Ukiwa mji kama wa Dar es salaam
utasikia stori nyingi za Mboga 7. Au ukiwa maeneo ya mijini hii stori ya mboga
7 imezoeleka sana kusimuliwa. Lengo ni kuelezea familia yenye uwezo wa kuandaa
mlo mmoja ukiwa umesheheni mboga za kila aina(nyingi). Lakini kwa wakazi wa Nyasa na Kijiji
cha Lundu suala la Mboga 7 ni kawaida sana. Tofauti iliyopo ni kuelezea
mazingira tu. Pengine watu wa mjini “Mnalamba lamba tu, hamshibi kisa hamna
mboga”. Njoeni Lundu.
Showing posts with label uzuri. Show all posts
Showing posts with label uzuri. Show all posts
February 23, 2018
MBOGA 7
February 17, 2018
WIKIENDI NJEMA WASOMAJI WETU NA PICHA ZA MAENEO YA UZAMIAJI WA SAMAKI LUNDU, NYASA
Eneo hili ni miongoni mwa yanayotumiwa na wazamiaji wengi
kupata samaki. Uzamiaji wa samaki katika eneo hili hutafutwa samaki wa mapambo. Kijiji cha Lundu hutumika sana kutafuta samaki wa mapambo. Kuna samaki wazuri mno wanaotafutwa hivyo wazamiaji hutegemea kijiji hiki kujipatia samaki hao.
![]() |
| Watoto wakioposha samakini karibu na jiwe Stima (Liganga Stima). |
February 16, 2018
MBUFU NI AINA YA SAMAKI KUTOKA HAPA KWETU NYASA
February 05, 2018
MIONGONI MWA SAMAKI WANAOPATIKANA ZIWA NYASA
January 27, 2018
MIONGONI MWA SAMAKI WANAOPATIKANA ZIWA NYASA
December 27, 2017
NI NYASA PEKEE HUPATIKANA AINA HII YA SAMAKI KATIKA DUNIA HII
SAMAKI ZIWA NYASA
MUHIMU; Pichani ni ufukwe wa
Lundu upande wa kaskazini-magharibi unaitwa "Bandarini". Ni sehemu
iliyokuwa inatumiwa na meli za MV. Iringa na MV.Songea kutia nanga. Katika
ratiba iliyopo Meli mpya za mizigo ya MV.Ruvuma na MV Njombe hazitatia nanga
hapa kwetu.
Lundu, Nyasa
Disemba 22/2017.
SALAMU KUTOKA LUNDU, ZIWA NYASA
Nawasalimu enyi
waungwana nikiwa nimeketi katika ngazi za Kanisa Katoliki ambalo lilijengwa
mwaka 1946 ikiwa ni mwaka mmoja baada ya kumalizwa vita vya dunia. Mahali hapa
nilipatiwa daraja la Kipaimara.
Kinachoshangaza
jengo hili limekuwa imara maradufu. Jengo hili halina mambo yenu ya #ExpansionJoints. Jengo la Kanisa hili lilijengwa na waafrika wakisimamiwa
na Wamisionari wa Shirika la Benedictine Fathers la Kijerumani. Kwa mujibu wa
historia rasmi iliyohifadhiwa hapa matofali ya jengo hili yalifyatulia kijiji
cha Liweta na Lundu kutokana na udongo mzuri. Aidha, matofali hayo
yalisafirishwa kwa Boti ya Stella Maris.
Wasalaamu!
"Bruda" Markus Mpangala OSB
Lundu, Nyasa.
Disemba 20/2017.
"Bruda" Markus Mpangala OSB
Lundu, Nyasa.
Disemba 20/2017.
MUHIMU; Salamu
hizi ziliandikwa kabla ya tarehe ya leo.
December 11, 2017
WAZIRI MKUU ATAMBUE NYASA IMEJAA UTAJIRI-2
Na
MARKUS MPANGALA
SEHEMU ya kwanza ya makala haya
katika safu hii tulichagiza kuwa agizo lililotolewa na Waziri mkuu katika
hotuba yake akimwagiza Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamis Kigwangala kuanzisha
Mamlaka ya Fukwe za Bahari na Maziwa ili kutangaza utalii na kuendeleza fukwe
ambazo hazina shughuli kwa madhumuni ya kukuza utalii Kanda ya Kusini na
mengineyo. Endelea kusoma….
Madhali linalozungumzwa ni
kuhakikisha fukwe zinakuwa na tija ni muhimu pia kuikumbusha mamlaka husika
kuwa wilaya ya Nyasa inao utajiri mkubwa sana wenye tija kupitia sekta ya
utalii ambayo kihistoria maeneo mengi bado ni mbegu bora n zenye kuvutia.
Si hilo, wilaya hiyo inao uwezo
wa kuwa na viwanda vya uzalishaji wa bidhaa mbalimbali lakini kwa sharti moja
muhimu; iwapo changamoto zinazoikabili Halmashauri zitattuliwa kwani zitakuwa
chachu ya kukuza mapato ya ndani. Hatuimwagii sifa hizo za bure bali yapo mambo
ya kuyaangalia kwa kina. Leo ninatoa mifano mingine ambayo kwa namna moja au
nyingine itawafumbua macho wasomaji na watu mbalimbali wanaofuatilia mfululizo
huu.
FUKWE
Sifa kubwa ya Ziwa Nyasa ni
kuwa fukwe bora na zisizo na uchafu wowote. Kama tulivyoona wiki iliyopita sifa
zilizotajwa na rafiki yangu Ilan kutoka Israel, ndivyo ukweli ulivyo. Katika Kijiji cha Mtupale
kilichopo Kata ya Chiwanda kuna fukwe za mawe ambazo ni kivutio adimu cha
utalii. Ukitembelea mwambao mwa ziwa Nyasa kuna maeneo mengi yenye fukwe za
mchanga unaovutia, lakini katika mwambao mwa Kata ya Chiwanda kuna fukwe za
mawe ambazo bado wawekezaji hawajafungua milango ya Utalii kanda ya Kusini.
![]() |
| Ufukwe wa Mchanga katika forodha ya Chivanga iliyopo kijijiji cha Lundu |
Ikumbukwe Kijiji hicho
kinapakana na kingine cha Chiwindi ambacho ndicho cha mwisho kabla ya kuingia
mpaka kati ya Tanzania na Msumbiji. Eneo hili linao ubora wa hali ya juu. Zipo fukwe zingine zenye
kuwavutia watu ni Ndengere, Ngindo, Lundo, Lipingo, Mkali,
Hongi,Liuli,Kihagara,Mkili, Lundu,Mbaha, na Ndumbi kwa kuzitaja chache ni
sehemu ambazo zinahitaji nguvu kidogo sana za uwekezaji kabla ya kuleta tija
kwa wawekezaji. Ikumbukwe kijiji cha Ndumbi ndicho chenye bandari ambayo Makaa
ya Mawe yanayochimbwa na Kampuni ya TanCoal. Ni mahali ambapo unaweza kutumia
darubini kuitazama nchi jirani ya Malawi kwa ufasaha.
December 09, 2017
SALAMU KUTOKA LUNDU, ZIWA NYASA
Nipo kijijini kwetu Lundu kwa
muda wa mwezi mmoja sasa. Naendelea kukusanya taarifa mbalimbali zinazofaa
kuchapishwa hapa barazani “Karibuni Nyasa”. Kama tunavyoona habari mbalimbali za utalii,
basi ndivyo utakavyosikia habari usizowahi kuzijua kutoka mwambao wa Ziwa
Nyasa. Mazingira yanayovutia mno, yenye kuhitaji kutembelewa.
Kuna picha mbili; ya kwanza
nikiwa katika Mto Chipapa, uliopo mtaa wa Likwambe hapa hapa kijijini Lundu. Ni
mto ambao miaka 1990 ulikuwa ukitiririsha maji yake mwaka mzima kwa ufasaha. Lakini
sasa mambo yamebadiliika, hakuna uwezekano huo. Kwahiyo mto huo unangojea msimu
wa masika kama hivi sasa uweze kuwa na maji ya kutiririsha hadi Ziwa Nyasa.
November 30, 2017
KITOWEO NA MANDHARI YA KUVUTIA YA LIULI, NYASA
Picha ya kwanza (juu)
inaonyesha utulivu wa Ziwa Nyasa katika bandari ya Liuli, wilayani Nyasa. Ikumbukwe Ziwa Nyasa linasifika kwa mawimbi
makali lakini pia linakuwa na utulivu kama huu pichani.
Picha ya Pili (chini)
inaonyesha samaki aina ya Mbufu ambao wamekuwa wakipataikana kwa wingi katika
ZIwa hilo. Samaki hao huvuliwa maeneo mengi zaidi ya mwambano wa Ziwa Nyasa. Ni
miongoni mwa kitoweo kinachopendwa zaidi na wenyeji na wageni.
November 24, 2017
JIWE LA POMONDA NA FORODHANI PANAWEZA KUTUPATIA WATU WA 'DIVING' KATIKA MASHINDANO YA OLIMPIKI.
NA HONORIUS MPANGALA
LICHA
ya kuwa mazingira mazuri na yenye kila aina ya vivutio lakini wafrika
tunashindwa kuwa wabunifu wa katika kuyafanya kama fursa.Mungu aliiumba Afrika
hivi ilivyo na kuweka jiografia ambayo nyakati zote watu Wa mataifa ya ulaya
wamekuwa wakivutiwa nayo.
![]() |
| Mmmoja wa Warukaji katika Jiwe la Pomonda, Ziwa Nyasa |
Iko
michezo mingi inayochezwa Ulaya na Amerika inatokana na jinsi wenzetu walivyo
makini katika kutumia mazingira yao katika kujipatia fursa ya maisha yao.
Nyakati zote mataifa ya wazungu yamekuwa na michezo mingi ambayo ina mashabiki
na wanafanya vyema,hakuna michezo ambao unakosa mashabiki Amerika na Ulaya.
Madhumuni
afya,
amani na upendo,
Nyasa,
utalii,
uzuri
November 22, 2017
FUKWE ZA LUNDU, KARIBUNI ZIWA NYASA
Hapa ni Forodha ya Lundu. Eneo hili lina fukwe mzuri sana kama huu. Picha ya Juu ni upande wa Kusini mwa forodha. Picha ya chini ni upande wa kaskazini magharibi mwa forodha hiyo. Ufukwe huu umepokea wageni kutoka Ujerumani, Italia, na wengineo ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Karibuni sana Lundu. Karibuni Wilaya ya Nyasa.
October 21, 2017
TABASAMU NA KITABU
Madhumuni
afya,
amani na upendo,
malezi,
mawazoni,
Nyasa,
Teknolojia,
urafiki,
utalii,
utamaduni,
uzuri,
vicheko,
Vitabu,
wageni,
wazo
October 05, 2017
DAR ES SALAAM TANZANIA
Subscribe to:
Posts (Atom)



















