Showing posts with label Maarifa. Show all posts
Showing posts with label Maarifa. Show all posts
March 07, 2018
KITABU KIPYA KUTOKA KWA MWANDISHI BEKA MFAUME
March 01, 2018
USHAURI KWA RAIS: NAKUOMBA KUBALI TUENDELEE KUCHANGISHANA
NA.HONORIUS
MPANGALA
KWANZA kabisa nianze na kukusalimia shikamoo
mheshimiwa Rais wangu, Dk. John Pombe Magufuli. Najua hii kazi ni ngumu kama
usemavyo wewe mwenyewe lakini sina budi kukuombea uione nyepesi ili uweze
kupata nguvu ya kututumikia vyema kama yalivyokuwa malengo yako siku unaenda
kuchukua fomu ya kugombea nafasi hiyo.
Mheshimiwa nikiwa safarini kuelekea makao makuu
ya nchi yetu Dodoma, katika gari nilipata tafakuri ambayo ilinifanya
nitoe kitabu changu cha kuandika kumbukumbu na kuhifadhi mawazo yangu ambayo
nimeona nikuandikie.
Hoja yangu kubwa ambayo ilikuwa ikizunguka katika
kichwa changu ni ile niliyokumbuka kauli yako ya kupiga marufuku wananchi
kuchangishwa mchango wowote katika shule za serikali.
February 26, 2018
ZAWADI YA VITABU KWA MARA NYINGINE
JUMAMOSI Februari 24 mwaka huu nilipatiwa
zawadi ya vita viwili kutoka kwa Bwana Ragin Mmbaga, kama vinavyoonekana
pichani. Vitabu hivyo vimeandikwa na Bwana Johne Wisse. Kuna kitabu cha TONE LA DAMU cha lugha ya kiswahili na THE BROKEN CAMPUS RULE cha lugha ya Kiingereza.
Ninawashukuru kwa kujali
kuwa visima vya maarifa. Hakika mwaka huu nimeanza kwa furaha kubwa kwani huyu
anakuwa mtu wa tatu kuniletea vitabu kibaruani kwangu.
Usomaji wa vitabu ndicho kitu
ninachokipenda zaidi. Ndicho kilevi au kitu ambacho kinachukua muda wangu wote
kuhakikisha nafurahi. Zaidi ya hapo navutiwa na mchezo wa soka. Vitabu ni kitu
muhimu sana. Namshukuru Ragin Mmbaga kwa niaba ya John Wisse. ASANTENI SANA
-MARKUS MPANGALA
January 22, 2018
UCHAMBUZI WA VITABU KILA IJUAMAA
Kwa mwezi safu hii inachambua vitabu vinne (4). Kwa mwaka inachambua vitabu 48. Ni safu maalumu kwa uchambuzi wa vitabu pekee. Ni safu iliyodumu kwa miaka minne sasa ndani ya gazeti hili. Ni safu inayopendwa na kampuni za uchapishaji wa vitabu, waandishi na wasomaji pia. Ni safu inayotanua masimulizi au maarifa yaliyomo.
Una kitabu chako wataka
kichambuliwe? Wenzako wanakuja, kwanini wewe usubiri u! Ongea nasi, uwafikie
wadau wengi…..
January 04, 2018
ZAWADI YA MWAKA MPYA 2018! KITABU
![]() |
| Adella |
Mojawapo ya mkasa uliomo kitabu ni ule wa familia ya George
Liundi, mkewe Doris Liundi na watoto wao (Nadhani wengine wamewahi kusikia
masimulizi ya maisha ya Taji Liundi).
December 30, 2017
VITABU 50 NILIVYOSOMA MWAKA 2017
NAWASILISHA orodha ya vitabu
nilivyosoma mwaka 2017. Ukitazama orodha zangu za usomaji vitabu utabaini kuwa
ya mwaka imeongezeka. Nimesoma vitabu 50 na kuna mabaki kadhaa hayaguswa
kabisa.
Mwaka 2017 nimejikuta nikiwa nimeongeza
uwezo wa kusaka maarifa zaidi kutokana na ongezeko la vitabu ingawa sina
desturi ya kupanga idadi yake.
Kwa mwaka 2018 ninatarajia
kuongeza maarifa zaidi katika vitabu vya biashara na uchumi, lakini haina maana
nitasoma vingi kuzidi ‘ala za roho” (riwaya). Pamoja na changamoto za majukumu
na mengineyo, suala la vitabu limebaki kuwa nyeti maishani mwangu.
December 04, 2017
MFADHILI WA DHIKI
November 25, 2017
UCHU WA MADARAKA DHIDI YA UZALENDO
KITABU: ZIMBABWE: STRUGGLES-WITHIN-THE-STRUGGLE (1957-1980)”
MWANDISHI: PROFESA
MASIPULA SITHOLE
MCHAMBUZI: MARKUS MPANGALA
JESHI la Zimbabwe limetangaza wiki iliyopita kuchukua madaraka nchini humo na kumwondoa Rais Robert Mugabe ambaye ametawala nchi hiyo kwa kipindi cha miaka 38 hadi sasa. Kutokana na hali hiyo tunalaizmika kukumbuka namna mwanazuoni Profesa Masipula Sithole alivyobainisha matatizo ya Zimbabwe kupitia kitabu chake cha “Zimbabwe: Struggles-within-the-struggle (1957-1980)”
JESHI la Zimbabwe limetangaza wiki iliyopita kuchukua madaraka nchini humo na kumwondoa Rais Robert Mugabe ambaye ametawala nchi hiyo kwa kipindi cha miaka 38 hadi sasa. Kutokana na hali hiyo tunalaizmika kukumbuka namna mwanazuoni Profesa Masipula Sithole alivyobainisha matatizo ya Zimbabwe kupitia kitabu chake cha “Zimbabwe: Struggles-within-the-struggle (1957-1980)”
November 23, 2017
FREDDY MACHA ALIVYOLIZUNGUMZIA JUKWAA LA KISWAHILI SOCIETY
NA
MARKUS MPANGALA
SWALI: Naam, shikamoo Mzee Macha?
SWALI: Naam, shikamoo Mzee Macha?
FREDDY
MACHA; Marahaba. Habari zako bwana! uko wapi wewe siku hizi? Maana tangu
tuliposalimiana pale Soma Café,Mikocheni na baadaye Nyumba ya Sanaa, Dar es
Salaam wakati wa warsha nilizoendesha huko.
SWALI;
Nipo hapa Bongo naendelea vema tu. Ni kweli, kitambo hatujawasiliana, pia
nilifaidika sana na warsha zako hata hivyo si neno, tutaongea kidogo leo.
![]() |
| Freddy Macha |
FREDDY
MACHA; Asante. Nadhani leo unalo la kuongea zaidi. Karibu.
SWALI;
Ni kweli, nahitaji mengi kutoka kwako mzee wangu. Kiu yangu ni huu mradi wa
Kiswahili Society, kwani umeeleza mahala fulani nikasoma nami nimevutiwa ili
niwaarifu wasomaji. Je mradi huu ulianza lini na wapi?
FREDDY
MACHA; Umeanzishwa na wanafunzi na Wahadhiri wa Kiswahili pale chuo cha lugha
cha SOAS (School of Oriental and African Studies) hapa London,Uingereza.
SWALI:
Nini dhumuni la kuanzishwa kwa Kiswahili Society?
FREDDY
MACHA; Kuunganisha Wazungumzaji wa Kiswahili duniani lakini hasa hapa
Uingereza.
SWALI:
Nashukuru sana. Ndugu Macha, wewe ni Mwanamuziki,Mwanafasihi,na Mwandishi
mkongwe. Katika fani hizi kuna mambo mengi umejifunza kutoka bara letu la
Afrika,Latin Amerika,Marekani na sasa Ulaya. Unadhani jamii za watu wa Ulaya
hususani Uingereza zinaweza kuhamasika kukiendeleza Kiswahili?
November 15, 2017
ULINZI WA FAMILIA UPO MIKONONI MWETU
KATIKA kitabu hiki….. mhusika Ttiisa
anafungua albamu. Ina picha nzuri kila anapofunua. Moja kwa moja anatupia jicho
picha ya Suuna.Ni Suuna kipenzi chake.
Aliyeingia nae penzini kwa miaka miwili (sasa), bila kujali namna Suuna
alivyoleta ugonjwa wa Ukimwi ktk penzi lao (mechi za ugenini?).
Katika albamu hiyo hiyo Ttiisa
anatazama pia picha ya Ggenza, mtoto wake aliyekuwa na umri wa miezi minne tu
lakini alifariki dunia. Kulikoni? Riwaya inakupa jawabu
**************
Ttiisa ana ukimwi. Amekutana na
Dona ambaye hana kazi (hana ajira wala hajajiajiri). Makutano yao yanaleta
matatizo makubwa ambayo ni somo kwa maisha ya Kampala ya leo (Uganda). Maisha
yao hayaeleweki. Sasa walifanyaje hadi kueleweka? ...
Ndo utamu wa nakala ngumu(hard
copy) unafunua ukurasa mmoja hadi mwingine kisha unapambia mate kwa
mbaaaaali....
#ThanksMolio.B.#
November 12, 2017
NANA YAA ASANTEWAA: MALKIA WA MILKI YA ASHANTI ALIYEWAKINGIA KIFUA WAKOLONI WAINGEREZA.
Na Kizito Mpangala
Alizaliwa mwaka 1863 katika
mji wa Besease katika jamii ya Ashanti yenye dhahabu nyingi, Ghana ya sasa, magharibi
mwa Afrika. Kaka yake Nana Akwasi Afrane alikuwa ndiye Edweso (kiongozi, au
chifu) wa milki ya Ashanti wakati huo. Nana Yaa Asantewaa akiwa bado binti
alijishughulisha sana na kilimo.
Kaka yake (chifu Akwasi) alipokuwa
Edweso (kiongozi) alituma askari wake kwenda mapiganoni dhidi ya wakoloni. Baadae
aliwekwa kizuizini na wakoloni katika visiwa vya Ushelisheli pamoja na mfalme
Prempeh I. Akiwa kizuizini, Nana Akwasi Afrane alimteua dada yake NANA YAA
ASANTEWAA kuwa malkia wa milki ya Asante.
Mwaka 1899 gavana
wa wakoloni Waingereza Frederick Hodgson aliitisha mkutano mjini Kumasi ili
kulazimisha apewe kiti kilichotengenezwa kwa dhahabu tupu ambacho ni alama
takatifu ya Ashanti ambapo askari wa kikoloni walishindwa kukipata kiti hicho,
hii ni baada ya kufikiri kwamba ugumu wa kuwatawala Waashanti ungeisha baada ya
kupata kiti hicho cha dhahabu. Nana Yaa Asantewaa alimteua mjukuu wake mkubwa
kuwa mkuu wa miliki ya Ashanti mara baada ya kufariki kaka yake.
Madhumuni
elimu,
Historia,
kumbukumbu,
Maarifa,
uongozi
November 08, 2017
UCHAMBUZI WA TAMTHILIYA YA BLACK MAMBA
KITABU:
BLACK MAMBA
Black Mamba ni tamthiliya
iliyoandikwa na John Ruganda kutoka nchini Uganda. Namba za usajili ni 978-9966-46-378-X
na kuchapiswa na East African Educational Publishers. Kina jumla ya kurasa 70
tu. Wahusika wa tamthilya hii ni Profesa Coarx (kitivo cha sosholojia), Berewa
mfanyakazi wa Profesa Coarx, Namudd mke wa Berewa, Odiambo mwanafunzi wa
shahada ya kwanza ya Sosholojia, Catherine Smith mkufunzi mpya kitivo cha
Sosholojia, Ofisa wa Polisi na msaidizi wake. Na mhisika msaidizi ni Namatta
ambaye ni kahaba.
MWANDISHI:
JOHN RUGANDA
MCHAMBUZI:
KIZITO MPANGALA.
November 04, 2017
KITABU CHENYE UTATA KUHUSU RAIS ZUMA CHAPIGWA MARUFUKU
PRETORIA, AFRIKA KUSINI
MAJASUSI wa Afrikia Kusini wanataka kufutiliwa mbali kwa
kitabu kipya chenye utata kuhusu madaia yua rais Zuma kujilimbikizia fedha
kimakosa ,wakisema kuwa kitabu hicho kimajaa makjosa na kinakiuka sheria ya
ujasusi.
Shirika hilo la Ujasusi limetishia kwenda mahakamani iwapo
wachapishaji wa kitabu hicho NP watakataa kukifutilia mbali kitabu hicho kwa
Jina “The Presidency Keepers: Those Keeping Zuma in Power and Out of Prison''-Wale
wanaomueka Zuma mamlakani na kutokwenda jela, kilichotungwa na mwandishi
aliyeshinda tuzo la uandishi wa uchunguzi Jacques Pauw.
Kitabu hicho kinadai kwamba Rais Zuma kwa muda wa miezi
minne alipokea mshahara kutoka kwa mfanyibiashara mmoja mbali na mshahara
anaolipwa na serikali na kwamba hakuutangaza mshahara huo kwa watoza ushuru wa
taifa hilo.
Baada ya nakala za kitabu hicho kuchapishwa siku ya Jumapili
katika gazeti moja, msemaji wa bwana Zuma alitoa taarifa ,akikana makosa yoyote
dhidi ya rais Zuma akidai kwamba alikuwa mwathiriwa wa kampeni mbaya ya
kumchafulia jina.
"Maswala ya ulipaji wa kodi ya rais hayana makosa
'',ilisema taarifa hiyo.
Nakala za kitabu hicho zinauzwa kwa kasi huku raia
wakijaribu kukinunua kabla ya kuisha katika soko.
©BBCSWAHILI
November 02, 2017
FURSA: SEMINA YA WANAZUONI CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM
KAMPUNI YA MKUKI NA NYOTA WAINGIA SOKO LA VITABU CHINA
NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM
KAMPUNI ya Mkuki na Nyota ambayo hujishughulisha na uchapaji wa vitabu imetanua wigo wa soko lake la uchapishaji na utangazaji wa vitabu baada ya kusaini makubaliano na Shirika la World Affairs Press (WAP) la nchini China.
Akizungumza baada ya kusaini makubaliano
hayo Mkurugenzi wa MNN, Mkuki Bgoya amesema kuwa wamesaini Makubaliano na Shirika
la World Affairs Press (WAP) ya China kufanya kazi pamoja katika miradi
mbalimbali ya kuchapisha na kuvitangaza vitabu ikiwa ni njia mojawapo ya
kutanua soko la kampuni hiyo barani Asia.
Mkuki na Nyota ni kampuni
mashuhuri kwa uchapaji wa vitabu ambayo ilianzishwa mwaka 1992 jijini Dar es
salaam. Mwanzilishi wa kampuni hiyo ni Walter Bgoya ambaye alitumia uzoefu wake
wa miaka 18 ya kuwa Meneja Mkuu wa Tanzania Publishing House.
Madhumuni
falsafa,
habari,
kazi,
kiswahili,
kitabu,
Maarifa,
Maendeleo,
maisha,
Malengo,
Mgodi Unaotembea,
Nyasa
October 27, 2017
KWANINI WILAYA YA NYASA IMESHIKA MKIA KATIKA MATOKEO YA DARASA LA SABA?
![]() | |
| RAYMOND NDOMBA, SONGEA |
Mawazo yangu
ni haya; Pamoja na sababu nyingi zilizosababisha matokeo hayo ya aibu kubwa.
Wazazi wanapaswa kubeba lawama kubwa. Wengi wao hawafuatilii maendeleo ya
watoto wao, pia makuzi na malezi mabaya.
Miaka
ya hivi karibuni (kuanzia mwaka 2000), Wazazi wengi katika wilaya ya Nyasa
hawajali elimu, hawajigusi katika ufuatiliaji wa watoto wao kielimu na hata
kitabia (Angalia matokeo ya mitihani ya Taifa ya shule za msingi na sekondari
kunzia miaka hiyo ya 2000 kwa shule kongwe ndani ya wilaya).
Madhumuni
elimu,
habari,
Linda,
liuli,
lundu,
Maarifa,
Mbaha,
mbamba bay,
Mgodi Unaotembea,
na Uchumi,
Nyasa,
Nyumbani,
Ruvuma,
Songea,
uchambuzi
October 26, 2017
MWALIKO; WOTE MNAKARIBISHWA KWENYE MJADALA HUU
October 21, 2017
UCHAMBUZI WA KITABU CHA UHAMASISHAJI
KITABU:
ISHINDE TABIA YA KUGHAIRISHA MAMBO
MWANDISHI:
JOEL NANAUKA
MCHAMBUZI:
MARKUS MPANGALA
JOEL NANAUKA ni miongoni mwa
waandishi wazuri katika vitabu vya uhamasishaji na utambuzi. Kitabu chake cha
“Ishinde Tabia ya Kughairisha Mambo” kimechapishwa na kampuni ya Benison
Communication &Printing iliyopo Dar es salaam na kupewa nambari za usajili
ISBN 978-9987-761-99-9.
Madhumuni
Historia,
Maarifa,
Maendeleo,
Mafanikio,
mila na desturi
October 18, 2017
RIWAYA YA WANG LIPING
KITABU: DOUDOU
NA MAMA WAKWE ZAKE
MWANDISHI: WANG
LIPING
MCHAMBUZI: KIZITO
MPANGALA
Doudou
Na Mama Wakwe Zake ni hadithi iliyoandikwa kwa lugha ya Kichina na mwandishi
Wang Liping na kutafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili na wakalimani Chen Lianying
na Han Mei. Kitabu hiki kina jumla ya kurasa 261 na kimegawanyika katika sehemu
24 za masimulizi yenye mtiririko mzuri ambapo sehemu inayofuata inategemea
mhimili kutoka sehemu iliyopita. Kimechachapishwa na Zhenjiang Literature and
Art Publishing House kikiwa katika lugha ya kichina na baada ya kutafsiriwa kwa
Kiswahili kimechapishwa na Mkuki Na Nyota jijini Dar es Salaam Tanzania na kupewa
namba za usajili (ISBN) 978 – 9987 – 08 – 284 – 1. Shukrani kubwa ziende kwa wakalimani Chen Lianying na Han Mei kwa kutangaza lugha ya Kiswahili.
Ni hadithi
inayofahamisha maisha ya kawaida ya Wachina lakini mafundisho yake yanafaa kwa
kila mmoja wetu duniani. Hadithi hii kwa mara ya kwanza iliingia nchini
Tanzania ikiwa kama mlolongo wa tamthiliya ambapo ilikuwa imefanyiwa
marekebisho ambayo yalifanya mazungumzo ya wahusika yasikike kwa Kiswahili. Ilikuwa
ikionyeshwa na shirika la habari la taifa (TBC) mwaka 2011.
September 29, 2017
UTAFITI: UHANDISI NI FANI INAYOLIPA ZAIDI
Aidha, wanafunzi wale ambao tayari wameingia katika soko la ajira katika kazi ya mauzo au biashara ya hisa ni miongoni mwa wenye fursa kubwa kuwa katika sehemu watu matajiri duniani.
Kwa mujibu wa utafiti uliyofanywa hivi karibuni na shirika la ajira la Aaron Wallis, ambalo utafiti wake umeangalia watu matajiri duniani zaidi 100 ili kuona kama kuna uwiano au uhusiano wowote kati ya taaluma yao ya kwanza na jinsi walivyokuwa matajiri au kutengeneza utajiri.
Ripoti hiyo ilibaini kwamba kazi yao ya kwanza, kati ya mabilionea wakubwa wa juu waliajiriwa kwa mara ya kwanza katika mashirika ambalo sio yao. Pia kuna wajasiriamali ambao walianza kampuni zao wenyewe na wengine wale walioajiriwa katika biashara za kifamilia katika nafasi masoko na mauzo.
Mabilionea 10 wa mwanzo kati ya 53 ambao waliajiriwa katika shirika ambalo sio yao wakati mabilionea tisa tu walianza kazi yao kama mfanyabiashara wa hisa au mauzo.
Utafiti huo pia uligundua kuwa matajiri wakubwa duniani 75 kati ya watu 100 akiwemo Bill Gates, Warren Buffet, George Soros na Jeff Bezos wana elimu ya ngazi ya shahada tu.
Kati ya hao 75, matajiri 22 walisomea shahada katika taaluma ya uhandisi (ikiwa ni pamoja na mwanzilishi wa mtandao wa Amazon, Jeff Bezos na mwanzilishi wa Google Larry Page, aidha matajiri 16 walisomea masuala ya biashara ambapo 11 wamesoma taaluma ya fedha na uchumi.
Mabilionea 30 kati ya 100 wanautajiri wa kurithi au wanafanya kazi katika biashara ya kifamilia, wakati 17 walianza kampuni zao wenyewe. Mwezi Julai mwaka huu, muda mfupi tajiri Jeff Bezos alichukua nafasi ya Bill Gates kuwa mtu tajiri zaidi duniani baada ya kuongezeka kwa hisa katika mauzo ya mtandao kabla ya ripoti yake ya mapato, lakini hisa zilishuka tena na Gates alirejea katika nafasi ya kwanza.
Bill Gates ambaye ana utajiri wenye thamani ya dola za Marekani bilioni 87, na amekuwa mtu tajiri zaidi duniani tangu mwaka 2013. Billionea huyu mwenye moyo wa kusiadia ametoa dola bilioni 31.1 ya utajiri wake katika kusaidia jamii kupitia taasisi mbalimbali, wakati Jeff Bezos ametoa dola milioni 100 kwa mujibu wa jarida la Forbes la nchini Marekani.
Hata hivyo, ripoti imebaini kuwa matajiri wengi katika 100 wamesomea shahada ya kwanza ya uhandisi kama orodha ilivyoeleza. Matajiri wakubwa 22 duniani wanataaluma ya uhandisi, ambapo matajiri 16 wamesomea masuala ya biashara, katika fedha na uchumi (11) sheria (6) sayansi ya kompyuta (4) historia (3) Falsafa (2), Siasa (2), lugha ya Kiingereza (2), Historia (2), Hisabati (2) na masuala ya madawa (1).
©MTANZANIA
Subscribe to:
Posts (Atom)
















