Showing posts with label kitabu. Show all posts
Showing posts with label kitabu. Show all posts

March 12, 2018

KITABU KUHUSU CHINA

Nimemsoma Rais Wa Jamhuri ya watu wa China Mh. XI JINPING katika kitabu chake "THE GOVERNANCE OF CHINA" -Nilichojifunza nakubaliana na mtendaji mkuu wa EPZ Kanali Mstaafu Simbakalia kwamba Chinese are prepared to learn from others but will always import and make that experience relevant to their conditions, traditions and values. That’s why they have Communism “with Chinese characterstics” and Market Economy “with Chinese Characteristics” and so on.
 The Chinese don’t buy the “copy and paste” stupidity of “best practice” from Europe that purports to know what is good and works for everybody (Nakushukuru Sana Comrade Hussein Mtoro kwa zawadi ya kitabu hiki-Hotuba za JINPING zina mafunzo mengi.

©MKUU WA MKOA WA SIMIYU,

ANTONY MTAKA

March 07, 2018

KITABU KIPYA KUTOKA KWA MWANDISHI BEKA MFAUME

February 28, 2018

RIWAYA YA NYASITIKI


Nyastiki ni kitabu cha Riwaya kinacho mzungumzia binti aliyefeli mtihani wa darasa la saba na baadae anarudi darasani kusoma.
Nyastiki anakutana na vikwazo vingi lakini hakati tamaa,pia kwenye kitabu cha Nyastiki kimezungumzia namna kina mama wa kambo wanavyotesa watoto hao wa kambo,
Pia namna kina baba wanavyotelekeza familia zao na kuwaachia wakina mama mzigo wakulea familia peke yao.
Nakala ya riwaya hii inapatikana kwa tsh 5000/= tu
Weweza kukipata kupitia

+255712640303
+255767640303
AU email adress
maria.mihanjo@gmail.com

February 26, 2018

RIWAYA: SAA 72

Ijumaa iliyopita ndugu Japhet Nyang’oro Sudi aliwasiliana nami kunijulisha kuwa nimetunukiwa zawadi ya kitabu chake. Yeye ni mwandishi wa riwaya ya SAA 72. Hima jumamosi nikawasili kwa bwana George (Muuza vitabu huyu; simu yake; 0713 454152). George huuza vitabu vyake pembeni ya sanamu la Askari  jijini Dar es salaam (Posta Mpya). ana vitabu vingi, waweza kulonga naye kujipatia nakala zaidi. Nilianza kusoma kitabu hicho Jumapili asubuhi yapata saa 4 hivi, hadi saa 2 usiku. Nikatamatisha. Kina kurasa 202.
Masimulizi ya kitabu hiki ni kuhusiana na mgogoro wa vita vya wenyewe kwa wenyewe unaoendelea nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ambapo Joseph Katanga anaachiliwa huru na Makahama ya kimataifa ya Uhalifu (ICC) kwa madai ya kubadilika kitabia). Lakini Katanga hakubadilika chochote. Alitumia kila njia kuendesha maasi kwa wanavijiji, na kudhoofisha utawala waDRC. Machache tunayoweza kujifunza.

February 02, 2018

UCHAMBUZI WA KITABU: DIWANI YA SIWACHI KUSEMA

MWANDISHI: MOHAMMED K. GHASSANI
MCHAMBUZI: MARKUS MPANGALA
NA MARKUS MPANGALA

MWAKA 2017 nilipatiwa zawadi ya vitabu vitano vya ushairi kutoka kwa mwandishi wa habari wa Idhaa ya Kiswahili ya Ujerumani (DW), Mohammed Khelef Ghassani. Vitabu hivyo ni Siwachi Kusema, Machozi Yamenishiya, Kalamu ya Mapinduzi na Adamo. Leo tunachambua diwani ya  “Siwachi Kusema; Uhuru U kifungoni” ambayo imechapishwa mwaka 2016 na kampuni ya Zanzibar Daima Publishing yenye makao yake mjini Bonn nchini Ujerumani. Diwani hii imepewa nambari ISBN 978-15-34660-16-8.


‘Siwachi kusema’ ni mwendelezo namna ya mwandishi huyo ya kusema na kuyasemea yale yanayotokea mbele katika jamii yake. mambo ambayo yanaikwaza jamii hiyo kutokana na sababu mbalimbali. 

Mathalani katika dibaji ya diwani hii mwandishi anasema, “Mwanadamu anayelazimishwa kwasababu yoyote ile kuacha kutoa kauli yake juu ya yale yanayojiri mbele ya macho yake, yale yanayomuhusu na kuyaathiri maisha yake, bsi huyo ni mithili ya mtu aliyezibwa pumzi kwa matambara au mateka aliyetiwa jiti la roho. Huwa si mtu huru, si mtu kamili, si mtu mtu,”(Uk.Xi).

Mkusanyiko wa mashairi uliopo katika diwani hii umegawanyika katika maeneo tofauti. Kuanzia mapenzi na ndoa,ukiwa au upweke wa baadhi ya watu hapa duniani, siasa na haki za binadamu, masuala ya dini, misaada kadhalika.
Tunaweza kutazama mifano hayo katika baadhi ya mashairi. 

Shairi la ‘Mwanangu Nakupe Mke’ (Uk.14) mwandishi anaandika,
“Mwanangu nakupa mke, nakuwekea kikao,

Awe wako uwe wake,wamoja toke oleo,

Basi maneno yashike, na wasia nikupao,

Mkeo awe ni nuru.

January 26, 2018

UCHAMBUZI WA KITABU: SAFARI YA YERUSALEM KUTAFUTA AMANI

NA MARKUS MPANGALA
BOUTROS Boutros Ghali aliwahi kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kati ya mwaka 1992 hadi 1996 amefariki dunia Februari 16 mwaka 2016 akiwa na miaka 93.

Leo tunachambua kitabu chake cha “Egypt's Road to Jerusalem:: A Diplomat's Story of the Struggle for Peace in the Middle East” kilichozindualiwa rasmi Mei 20, 1997. Kitabu hicho kina jumla ya kurasa 366, kimechapishwa na Random House(1997) na kikiwa katika lugha ya kiingereza. Boutrous amekipatia namba ISBN-10: 0679452451.

Boutros Ghali anatuelezea miaka minne ya uzoefu wake katika utawala wa aliyekuwa Rais wa Misri, Anwar as-Sadat. Anatuonyesha namna alivyochaguliwa kwenye uwaziri wa mambo ya nje mwaka 1977 na kifo cha rais Sadaat mwaka 1981. 

Katika kitabu hiki Boutros Ghala anadhihirisha umahiri alioonyesha katika masuala ya diplomasia wakati wa kusaka amani ya mashariki ya kati. Ikumbukwe eneo la mashariki ya kati limekuwa kwenye migogoro ya muda mrefu kiasi kwamba ufumbuzi umekuwa mgumu. 

Ni eneo ambalo mwandishi wa kitabu hicho anatukumbusha hatua kwa hatua walizokuwa wakichukua katika kuhakikisha amani inarejea mashariki ya kati. Anatuonyesha namna ambavyo Misri na Israel zilivyokuwa zikifanya juhudi za kumaliza uhasama wao. 

November 25, 2017

UCHU WA MADARAKA DHIDI YA UZALENDO

KITABU: ZIMBABWE: STRUGGLES-WITHIN-THE-STRUGGLE (1957-1980)”
MWANDISHI: PROFESA MASIPULA SITHOLE
MCHAMBUZI: MARKUS MPANGALA
JESHI la Zimbabwe limetangaza wiki iliyopita kuchukua madaraka nchini humo na kumwondoa Rais Robert Mugabe ambaye ametawala nchi hiyo kwa kipindi cha miaka 38 hadi sasa. Kutokana na hali hiyo tunalaizmika kukumbuka namna mwanazuoni Profesa Masipula Sithole alivyobainisha matatizo ya Zimbabwe kupitia kitabu chake cha “Zimbabwe: Struggles-within-the-struggle (1957-1980)”

November 20, 2017

KONGAMANO LA KUMBUKIZI YA FIDEL CASTRO


Jukwaa la Wajamaa Tanzania, Taasisi ya Usomaji na Maendeleo "Soma" na Rastafarai United Front wanashirikiana kuandaa kongamano la kumkumbuka El Commandante Fidel Castro siku ya Jumamosi, tarehe 25/11/2017. Mahala itakuwa kwenye ukumbi wa Soma Book Cafe; na muda ni saa 7 mchana hadi saa 12 jioni.
WOTE MNAKABISHWA. HAKUNA KIINGILIO!
"Mwambie Comrade amwambie Comrade"

November 04, 2017

KITABU CHENYE UTATA KUHUSU RAIS ZUMA CHAPIGWA MARUFUKU



PRETORIA, AFRIKA KUSINI

MAJASUSI wa Afrikia Kusini wanataka kufutiliwa mbali kwa kitabu kipya chenye utata kuhusu madaia yua rais Zuma kujilimbikizia fedha kimakosa ,wakisema kuwa kitabu hicho kimajaa makjosa na kinakiuka sheria ya ujasusi.

Shirika hilo la Ujasusi limetishia kwenda mahakamani iwapo wachapishaji wa kitabu hicho NP watakataa kukifutilia mbali kitabu hicho kwa Jina “The Presidency Keepers: Those Keeping Zuma in Power and Out of Prison''-Wale wanaomueka Zuma mamlakani na kutokwenda jela, kilichotungwa na mwandishi aliyeshinda tuzo la uandishi wa uchunguzi Jacques Pauw.

Kitabu hicho kinadai kwamba Rais Zuma kwa muda wa miezi minne alipokea mshahara kutoka kwa mfanyibiashara mmoja mbali na mshahara anaolipwa na serikali na kwamba hakuutangaza mshahara huo kwa watoza ushuru wa taifa hilo.

Baada ya nakala za kitabu hicho kuchapishwa siku ya Jumapili katika gazeti moja, msemaji wa bwana Zuma alitoa taarifa ,akikana makosa yoyote dhidi ya rais Zuma akidai kwamba alikuwa mwathiriwa wa kampeni mbaya ya kumchafulia jina.

"Maswala ya ulipaji wa kodi ya rais hayana makosa '',ilisema taarifa hiyo.
Nakala za kitabu hicho zinauzwa kwa kasi huku raia wakijaribu kukinunua kabla ya kuisha katika soko.

©BBCSWAHILI

November 03, 2017

UCHAMBUZI WA KITABU: IT CAN'T BE TRUE



KITABU: IT CAN’T BE TRUE
MWANDISHI: JOHN MWAKYUSA
MCHAMBUZI: MARKUS MPANGALA

HII ni mara yangu ya kwanza kusoma riwaya ya mwandishi John R.P. Mwakyusa, mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam. Riwaya inaitwa “It Can’t Be True: A Story from Uganda-the Pearl of Africa”, na kuchapishwa kwa mara ya kwanza mwaka 2017 na kampuni ya Partridge Publishing ya India.

November 02, 2017

KAMPUNI YA MKUKI NA NYOTA WAINGIA SOKO LA VITABU CHINA


NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM

KAMPUNI ya Mkuki na Nyota ambayo hujishughulisha na uchapaji wa vitabu imetanua wigo wa soko lake la uchapishaji na utangazaji wa vitabu baada ya kusaini makubaliano na Shirika la World Affairs Press (WAP) la nchini China.
 
Akizungumza baada ya kusaini makubaliano hayo Mkurugenzi wa MNN, Mkuki Bgoya amesema kuwa wamesaini Makubaliano na Shirika la World Affairs Press (WAP) ya China kufanya kazi pamoja katika miradi mbalimbali ya kuchapisha na kuvitangaza vitabu ikiwa ni njia mojawapo ya kutanua soko la kampuni hiyo barani Asia.

Mkuki na Nyota ni kampuni mashuhuri kwa uchapaji wa vitabu ambayo ilianzishwa mwaka 1992 jijini Dar es salaam. Mwanzilishi wa kampuni hiyo ni Walter Bgoya ambaye alitumia uzoefu wake wa miaka 18 ya kuwa Meneja Mkuu wa Tanzania Publishing House. 

October 09, 2017

"BIASHARA NI KAMA VITA" –(1)

NA MARKUS MPANGALA
 
NOVEMBA 8 mwaka huu Bunge la Jamhuri ya Muungano lilikataa kusaini mkataba wa Ushiriakiano na Jumuiya ya Ulaya (EPA) ambao mchakato wake ulianza mwaka 2001. Mwanazuoni Yash Tandon ni ameeleza kwa kina ubaya na hatari ya mkataba wa EPA kupitia kitabu chake cha “Trade Is War; The West’s War Against the World,’ chenye jumla ya kurasa 196. Kitabu hichi kimechapwa mwaka 2016 na Kampuni ya Mkuki na Nyota na kikapewa nambari 978-9987-75-342.
 Tandon anasema Afrika inatakiwa kuwa makini kwenye mikataba ya aina hiyo. Anaelezea jinsi Marekani, Ulaya na Japana zinavyolitumia Shirika la kibiashara duniani (WTO) kwa madhumuni ya kuchota rasilimali za mataifa madogo. EPA (European Partnership Agreement) ni mojawapo ya silaha kubwa iliyopangwa kuchota rasilimali na kuua soko Afrika mashariki. EPA inataka asilimia 80 ya masoko ya ndani yaachwe wazi na kuruhusu kuingizwa bidhaa za Ulaya.