Showing posts with label na Uchumi. Show all posts
Showing posts with label na Uchumi. Show all posts

January 11, 2018

KUFUNGWA KWA BENKI TANZANIA.

NA LAMECK KUMBUKA, USWISI
BENKI zinafungwa sio ishara njema kwa ucuhumi, lakini tufikirie pia sababu nyingine mbali na lile tunaloshabikia sana la “kuporomoka kwa uchumi”. Unajua kuwa idadi ya watu wenye simu na idadi ya watu wanaotumia huduma ya pesa kwa simu imepita zaidi sana idadi ya watu walio na Account benki?
Benki nyingi zilikuwa zinategemea wateja wa kawaida, amabao ndio idad kubwa ya watanzania. Bahati mbaya  Benki nyingi zilishindwa kujibu matakwa ya watu wa kijijini ambao ndo hufanya idadi kubwa ya watanzania wengi (hata wale wanaoishi mjini, wako Connected sana na ndugu jamaa marafiki, na miradi yao vijijin. Kile kilichoshindwa kufanywa na benki hizo, kinafanywa na huduma za simu, Mzunguko wa pesa umehamia kwenye simu sio tena katika mabenki.

November 08, 2017

MABALOZI WETU WASIWE WAZITO KUJENGA UCHUMI

NA GABRIEL MWANG’ONDA 

RAIS John Magufuli ametimiza miaka miwili madarakani tangu alipoapishwa Novemba 5 mwaka 2015. Miaka hiyo serikali imefanya mambo mengi ambayo si lazima kueleza hapa leo. Lakini itoshe kusema lipo jambo ambalo ninajikita nalo ili kuangazia miaka hiyo. Ni dimplomasia ya uchumi.

Diplomasia ya Uchumi (Economic diplomacy) limekuwa somo gumu sana kueleweka kwa mabalozi wetu. Yaani sisi wengine tumeiimba mpaka tukaona tupumzika tu kwasababu somo limekuwa gumu sana kwa balozi zetu. Binafsi nimeliongelea sana kwenye ma redio nyingi hapa ndani ya nchi na nje pia, lakini ndugu zetu wameamua kutoelewa tu hii dhana kitu ambacho kinaligharimu sana Taifa letu.
Ufukwe wa Ziwa Nyasa mkoani Ruvuma. Ni miongoni mwa vivutio vya utalii.
Kila balozi utakae onana nae ukimuongelesha kuhusu hii diplomasia ya uchumi anasingizia udogo/ufinyu wa bajeti. Lakini hiki kamwe hakiwezi kuwa kikwazo kwa mtu mzalendo mwenye ubunifu alienuia kwa dhati kabisa kuitumikia nchi.

Si mambo yote yanahitaji fedha nyingi kuyafanya kuhusu hii dhana ya diplomasia ya uchumi. Balozi zetu hata utume baraupepe kwa vitu ambavyo ni vya kawaida sana bado hutojibiwa kabisa. 

October 27, 2017

KWANINI WILAYA YA NYASA IMESHIKA MKIA KATIKA MATOKEO YA DARASA LA SABA?



RAYMOND NDOMBA, SONGEA
WILAYA ya Nyasa iliyopo mkoa wa Ruvuma imekuwa ya mwisho katika matokeo ya darasa la saba mwaka huu 2017 kimkoa. Swali la kujiuliza ni kwanini hali hiyo imetokea. 


Mawazo yangu ni haya; Pamoja na sababu nyingi zilizosababisha matokeo hayo ya aibu kubwa. Wazazi wanapaswa kubeba lawama kubwa. Wengi wao hawafuatilii maendeleo ya watoto wao, pia makuzi na malezi mabaya.

Miaka ya hivi karibuni (kuanzia mwaka 2000), Wazazi wengi katika wilaya ya Nyasa hawajali elimu, hawajigusi katika ufuatiliaji wa watoto wao kielimu na hata kitabia (Angalia matokeo ya mitihani ya Taifa ya shule za msingi na sekondari kunzia miaka hiyo ya 2000 kwa shule kongwe ndani ya wilaya). 

October 04, 2017

KITAI NI ENEO ZURI KWA UWEKEZAJI

Pichani ni sehemu ya mji wa KITAI. Mahali hapo ni makutano ya barabara za Songea-Mbinga, Mbinga-Lituhi, Songea-Lituhi, mkoani Ruvuma ambapo kunajengwa Kituo cha usambazaji wa umeme vijijini (REA). Hilo eneo kushoto, na upande wa kusini ni tambarare na ambalo halikumbwi na mafurikio. Panafaa sana kufungua mradi wa uwekezaji hapa ni kiunganishi cha wilaya tatu za Mbinga, Songea na Nyasa. Sifa yake kubwa ni kuzikutanisha wilaya hizo na kuwa eneo la katikati katika kupata huduma za kibiashara n.k