Mchoraji Nathan Mpangala.
Showing posts with label katuni. Show all posts
Showing posts with label katuni. Show all posts
January 29, 2014
KATUNI ELIMISHI KWA WANANCHI
Madhumuni
katuni,
kumbukumbu
November 13, 2008
kipindupindu kiingie ikulu

sikujua uchungu, sononeko la moyo
akili yagota kwangu, moyoni harijojo
ghadhabu yanisibu,adhuhuri si kikomo
dibaji ya nini,uchafu mitaani?
kila leo twaumwa,vichomi na kuhara
miili yatuuma,akili nayo yagoma
maji haba salama, twanywa ya visima
dibaji ya nini uchafu mitaani?
kipindupindu chapindua,kinyesi kuwa maji
mwili kukongoroka,acheni dhihaka jamani
kila leo twanya uharo, ikulu vipi?
dibaji ya nini,uchafu mitaani
kipindupindu ikulu,napenda kitinge
waharishe wakuu,nasi tupumzike
aghalabu isiwe vigumu, wanye uharo preeee
wakome na kuona mashudu,wanune au wacheke?
dibaji ya nini,uchafu mitaani
ngoja kipindupindu kiingie ikulu
ooooh alamsiki waungwana wema
June 29, 2008
Sitaki Ushahidi....Je ndivyo Ilivyo?
Naandika haraka haraka leo nina mpango wa kwenda kuogelea mpaka usiku kwani kila siku natumbukia tu kidogo lakini leo ni kuogelea kwelikweli.Mmmm sasa ebu tazama katuni hiyo halafu fikirisha ubongo wako.Jaribu kujenga picha ya watoto yatima kisha fikiria wanaolea watoto hao halafu jaribu kuyafikiria mahitaji ya kiuchumi yaani kipato cha maisha.Sitaki kutoa jawabu ila jaribu kutafakari.KWA HERI mimi sitaki ushahidi lakini ndivyo ilivyo?.Ooo sijasahau...karibu sana kaka Mbilinyi katika gazeti hili la nyasa.....karibu ule vitoweo vitamu......Jamani nakwenda kuogelea webnzangu wameshaanza ona waleeee..huwaoni?utajiju..
April 14, 2008
Mitandao Imetekwa Nyara,Kaa Chonjo!!
Nimejikuta nikishindwa kuangua kicheko,yaani nimecheka mpaka jamaa hapa pembeni ninavyoandika akajiuliza hili jamaa vipi?Unajua kwanini?Kipindi hiki hapa nyasa kuna dhoruba kaqli mawimbi yanapiga toka upande wa kaskazini kwenda kusini,basi wanyasa wanaona hii kero,lakini hawajaacha kuvua samaki shauri ni kitoweo chao.Basi jamaa kanishtua hapa nyasa anahisi harufu ya kutekwa nyara mitandao ulimwenguni kwahiyo wanaoblogu na wenye tovuti wawe makini.Nikabisha sikubali bila kuona,lakini nikakumbuka kublogu mpaka niingie mjini Mbinga,Looh! nikakumbuka jambo nililosoma kwa Mwalimu wangu Ndesanjo Macha pale jikomboe.Kumbe jamaa ananishtua hilo wakati nilikuwa nalo kichwani kitambo.Ni Hivi hakika mitandao imetekwa nyara kila anayeblogu akae chonjo saa ya hatari lakini kwa wanyasa tunaweza kujificha ndani ya maji lakini usiulize tutapaje pumzi...sawa..?.Mmmh!!utajuaje kama natania?Jamani mnamkumbuka yule mwizi wa kura za haki kule Kenya?Juzi hapa kateua mawaziri 44 nadhani hii sherehe ya kutafuna mali,basi kateka nyara mtandao; bonyeza hapa http//www.twitter.com/MwaiKibaki,ngoja nisubiri majibu yako..
March 19, 2008
Machi Mwaka 2002;Yasinta Kwanini,kisa kinaendelea.
Nimerudi na kisa kileee kinachonihusu pengine zaidi ya kunihusu na kinawahusu wengine,mimi sijui.Hebu ngoja nikiandike tena hapa maana siyo mimi labda wengine kinawahusu.Mwezi machi 2002,Yasinta katoroka kwao,kamkimbia baba,mama na nduguze,wala hataki kusema anakokwenda.Nyumbani wazazi wanashangaa mwenetu tumpendaye kaondoka bila kuaga ni maajabu hayo.Yasinta katua Mbinga mjini,katulia stendi na raifikiye Vumilia wanapiga soga za hapa na pale lakini hatimaye mnyasa anatokea,ana-afro, katweta ghafla anajiuliza huyu binti vipi?Haya soga za hapa na pale wanakumbushana na mnyasa enzi wakiwa shule,lakini mnyasa anauliza kulikoni upo hapa? mara ghafla Yasinta anaomba "tafadhali ukiulizwa kuhusu kuniona mimi{yeye}usiseme".Mnyasa anashangaa kumbe binti katoroka nyumbani kumfuata mpenzi?Jamani kupenda tabu,mapenzi ni kikohozi kuficha huwezi aliimba Fresh Jumbe.Binti amependa hataki shule hataki kusikia maonyo ya wazazi,masikio kaziba pamba,mahaba yamekolea, lakini kwakuwa mnyasa anamjua vema akasaili hee mwenzangu nimesikia hutaki shule kulikoni?Sipewi jibu, nazungushwa huku na huko binti anajiona kumaliza kidato ni mwisho hakuna tena hamu ya shule kisa mapenzi mmh.Mwishowe mnyasa anashauri vipi uahirishe safari,looh.. akaambiwa alipe nauli aliyolipia tiketi kisha awezekuahirisha safari,mnyasa akaduwaa akasema huyu siku hizi kawa mbogo wa mapenzi.Lakini kwani mnyasa akawa anajua hapa anapenda lakini kwa mtindo huu acha ajifanye hana hizo hela,unajua shilingi ngapi?Watu wa Mbinga wanajua wakati huo nauli mpaka makao yetu makuu Songea ni....samahani sitasema.Binti anasafiri anakwenda kuonana na mpenzi wake,waubani wake, mwandani wake,yaani ampendaye.Mmh wapi bwana yako wapi hayo mapenzi mathubuti?kuna kuacha shule tena?Mbona yupo huko.......kwenye baridi anasoma,sijui kwa ari au ndiyo wasomi wetu wa siku hizi.Kifupi alicharukia mapenzi,akaona ganda la mua la jana........na masikitiko ya mnyasa kwa kuwa alimpenda basi katoa kauli za kulaani na bado zinamtesa,yako wapi mbona bado kasheshe inaendelea?Maisha ya Lundo yalikuwa ni simulizi murua.Ngoja nikomee hapa kwa leo.
Madhumuni
katuni,
kumbukumbu,
lundo,
Nyasa,
soga
September 13, 2007
Katuni Nazipenda sana
Kuna katuni zinazochorwa wakati mwingine zinaweza kukufanya uwe na munkari a kufikiri.
kwani wachoraji wake wanaweza kuchora picha ambazo ni kama habari nzima za za magazetini kwa siku nzima.
kuna katuni za Simon Regis,Masudi Kipanya na Nathani Mpangala.Hawa jamaa wananifanya niwaone kama wanahabari wasioandika chochote bali wanakupa mchoro kisha sentensi moja baadaye tafakari mwenyewe.
Hoja yangu ni kwamba michoro ina habari tamu kuliko habari za uwongo za vyombo vya habari.
Namaanisha kwamba habari lazima ziwe na maudhui ya kuwafanya watu wapate maarifa si habari zinazosifia vigogo na uharamia wa kicheko kama ni ngonjera njema.
MUHIMU; Nitawaeleza habari kutoka nyasa kwa kila kijiji cha mwambaoni humo hususani mkoa wangu wa ruvuma na wilaya yangu ya Mbinga jimbo la Mbinga magharibi.
twende pamoja maana nisera yangu kuu kuhusu nyasa
kwani wachoraji wake wanaweza kuchora picha ambazo ni kama habari nzima za za magazetini kwa siku nzima.
kuna katuni za Simon Regis,Masudi Kipanya na Nathani Mpangala.Hawa jamaa wananifanya niwaone kama wanahabari wasioandika chochote bali wanakupa mchoro kisha sentensi moja baadaye tafakari mwenyewe.
Hoja yangu ni kwamba michoro ina habari tamu kuliko habari za uwongo za vyombo vya habari.
Namaanisha kwamba habari lazima ziwe na maudhui ya kuwafanya watu wapate maarifa si habari zinazosifia vigogo na uharamia wa kicheko kama ni ngonjera njema.
MUHIMU; Nitawaeleza habari kutoka nyasa kwa kila kijiji cha mwambaoni humo hususani mkoa wangu wa ruvuma na wilaya yangu ya Mbinga jimbo la Mbinga magharibi.
twende pamoja maana nisera yangu kuu kuhusu nyasa
Madhumuni
katuni
Subscribe to:
Posts (Atom)