwa karibu na MKWERE(katikati) ni kituko kikubwa. mwenye shati rangi ya Bluu ni mfanyakazi mwenzangu EZEKIEL TENDWA