Showing posts with label lundo. Show all posts
Showing posts with label lundo. Show all posts
January 19, 2018
HAPO NI ENEO LA LWIKA KATIKA KIJIJI CHA LUNDO
Madhumuni
kazi,
kumbukumbu,
lundo,
Maendeleo,
maisha
October 17, 2017
TAKWIMU MUHIMU ZA WILAYA YA NYASA HADI OKTOBA 2017
1. Total Number of
Hamlets in the District = 4252. Total Number of Households for Nyasa dc = 31,146
3. Total Female Population for Nyasa dc = 74,768.
4.Total Male Population for Nyasa dc = 71,392.
5. Total Population for Nyasa dc = 146,160.
6. Total Number of Secondary school = 14
7. Total Number of Primary School = 106
Total Number of Villages = 84
8. Total Number of Ward = 20
9. Total Number of Division = 3
CHANZO: Nyasa dc statistics
September 29, 2014
USAJILI WA CHAMA CHA WALIOHITIMU SEKONDARI YA LUNDO
Jumamosi
tarehe 27.09.2014 Msimbazi Centre-Dar es Salama kilifanyika kikao cha wanajamii
wote waliosoma katika sekondari ya Lundo.
Kikao kingine kitafanyika siku ya jumamosi tarehe 4.10.2014 ikiwa na lengo la kukamilisha kusaini nyaraka husika za usajili.
Aidha, ili kuwezesha wenzetu waliopo mikoani kushiriki kwenye suala hili, Katiba yetu itatambua "Chapters" kwa mikoa tofauti ambapo wale walio nje ya Dar es salaam wataweza nao kukutana kama ilivyo kwa Dar.
Mpaka kikao cha leo tumeweza kukusanya jumla ya kiasi cha Tshs. Laki Nne (400, 000 ) kutoka kwa wajumbe walioguswa, tunawashukuru sana.
Tunaendelea kuwahamasisha wote.... tuendelee kushirikiana.
Kwa wale watakaoguswa tulikubaliana kikao cha kwanza kuwa tuendele kuwasilisha michango yetu kwa Mhazini (0715008688). Kwa lengo la awali, tunaangalia upatikanaji wa vifaa vya kufundishia na tutaendelea kwenye hatua ya pili ya kushughulikia ukarabati wa majengo kwa kadri tutakachopata.
Madhumuni
lundo
March 09, 2013
LUNDO SEKONDARI INA HALI MBAYA SANA KIELIMU
![]() |
| Richard Mwanja |
Na Richard Mwanja, Dar es Salaam
Tangu kutanagazwa matokeo ya kidato cha nne shule mbalimbali
zimekuwa na matokeo mabaya sana. Miongoni mwa
shule hizo ni Lundo sekondari ambayo ilikuwa ikisifika kwa ubora wa wahitimu na
matokeo mazuri.
Lundo sekondari iliwahi kuweka rekodi ya kufaulu wanafunzi
wa kidato cha pili, hivyo hakuna aliyefeli kwa mwaka 1999. Sifa nyingi za shule hii ilikuwa nidhamu na wanafunzi kupenda masomo huku wakikabiliana na hali ya maisha na kuyazoea.
Wengi waliohitimu hapo wamefanikiwa kuwa watumishi imara na kuzalisha wanamapinduzi wazuri kifikra ambao wanaendelea kusukumu gurudumu la maendeleo ya wilaya ya Nyasa, na mkoa wa Ruvuma kwa ujumla pamoja taifaletu la Tanzania.
Lakini kwa sasa hali
ni tofauti. Licha ya kusifika wakati wa uongozi wa mkuu wa shule Bwan
Ndunguru, sasa hali imekuwa mbaya sana. Maskini Lundo Sekondari.......masikini
wilaya yetu Nyasa....
Inasikitisha kuona shule ile tuliyosoma, shule ile iliyokuwa
kinara kwa ufaulu wa kidato cha nne tangu miaka ile ya 90's hadi mwanzoni mwa
2003.... Leo hii shule ni ya division 4 na 0 tuu.... Kwa mtazamo
Wangu kutokana na vile nilivyokuwa nikifuatilia matokeo ya shule hii kwa miaka
kadhaa,nimegundua shule imekosa Uongozi....
Samahani kwani huenda nitakuwa nimewagusa wengine moja kwa
moja,lakini kwa nini wakati ule wa mzee Ndunguru mambo hayakuwa hivi.... Imeniuma kwa ujumla wa matokeo Kitaifa,lakini nimeumizwa
zaidi na matokeo ya shule zetu wilayani Nyasa.... Sitaki kuamini kama Sisi ni
Vilaza; Hapana!!
November 01, 2012
JAMES ZOTTO ALIPOZUNGUMZIA MGOGORO WA ZIWA NYASA, KABLA YA KUWASILISHA UTAFITI WAKE KWENYE UMOJA WA AFRIKA NCHINI ETHIOPIA
Mgogoro wa mpaka Malawi na Tanzania: siasa na ukweli
Na James Zotto, University of Dar es Salaam
Ndugu zangu watanzania, naamini mnafuatilia vizuri tatizo la mpaka wetu wa ziwa Nyasa na Malawi! Na pia mmefanikiwa kusikia au kusoma hotuba ya Waziri wa Mambo ya nje, Benard Membe. Nilishtushwa kidogo na hotuba hiyo. Niharakishe kusema, mimi napenda utaifa wangu na uzalendo wangu. Lakini napenda sana kutetea mambo yangu kwa kukubali ukweli, kujua hali halisi, kukubali hata zile zinazonipinga, ili nami nijipange kujenga joja. Niongeze tu kuwa, eneo hili nafanyia study yangu ya PhD. Sidhani kama nipo sahihi zaidi na lengo langu si kusema nani anamiliki nini!
James Zotto akiwa pembezoni mwa ziwa Nyasa.
Ukweli ninaofahamu, tatizo si kubwa sana kama tunavyolifikiri, na pengine tutachukua muda kupitia nyaraka zote muhimu.
Kwanza, tunahitaji kwenda Idara ya Kumbukumbu ya Uingereza(Public Records Office). Pili tunapaswa kufuatilia Colonial Archives Potsdam, Ujerumani.
Aidha, tufuatilie pia Malawi National Archives, Tanzania National Archives, Maktaba Chuo Kikuu cha Dar es salaam(UDSM) na Chancellor College Malawi. Ninaamini ubishi utaisha kwa kuwa nyaraka zote zipo.
Naomba nianze kujadili kwa kuweka angalizo katika suala hili ili ikilazimika, Malawi wasalimu amri kwa njia yoyote tutakayoamua, nitasema hapo baadaye.
Angalizo lenyewe: ziwa Nyasa liligawanywa na mabeberu wa Kiingereza, Kijerumani na Kireno. mkataba wa mwaka 1890 uitwao Anglo-German Agreement, unasema mpaka wa uliokuwa miliki ya Ujerumani au kwa kiingereza German East Africa (Tanzania Bara ya leo) na Nyasaland (Malawi ya leo) unapita kando kando ya ziwa Nyasa kutoka mto Ruvuma(mkoani Ruvuma) mpaka mto Songwe(mkoani Mbeya).
Mkataba huo upo katika nyaraka nyingi sana. Mathalani katika Sheria za Kimataifa (International Law) wanafahamu jambo hilo na sina shaka ndugu zetu wanasheria wa kimataifa (International Lawyers) wanaelewa nini nazungumza!
Sehemu nyingine ilikuwa ya mkataba ilikuwa mwaka 1891 kati ya Ujerumani na Ureno. Kulingana na mkataba huo, walikubaliana kuwa mipaka ilianzia mto Ruvuma kuelekea Portuguese East Africa (Msumbiji ya leo).
Mkataba mwingine ulikuwa ni kati ya Ureno ambayo ikawekeana mipaka na British Nyasaland (Malawi), kwahiyo, kipindi cha Ujerumani, mipaka inasomeka 'it passes along the shore of the lake (Nyasa).”
Hata hivyo kuliwahi kutokea mabadiliko ya mipaka hiyo. Mabadiliko ya mipaka yalianza kipindi cha ukoloni, kabla ya Ujerumani kuondoka.
Kikwete na Banda
Marekebisho ya mipaka yalifanyika kati ya Ujerumani na Ureno kwa kusogeza mipaka mbele na kutamka, “0.5 KM from the original tripartite point” na vijisiwa vya mto Ruvuma vikagawanywa. Mipaka hiyo ipo hivyo hadi leo.
Na eneo lingine ni kati ya Uingereza na Ureno, ambapo, kisiwa kilichopo eneo la Malawi kinamilikiwa na Msumbiji mpaka leo na eneo la ardhi lililopo Msumbiji linakaliwa na Malawi.
Huo ulikuwa mkataba wa marekebisho na ipo hivyo mpaka leo. Kwahiyo, tulivyorithi mipaka, tumerithi na mabadiliko haya na hivyo hatuwezi kugombana na Msumbiji wala Msumbiji hawawezi kugombana na Malawi.
Mpaka wetu na Malawi haukurekebishwa popote pale mpaka Ujerumani ilipoondoka nchini. Nafikiri viongozi wajiandae pia kwa hili ili tuweze kuwashinda ndugu zetu wa Malawi.
Marekebisho ya mipaka kipindi cha Uingereza:- sote tunajua German East Africa, ni sisi(Tanzania) pamoja na Rwanda na Burundi tuligawanywa katika sehemu kuu mbili.
Mosi, tulipokuwa chini ya League of Nations tukiangaliwa na Uingereza. Kuna mambo nahitaji tuweke sawa ili kuongeza hoja kwa mheshimiwa waziri wa mambo ya nje, Bernad Membe.
Tulipokuwa chini ya League of Nations, tukaitwa ‘Mandated Territory’, na Uingereza ikawa ni ‘Mandatory Power’. Turudi katika Kamusi tutofautishe “a an annexed colony and a mandate.”
Mpaka ukawekwa kati ya Ubelgiji na Uingereza, uliitwa The Milner-Orts Agreement of 1922! Naam, katika mkataba huu, mto Kagera ulikatwa katikati , hivyo hadi naandika makala hii mipaka hiyo tumerithi hivyo.
Hapakuna mahali popote pale ambapo eneo la ziwa Nyasa kama palirekebishwa kwa njia ya mkataba baina ya Nyasaland State na Tanganyika State.
Isipokuwa tofauti na Mandates zote, Tanganyika pekee, ilikuwa na tofauti ndogo, ambapo mpaka wake wa ziwa Nyasa ukapewa wanachoita 'Wording'. Na hivyo, ramani ya Tanganyika na Official Records zikaonyesha kuwa mpaka umepita katikati ya ziwa Nyasa!
Hapa ndipo tatizo linapoanza na sisi tumeshindwa kusogea mbele kidogo. Ninachokisema hapa kipo pale National Archives Secretariat Files, Accession Numbere AB 8 na AB 30!
James Zotto akiwasilisha utafiti wake kuhusu mgogoro wa mpaka wa Ziwa Nyasa.
Nafikiri hotuba yote ya mhehimiwa Waziri Membe imetokana na Files hizo, ndizo walizopelekewa. Ndugu zangu watanzania, ni muhimu kujadili zaidi ya hapo.
Twende mbele kidogo, ni kweli kama mheshimiwa alivyosema katika hotuba yake, ramani nyingi kuanzia mwaka 1922 hadi mwaka 1939 zinaonyesha mpaka upo katikati ya ziwa Nyasa!
Je, ukweli huu utatutosha pekee mbeleni tukifikishana mbali? Hapana, tuendelee kusaidiana kwa hili, nafikiri ujumbe utawafikia tu.
Waziri Membe hakusema kuwa ramani zingine, japo chache muda huu na Official Reports hazionyeshi mpaka au zinaonyesha mpaka upo chini. Lakini ni chache! Kwanini hili?
Bado natafuta majibu, lakini kwa haraka, tunaweza kusema kuwa Uingereza ilitamani Tanganyika iwe koloni lake na si Mandate! Na pia ilishinikizwa na wawekezaji na hata jeshi ilisema afadhari waiteke ili liwe koloni na waachane na Mandate!
Nahitaji tuelewe maana ya mandate. Hii yote ilitokea baada ya gavana Donald Cameroon, wa Tanganyika kusema kuwa “Tanganyika is a part of the British empire and it will remain so”.
Hii ni siasa na si ukweli kama unaelewa maana ya kuwa wao hawakuwa wamepewa koloni kama mali yao, bali kuliangalia hadi wananchi wapate 'akili' ili wapewe uhuru!
Kwa hiyo na kimsingi, kwa maana ya sheria ya kimataifa, Tanganyika haikuwa Part ya British Empire kama yalivyo makoloni yaliyotekwa moja kwa moja na Uingereza yenyewe!
Hapa pakatokea mvutano mkubwa sana katika House of Lords na House of Commons! Na hivyo basi, mtafaruku huu wa mipaka ulianzia hapo, hivyo hata waingereza wenyewe walivutana kuhusu mipaka.
Kwa mfano, mwaka 1926, wajumbe wa mabaraza waliibana serikali iseme mipaka ya Tanganyika na ule wa ziwa Nyasa! Mabishano, kama haya yetu leo yalikuwa makubwa, ila si kwa kutishiana kwa kuwa walikuwa wenyewe na walitaka kuwekana sawa!
Rais Kikwete na Joyce Banda walipokutana katika kikao cha SADC mjini Maputo, Msumbiji.
Naam, ndipo Secretary of state for colonies alibanwa na mjadala ulikuwa wa kisheria zaidi ukihoji Status of the Mandate, British Empire n.k, na kama waingereza wana mamlaka ya kujipangia kuhusu koloni walilokabidhiwa kuliangalia(nieleweke na sio kulimiliki koloni).
Mwishowe wenye dhamana(Waingereza) walisema kwamba, hata wao wanashindwa kuelewa, 'What exactly is the sovereignty of Tanganyika lying', jamani mnamwelewa huyu mtu wa kiingereza?
Kwamaana hiyo, haelewi vizuri mipaka yetu, ambayo wenyewe ndo wameirekebisha au kuipa 'Wording'! hivyo, tatizo linaanzia hapa na si muda mwingine wowote!
Jambo kubwa ambalo Waziri Membe hakusema ni hili: kuanzia mwaka 1939, mambo yalibadilika na hawa hawa watu(Wakoloni) tunaochukua ushahidi kutoka kwao, wakafanya madudu!
Na ilipoisha vita ya pili ya dunia, jamani oneni haya, hawa waingereza katika ramani zao, tena nyingi mno, tuangalie East Africana Section ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam, katika sehemu ya Thesis, kuna Cabins 3 zimejaa ramani na bado ni mpya sana kutokana na kutunzwa na pia kutotumika sana.
Zinaonyesha, bila shaka yoyote, kuwa mpaka wa Tanganyika na Nyasaland unapita pembeni mwa ziwa na sio katikati! Nieleweke naonyesha tu mambo yalivyo ili tuweze kuchukua hatua zaidi.
Hotuba ya Waziri Membe, iliishia nyaraka za mwaka 1939! Kumbe hawa jamaa walichora tena ramani zote zikionyesha mpaka upo pembeni mwa ziwa! Kwanini hili? Natafuta majibu.
Lakini kwa haraka naweza nikakisia mambo mawili. Mosi, karibu na vita vya pili vya dunia, ilisikika tetesi kule duniani(ughaibuni) kuwa, Ujerumani inarudi na inakuja kuchukua makoloni yake.
Tukitaka kuhakikisha jambo hili, tusome National Archives of Tanzania, Secretariat Files zote zenye kichwa cha habari, 'The future of Tanganyika in British Empire'.
Kwa hiyo, waingereza walihofia kutimuliwa na kurudi kwa wajerumani, na hivyo, wakarudisha ule mpaka wa awali wa mwaka 1890 unaotumiwa tena na Malawi kwa sasa!
Na pia, katika kipindi hicho, baada ya kumalizika vita hivyo, Tanganyika ikawa chini ya Umoja wa Mataifa(United Nation Organisation), ambapo ilipewa Trusteeship Status!
RAMANI YA ZIWA NYASA.
Maana ya hii ni rahisi kuliko Mandate! Kwanini? Hii ilimaanisha ‘to be granted immediate independence’! maana ya neno ‘immediate’ hapa ni kwamba, kwa tafsiri yangu, waingereza walifahamu wanatimka mapema mno kwani mkataba unasema hivyo.
Nafikiri, wakarudisha ramani zikionyesha mpaka upo pembeni mwa ziwa na kitabu cha ‘Nyasaland’ cha mwaka 1958, kinaonyesha mipaka ya Nyasaland na ziwa lote likiwa kwao!
SASA TUFANYE NINI WATANZANIA?
Tukitaka kuwashinda watu wa serikali ya Malawi, lazima tukisome vizuri kipindi hiki na tuelewe ukweli, hoja zipi zinawapa kiburi. Na hoja zipi sisi tuzitumie kupambana nao, tunaweza!
Kwahiyo hatima ya nchi yetu haikujulikani itakuwaje. Kipindi hiki, pamoja na mipaka yake pia, tujiulize, kwa maana ya Mandate, waingereza walikuwa na ‘Legal Authority 'kurekebisha' mpaka wa ziwa nyasa?
Na je makosa waliyofanya waingereza, ndio Legal backing yetu sisi Watanzania? Hebu tuzame tena tutafute ukweli zaidi ili tuwashinde hawa jamaa wa Malawi!
Tulishindwana na Uingereza kurekebisha mipaka. Mwalimu Nyerere, alisubiri hadi Malawi ipate uhuru, ndipo akatoa miaka mitatu tu na asingetambua mipaka ya kikoloni(Soma Hansard, 1962).
Malawi walipopata uhuru, kukawa na matatizo ambayo Waziri Membe aliweza kuyaeleza. Nampongeza kwa hilo, ni dhahiri mwaka 1964 wakati wa mgogoro wa baraza la mawaziri la Malawi, na baadhi ya mawaziri kutorokea nchini kwetu kupitia ziwa Nyasa, Rais Kamuzu Banda akaona ziwa ni infiltration route!
WAZIRI MEMBE akinawa maji ya ziwa Nyasa mjini Mbamba Bay.
Sera zetu za mambo ya nje za Tanzania zilikuwa tofauti na Malawi. Tanzania ilikuwa nchi iliyoongoza ukombozi wa nchi za kusini mwa Afrika, wakati wenzetu Malawi wakaunga mkono Makaburu na Wareno na wakawa na balozi sehemu hizo
Rais Banda akagombana na Mwalimu Nyerere, na matukio ya kutishiana kijeshi yalijitokeza kati ya miaka ya 1967-8; matusi na kejeli zikatawala kati yetu na wao.
Tunakumbuka tuliimba, .....kipara cha Kamuzu Banda kina magamba”, tuliimba tukiwa jeshini hayo. Mwalimu Nyerere akasema suala mipaka ni hadi Malawi itakapota Sensible Leader akitokea Malawi ndipo tutajadili tena, sio utawala ule wa Kamuzu Banda!
Kipindi chote hicho tulikuwa kimya, na kuanzia mwaka 1975, hatukuwa na tatizo, lakini sio kusema kuwa tulitatua tatizo la mipaka yetu na Malawi!
Tulikaa kimya! Mipaka haina tatizo isipokuwa ni time bomb ambapo ikitokea rais mwendawazi akamwaga petroli tu, basi ni vurugu kubwa!
Tuliirithi kupitia Article III ya Azimio la Umoja wa Afrika la mwaka 1964(OAU Charter, 1964), baadaya ya majadiliano makubwa na wengi wakaridhia “uti possidetis, ita possidetis principle” (so as you exist, so may you exist).
Kama kawaida yetu tulinakili kanuni za mipaka za kibeberu za Westphalia(Westphalia border inviolability)! Hatukupata muda mwingi wa kutafakari na kuangalia kila mpaka na matatizo yake....tulirithi na matatizo na yanatutatiza leo!!!
UTATUZI WA MGOGORO: Tusonge mbele! Nakiri tuna namna tatu ya kulimaliza;- moja ni kwa majadiliano ya kawaida(Diplomacy) kama Waziri Membe alivyosema katika hotuba yake.
Pili ni kupigana vita (war is another means of diplomacy). Ndugu zangu watanzania nadhani mnataka kuniona kichaa kutamka hilo! Huo ndo ukweli, atakayeshindwa atasalimu kama ilivyokuwa kwa Uganda na sisi watanzania.
WAZIRI WA MAMBO YA NJE, BERNARD MEMBE.
Tatu; ni Mahakama ya Kimataifa(International Court of Justice) hapa nina wasiwasi. Kama nyaraka zenyewe ni zile za Waziri Membe tu, sijui kama tutafanikiwa kushinda kesi.
Tutulie, tuite wataalamu wetu wajikite ndani sana. Ni kweli kama alivyosema Waziri Membe kwenye hotuba yake kwa kunukuu kesi nyingi na zilizoshinda, na kwa kusema kuwa, tukienda mahakama ile sisi ndo tutashinda.
Nina shaka, tumejipa favour ya verdict, kabla ya kesi. Sijui, ila nina shaka kubwa, kuna kushinda, kushindwa au suluhu! Ninashaka tena na tena!
Mimi ni mzalendo, nataka ukweli kwa njia ya mahojiano na kuumiza kichwa, tutetee mali zetu tukijua tunawashinda kwa hoja.
WASIWASI: Inasemekana kuna mafuta ziwani, kwahiyo tujue Marekani na washirika wake hawako mbali! Kampuni ya Surestream ya Uingereza ndio ilipewa leseni ya kutafiti mafuta na utawalawa Bingu wa Mutharika.
Lakini, tujue operesheni ya majeshi ya kibeberu na huyu mama Joyce Banda, ambaye ni mpwa wa Kamuzu Banda, anapata wapi hiki kiburi? Nyuma yake kuna nini na nani? Tuangalie haya pia.
HITIMISHO: Tusiwe na hoja moja tu mkononi kama ndio water-tight evidence yetu kwa serikali na wananchi kwa ujumla. Tujaribu kuzibishanisha hoja zetu. Na hoja nzuri ni zile zinazopingana nasi na tusizozipenda, tukizielewa na kuzikubali ndipo tutajipanga namna ya kuzigalagaza. Tumwelewe vizuri adui yetu. Mungu ibaraki Tanzania, ziwa Nyasa, wanyasa, na watanzania! Tusing'ang'anie tu Reparian Law.
James Zotto ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam(UDSM).
Madhumuni
Biashara,
Chiwanda,
chiwindi,
dondoo,
kumbukumbu,
kwambe,
liuli,
lundo,
lundu,
Mafanikio,
Matenje,
mawazoni,
Mbinga,
mbmba bay,
ng'ombo,
ngoma,
Nyasa,
siasa.
October 22, 2012
UJENZI WA ZAHANATI KATIKA WILAYA YA NYASA
Jengo la hapo chini ni Zahanati ya ya Kijiji cha Mbaha baada ya kukamilika kwa ukaratabati wake. Kijiji chicho kipo katika Kata ya Mbaha, kwenye Tarafa ya Ruhuhu iliyopo wilaya mpya ya Nyasa. Juhudi za usambazaji wa huduma za afya zimekuwa kubwa ili kusogeza huduma kwa wananchi wa maeneo hayo na kupata huduma za afya kwa usahihi. Hii ni harakati mojawapo ya maendeleo, kama inavyosemwa MTU NI AFYA.
Jengo la hapo chini ni Zahanati ya ya Kijiji cha Luhindo likiwa katika awamu ya kwanza ya kukamilisha kuwa kituo kidogo cha afya. Juhudi za usambazaji wa huduma za afya zimekuwa kubwa ili kusogeza huduma kwa wananchi wa maeneo hayo na kupata huduma za afya kwa usahihi. Hii ni harakati mojawapo ya maendeleo katika wilaya ya Nyasa
Jengo linalofuata hapo chini ni Zahanati ya ya Kijiji cha Mitawa baada ya kukamilika kwa ujenzi wake. Kijiji chicho kipo katika wilaya mpya ya Nyasa. Hii ni harakati ya kusogeza huduma za afya kwa usahihi. Hii ni harakati mojawapo ya maendeleo kwa wananchi, ingawa juhudi zinahitajika.
Ujenzi wa Zahanati ya ya Kijiji cha Mkali kilichopo katika Kata ya Lipingo, kwenye Tarafa ya Ruhekei iliyopo wilaya mpya ya Nyasa. Ujenzi wa kituo hicho unaendelea.
Katika jamii yoyote suala la kupiga hatua ni muhimu sana. Na jamii haiwezi kupiga hatua kama haijaanza kutengeneza hatua husika. ili mafanikio yapatikane ni lazima juhudi zifanyike, ni muhimu kutunza kile kinachoanza kutengenezwa ili tuweze kuboresha. Pengine Zahanati hizi zisiwe na kiwango bora cha huduma za afya. lakini ni heri kuanza kwa hatua hiyo kuliko kutokuwepo kabisa. Nchi yako kwnaza.
PCIHA ZOTE NA Hoops Kamanga, Nyasa
Madhumuni
habari,
kumbukumbu,
lundo,
Nyasa,
Uchumi
October 08, 2008
maswali magumu
Mwanablogu Yasinta Ngonyani aliandika kuhusu yeye katika blogu yake. Ilikuwa Agosti 23, 2008 kwamba udadisi kwake ni sehemu ya maisha, akaongeza kwamba katika hali hiyo amejikuta amepoteza baadhi ya marafiki hasa wale wasiopenda maswali yake yaani walikuwa wakikerwa na maswali yake. Mimi sijui walikerwa kwasababu gani, wao wanajua. Sasa mimi namfahamu kiasi dadangu Yasinta, jamani hapo ni kiboko ya maswali yaani jamaa anauliza maswali mpaka unaona hee huyu vipi? Ukweli mmoja ya waathirika ya maswali yake ni Mnyasa hapa lakini kawaida ya Mnyasa ni uvumilivu na utulivu ndiyo uliobaini kwamba uulizwaji kwake maswali ni njia yake ya uwasilishwaji wa urafiki tofauti na wengine walivyokuwa wakidhani. Jamani dadangu anamaswali mpaka unaweza kuungua utadhaniumeunguzwa na moto. Sasa huwa najiuliza vipi mjomba wangu Erik na Camilla watakuwaje? nikajikuta nimegota,nimeishiwa maneno ya kuwatabilia. Lakini maswali yake yanakufanya muda wote uwe unafanya kazi ya kujibu na usipojibu heee umemkimbia au la. Jamani mimi nilivumilia na nimekubali kwamba kama alivyoandika ni kawaida yake kwahiyo naona poa tu. Habari ndiyo hiyo, kublogu/kuandika unachopenda
September 21, 2008
hapo vipi? hapo sawa? mimi sijui
naam ni masika katika barabara za kwenda ghuba tamu sana ya Mbamba bay. hivi unajua kila nikikanyaga mbamba bay najihisi kuzaliwa upya? kwanini-kwasababu ya sababu na nakupenda sana
Madhumuni
habari,
Hisia za moyo,
lundo,
maisha,
mbamba bay,
Nyasa,
urafiki,
wageni
April 19, 2008
Nyasa,Mila,Desturi+Miaka 14 Ughaibuni
Kuna habari moja imenifurahisha sana. nimjikuta nikiwa katika tafakari kuhusu habari yenyewe. lakini ni jambo muhimu kukumbuka mambo ya nyumbani nyasa kwa wale mliopo ughaibuni.Hii habari lazima tuitafakari sisi wanyasa ambao tumeishi sana na wamisionari hivyo twayajua mengi.Soma habari nzima ,bonyeza hapa www.ruhuwiko.blogspot.com inahusu namna maisha ya wazungu yanatawaliwa na ubinafsi na kujitegemea mwenyewe kinyume na wanyasa tuombao chumvi kwa majirani zetu.ughaibuni haipo hiyo....utaomba kwa nani
Madhumuni
lundo,
mila na desturi,
Nyasa,
ughaibuni
April 02, 2008
Hebu Msome Mnyasa huyu jifunze maisha
Malezi ya familia ni magumu pale unapokutanisha tamaduni mbili tofauti.Hili anatuelimisha dada yetu huyu yale anayoyaona huko ughaibuni na kwetu afrika hususani kwa wanyasa.Lakini ni habari njema kwani kila siku watu wanahitaji kujifunza mapya na kama alivyopata kusema Mwanafalsafa Galileo kwamba huwezi kumfundisha mtu kitu kama hajachukua hatua za kujifunza,sasa tuchukue jukumu tujifunze muda ndiyo huu.Hebu soma habari nzima jionee mwenyewe mambo hayo,wanyasa mpoooo!!!!
www.ruhuwiko.blogspot.com
www.ruhuwiko.blogspot.com
Madhumuni
familia,
kumbukumbu,
lundo,
ughaibuni
March 19, 2008
Machi Mwaka 2002;Yasinta Kwanini,kisa kinaendelea.
Nimerudi na kisa kileee kinachonihusu pengine zaidi ya kunihusu na kinawahusu wengine,mimi sijui.Hebu ngoja nikiandike tena hapa maana siyo mimi labda wengine kinawahusu.Mwezi machi 2002,Yasinta katoroka kwao,kamkimbia baba,mama na nduguze,wala hataki kusema anakokwenda.Nyumbani wazazi wanashangaa mwenetu tumpendaye kaondoka bila kuaga ni maajabu hayo.Yasinta katua Mbinga mjini,katulia stendi na raifikiye Vumilia wanapiga soga za hapa na pale lakini hatimaye mnyasa anatokea,ana-afro, katweta ghafla anajiuliza huyu binti vipi?Haya soga za hapa na pale wanakumbushana na mnyasa enzi wakiwa shule,lakini mnyasa anauliza kulikoni upo hapa? mara ghafla Yasinta anaomba "tafadhali ukiulizwa kuhusu kuniona mimi{yeye}usiseme".Mnyasa anashangaa kumbe binti katoroka nyumbani kumfuata mpenzi?Jamani kupenda tabu,mapenzi ni kikohozi kuficha huwezi aliimba Fresh Jumbe.Binti amependa hataki shule hataki kusikia maonyo ya wazazi,masikio kaziba pamba,mahaba yamekolea, lakini kwakuwa mnyasa anamjua vema akasaili hee mwenzangu nimesikia hutaki shule kulikoni?Sipewi jibu, nazungushwa huku na huko binti anajiona kumaliza kidato ni mwisho hakuna tena hamu ya shule kisa mapenzi mmh.Mwishowe mnyasa anashauri vipi uahirishe safari,looh.. akaambiwa alipe nauli aliyolipia tiketi kisha awezekuahirisha safari,mnyasa akaduwaa akasema huyu siku hizi kawa mbogo wa mapenzi.Lakini kwani mnyasa akawa anajua hapa anapenda lakini kwa mtindo huu acha ajifanye hana hizo hela,unajua shilingi ngapi?Watu wa Mbinga wanajua wakati huo nauli mpaka makao yetu makuu Songea ni....samahani sitasema.Binti anasafiri anakwenda kuonana na mpenzi wake,waubani wake, mwandani wake,yaani ampendaye.Mmh wapi bwana yako wapi hayo mapenzi mathubuti?kuna kuacha shule tena?Mbona yupo huko.......kwenye baridi anasoma,sijui kwa ari au ndiyo wasomi wetu wa siku hizi.Kifupi alicharukia mapenzi,akaona ganda la mua la jana........na masikitiko ya mnyasa kwa kuwa alimpenda basi katoa kauli za kulaani na bado zinamtesa,yako wapi mbona bado kasheshe inaendelea?Maisha ya Lundo yalikuwa ni simulizi murua.Ngoja nikomee hapa kwa leo.
Madhumuni
katuni,
kumbukumbu,
lundo,
Nyasa,
soga
February 21, 2008
LUNDU na LUNDO ni vijiji tofauti
Lundu ni kijiji kilichopo ukanda wa nyasa katika kata ya Mbaha,na kwa urahisi unaweza kufika kijiji hiki kwa kupitia Lituhi ama toka Mbinga kwa kupitia Ngumbo na maeneo yanayoweza kukurahisishia usafiri hususani wa meli kwa kupitia Mbamba bay au Itungi-kyela na kushuka bandari ya LUNDU.Ni kijiji ambacho Mimi nimetokea na kuishia mpaka sasa.LUNDO ni kijiji kilichopo kilometa chache sana toka mji wa Mbamba bay au kutoka mji wa Liuli.Ni kijiji ambacho kina sekondari na kumbukumbu ya kutunza wakimbizi wa Msumbiji kabla ya kurejeshwa mwaka 1995 baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe kwisha ambavyo RENAMO walipigana na wenzao wa FRELIMO.Ingawa vijiji hivi wilaya ya Mbinga lakini vinatofautiana na kwa herufi za mwisho tu,na Lundu ni kijiji kilichopo na uhusiano na vijiji vya mbali kidogo vya Manda.Sifa na tofauti yake ni kwamba Lundu ni bandari ndogo katika shughuli za usafiri katika ziwa nyasa na Lundo ni kumbukumbu ya wakimbizi,sekondari na mashamba makubwa ya kilomo cha mpunga na hata Rais Jakaya analijua hilo.
February 07, 2008
Wanyasa kwa Samaki huwatoi kabisa,.. Hata wakiwa Ughaibuni..
Nilijikuta najiuliza hivi hawa wanyasa bila samaki ingekuwaje?Basi ni hivi nimepata waraka kutoka Ughaibuni,yaani dadangu huyu huko Ughaibuni anakwambia anakumbuka Magege yakiwekwa chumvi na pilipili pembeni we acha kabisa..Lakini usishangae nimepataje hii habari kwani utajua kuwa nipo hapa nyasa.Jibu ni ndiyo lakini nimeibukia hapa Mbinga hapa kama kawaida kudandia maisha.Dada anakumbuka samaki wa ziwa nyasa yaani njozi zote mambo ya nyumbani.Wanyasa, hebu soma sehemu ya ujumbe huu "Nimevutiwa na Blogu yako,mimi mnyasa yaani nakumbuka nilipokuja mwaka jana mwezi novemba nilipewa magege na chumvi kisha na pilipili yaani acha nijichane we acha tu nyumbani bwana".Mtoto wa kinyasa utamjua tu si unaona alivyochambua aina ya samaki hao? yani anajua viungo vyake na bila shaka liapewa samaki wa kuchomwa.Ukitaka kujua yuko wapi hebu peruzu jiografia nchi ya Sweden ilipo ndipo utajua ninachokisema.Dada yupo ughaibuni lakini hajasahau nyumbani {Tanzania}anakuja kutembelea,Je wengine mpo?Lakini ndugu yangu Ndesanjo anatembelea sana Jeff na wenzake.Mwenzetu anakumbuka samaki lakini amesahau dagaa,kambale,ntaka,mandongo,mbasa,ngogo n.k ndiyo nyasa hiyo watu wanaselebuka kwa raha kama dada yetu anavyoselebuka toka ughaibuni na samaki wa nyasa. Wanyasa kwa samaki huwatoi kabisa....yaani mpaka ughaibuni?
Madhumuni
habari,
kumbukumbu,
lundo
Subscribe to:
Posts (Atom)














