![]() |
| Honorius Mpangala, 0628994409 |
AKIWA katika kampeni za urais mwaka 2005 Rais mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete katika ardhi ya Kyela Mkoani Mbeya alihaidi meli. Alirudia tena kauli hiyo alipokuwa katika ardhi ya Mbamba Bay Mkoani Ruvuma. Baada ya kipindi cha utawala wake hatimaye meli alizoahidi tayari zimeonwa na Wanyasa.
MV Njombe imekamilika na kufanikiwa safari moja ya majaribio kutoka Bandari ya Itungi
hadi Mbamba Bay. Yapo mambo ambayo ni
fursa kwa wakazi wa Nyasa kutokana Meli hii. Kama inavyoitwa ni meli ya mizigo
ni chombo kitakachoweza kuwainua kiuchumi wakaza wa Nyasa kama watakitumika
ipasavyo. Kuinuka kiuchumi kutatokana na kujikita katika shughuli ambazo wakazi
wake watajishughulisha na shughuli kama ilivyo kilimo biashara na hata ufugaji
wa kisasa na wenye tija katika maisha ya leo.
Kilimo
cha biashara ni moja ya ujasiriamali ambao watu wengi wamekuwa
wakijishughulisha nao. Katika mwambao wa Ziwa Nyasa hususani wilaya Nyasa yapo
mabonde ambayo yanaweza kufanyika kilimo cha mazao ya muda mfupi na kwa mfumo
wa kilimo cha umwagiliaji, na kile cha kutegema mvua na kuleta tija.





