Showing posts with label Michezo. Show all posts
Showing posts with label Michezo. Show all posts

March 26, 2018

SIMBA, YANGA WANAIMBA KIMUNGU WANACHEZA KISHETANI.

Na. HONORIUS MPANGALA 
Nilikuwa nchini Jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo April 4, 2015 siku ya pasaka. Kulikuwa na mchezo wa wa mtoano kuelekea kwenye makundi klabu bingwa Afrika kati ya Tp Mazembe wenyeji dhidi ya Orlando Pirates. Mitaani kila uliyemwona alikuwa amevalia jezi ya Mazembe na akizungumza kuhusu Mazembe huku wakielekea uwanjani Estadio de Mazembe. 

Nilimuuliza mlinzi wa eneo nilioenda kuhusu mashabiki FC Lupopo hawawezi kwenda uwanjani? Akanijibu hata Mimi ni Lupopo lakini inapokuja uwakilishi wote tunakuwa wamoja. Akanieleza hata uwanjani huioni jezi ya Lupopo. Mechi ile ilimalizika kwa TP kupata matokeo ya goli tatu kwa moja yaliyofungwa na Ranford Kalaba,Mbwana Samata na Rogers Asale. 
SIMBA

Nilikaa na mlinzi yule tukisikiliza matangazo ya redio kwa lugha ya kifaransa naye alinitafsiria kwa kiswahili cha kikongo. Wakati magoli yote yanaingia katika lango la Orlando alikuwa akisimama na kushangilia. Huo ndio utofauti wetu na wao inapokuja suala la michuano ya kimataifa.
Sababu ya pili ambayo inapelekea timu zetu za kitanzania kuwa na wakati mgumu ni kwa upande wa wachezaji. Upande Huu unatokana na ile hali ambayo wachezaji wanaichukulia katika mchezo. Huweza kuingia uwanjani wakiwa wamejiamini sana lakini ni kelele za dakika chache toka kwa mashabiki wanao wafahamu zitawafanya wachanganyikiwe.

March 02, 2018

MO IBRAHIM,INUKA JIPUKUTE VUMBI UENDE

Na.Honorius Mpangala
MABADILIKO ya bechi la ufundi katika klabu yoyote huja na matokeo chanya na hasi kulingana na mwenendo wa timu au klabu kwa ujumla.Katika hilo kuna mambo huenda yakawa tofauti kwa wachezaji walioonekana kupata sana nafasi kabla ya mabadiliko.Unayakumbuka maisha ya mchezaji wa Chelsea John Mikel Obi baaada ya kutumuliwa kwa Jose Mourinho pale klabuni.Ujio wa Guus Hindik ulirudisha kwenye hali ya kupata nafasi hadi kufikia hatua ya mashabiki wa kitazania walimpachika jina la Ombeni Sefue.

Kupachikwa kwa jina la Ombeni Sefue kwa Obi kulitokana na jinsi alivyoonekana kutotumika wakati wa Mourinhona alipofika Hidink akaanza kumpa nafasi.Hii ilifananishwa na Sefue wakati wa utawala wa awamu ya tano alivyokuwa hasikiki katika serikali hadi ilipoingia serikali ya awamu ya tano.


Mabadiliko ya makocha yanakuwa yenye kuleta mabadiliko katika vikosi kutokana na kila kocha hupenda kuja na falsafa zao.Hili ndilp lililomkumba mchezaji fundi wa mpira aliyepita katika mashamba ya miwa pale Manungu Turiani Mohammed Ibrahim.Hadi klabu ya Simba inafikia hatua ya kukubali uwezo wake na kumsajili ni kutokana na kile alichokuwa akikifanya akiwa na klabu ya Mtibwa Sugar.

Simba waliamua kufanya usajil ulijumuisha wachezaji watatu kwa pamoja toka Mtibwa sugar yaani waliwasajili Mzamiru Yassin,Shiza Kichuya nay eye Mo Ibrahim ambao walikuwa mhimili mkubwa wa klabu hiyo yeneye maskani yake katika mashamba ya miwa Manungu Turiani.

February 14, 2018

MATOKEO YA MECHI KATI YA YANGA vs MAJIMAJI F.C.

Kimsingi Yanga ilizidiwa hata muliki wa mpira lakini ndiyo wameshinda. Majiamji ilikuwa pungufu baada yamchezaji mmoja kupewa kadi nyekundu.

MSIMAMO WA LIGI KUU TANZANIA ARA

AFCON 2019: TUSIJISAHAU MWAKANI SIYO MBALI.

NA SAMWEL CHITANYA.
 
MWAKA 2017 utabaki kuwa mwaka unaokumbukwa na Watanzania wapenda soka. Mwaka huo ni mwaka ambao timu yetu ya vijana Serengeti Boys ilishiriki kwa Mara ya kwanza mashindano ya vijana kwa Afrika tangu Tanzania iwepo. Ushiriki huo ulikuja baada ya miaka 37 tangu Tanzania iliposhiriki kwa Mara ya kwanza fainali za kombe la Mataifa ya Afrika maarufu kama AFCON mnamo mwaka 1980.
Kikosi cha Serengeti Boys
Ilkuwa ni Furaha kubwa sana kuwaona vijana wa Serengeti Boys wakiwa wanashindana na timu kama Mali,Niger, Congo na timu nyinginezo zilizoshiriki mashinano Yale. Ingawa hatukufanya vema sana lakini angalau nasi tulionekana kama tunaweza. Nani alikuwa hafurahii kumuona Ramadhan Kabwili akiwa langoni na wenzie kama akina Ally Nganzi, Nasho Naftari, Nickson kibabage, Abdi Suleiman, Said musa, Yohana Nkomola kwa kuwataja wachache. 

February 09, 2018

LEODGER CHILLA TENGA AMETEULIWA KUWA MWENYEKITI MPYA WA BARAZA LA MICHEZO (BMT)


February 08, 2018

WACHEZAJI WANAVUMILIA MENGI YA MASHABIKI ILA NYOSO KATUONYESHA MOYO WAKE.

NA. HONORIUS MPANGALA
Moyo umeundwa na nyama pamoja na mishipa mingi inayofanya kazi ya kusukuma damu Kwa pande zote.Ni moyo huu huu ambao wengi husema unawauma baada ya kuwasibu mambo ambayo hawata furahishwa nayo. Ni moyo pia ambao humfanya mtu akajisikia amani na furaha baada kuona moyo umeridhika na kufurahishwa na jambo fulani.

Katika Maisha ya kawaida kumekuwa na maneno chungu nzima yanayoweza kuhusisha moyo.Iko misemo kama 'Nina moyo wa nyama' pia imeibuka mingine ya kusema ' moyo sukuma damu sio vingine'. Yote hutokea kwasababu tunajua moyo ndo injini ndogo baada ya ubongo katika kuamua na kuatoa maamuzi ya kuchukizwa au kufurahishwa.Licha ya ubongo kudhibitiambo yote yanayomhusu binadamu lakini moyo niku cha aina yake katika mwili Wa bindamu.  
Tukio alilolifanya Juma Nyoso kwa shabiki wa Simba lina mafunzo pande zote mbili.

Upande Wa kwanza ni Kwa mashabiki Wa soka. Wanatakiwa kutambua wachezaji ni bindamu kama walivyo wao. Kila tendo afanyo mchezaji wakati mwingine hulifanya katika mazingira ya akili ya kawaida kama walivyo binadamu wengine. Ila itashi Wa mashibiki tumefikia hatua ya kuona wachezaji kama kitu Fulani chenye uhitaji tofauti na walivyo binadamu wengine.

January 24, 2018

JE WAJUA KUMHUSU PATO NGONYANI?

JINA lake anaitwa Pato Ngonyani. Ni mchezaji wa klabu ya Yanga jijini Dar es salaam. Pato Ngonyani ni mzaliwa mjini Songea katika eneo la Hanga Monasteri. Alisoma  Solifo Sekondari.

January 18, 2018

KABWILI ASINGEKUBALI KUFUNGWA PENATI TANO ZA URA.

Na. HONORIUS MPANGALA
MIONGONI mwa utofauti ambao binadamu tunao ni jinsi ya kuzitumia akili zetu. Utofauti huo huweza kumtofautisha yule mwenye uwezo mkubwa katika kubaini jambo na kutafuta ufumbuzi na mwingine kubaini jambo kunachukua muda na kulifanyia ufumbuzi. Licha kuaminika kuwa tuko sawa lakini katika baadhinya nyanja hatuwezi kuwa sawa ndo maana wako warefu na wemgine wafupi ukiwalinganisha hao unapata utofauti. 

Yanga moja ya akili kubwa waliyoitumia kufanikisha saini ya Ramadhani Awam Kabwili Kwa mkataba Wa miaka mitano. Sijajua nani alisimamia kusaini Kwa Yohana Nkomola maana nilifikiri nae wangemalizana nae Kwa mtindo kama Wa Kabwili. Hata hivyo Kwa vile yuko katika milki yao wataweza kutenda jambo nae siku za usoni.


Licha ya mashaka makubwa wanayokuwa nayo mashabiki dhidi ya wachezaji vijana katika vikosi mbalimbali vya timu,ila hao ndio watu makini sana katika kitenda licha ya kwamba kuamua jambo kwao kunaweza kuwa na wasiwasi Wa hofu ya kuogoa kukosea. Wapo ambao wanakuzwa katika misingi ya kuamua Kwa kutenda Kwa wakati na kuamua Kwa ufasaha licha ya umri wao kuwa mdogo.

December 09, 2017

NIMEWASILI SONGEA, NAWASALIMU WACHEZAJI WA MAJIMAJI FC

Safari yangu ilianza katika Kituo cha Mabasi cha Morogoro.

Nikiwa na rafiki zangu Jerry Tegete na Six ndani ya uwanja wa Majimaji mjini Songea.
Nilianza safari yangu mkoani Morogoro kwenda Songea. Nimepitia njia ya Iringa, Mafinga, Njombe na kisha kuingia Songea. Baada ya kuwasili hapa Songea, kitu cha kwanza nimewatembelea rafiki zangu wawili ambao ni wachezaji wa klabu ya Majimaji FC ya mjini Songea wakiwa kwenye mazoezxi ya ya uwanja wa Majiamji. Ni Jerryson Tegete na Six Ally Mwasekaga.
Nitakuwapo hapa kwa siku kadhaa, kabla ya kuelelea Ziwani Nyasa. Tukutane ziwani kwenye ‘Show’ za ‘Cliff diving’.

Honorius Mpangala,
Desemba 12/2017
Songea, Ruvuma.

November 23, 2017

ABDI BANDA AMETUONYESHA MAANA YA “SOKA LA KULIPWA”

Abdi Banda
NA HONORIUS MPANGALA
KATIKA pambano la kirafiki kati ya Tanzania na Benin pale mjini Porto Novo nilimshangaa Abdi Banda. Kama tumjuavyo Banda ni kiraka katika kucheza soka anauwezo wa kucheza nafasi za ulinzi kama mlinzi wa kushoto, beki ya kati na kiungo wa ulinzi kwa usahihi mkubwa. 

Sasa alichokuwa akikifanya pale Benin alikuwa anatuonyesha utulivu wa akili yake katika maeneo hayo mawili yaani kumudu hulka yake na kuwa mzuri katika kucheza soka lenyewe. Banda alikuwa mtu aliyewatuliza wachezaji wenzake waliokuwa wamepatwa na hasira kwa maamuzi ya mwamuzi wa mchezo ule. Kwa penati iliyotolewa na mwamuzi ambayo mpira ulionekana wazi kuguswa na mchezaji wa Benin lakini pigo likawa kuelekea katika goli la Tanzania. 

November 22, 2017

MISS TANZANIA-MAREKANI ALIPOKUTANA NA MHARIRI WA BLOGU HII

Miss Tanzania-Marekani ambaye alishika namba namba mbili kwa mwaka 2017,  Neema Olory akisalimiana na mhariri wa blogu hii, Markus Mpangala baada ya kutambulishwa kwake na mhariri wa gazeti la michezo la Bingwa, Mwani Nyangassa (mwenye shati jeusi). 

Neema alitembelea leo Jumatano katika Ofisi za Kampuni ya New Habari (2006) Limited, wazalishaji wa magazeti ya Bingwa,Mtanzania, Rai na Dimba. Blogu yetu ya Karibuni Nyasa inamkaribisha Wilayani Nyasa kujionea utalii, shughuli za uchumi na maendeleo zinazofanywa na wananchi wa mwambao wa Ziwa Nyasa.

November 15, 2017

MAYANGA,UMEKUBALI YAISHE KWA MOLLEL?


Na Honorius Mpangala
ORGENESS Mollel ni moja ya vijana wa kitanzania wanaocheza soka Ulaya. Ni katika klabu ya Famalecao ya Ureno ndiko anakocheza kijana huyu Wa kitanzania. Kwa kipindi amacho kocha Mkuu Wa taifa Stars Salum Mayanga amekuwa muumini Wa kuwapa nafasi wachezaji wanaocheza soka nje ya Tanzania. Jambo afanyalo Kocha huyu unaweza kusema kama ni chachu ya kuthamini uwezo Wa wachezaji hao wanaowakilisha taifa letu nje ya mipaka ya Tanzania. 

November 10, 2017

MAJIMAJI FC KUFANYA ZIARA NYASA

 Na Mwandishi Wetu
 
KLABU ya Majimaji ya mjini Songea inatarajia kufanya ziara ya kimichezo katika wilaya ya Nyasa. Katika ziara hiyo Majimaji wanatarajiwa kucheza 
mechi mbili za kirafiki, Novemba 11 na 12 wilayani hapa. 

November 08, 2017

WAAMUZI WETU NA MITIHANI YA SIMBA NA YANGA



NA HONORIUS MPANGALA

TANZANIA ni miongoni mwa nchi zinazotajwa kuwa na amani na hii ni kutokana na muingiliano wa mambo manne.  Yako makundi yaliyojikita katika masuala ya dini, siasa, ushabiki wa soka na mwisho hali ya kuoleana.

Kupitia makundi hayo manne kunapelekea jamii ya watanzania kuishi pamoja. Makundi hayo hukutanisha watu tofauti kutokana na ufuasi wake. Haitakuwa ajabu unapomuona Waziri wa Mambo ya Ndani na kada wa CCM Mwigulu Nchemba akikaa jukwaa moja na kiongozi wa upinzani Freeman Mbowe na kuipa hamasa klabu wanayoipenda ya Yanga. Pia haitashangaza kwa kiongozi mkuu wa chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe kukaa pamoja na Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa na kuipa hamasa klabu yao pendwa ya Simba. Hayo yote hufanyika bila kujali itikadi za kisiasa walizonazo.

October 27, 2017

WAAMUZI WA SOKA KATIKA JICHO LA JAMII.

NA HONORIUS MPANGALA
 
WAAMUZI wa soka wamekuwa wakitazamwa tofauti kulingana na wao wenyewe wanavyojiweka katika jamii ya wapenda soka. Wako ambao wameifanya fani hiyo kuwa moja ya vitu ambavyo vinaweza kuwapatia nafasi ya kucheza matangazo. Pia wapo ambao jamii imewachukulia tofauti kutokana na mitazamo yao.
Jonasia Rukyaa.
Kuna mitazamo hasi kwa baadhi ya wapenda soka waonapo waamuzi wa kike wakichezesha mchezo. Mitazamo hiyo inatokana na asili ya mchezo wenyewe unavyochukuliwa kama ni wa wanaume. Licha ya wanawake kuucheza lakini bado mitazamo hiyo imekuwa ngumu kuwatoka baadhi ya wapenda soka. Ndo maana hata wale wanawake wanaocheza soka ukiwatazama utafikiri wanaume Kwa baadhi yao.

Tanzania ina Mwamuzi wa kati maarufu Jonasia Rukyaa ambaye anafanya vizuri sana. Alikuwepo katika mashindano ya Afcon ya wanawake ikiyofanyika Kameruni. Pia baada ya kushiriki katika kliniki ya waamuzi Kule Ureno mwaka huu amekuwa na mwaliko 'appointment' ya uwepo katika kombe la dunia. Na yupo katika mshindano ya kombe la dunia la vijana wa chini ya miaka 17 Iliyofanyika India. 

October 17, 2017

UTAMU WA WIMBO WA TAIFA UKO KOMBE LA DUNIA.

NA. HONORIUS MPANGALA
 
ILIKUWA miaka Sita ya Ubabe wa soka barani Afrika kuanzia mwaka 2006 hadi 2012. Kila mpenzi wa soka alimfahamu Hassan Shehata,kila mpenzi wa soka alimfahamu Waile Gomaa. Ilikuwa nyakati za Misri kunyanyasa mataifa mengine ndani ya bara la Afrika. Ilimchukua Kameruni miaka tisa kulipiza manyanyaso aliyopata toka kwa Misri ya kiumeni mwaka 2008 pale Ghana.
Ni Misri ambayo iliipa hasara CAF kuunda kombe lingine la Afcon baada ya kulibeba lile awali Mara nne Mfululizo. Mwaka 2006 fainali zilizoandaliwa na Misri wakikutana na Ivory coast ya Didier Drogba.
KIKOSI CHA MISRI

Fainali ile iliisha kwa matuta na wenyeji kutwa taji. Licha ya kuwa na kikosi ambacho kilikuwa na vijana taklibani Saba wakitoka kikosi cha Al Ahly ambayo ilikuwa moto wa kuotea mbali. Hapa nawazungumzia Mohammed Barakat,Saeed Moward,Essam El Hadary,Ahmed Hassan,Hossam Hassan,Mohammad Mido,Mohammed Aboutrika na wengineo. Ilikuwa ni kikosi kilichojaa vipaji kikiwa na hamasa kubwa kutoka kwa kocha mzawa Hassan Shehata kiliwafanya wapinzani wafikirie Mara mbili zaidi.

October 02, 2017

NI VIGUMU KUREJESHA ZAMA ZA RTC NA RELI KIGOMA.

NA. HONORIUS MPANGALA
WENGI wanapajua kwa jina la utani mwisho wa reli. Ni kigoma mkoa wa kanda ya Magharibi ukiwa na sifa kemkem katika kila nyanja iwe medani ya siasa,sanaa na hata soka. Kabila la Waha ndio wenyeji wa mkoa huo lakini yako makabila mengine. Wako wabembe na wanyema pia. Moja ya nyimbo bora za bongo fleva 'Leka tutigite' wa Kigoma All stars ni kati alama ambayo inatumika kuutambulisha mkoa huo.Hifadhi ya Gombe na Mahale ambayo ina sokwe ni miongoni mwa kivutio , pia meli kongwe duniani iliyoundwa na wajerumani mwaka 1913 katika maandalizi ya Vita ya kwanza ya dunia MV Liemba iko Kigoma na ingali inafanya kazi hadi Leo.
Umati wa wapenda soka mkoa wa Kigoma wakitazama mechi ya fainali ya mashindano ya kugombea ng'ombe katika uwanja wa Lake Tanganyika.

September 16, 2017

TAKWIMU ZA MECHI YA LEO

Majimaji ya mjini Songea leo ilipepetana na bingwa mtetezi Yanga kwenye uwanja wa Majimaji mjini Songea. Pambano hilo limemalizika wka sare ya 1-1. Tazama takwimu,

Tutakuwa tukikuletea "MECHI YA LEO: TAKWIMU" kila wikiendi.

September 15, 2017

KADI NYEKUNDU 169 ZA KOMBE LA DUNIA



NA HONORIUS MPANGALA

KADI ya 1 nyekundu ilitoka July 14,1930 kwa PLACIDO GALINDO mchezaji wa Peru. Katika mechi kati ya PERU VS ROMANIA. Kadi ilitoka dakika ya 54 ya mchezo.
Kadi ya 141 nyekundu ilitoka July mosi,2006 dakila ya 62 kwa WAYNE ROONEY. katika mchezo wa Ureno vs England kwenye fainali za Kombe la dunia nchini Ujerumani.
Kadi ya 142 ilitolewa kwa ZINEDINE ZIDANE, July 9,2006 dakika ya 110 mechi kati ya Ufaransa vs Italia.

Kadi ya 169 ilitolewa juni 29,2014 baada ya kupatikana kadi mbili za njano kwa OSCAR DUARTE wa COSTA RICA. Njano ya kwanza dk ya 42, ya pili dakika ya 66 na kufanya kuwa nyekundu. Mechi kati ya Costa Rica na Ugiriki,pale nchini Brazil.
Ligi kuu ya England mchezaji wa kwanza kupata kadi nyekundu ni DAVE WAGSTAFFE wa Blackburn Rovers. 

NB: Imeandaliwa kwa msaada wa mtandao.

October 09, 2013

DIEGO COSTA ANAWEZA KUICHEZEA HISPANIA




Na Olle Bergdahl Mjengwa, Sweden
MSOMAJI, mchezaji anayewashangaza wengi msimu huu ni mchezaji maarufu wa Atletico Madrid, Diego Costa.
Nikiandika makala hii, Diego Costa amefunga mabao nane katika mechi saba katika ligi ya Hispania. Wiki hii mechi za kufuzu Kombe la Dunia zinachezwa.
Kinachowashangaza  wengi ni kwamba Diego Costa aliyezaliwa na  kukulia Brazil, na mwenye miaka 24 ,  hajawahi kucheza mechi ya mashindano dhidi  ya timu ya taifa ya Brazil. 

 Mchezaji huyo ameishi  Hispania tangu mwaka 2007. Ana uraia ya Kihispania pia. Kwa hiyo, mchezaji huyo anaweza kuichezea timu ya taifa ya Hispania.

Sheria za FIFA zinasema  mchezaji akicheza mechi moja ya ushindani na timu moja ya taifa, mchezaji huyo atabidi kuichezea timu hiyo katika kipindi chake chote cha kucheza mpira. Lakini, Diego Costa amecheza mechi moja tu na timu ya taifa ya Brazil na ilikuwa mechi ya kirafiki dhidi ya Italia mwaka huu.  Kwa hiyo, Diego Costa bado hajacheza mechi ya ushindani na Brazil, na kwa hiyo anaweza kuichezea timu ya taifa ya Hispania.

 Lakini, chama cha soka cha Brazil hawataki Hispania kumwita Diego Costa kucheza mechi za kufuzu Kombe la Dunia akiwa na Hispania. Diego Costa alipata uraia wa Hispania mwaka huu, lakini chama cha soka cha Brazil wanaamini mchezaji huyo ni Mbrazili na wamewambia FIFA kwamba Costa hajacheza mechi ya ushindani na timu ya taifa ya Brazil kwa sababu hawana mechi za kufuzu kwa kuwa  fainali za Kombe la Dunia zitachezwa Brazil mwakani.

FIFA wameamua kwamba Diego Costa hata ruhusiwa kucheza mechi za kufuzu fainali za  Kombe la Dunia wiki hii na wiki ijayo, na haruhusiwi kuichezea timu ya taifa ya Hispania wala ya Brazil mpaka FIFA wakimaliza utafiti juu ya suala hilo, na hivyo wataamua kama Diego Costa anaruhusiwa kuichezea timu ya taifa ya Hispania au hapana.

Vyombo vingi vya habari vinaamini kwamba FIFA watamruhusu Diego Costa kuichezea timu ya taifa ya Hispania, na kwamba  mchezaji huyo amemwambia Del Bosque, kocha wa timu ya taifa ya Hispania kwamba anataka kuichezea timu hiyo. Bila shaka, Hispania wanahitaji mchezaji kama Diego Costa. Timu ya taifa ya Hispania kwa muda  mrefu hawajakuwa na mshambuliaji anayefunga mabao mengi  katika timu ya taifa na timu ya klabu.

Hispania wamebaki na mechi mbili tu za kufuzu kucheza fainali za Kombe la Dunia. Na wana nafasi kubwa kuchukua nafasi ya kwanza katika kundi lao, hivyo,   watafuzu kucheza fainali za  Kombe la Dunia. Lakini, Costa atakosa mechi hizi. Hata hivyo, naamini kwamba kama Costa ataendelea kuwa katika hali nzuri ya kimpira, basi, mchezaji huyo atachukua nafasi katika kikosi cha kwanza cha Hispania kama anaruhusiwa kuichezea timu hiyo.

Brazil na Hispania walikutana katika fainali ya kombe la mabara mwaka huu. Hispania walifungwa mabao matatu kwa bila. Labda Hispania na Brazil watakutana katika fainali ya Kombe la Dunia mwakani. Del Bosque anajua kwamba kama Diego Costa anaichezea timu yake, basi, Hispania watalipiza   kisasi.