Showing posts with label uchambuzi. Show all posts
Showing posts with label uchambuzi. Show all posts

March 16, 2018

FURAHA, EASTERLIN PARADOX NA MARIANO ROJAS

NA EZEKIEL KAMWAGA
 
JANA, ripoti kuhusu utafiti wa kimataifa ulioonyesha kwamba nchi yetu ina hali mbaya kwenye kigezo cha furaha kwa watu wake ilizua mjadala wa aina yake. Kuna walioupinga utafiti huo moja kwa moja kwa hoja kwamba ziko nchi zina vita wakati huu na haiwezekani wananchi wake wakawa na furaha kuliko sisi. Wengine wakapinga tu kwa sababu huwa wanapinga. Wengine wakaunga mkono kwa sababu za kisiasa tu.

Kitu kikubwa ambacho nilikiona jana ni kwamba wengi wetu tulitoa maoni kabla hata ya kuisoma ripoti yenyewe. Na hili ndilo tatizo kubwa ambalo wengi wetu tunalo. Tunapenda kutoa maoni katika mambo ambayo ufahamu wetu ni mdogo sana. Nafurahi kwamba nilijipa muda kuisoma ile ripoti jana. Hapa chini ni mawazo yangu baada ya kuisoma. Nimeyagawa mawazo yangu katika pande mbili tofauti; kabla ya kuisoma ripoti hiyo na baada ya kuisoma.

KABLA YA KUISOMA
Mimi ni muumini wa dhana kwamba furaha ni jambo gumu sana kulipima kwa mwanadamu. Nimewahi kuandika humu mitandaoni kwamba kuwa na furaha si jambo unaloweza kulipima kwa sababu ya wingi wa mali au marafiki.

February 02, 2018

UCHAMBUZI WA KITABU: DIWANI YA SIWACHI KUSEMA

MWANDISHI: MOHAMMED K. GHASSANI
MCHAMBUZI: MARKUS MPANGALA
NA MARKUS MPANGALA

MWAKA 2017 nilipatiwa zawadi ya vitabu vitano vya ushairi kutoka kwa mwandishi wa habari wa Idhaa ya Kiswahili ya Ujerumani (DW), Mohammed Khelef Ghassani. Vitabu hivyo ni Siwachi Kusema, Machozi Yamenishiya, Kalamu ya Mapinduzi na Adamo. Leo tunachambua diwani ya  “Siwachi Kusema; Uhuru U kifungoni” ambayo imechapishwa mwaka 2016 na kampuni ya Zanzibar Daima Publishing yenye makao yake mjini Bonn nchini Ujerumani. Diwani hii imepewa nambari ISBN 978-15-34660-16-8.


‘Siwachi kusema’ ni mwendelezo namna ya mwandishi huyo ya kusema na kuyasemea yale yanayotokea mbele katika jamii yake. mambo ambayo yanaikwaza jamii hiyo kutokana na sababu mbalimbali. 

Mathalani katika dibaji ya diwani hii mwandishi anasema, “Mwanadamu anayelazimishwa kwasababu yoyote ile kuacha kutoa kauli yake juu ya yale yanayojiri mbele ya macho yake, yale yanayomuhusu na kuyaathiri maisha yake, bsi huyo ni mithili ya mtu aliyezibwa pumzi kwa matambara au mateka aliyetiwa jiti la roho. Huwa si mtu huru, si mtu kamili, si mtu mtu,”(Uk.Xi).

Mkusanyiko wa mashairi uliopo katika diwani hii umegawanyika katika maeneo tofauti. Kuanzia mapenzi na ndoa,ukiwa au upweke wa baadhi ya watu hapa duniani, siasa na haki za binadamu, masuala ya dini, misaada kadhalika.
Tunaweza kutazama mifano hayo katika baadhi ya mashairi. 

Shairi la ‘Mwanangu Nakupe Mke’ (Uk.14) mwandishi anaandika,
“Mwanangu nakupa mke, nakuwekea kikao,

Awe wako uwe wake,wamoja toke oleo,

Basi maneno yashike, na wasia nikupao,

Mkeo awe ni nuru.

January 31, 2018

UCHAMBUZI WA KITABU: "AMEZIDI"

MWANDISHI: SAID AHMED MOHAMED

MCHAMBUZI: KIZITO MPANGALA

AMEZIDI ni tamthiliya iliyopgwa chapa na East African Educational Publishers (Nairobi, Kampala, na Dar es Salaam) ambapo chapa ya kwanza ilitolewa mwaka 1995. Kitabu hiki kimesajiliwa kwa namba za usajili ISBN 9966-46-752-1.

Tamthiliya hii imegawanyika katika maonyesho kumi ya jukwaani ambapo kila onyesho lina ujumbe ambao unailenga jamii ya Afrika kwa ujumla hasa katika suala la maendeleo ya liuchumi, kielimu kijamii na kadhalika. Wahusika wakuu wa tamthiliya hii ni Ame na Zidi. Maonyesho haya yote na tamthilya yenyewe kwa ujumla ni cmhezo wa mawazoni tu!
Ame na Zidi wanajikuta katika umasikini mkubwa katika bahari iliyojaa mali. Katika hali hii ya uhitaji wanatambua kuwa hawana lingine la kufanya ila kuomba misaada ili wayatosheleze mahitaji yao. Msaada unapokuja unaleta madhara mengi zaidi.

Onyesho la kwanza linaonyesha Zidi akiwa anamwamsha nduguye Ame aliyekuwa amelala kukiwa kumeshakuchwa. Zidi anamwonyesha Ame mihogo miwili aliyotoka kuitafuta ili wapate kuila.

Onyesho la pili linaonyesha Ame na Zidi wakiwa katika kasri lao wanalisifia kasri hilo lililojaa samani nyingi kutoka Paris (Ufaransa) na vito mbalimbali pamoja na mazuria kutoka Iran.

January 18, 2018

HAKUNA CHAMA KINACHOENDESHA MAISHA YA MPIGA KURA.

NA HONORIUS MPANGALA, BAHI
NILIPOKUWA mdogo niliamini maisha ni jambo ambalo liko tofauti na la kuogofya sana katika jamii. Sababu kubwa ni pale nilipokuwa nayasikia maneno kama “Usicheze na maisha”. Fikra zangu zilinipeleka kuwa maisha ni jitu linalotisha sana katika jamii.

Baada ya makuzi nikapata misemo kama “Maisha yenyewe ndiyo haya haya” nikaanza kutambua kumbe mwenendo wa kuanzia asubuhi unaamka hadi usiku unaingia kulala hizi harakati zote ufanyazo ndiyo maisha yenyewe.

Katika vipindi ambavyo wapiga kura na wananchi wa kawaida toka vyama vya siasa wanajiona kama na wao ni wenyechama basi ni katika kampeni za uchaguzi. Kipindi hiki kila mwanachama anajiita ni mwenyechama. Ni kipindi ambacho watu hao hudiriki kunukuu maneno ya wagombea wao na kuiaminisha hadhira aliyonayo kuwa chama chetu kitatekeleza mambo kadha wa kadha.

November 08, 2017

MABALOZI WETU WASIWE WAZITO KUJENGA UCHUMI

NA GABRIEL MWANG’ONDA 

RAIS John Magufuli ametimiza miaka miwili madarakani tangu alipoapishwa Novemba 5 mwaka 2015. Miaka hiyo serikali imefanya mambo mengi ambayo si lazima kueleza hapa leo. Lakini itoshe kusema lipo jambo ambalo ninajikita nalo ili kuangazia miaka hiyo. Ni dimplomasia ya uchumi.

Diplomasia ya Uchumi (Economic diplomacy) limekuwa somo gumu sana kueleweka kwa mabalozi wetu. Yaani sisi wengine tumeiimba mpaka tukaona tupumzika tu kwasababu somo limekuwa gumu sana kwa balozi zetu. Binafsi nimeliongelea sana kwenye ma redio nyingi hapa ndani ya nchi na nje pia, lakini ndugu zetu wameamua kutoelewa tu hii dhana kitu ambacho kinaligharimu sana Taifa letu.
Ufukwe wa Ziwa Nyasa mkoani Ruvuma. Ni miongoni mwa vivutio vya utalii.
Kila balozi utakae onana nae ukimuongelesha kuhusu hii diplomasia ya uchumi anasingizia udogo/ufinyu wa bajeti. Lakini hiki kamwe hakiwezi kuwa kikwazo kwa mtu mzalendo mwenye ubunifu alienuia kwa dhati kabisa kuitumikia nchi.

Si mambo yote yanahitaji fedha nyingi kuyafanya kuhusu hii dhana ya diplomasia ya uchumi. Balozi zetu hata utume baraupepe kwa vitu ambavyo ni vya kawaida sana bado hutojibiwa kabisa. 

SASA NAMWELEWA HILARY CLINTON

NA  MARKUS MPANGALA
 
WAKATI wa kampeni za Uchaguzi nchini Marekani mwaka 2016, aliyekuwa mgombea wa urais kwa tiketi ya chama cha Democrat, Hilary Clinton alisema: “Kama mgombea (wanasiasa) anakasirishwa na sentensi moja iliyoandikwa kwenye mtandao wa kijamii basi huyo hafai kupewa mkoba wa nyuklia, maana vidole vyake vitabonyeza wakati wowote,”. 
 
Tafsiri ya Kiswahili ni yangu kwa sababu ninahitaji kurahisisha kueleweka hoja yenyewe. Maneno ya Hilary Clinton yalimlenga mgombea wa chama cha Republican, Donald Trump ambaye alishinda uchaguzi huo baadaye.

Clinton aliamini kuwa kitendo cha Trump kukasirishwa na sentensi zinazoandikwa kwenye mitandao ya kijamii ikiwamo yeye mwenyewe kujibu mapigo au kuwatisha watu, ilikuwa ni ishara ya mtu ambaye hawezi kustahimili ukosoaji au kukosolewa pale anapokuwa kiongozi.

Kwamba ili uwe kiongozi unatakiwa kustahimili au kama wasemavyo wahenga lazima uwe na ngozi ngumu hata kama utapigwa mishale ya kila namna. Hii ndiyo changamoto inayotukabili vijana, viongozi wa kila ngazi na watendaji mbalimbali kwenye vyombo vya uamuzi kwa maslahi ya Watanzania. 

Mara nyingi tumesikia wanasiasa au wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi wakijiapiza kufanya jambo hili au lile. Wengine wanatajwa kuudhika kutokana na maneno kadhaa yanayozungumzwa kwenye mitandao ya kijamii.

Tunafahamu kuwa ipo sheria ya mtandao na maudhui, ambapo inalenga kudhibiti nidhamu pamoja na kukabiliana na “hatari” yoyote inayoitwa kama udhalilishaji (Cyber Bullying), matusi na hulka mbaya dhidi ya viongozi au watu wa kada mbalimbali. 

Lakini katika kipindi hiki kuna jambo limenishangaza. Nashangaa kuona wanasiasa wetu nchini wanakasirishwa na ‘status’ zinazondikwa huko Facebook, Twitter, Instagram na kwingineko. 

UCHAMBUZI WA TAMTHILIYA YA BLACK MAMBA

KITABU: BLACK MAMBA
MWANDISHI: JOHN RUGANDA
MCHAMBUZI: KIZITO MPANGALA.

Black Mamba ni tamthiliya iliyoandikwa na John Ruganda kutoka nchini Uganda. Namba za usajili ni 978-9966-46-378-X na kuchapiswa na East African Educational Publishers. Kina jumla ya kurasa 70 tu. Wahusika wa tamthilya hii ni Profesa Coarx (kitivo cha sosholojia), Berewa mfanyakazi wa Profesa Coarx, Namudd mke wa Berewa, Odiambo mwanafunzi wa shahada ya kwanza ya Sosholojia, Catherine Smith mkufunzi mpya kitivo cha Sosholojia, Ofisa wa Polisi na msaidizi wake. Na mhisika msaidizi ni Namatta ambaye ni kahaba. 

October 27, 2017

KWANINI WILAYA YA NYASA IMESHIKA MKIA KATIKA MATOKEO YA DARASA LA SABA?



RAYMOND NDOMBA, SONGEA
WILAYA ya Nyasa iliyopo mkoa wa Ruvuma imekuwa ya mwisho katika matokeo ya darasa la saba mwaka huu 2017 kimkoa. Swali la kujiuliza ni kwanini hali hiyo imetokea. 


Mawazo yangu ni haya; Pamoja na sababu nyingi zilizosababisha matokeo hayo ya aibu kubwa. Wazazi wanapaswa kubeba lawama kubwa. Wengi wao hawafuatilii maendeleo ya watoto wao, pia makuzi na malezi mabaya.

Miaka ya hivi karibuni (kuanzia mwaka 2000), Wazazi wengi katika wilaya ya Nyasa hawajali elimu, hawajigusi katika ufuatiliaji wa watoto wao kielimu na hata kitabia (Angalia matokeo ya mitihani ya Taifa ya shule za msingi na sekondari kunzia miaka hiyo ya 2000 kwa shule kongwe ndani ya wilaya). 

WAAMUZI WA SOKA KATIKA JICHO LA JAMII.

NA HONORIUS MPANGALA
 
WAAMUZI wa soka wamekuwa wakitazamwa tofauti kulingana na wao wenyewe wanavyojiweka katika jamii ya wapenda soka. Wako ambao wameifanya fani hiyo kuwa moja ya vitu ambavyo vinaweza kuwapatia nafasi ya kucheza matangazo. Pia wapo ambao jamii imewachukulia tofauti kutokana na mitazamo yao.
Jonasia Rukyaa.
Kuna mitazamo hasi kwa baadhi ya wapenda soka waonapo waamuzi wa kike wakichezesha mchezo. Mitazamo hiyo inatokana na asili ya mchezo wenyewe unavyochukuliwa kama ni wa wanaume. Licha ya wanawake kuucheza lakini bado mitazamo hiyo imekuwa ngumu kuwatoka baadhi ya wapenda soka. Ndo maana hata wale wanawake wanaocheza soka ukiwatazama utafikiri wanaume Kwa baadhi yao.

Tanzania ina Mwamuzi wa kati maarufu Jonasia Rukyaa ambaye anafanya vizuri sana. Alikuwepo katika mashindano ya Afcon ya wanawake ikiyofanyika Kameruni. Pia baada ya kushiriki katika kliniki ya waamuzi Kule Ureno mwaka huu amekuwa na mwaliko 'appointment' ya uwepo katika kombe la dunia. Na yupo katika mshindano ya kombe la dunia la vijana wa chini ya miaka 17 Iliyofanyika India. 

October 16, 2017

“RAIS ANA MIAKA 31”


Sebastian Kurz
JUMAMOSI nilikuwa nasoma makala ya James Masters kwenye tovuti ya CNN. Sentesi yake ya kwanza ilinivutia sana, “Ulikuwa unafanya nini ulipokuwa na umri wa miaka 31? Ingawa aliendelea na mengine lakini staili pekee haikuwa kivutio bali mtu aliyekuwa akizungumzwa alivutia zaidi.
James Masters alikuwa anamzungumzia Sebastian Kurz ambaye amewahi kuwa waziri wa  Ushirikiano wa Kimataigfa tangu mwaka 2013 akiwa na miaka 27.  Sebastian  Kurz ambaye amekuwa Kansela wa Austria mwenye umri mdogo zaidi kwani sasa hivi ana miaka 31 tu. 

Ni mwenyekiti wa chama cha  OVP. Sebastian kuanzia jana jumapili aanaongoza serikali ya Austria ( kama vile Rais hapa kwetu) baada ya chama chake kushinda viti vingi vya bunge. 

December 18, 2012

AIBU NA KASHFA KWA TANZANIA NA KENYA

Kuna taarifa huko Hong Kong kukamatwa kwa meno ya tembo kutoka Tanzania na Kenya.
Katika hali inayoshangaza juu ya idara zetu za uhamiaji, pamoja na ulinzi wa rasilimali zetu, ni wazi tunahitajika kufanya mapinduzi makubwa juu ya kulinda mali zetu.
Hii ni moja ya jambo linalosumbua akili za wananchi kwani haiwezekani tukakosa uadilifu kiasi cha ksuhindwa kulinda mali zetu.   Najiuliza tu, tuombe ile kesi ya wahusika ifike mahali pazuri kwa kuwatia hatiani.

SOMA HAPA ZAIDI KUJIKUMBUSHA

October 27, 2012

NYUMBANI LUNDU

Picha hii inaonyesha maeneo ya kijiji cha Lundu. Maeneo hayo ni mtaa wa Maliwa au Missionari, na wka upande wa magharibi kushoto unaonekana mlima ambao unaitwa Chipyaghela. Kisha maji ya ziwa Nyasa yanaonekana. Huu ndio mji ulionikuza na kunilea, katika mitaa yangu ya Maliwa, au missionari.
Picha hii imepigwa na kaka Egbert Jeremy aliyeko wilaya ya Nyasa katika shughuli za ujenzi wa miundo mbinu. Lundu ni miongoni mwa vijiji ambavyo anaendelea kujenga miundombinu ya wilaya hiyo. Karibuni kuwekeza wilaya ya Nyasa ambayo imeanza kutoa fursa mbalimbali. KARIBUNI NYASA

October 22, 2012

NAFASI YA KAZI OKTOBA 18, MWISHO OKTOBA 31, 2012

Kwa wale wanaohitaji nafasi za kazi katika Sekretarieti ya AJIRA nchini. Wanaweza kuangalia nafasi ya kazi katika tovuti ya sekretarieti hiyo kwa ku-dowloand tangazo zima;

SOMA HAPA

October 18, 2012

TANGAZO LA USAILI KWA WAOMBAJI WA KAZI SEKRETARIETI YA AJIRA NCHINI

Serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania inawatangazia wote walioomba nafasi za kazi wanatakiwa kwenye USAILI ifikapo tarehe 25 oktoba hadi tarehe 02 Novemba, hizo zitakuwa siku za usaili kwa waombaji nafasi za kazi.

TAARIFA ZAIDI SOMA HAPA

July 21, 2010

MAKALA MPYA; TANZANIA; Azimio la Arusha na miluzi ya ubepari

TANZANIA; Azimio la Arusha na miluzi ya ubepari (1)

Nmesoma mara nyingi hoja za madai kwamba sera za Ubepari ni nguzo ya uchumi wa dunia. Katika kupitia hoja hizo, nakubaliana nao kwa kiwango fulani lakini iko haja ya kuchanganua zaidi na namna ya kuinua kiwango cha hoja zao. Dai lao la kukumbatia ubepari linatokana na mfumo wa soko huria uliobuniwa na kupigiwa mbiu sana na Adam Smith ambaye aliandika katika kitabu chake cha Wealth of the Nation.

Baada ya kukaa kimya kwa kipindi kirefu licha ya kushawishiwa na wale wanaoniamini kuwa ninaweza kuzichambua sera hizo- nilipanga kunyamaza na kuangalia mustakabali wa uchumi wa dunia. Niliamini muda utasema, na sasa nimeamua kusema kwamba Miluzi mingi ya Ubepari inampoteza Mbwa mwelekeo’. ...................

                   Usipitwe, isome yote

May 31, 2010

PENDEKEZO LA WASTANI LA MFUMO MFUMO WETU WA UTAWALA

Pendekezo la wastani la mfumo wetu wa utawala.

Na Markus Honorius Mpangala, Mbinga-Ruvuma

Msingi mkubwa wa kujitawala ni maamuzi ambao yanasimamia madhumuni yaliyomo katika makabrasha yetu. Maamuzi haya yanawalenga watu wetu waliomo bila kujari kabila,nasaba na uenyeji wao. Ilimradi walengwa ni raia halali wa Tanzania.

Ziko njia nyingi za maamuzi ambayo humaanisha muundo wa utawala. Njia hizi hushirikisha pamoja kati ya wananchi,serikali yao na wawakilisha wa majimbo,kata na kadhalika. Mfumo huu unajikitia kuonyesha kuwa taifa letu linaoubunifu wake kiutawala.

Tunaweza kuunda mifumo mipya au kuikarabati ile ya zamani katika ngazi za mikoa,wilaya,tarafa, kata na vijiji. Maeneo haya ndiyo huunda taifa ambalo leo tunajivunia na kujiita Watanzania wenye Jamhuri ya Tanzania.
Usipitwe Isome