Showing posts with label urafiki. Show all posts
Showing posts with label urafiki. Show all posts

February 14, 2018

HARUFU YA PILAU LA MAMA BONI ILIWAVUTA ASLAY NA NANDY.

NA HONORIUS MPANGALA
Ni mwendo wa Kilometa 30 kutoka Mlandizi ili ufike Kijiji cha Matimbwa. Pia ni kilometa 8 ukitokea Bagamoyo Mjini ili ufike hapo kijijini. Ilinichukua masaa yasiyo zidi manne kutoka Morogoro hadi nafika kijijini hapo. Yawezekana ikawa ni jina la kijiji ambacho wengi wao wasiweze kukifahamu kama ilivyo Msata katika wilaya hiyo ya Bagamoyo. Ni eneo la jimbo la mheshimiwa Shukuru Kawambwa. Wakazi wake wengi wakiwa Wazaramo,huku Wakwere nao wakiwepo kwa kiasi.
Nyumba mojawapo iliyoko katika video ambapo Nandy kaonekana kaegemea kwenye ukuta huku akiimba
Wakati napanda gari Mlandizi wenyeji wangu Mathayo Venance na Saidi Zimbwe wakanipa maelezo shukia kituo cha Matimbwa Magengeni. Nilikuwa na shauku ya kuijua Matimbwa na Bagamoyo kwa kweli na nilifika salama na kufanya kazi yangu vyema. Jambo kubwa ninalotaka kuwajuza sio mimi nilisafiri vipi kufika huko. Bali nataka nikupe umaarufu wa Matimbwa ambao hata mtayarishaji wa picha mnato Hans Cana autambue vyema.

Ni katika picha mnato ya wimbo wa ‘Subakheri mpenzi’ ulioimbwa na Aslay na Nandy ulimfanya mtayarishaji Hans Cana awapeleke Kijiji cha Matimbwa na kufanya video huko. Kama umjuavyo msanii Aslay huwa mtu wa kupenda picha mnato ambazo hupendwa na watu wa viwango vyote vya Maisha. Hupenda kufanya video akiwa kijijini na huvaa uhusika haswa uhalisia Wa mazingira. 
Pikipiki iliyotumika katika wimbo wa Subakheri Mpenzi

February 01, 2018

MARA PAAP! NAHODHA WA AZAM F.C ANAPOKUTANA NA MHARIRI MSAIDIZI WA BLOGU HII

Himid Mao akiwa na Kizito Mpangala

January 04, 2018

ZAWADI YA MWAKA MPYA 2018! KITABU

Adella
ADELLA ABELL ni mtani wangu. Jirani yangu nyumbani. Sahibu wangu. Dada yangu. Ni msomaji mzuri wa vitabu. Katika kuanza mwaka mpya amenipatia zawadi ya kitabu hiki chenye masimulizi ya visa, mikasa, kesi,upelelezi na hukumu mbalimbali zilizowahi kutolewa na mahakama ndani na nje.
Mojawapo ya mkasa uliomo kitabu ni ule wa familia ya George Liundi, mkewe Doris Liundi na watoto wao (Nadhani wengine wamewahi kusikia masimulizi ya maisha ya Taji Liundi).

November 20, 2017

KONGAMANO LA KUMBUKIZI YA FIDEL CASTRO


Jukwaa la Wajamaa Tanzania, Taasisi ya Usomaji na Maendeleo "Soma" na Rastafarai United Front wanashirikiana kuandaa kongamano la kumkumbuka El Commandante Fidel Castro siku ya Jumamosi, tarehe 25/11/2017. Mahala itakuwa kwenye ukumbi wa Soma Book Cafe; na muda ni saa 7 mchana hadi saa 12 jioni.
WOTE MNAKABISHWA. HAKUNA KIINGILIO!
"Mwambie Comrade amwambie Comrade"

November 10, 2017

ZAWADI YA VITABU

Zawadi ya vitabu niliyopewa na Molio Baldwin. Asante sana rafiki
Mimi na Molio Baldwin ni marafiki Facebook. Tumetimiza miaka mitano ya urafiki wetu kwa kufanya kitu tofauti. Sote ni wapenzi wa kusoma vitabu. Badala ya maneno ya pongezi tuliamua kununuliana vitabu vitano kadiri ya umri wa urafiki wetu. Leo nimepokea zawadi yangu ya vitabu (pichani). 

October 26, 2017

MWALIKO; WOTE MNAKARIBISHWA KWENYE MJADALA HUU


October 21, 2017

TABASAMU NA KITABU


Ragin Mmbanga (kushoto) na Markus Mpangala (Kulia)
Huyu ni rafiki yangu. Anaitwa Ragin Mbaga, ila tuwapo farashani hupendelea kumwita "Mzee wa bustani ya usomaji". 

September 18, 2017

WAKIMBIZI WA BURUNDI WAREJEA KWAO


Maofisa wa uhamiaji wa Burundi wakiwapokea wakimbizi wa nchi hiyo waliokuwa wakiishi Tanzania.


 PICHA; Honorius Mpangala

August 15, 2013

NIKIWA NA MARAFIKI KWENYE MKUTANO WA KUNDI LA WAZO LANGU


June 03, 2013

RAFIKI MWEMA NA UPENDO

Umemuona huyu, Anaitwa Tamu, Ananoga kama ulivyo Utamu. Ana upendo Mtamu. Tabia yake Tamu, Hisia zake Tamu, Akili zake Tamu, Mambo yake Matamu, Maisha yake Matamu, Mwendo wake Mtamu, Alipata malezi Matamu, Kazi zake Tamu, Uwezo wake Mtamu. ....... Ushajua UTAMU ni nini? Una uhakika URAFIKI sio Mtamu kama ilivyo Tamu yenyewe?

December 29, 2012

SIKU NILIPOHOJIWA NA DANIEL R. GINGO


Daniel Gingo akionyesha moja ya kitabu alichoandika.
NB: Wiki kadhaa zilizopita rafiki yangu huyu aliamua kujadiliana nami jambo muhimu kuhusu sekta ya habari hapa nchini. Haya ndiyo tuliyoongelea japo kwa ufupi kutokana na muda mchache. Karibuni........
DANIEL GINGO: Kuna huu mfumo ambao vyombo vyetu vinautumia kutuhabarisha habari za Ulimwengu kwa mfano: Gazeti la The Gurdian, linaweza likawa na kurasa hata sita zilizosheheni habari kutoka Reuters, BBC, UPI, AP na Xinhua ya China.
TBC: inaweza kusheheni habari kutoka RT au Al-Jazeera, ITV inaweza ikawa na habari za CNN, BBC, na vipindi kibao ambavyo hatujavitengeneza hapa nchini, na wakati mwingine tunavilipia. Je, mfumo huu unavinufuaisha vyombo vyetu vya habari au tunakuwa victims?
MARKUS MPANGALA: Nadhani kila TV inakuwa na makubaliano na kituo cha nje. Kuna mikataba ya kurusha matangazo baina ya TV zetu na za nje.
Kama STAR TV na DW. .....kimsingi hii ni moja hasara kubwa tunayopata katika sekta ya habari na jamii yetu. Sababu CNN, DW, BBC, RT na wengineo hawana muda wa kuonyesha vipindi vya TV zetu.
Hili ni tatizo kubwa sana nadhani TCRA inatakiwa kuwa na mchakato wa kupiga marufu au kupunguza muda wa vipindi vya TV za nje. Channel Ten wao wana SKY NEWS.
Kwa kweli ni hasara sababu badala ya kumuonyesha mkulima wa kisasa sisi tunaonyesha Beckham akiwa mitaa na watoto wake.
Kwa kweli mimi hata DIRA YA DUNIA nimeshindwa kukiangalia sababu malengo ni yale yale kuwa afrika chafu na makamasi.
DANIEL GINGO: Hasara inakujaje kwetu hapo?
MARKUS MPANGALA: Kwanza, tunapoteza nafasi ya kuhabarisha habari nyingi za kwetu. Pili, tunashindwa kuzitangaza habari zetu kupitia hao hao tunaokubaliana nao kurusha vipindi vyao.

Markus Mpangala katika tafakari zaidi kabla ya kujibu maswali.
DANIEL GINGO: Na wao wanafaidikaje?
MARKUS MPANGALA: Lazima tuchukue nafasi ya kuonyesha mambo ya kwetu, sio kuhamisha tu ya nje na kuyaleta.
Kwa mfano kama TV inakuwa na saa 4 za kuonyesha mambo ya Russia. je Russia wanatumia saa ngapi kuonyesha ya kwetu?
Kwa maana nyingine sisi kazi yetu ni kubebeshwa tu habari za CNN, BBC na kuzirusha huku, lakini wao hawana muda na habari za mkulima wa viazi kule mbeya.
DANIEL GINGO: Tena wakati mwingine tunazipokea bila hata kuzihariri, zikiwa za uongo wanazirusha hivyo hivyo. Nikuulize swali la nyongeza?
MARKUS MPANGALA: Na ukweli kabisa huo. Ili kupunguza lazima TCRA ichukue hatua, wengi wanadhani China ni wajinga kuzuia CNN, BBC, Facebook na mengine kujaza habari zao kule China. Lakini naona walikuwa na hekima zaidi. Siku hizi habari zingine mbovu kabisa kwenye hizoTv za nje basi tu.
DANIEL GINGO: Lakini. Ikiwa TCRA watafanyia kazi ushauri huo, unadhani tunaweza kumudu kujaza nafasi zilizoachwa wazi na CNN, BBC, Hollywood nk?
MARKUS MPANGALA: Tunaweza kabisa. tunayo mambo mengi nchi hii hayatangazwi. Mfumo wetu wa habari bado unategemea, sio kujitegemea kuendesha mambo.
Ninaposema kutegemea ni ile hali ya kungojea matukio au habari fulani, badala ya kujitegemea kwakuwa na vipindi vingi vyenye tija kwa taifa.
Nina uhakika CNN au nyingine haiwezi kuwa kila kitu nchini. Hakika nakuambia, tunaweza kuwa na habari nyingi iwapo vyombo vyetu vya habari vitaanza kujitegemea.
DANIEL GINGO: Ninamaanisha hivi: Je, vyombo vyetu vya habari vina pesa na nyezo za kutosha kwenda Rubili kule Kagera, Rusumo kule Ngara, Kizorogoto kule Morogoro, Makiungu kule Singida, Kilindi kule Handeni, Kerenge kule Korogwe nk kwa ajili ya ku-cover matukio?
MARKUS MPANGALA: Naam ndio maana nimesema vyombo vyetu vinaendeshwa kwa Kutegemea sio Kujitegemea. Kwahiyo kujitegemea ni kama hivyo unavyosema, je vitaweza kwenda ku-cover story kule? Mimi nadhani inawezekana, na kilichokosekana ni msukumo.
Hawa Mwananchi kuna mtindo fulani wanaufanya kwa upande wa magazeti yao. Wana kitu fulani wanakionyesha lakini najua inahitaji gharama sana.
Hata hivyo ukitaka kuleta ufanisi katika vyombo vyetu lazima bajeti zao ziwe za kutosha kwa kuwekeza kwa ku-cover story sio posho na mengineyo. Tulichokosa ni Dhamira. Matokeo yake, Tunajikuta tunategemea tu.

October 27, 2012

NYUMBANI LUNDU

Picha hii inaonyesha maeneo ya kijiji cha Lundu. Maeneo hayo ni mtaa wa Maliwa au Missionari, na wka upande wa magharibi kushoto unaonekana mlima ambao unaitwa Chipyaghela. Kisha maji ya ziwa Nyasa yanaonekana. Huu ndio mji ulionikuza na kunilea, katika mitaa yangu ya Maliwa, au missionari.
Picha hii imepigwa na kaka Egbert Jeremy aliyeko wilaya ya Nyasa katika shughuli za ujenzi wa miundo mbinu. Lundu ni miongoni mwa vijiji ambavyo anaendelea kujenga miundombinu ya wilaya hiyo. Karibuni kuwekeza wilaya ya Nyasa ambayo imeanza kutoa fursa mbalimbali. KARIBUNI NYASA

October 22, 2012

NAFASI YA KAZI OKTOBA 18, MWISHO OKTOBA 31, 2012

Kwa wale wanaohitaji nafasi za kazi katika Sekretarieti ya AJIRA nchini. Wanaweza kuangalia nafasi ya kazi katika tovuti ya sekretarieti hiyo kwa ku-dowloand tangazo zima;

SOMA HAPA

May 25, 2011

KOERO U MZIMA, HONGERA SIKU YA KUZALIWA

Ni asubuhi na mapema, baada ya kujiweka sawa kwa kutoa jasho kidogo naamua kukaa kwenye kompyuta.
Huku nikiwa bado nahema kutokana na na kuweka afya vema ili kuanza siku.
Baada ya hapo najipa dakika ya kuipa upendeleo blog ya  VUKANI kwasababu nilijua ndiyo siku ya Koero Binti Mkundi kuzaliwa, nilitaka kuona ametuletea tunu  gani.
Hata hivyo nilichokiona baada ya kusoma nilibaki na simanzi. Uvumilivu ukanishinda machozi yakanilenga, mwili ukasawajika. Harara ya kuwasiliana na wadau wa VUKANI ikaanza.
Na kwakuwa nilikuwa kasi mno kuwahi majukumu, nikamuomba kaka Kaluse yapata saa moja hiyo asubuhi asome Blog ya VUKANI.
Nikamweleza na mtani wangu Fadhy, asome VUKANI.  Nilipokuwa naandika maoni, ghafla Waziri Ngeleja na Tanesco wakachukua umeme wao, ikabidi nisubiri mgawo.
Nikiwa naelekea kwenye majukumu, yapata saa mbili na dakika 29 asubuhi mtani wangu Fadhy alinijulisha atasoma VUKANI aone kuna nini.
Lakini nikamwomba anipe mawasiliano ya ya simu binti Mkundi kwakuwa namba niliyonayo kwa kweli inaninyima raha, simpati Koero.
Mtani wangu Fadhy akasema hana. Yapata saa 6 na dakika 10 mchana, Kaka Kaluse ananijulisha, “Nimesoma kaka. Imenigusa sana”.
Hakika Koero alinigusa hata mimi sio Kaluse peke yake, na Mtani wangu Fadhy. Nilijua Dada yangu kipenzi Yasinta atasoma mapema tu.
>>>
Koero u mzima,
Tatizo hakuna,
Ni shida ndogo,
Wala isikupe kihoro,
Mwaka 2009 mimi,
Mshituko nilipata,
Daktari akasema,
Markus dar haikufai,
Hukuugua masikio,
Leo yamekusibu,
Kubali hilo,
Nikasema si tatizo,
Bali uwezo umepungua,
Wala sihitaji kifaa,
Kwani naweza kuwasiliana vema,
Ila kuna wakati yanauma,
Yanapunguza uwezo kusikia,
Kama homa ya vipindi,
Nimeshazoea mimi.
Koero ijali afya,
najua umekubali hali,
Hadi leo umetuambia,
Imenigusa mno,
Imewagusa wengi hapa.
Mzee wa Lundunyasa anasema,
Koero tuko pamoja kwa shida na raha.
Tena umekuwa sehemu ya furaha ya wanablog,
Hongera mzee Mkundi
Kutuletea binti Mjuzi,
Mwenye vipaji pomoni.

January 24, 2011

KUFIKIRIA KULA UGALI NA HARUFU YA SAMAKI!!

Yasinta naye kwa mitego,
Yasinta kwa mapozi yupo,
Yasinta kwa faraja yupo,
Yasinta kwa malezi wamo,
Yasinta kwa miondoko, ipo,
aaah!! rafiki yangu nawe umo,
Na kwakuwa umo, basi nao wamo,
Ngoja, katika kufikiria kula ugali na harufu ya samaki Mbasa! Lol!
Shukrani kwa picha Blogu ya  MAISHA NA MAFANIKIO pamoja na VANGONI

January 13, 2011

NIPO SANA

KUNRADHI WAUNGWANA. INAONEKANA NAKOSA ADABU KWA KUTOTOKEA HAPA DIMBANI KWANGU, LAKINI PILIKA ZA JANUARI ZIMENISHIKA. NITARUDI PUNDE. POLENI RAFIKI ZANGU MNAONITAFUTA KUPITIA SIMU, UKWELI HATA SIMU SIJIHUSISHI NAYO. TUTAKUTANA KATIKA BARUA PEPE. NITARUDI NGOJA NIUSAKE UANAZUONI ZAIDI.

NAWAPENDA SANA, NAAMINI NINYI MWANIPA FURAHA

December 23, 2010

SIKUKUU NJEMA WANABLOGU WOTE WAHUSIKAO

Ningelichagua neno jema, basi lingekuwa AMANI  IWE NANYI. Kama ningelichagua neno baya basi ni WEWE MWANABLOGU UKIUGUA SIKU HIYO. Nawatakia mafanikio zaidi na Imani yangu iwe nanyi.
TULIPOKWARUZANA tuseme kwa pamoja. UPENDO ni jambo muhimu sana.
nakuambia neno hili la sikukuu. MIMI NINAHITAJI SANA UWEPO WAKO WEWE MWANABLOGU. BILA WEWE NISINGELIKUWEPO HAPA KUBLOGU.

December 02, 2010

PILIKAPILIKA HAZIKOMI

Julia Salmi& Mzee wa Lundunyasa
Julia Salmi,Mzee wa Lundunyasa na Leon Sambala
ni pale TaSUBa, Bagamoyo katika pilika za utamaduni na mishebeduo anuai.

August 04, 2010

TANGAZO LA NIA????

usiniulize, angalia tu

Kama unaweza kubaini hebu niambie hawa ni nani? Na je ni Tangazo la Nia au? Hii ilitokea pale hoteli la kibepari karibu na nyumba ya sanaa. Linaitwa Moven-kilele a.k.apeak a.k.a pick ilikuwa ijumaa iliyopita. Je ni tangazo la nia??? ha aha ha ha ha ha ha ha Nimewakamataaaaaaaaaaaaaa

July 17, 2010

NIKUPE NINI?

Nikupe nini ewe rafiki? Nifanye nini kwako rafiki mwema, usiyeficha msimamo wako na kukataa kile kisichokuwa chema? hakika wajua thamani ya urafiki, wajua thamani ya ukweli na upendo kwangu, Nitakupa nini rafiki yangu? Mangapi yangu yamesemwa na ukaambiwa lakini hujanificha?

Nifanye nini maana bado najiuliza kila siku? Najua tumetofautiana mara kadhaa lakini uzuri tunajadili yanakwisha. Najua habari kadhaa zangu umezipata na pengine unashindwa kunielewa misimamo yangu kadhaa. Lakini uzuri wajua tabia,mwenendo,misimamo,mitazamo na hadidu zangu za rejea.

NIKUPE nini ewe rafiki yangu? Sema sasa nijuwe maana kusubiri nishachoka nisije nikawa MVUMILIVU HULA MBOVU. Wajua ni kwanini tumekuwa hivi, wajua ni ukweli,bila simanzi, ni upendo na uwazi. Aaah! nitakupa nini ewe mwema. Naamini mungu ajua yakuwa twajua kwamba kiasi cha mambo tuyajuayo ni sehemu ya kujua tu ingawa pia hakutoshi kuyajua.

Asante rafiki kujibu hata maswali yaelekezwayo kwako lakini yanihusu mimi. Yote tisa naweza kukuita hakimu mzuri kwa kuhukumu vizuri  bila upendeleo Lol.... You know what it is rafiki. Daima umesimamia ukweli. Nakupenda sana rafiki yangu. Hivi ni nani atakaye tutenganisha? au huyu Mungu? ataweza kweli maana ananiogopa kila siku...... Lol

Napenda staili ya urafiki wetu mama, naamini ni ndugu sana kwa mengi mema. Zaidi nimeipenda picha inanikuna sana. JE URAFIKI UNASOMEWA DARASANI AU CHUO KIKUU? Thamani yeru ya urafiki ni pale tunapotazamwa kwa tofauti kumbe walaaaaaaa! Mungu mkubwa! THE SAME DRAMA