Showing posts with label mtupale. Show all posts
Showing posts with label mtupale. Show all posts

November 09, 2008

akili inachangamka sana + uzuri wake

October 01, 2008

zana za kazi hizi

Mitumbwi imetu;lizana baada ya kazi yake

September 21, 2008

haswaaaa na mchana kama huu njaa

hapa kazi hakuna kuremba

August 17, 2008

yaleyale ya kuvua kusaka kitoweo

mnyasa kwa kuwasaka samaki humuwezi yaani anajua majira ya kila aina kwa samaki mbalimbali.Karibuni nyasa,si unaona hapo walivyobize na kazi yao

August 14, 2008

kama kawaida yetu kuvua

hapo ni kama kawaida na shughuli za nyasa yetu kuvua kwa mitumbwi.umeona hiyo au haionekani

June 04, 2008

MV Songea inaingia Moja ya Vituo vyake Nyasa

Huna haja ya kuhofu,utamu wa nyasa ndiyo huuuuuuu.Ona watu wanangojea usafiri wao waupendao.

June 02, 2008

Mnyasa Kazini utamwambia Nini........Hapo vipi?

Mwangalie mwanaume wa shoka akiwa amekaza msuli kwa kupata kitoweo.Huyu ndiye mnyasa yaani hapa huwezi kumwambia aache ili akaishi maisha ya mjini ya kuuza machungwa eti umachinga..acheni hizo.Mh msije mkasema nadhihaki lakini ndiyo ukweli hamuuzi maji machafu na kuadi ni maji safu ta kunywa?eeeh bvasi jamani.Ngoja kwanza kuna wakati huwa naamini kuwa maisha ya wanyasa yanalindwa sana na mola wetu.Watu wanaweza kuishi katika hali ngumu lakini wale husikii magonjwa ama milipuko ya magonjwa kama maeneo ya mijini...kazi kwetu

May 11, 2008

Monile,Inyahi na Eena Monile Za Wanyasa

Leo kuna jambo moja limenishtua lakini lilinikuna sana.Jambo lenyewe nilikwisha kuandika Bloguni hapa.Unakumbuka kile kisa cha Yasina?kisome.Basi leo tumewasiliana si unajua mambo ya simu ukiingia mjini wakati kwetu nyasa tunategemea barua enzi zile za Posta.Maana wahenga wanasema usidharau nazi embe tunda la msimu au huwezi kumkonyeza mtu kwenye giza.Najua dadangu kule ughaibuni akisoma atashangaa kusikia nimewasiliana na yule ninayemsimulia katika kisa kile cha hivi kwanini,visa vipo vingi nitakumegea rafiki wewe tulia tuliii kama maji ya mtungini,hapa nyasa tunaita "chihulu".Achana na hilo leo tazama kichwa cha habari hapo juu.Maneno hayo yanawakilisha salamu ukiwa hapa nyasa,ole wako usipoyajua...aaah natania tu....Ni maneno ambayo kila mgeni huwa mwepesi kuyatamka kwakuwa ni maneno yanayowakilisha mambo ya kila siku kwa Wanyasa.Yote yanamaanisha kusalimiana,kujuliana hali,afya,uzima,furaha,kujuana.kujenga urafiki,kupata mambo mapya n.k si unajua kumsalimia mtu unapata thawabu?.Lakini maneno hayo yamekuwa lulu kwa dada Janeti yule aliyetua nyasa akaanza salamu yake "inyahi".Basi kaongeza ujuzi wa lugha hii ya nyasa yaani nimeambiwa kwamba sasa ana kasi sana ya kujifunza mambo ya nyasa kwani yanamvutia na amependa sana nyasa.Hii yote ni kama nilivyosema wazazi wanapaswa kuwaeleza watoto wao wapi wametokea na utamaduni wake ili wajue.Sasa mama yake amekuwa Mwalimu wa lugha hii kwa dada Janeti yaani imekuwa lulu kwake kujifunza lugha hii "kilugha".Jamani nyasa ni mahali ambapo wakoloni waliishi na wanakumbukumbu nyingi tu hivyo mambo ya historia tunayo wala hatuhitaji kufika huko mjini kwenu maana nasikia eti kuna makumbusho ya taifa huko Dar es Salaam, Tanzania.Hivi hayo makumbusho ya wapwani ndiyo ya Taifa?Mnayajua makumbusho yanavyokuwa?Njooni nyasa muone,au unafikiri kwanini wageni wakija wanakunwa sana na maeneo haya.Ngoja nitaandika mengi ya kihistoria na kumbukumbu.Nakomea hapa au unataka niendelee kuandika.....sema mwenyewe kama unasoma halafu bado unatamani......niendelee?Eena Monile,Inyahi na Monile ujifunze kabla ya kuja nyasa ewe msomaji..nikuongezee mengine.......hapana dadangu kule www.ruhuwiko.blogspot.com ataongeza au umesahau?aisee tutagombana unabisha?aaah Natania tu

September 30, 2007

Mtupale

MTUPALE; ni kijiji kinachopakana na kijiji cha mpakani cha CHIWINDI.Hiki ni kijiji ambacho hakitofautiani sana na vijiji vilivyopo nyasa kwani katika shughuli za kijamii na kiuchumi hutegemea pia uvuvi,kilimo,ufugaji n.k lakini hiki kina nyongeza zaidi kuliko chiwndi kwani kina mashamba mengi ya kilimo cha mpunga.Kwa kiasi kikubwa kilimo cha mpunga kina nafasi kubwa katika kijiji hiki kwani ardhi yake inakubali sana zao hilo,hivyo wakaazi wengi hujituma katika ulimaji wa zao hilo.Zao hilo huuzwa hata kwa majirani zao Malawi ambao ni umbali wa saa 1 na 30 kwa boti hivyo wengi hushirikiana nao wageni hao ili kujipatia kipato cha kila siku.Kwa asili kijiji hiki kina baadhi ya wakaazi ambao asili yao ni nchi za Msumbiji na Malawi,kwani waliingia Tanzania kabla ya uhuru hivyo wamekuwa raia kamili.Shughuli kubwa zifanywazo katika kijiji hiki hakuna tofauti na chiwindi isipokuwa hiki ni kijiji chenye wavuvi wengi wenye dhana za kawaida ambazo husaidia kupata samaki.Eneo lake ni tambarare kwa wastani na lina misitu ya kutosha kwa hali ya hewa nzuri,hupata mvua zake bila matatizo.Biashara nayo imekuwa sehemu ya wakaazi hao kwani hushirikiana na wale wa ng'ambo pia baadhi ya wakaazi wake hutumia biashara ya kubadilishana mazao kama zama za kale.maendeleo ni mazuri licha ya uduni wa hapa na pale.