Showing posts with label mapumziko. Show all posts
Showing posts with label mapumziko. Show all posts

October 17, 2017

MAONI YA MHARIRI: KWA WILAYA YA NYASA DUNIA HAIJABADILIKA?

Majuzi nimeona picha ya mwanadada mashuhuri katika mtandao wa Instagram, Mange Kimambi akionyesha majengo ya hospitali ya Lumeme wilayani Nyasa ikiwa na mazingira mabaya ya kufanyia kazi na ukosefu wa huduma muhumu. Pamoja na jengo lenyewe kutokamilika, lakini limekuwa likitumika hivyo hivyo.

Kwangu mimi ile ilikuwa habari kubwa sana kwa wilaya yetu ya Nyasa. Kama mwanahabari naamini kuripotiwa matukio au masuala yasiyofaa  ndani ya jamii ambayo haitoi habari za kutosha ni njia mojawapo kubwa ya kubadili mwenendo.

HAPA CHINI kuna Blogu ya JIMBO LA NYASA. Lakini habari za Jimbo husika ziliwekwa mara ya mwisho Januari mwaka huu. Nimejiuliza wasaidizi wa Mbunge wanafanya nini kama hawawezi kutoa taarifa za ofisi ya mbunge? Najiuliza hivi hatuoni umuhimu wa habari zetu zikiwa hadharani bila kujali mbaya au nzuri?

Je waanzilishi wa blogu ya JIMBO walikusudia tamasha au nini? BONYEZA HAPA KUTAZAMA.  Kimsingi habari za Jimbo la Nyasa ni lazima zitolewe wala kwa wananchi. Pili inadhihirisha "kuamini" kuwa NYASA ni ileile ambayo inaishi pasipo kuwa na habari zozote. Mtazamo huo si sahihi ndio maana wahusika wanaona "bora liende tu" huku wakisahau na kushindwa "KUMUUZA" mbunge. 

Nimejiuliza hadi leo hata kutengeneza ukurasa wa habari za mbunge kwenye mitandao hatuwezi kweli?  Hivi mahusiano ya mbunge na wapigakura wake yana maana gani? Naandika hapa kwasababu naamini wapo wahusika wanaofikisha ujumbe. Ningependa kuwakumbusheni kuwa "kutomuuza mbunge" katika ulimwengu wa kidigitali ni uzembe. Labda tunaweza kutembelea wananchi kila kona ya jimbo, lakini tunapawa kuelewa kuwa taarifa za huko ziwekwe sehemu maalumu kutunza kumbukumbu sio mambo ya "MASJALA" tena (hizo ni zama za kale mawe).

Kwa heshima nawakumbusha wasaidizi wa mbunge, kutoitendea haki blogu, kutozungumzia hata utalii ambao ni chachu ya kukuza mzunguko wa fedha wilayani kwetu ni UDHAIFU unaopaswa kurekebishwa.
Ninawatakieni majukumu mema. 
HABARI NI BIASHARA. HABARI NI UCHUMI.

MARKUS MPANGALA,
Oktoba 17/ 2017
Dar es salaam

November 20, 2012

KARIBUNI SANA NYASA, MLO WENYE VIRUTUBISHO VYA ASILI

                                                            KARIBUNI NYASA
Hilo tunaloweza kusema kuhusu wilaya ya Nyasa. Ni wakati wa kuburudika zaidi na kupata vyakula vyenye virubisho vya asili kama vinavyoonekana pichani.


November 02, 2012

AMBROCE NKWERA, KIZAZI KIPYA CHA WILAYA YA NYASA NDANI YA MAHAKAMA

Miaka mingi sana imepita wazee wetu wazaliwa wa wilaya za Mkoa wa Ruvuma wemekuwa wakifanya kazi katika sekta mbalimbali, lakini hawana muda wa kutosha kufikiria kurudi nyumbani Nyasa na kufanya kazi karibu na wakazi wao. Lakini wapo vijana wenye tofauti kiasi kikubwa na wazee kama Prof. Nkoma (TCRA), Prof Mpangala (UDSM), Jaji Samatta(Mahakama Kuu), Mataka(ATC) na wengine wengi sana ambao waliozaliwa na kukulia wilaya Nyasa. Aidha, inapendeza pia kuona mzaliwa wa wilaya ya Nyasa James Zotto, akifanya utafiti wake wa masomo ya juu(Masters) katika suala la Utatuzi wa mgogoro wa mpaka wa Ziwa Nyasa baina ya Malawi na Tanzania. Zotto ni mzaliwa wa mji wa Liuli katika wilaya ya Nyasa.
                                      
                                        AMBROCE NKWERA KAZINI MAHAKAMANI
Hata hivyo kijana AMBROCE NKWERA yeye alisukumwa na nia ya kuwatumikia watu wa wilaya ya Nyasa, lakini amejikuta akipangiwa wilaya ya Mbinga ambayo zamani ilikuwa pamoja na Nyasa. Kwa hakika sio hatua mbaya, bali lengo lake liliongozwa na kuwatumikia watu wa ukanda wa Mkoa wa Ruvuma hususani wilaya za Songea, Tunduru, Mbinga na Nyasa au Ludewa(Iringa).
Baada ya serikali kutangaza nafasi za kazi ya Uhakimu kwa wilaya kadhaa za Nyasa, ndipo kijana huyu akachukua uamuzi wa kuomba nafasi hiyo. Na hadi sasa anaitumikia jamii ya Tanzania hususani wilaya ya Mbinga hivyo kukamilisha ujenzi wa Taifa. Labda swali hapa ni kwanini aliamua 'KURUDI NYUMBANI' ambayo ni sera yetu nami nikiwa mfuasi wake?
Sababu kubwa ni kwamba kuna wafanyakazi waliowahi kuajiriwa na kupangiwa wilaya ya Mbinga ama maeneo ya Wilaya za mkoa Ruvuma halafu hawaendi kufanya kazi vituo vya kazi. Hii ilikuwa ikimkera na kuona kuna haja wazaliwa wa maeneo hayo wenye sifa kuomba kazi ili warejee na kuwatumikia watu wa nyumbani kwao. 

                                          
                                                     AKITOKA KAZINI
Lengo hilo lilifanikiwa baada ya Mahakama kuu kumwajiri AMBROCE NKWERA na kumwapisha huko wilayani Lushoto mkoa wa Tanga. Kwa sasa yeye anatumikia taifa kupitia wilaya ya Mbinga ambayo ni jirani na nyumbani kwao wilaya ya Nyasa.  Yeye ni miongoni mwa walioshauri kuanzishwa mahakama maalumu ya kuwahukumu watu wote wanaoshtakiwa kwa kosa la Ufisadi ambayo anasema sawa na wahujumu uchumi (tutachapisha mahojiano yake siku zijazo).
Kwa hakika anastahili sifa na kupongezwa sababu uamuzi wake licha ya shahada yake ya sheria, akaona kuna haja ya kwenda kufanya kazi maeneo ambayo wengi hawataki kufanya kazi, maana huwa wanaripoti na kuondoka moja kwa moja, hawarudi tena. 
AKIFURAHIA MANDHARI YA MBINGA
Sasa, roho yake imetulia atakuwa HAKIMU mzuri sana, mikono yake itatenda haki na sera yake ya kushawishi wasomi ambao ni wazaliwa wa Wilaya ya Nyasa au Mbinga na nyingine za mkoa wa Ruvuma kwamba ni vyema wakarudi nyumbani kuwatumikia wananchi wao kuliko kulalamikia wageni wanaotoka mikoa mingine kutopendelea kufanya kazi maeneo ya mkoa huo. Mabadiliko na maendeleo yatawafikia watu kwa watu kufanya jitihada za kufanya kazi kwa bidii. Hongera sana Mgosi wa Ndimba AMBROCE NKWERA.

August 05, 2011

NIPO MSITUNI NAJARIBU KUJENGA KAMBI

Nipo, najaribu kuwepo ili niweze kuhimili uwepo wangu.
labda niseme nipo msituni najaribu kujenga kambi. Najipendelea tu kwa leo.
nawasabahi waungwana. Nasema, amani iwe nanyi

June 09, 2010

BADO MFULULIZO WA MAWAZO

Jamani, sasa hivi ndiyo nataka kufunga haka kaofisi kangu niende nami nyumbani. Lakini najua nikifika tu kitu cha kwanza ni kuifungua kompyuta yangu ili niendeleza mambo yangu ya kukaa na tarakilishi. Na zaidi basi nitakaa nyuma ya DSTV niangalie soka au marudio ya Tenisi au vipi, na zaidi ule muziki wa Kwaito mtamu...... Nadhani mtani anajua utamu wa soka. TUACHE HILO.....

KUNA hili jambo nilikuwa najaribu kuwaza dakika chache hizi na hadi sasa naandika naendelea kuwaza. HIVI WEWE UNAMWAMINI NANI HASA KATIKA MAISHA YAKO? Yaani UNAVYOISHI KILA SIKU KUNA MTU UNAMWAMINI SANA? KWANINI?

Unajua katika maisha yetu haya kuna wakati unakuwa na marafiki wengi sana, na wengine wanaweza kukupotosha halafu ukajuta hapo baadaye. Labda utaniuliza mimi namwamini nani. Mwenzangu yupo mtu namwamini anaitwa Yasinta Ngonyani, ni sababu nyingi na ukweli NAMWAMINI SANA. Lakini ukiniambia nikwambia sababu za KUMWAMINI, sitakwambia....

Hebu jiulize wewe unayesoma hapa UNAYEMWAMINI NA KUMWAMBIA MAMBO YAKO, HASEMI KWA WENGINE MAMBO HAYO? au UNAMWAMINI KIASI GANI? Bado mfululizo wa MAWAZO TU.  ok naenda nyumbani, nimeimiss tarakilishi yangu aiseh

March 10, 2010

KWANINI UMEAMUA KUWA KAHABA? mmh Swali Gumu!

Ni kweli jamani mambo siyo haya tena, na kweli tunatakiwa kuwa makini. Lakini je ni kweli kwamba baadhi wa wanawake wanaamua kuwa makahaba kwasababu gani? Jamani ilibidi niombe radhi baada ya kumhoji binti fulani kwamba kwanini ameamua kuwa kahaba, kwanza alinitazama na kisha akaniuliza shida yako ni kwanini nimekuwa kahaba aua unataka nikupe huduma?

Ni kweli ikabidi niwe mpole, nikatuliza munkari, nikaanza kuongea kirafiki na binti huyo kwani sikuwa peke yangu bali rafiki zangu pia tumejumuika pamoja tunauliza swali hili.
Jawabu la binti huyu ni kwamba 'MAISHA', nikauliza tena je unaifurahia kwakuwa inakuingizia kipato? Nikajibiwa ni swali gumu kulijibu na nisingependa kuongelea hilo.

Nikawa na adabu, nikajaribu kudodosa tena, unajiamini vipi kukubalia kulipwa 10000 bila kutumia kondomu, na 5000 kwa kondomu? Nikajibiwa..... naomba iwe mwisho.... halafu akanitusi mse***** nini,. Ni matumaini yangu hakunilewa lakini baada hakika nakwambia akawa rafiki mwema tu licha ya kazi ya kuuza mwili wake.

Yaani ndani ya nusu saa amehudumia watu wawili wa vyumba tofauti, halafu katika trip hii kuna watu wana wake zao, na wanajivinjari kana kwamba wake zao hawawatoshi, na utadhani hii ni tour ya mwaka mzima wakati ni siku chache tu.

Suala la msingi nimejifunza sana neno 'MAISHA' kwasababu kila unayeongea naye kishkaji anakwambia MAISHA MTU WANGU. Sasa hapo najiuliza tufanye nini ili kuwaondoa watu katika ngome hiyo waliyopo? Sasa kwasababu wanalalamikia kuwa MAISHA, ni wazi hawa ni wahanga wa MAISHA ya kila siku, lakini ni MAISHA gani hayo?

Bila shaka nawe msomaji unaelewa anapokujibu MAISHA, na ikafika mahali kuna binti aliangusha kilio, tukamwomba msamaha, endapo tunamwudhi, lakini hakika nimebaini makahaba hawa kila mmoja analo DUKUDUKU lake, lakini hawajapata mahali sahihi pa kulisema suala hilo. Sijui ni DUKUDUKU gani, na labda ni MAISHA MTU WANGU.
Jamani nipo fasta nabasti kama pancha, sasa tunaenda zetu makumbusho ya watu wa kale hapa. Hii ndiyo BAGA-HEART mji mtamu nimeupenda jamani hadi raha......halafu mmoja akasema... nyie jamaa poa sana, oyaa nitakupeni namba zangu au vipi mkija tena tuwasiliane...... ha ha ha ha nikupe namba msomaji nawe upatiwe HUDUMA? Thubutu.... sikupi ng'ooooooooooooooooooooooooooooooooo, utajijuuuuuuuuuuu

March 08, 2010

NIMEIBUKIA WAPIIIIIIIIIII JAMANIIIIIII?

Kwa watu wangu woteeeeeeeeeeeeeeee hamyambu yambu jamani kanonooooooo??? Unajua nimeibukia wapiiii? Hebu angali hilo lipicha unadhani nipooo? Thubutu ukiweza nakupa zawadi niliyopata Makumbusho yao hapa.

KIFUPI
Nimeibukia BAGA-HEART a.k.a Bagamoyo nimezungunga mitaani kama chokoraa tangu kumekucha na muda ninaopata ni huu kuandika baada ya MICHAKATO kibaoo inayohusu.

Nipo najaribu kuanglia namna ninavyoweza kuibadilisha akili yangu na kujiangalia zaidi huku nikiambatana na rafiki zangu wenye hamu ya kujua sisi waafrika tupoje na majengo yetu ya kale yapoje, nyoooo. Si vibaya, ila nashukuru kuwa anaongeza kipato kwa serikali yetu adhimu duh!
Bagamoyo kwa upendo wa kuwaonyesha hawa wenye rangi za albino a.k.a washamba(natania, maana ananingalia huyu hapa) maana wakiona mishale na mikuki wanaduwaa meno 32 nje kama wamefumaniwa.... Lol ipo kazi
Si wamezoea kuona mibunduki ya akina Joji Kichaka.
Haya tazameni hiyo picha basii oneni wenyewe

February 23, 2010

HUJAMSOMA 'SUN TZU' KAZI KWAKO

Nafuta jasho, lakini bado linatililika tu, nahaha huko na huko kwenye maduka rasmi na yale ya wamachinga kuona kama naweza kupata. Lakini sijakata tamaa naendelea kusaka, ili kujifaliji nikaamua kununu kijitabu kidogo cha 100 THINGS TO DO BEFORE YOU DIE, napitisha mistari yake kidogo lakini kiu yangu ni kusaka kitabu cha SUN TZU cha THE ART OF WAR, ghafla najikuta nipo mitaaya Samora, naingia dukani natumbua mimacho kama nimebanwa na mlango, ..... na sasa najisikia fahari kwa raha najisomea aya kali na nadharia maridadi za huyu mtu. We acha tu THE ART OF WAR ni zaidi ya burudani waungwana.

January 08, 2010

USIONE VYAELEA...................


Sifa ya kwanza kula ndugu yangu, usisifiwe kwa kuongea. Utaongea kwa umahiri kama hujashiba? Utafanyaje kazi na iwe bora kama hujashiba? Ukitaka kusoma falsafa lazima ushibe, huwezi kusoma mistari ya MALCOLM X kama hujashiba vinginevyo utakimbilia kwa mbembelezaji Martin Luther King Jr. Unashiba halafu unakamata mistari ya Malcolm X halafu unapandisha mzuka sawia. Usione vyaelea................
na ukisiba soma mistari yangu KUHUSU UTATA WA WILLIAM SHAKESPEARE hapa

April 16, 2009

HATIMAYE: Wamefika nyasa, wamefika Mbamba bay

Wamisionari,watawa au tuseme watu wa dini au vipi? lakini kumbuka usiwe na kicheko kile cha nyege za kutaka kujua kulikoni lakini tulia tu nikuhabarishe mambo ya nyasa. Chipole kuna sekondari inaitwa St Agnes ni shule ya watawa wale nadhani ni pamoja na wale wa Wabendictino wa Peramiho( dada Yasinta, sahihisha).

Wamekwisha kutua Mbamba bay na hii ndiyo hoteli yao ambayo inatwa MBAMBA BAY HOTEL. Nakumbuka yupo dada Anna pale tuliyecheza naye enzi za Mwalimu, enzi za wewe baba na mimi mama au vipi? lakini siku hizi najua amesahau hakumbuki shauri kavaa utawa jamani duuh!1 sasa habari yenyewe ndiyo hiyo kwamba wameanzisha hii hoteli au shirika la utawa ambalo ni shemu ya Chipole.
haya wageni na wwale wasiojua kuogelea na wanaogopa kama dada Yasinta(eti anaogopa mamba) Karibuni sana. tovuti yao http://www.chipolestagnes.org/ (kama sijakosea0.picha kwa hisani yao

February 11, 2009

Hakuna kulala hapa

Vipi, unaonaje ukijiunga nao! Unaweza kweli mauno ya viuno kama Fifimoto wa Enomizizi au wewe ni laini yaani nyororo! Utaweza wewe mtoto wa geti kali mambo haya? Mtoto umekulia wapi kama siyo ndani kutazama kideo na propaganda za seleka za walami ughaibuni.
Nakumbusha umuhimuwa kunengua mitindo ya kwetu, hakuna kulala aiseh

January 01, 2009

20009+ YASINTA+ Wanablogu


2009 Pamoja daima.Wanablogu wote Nawatakieni mafanikio mema zaidi.Na kudumisha maendeleo ya Blogu zetu.Nimefurahi zaidi kwani jana nilikuwa na mwanablogu dada Yasinta,na kupiga gumzo la hapa na pale.Anatuandalia kitu kingine;tanzaniaresan2009.blogspot.com
NAWATAKIA SAFARI NJEMA.
ZIDUMU BLOGU ZETU na WANABLOGU DAIMA

November 19, 2008

zana za kazi zipo mapumzikoni

October 29, 2008

natabasamu jamani RAHA za hapa nyasa

tazama tabasamu hilo linavyoukita. tabasamu linakuita bila kinyongo. kaja huyu je wewe uliye jirani? karibu nyasa

October 07, 2008

weweeee mambo iko ukuuuuuu

jamani eti watu wa mjini nao wanabanjuka baharini. waone kwanza wanaogelea maji ya chumvi wakati kwetu maji salama kabisa

August 28, 2008

Karibuni nyasa

jionee fahari,nyasa nakupenda sana. kuna yeyote ana hoja kwamba hii siyo hali halilisi ya nyasa?jieleze

July 14, 2008

uzuri wa nyasa?ngoja nikuambie

Tazama vizuri usije ukafikiria hapa ni peponi..natania lakini karibu nyasa

July 02, 2008

Karibuni Tena Mbamba Bay

Ukitazama mbele kabisa unaona kama kuna majengo fulani-hapo ni karibu na Hoteli ya Neema.Yaani mahali pale ni pazuri sana kuna barabara toka uwanja wa hoteli hiyo mpaka ziwani yaani unabarizi tu taratibu siyo kwa usafiri bali matembezi.Kwa wapendanao wanajua matembezi lakini mnyasa hata sijui mimi kuvua samaki tu.Hili eneo lenye mawe pana uwazi mzurisana ambao hutumika kwa kujipumzisha nyakati za mchana.Hii ndiyo Mbamba Bay ndugu yangu karibu tena mmm lakini dadangu pale Ruhuwiko bloguni anaumia shauri amekosa sana utamu wa nyasa....ngoja nitakutumia basi la ungo uje kwa kasi kisha kurejea ughaibuni.

March 23, 2008

Shamrashamra,Vifijo,Shangwe na Mbwembwe za Wanyasa

Jana nilikuwa na wanyasa hapa kijijini kwetu,jambo la kwanza nililojiuliza ni je wanyasa watakula nini au watasherekea vipi sikukuu hii ya pasaka kwa wakristo.Nikawafuata wazee wa mila wajuao desturi na tamaduni zetu ili wanipe mbwembwe na shamrashamra za kale kwa wanyasa.Nikaambiwa nyakati hizi kwa vijana ni hatari sana kwani mengi ambayo kale hayakuwapo yapo,hivyo shangwe hizo ziendane na kujihadhari japo kidogo.Zamani wazee wetu walikuwa wakitayarisha samaki kwa ajili ya wanyasa waishio mijini ili wakija kupumzika kwao waone kweli wapo nyasa,lakini kipindi hiki ile hali ya kujali imepungua na chanzo ni kubadilika kwa mfumo wa maisha ya mwanadamu.Basi unaambiwa wanyasa wanacharaza ngoma za Lendeku,madogori na nyingine nyingi,vijana walichangamka jana wakasahau machungu ya kulima nyakati hizi.watoto wanarukaruka kwa mikogo kuifurahia sikukuu hii,wamebeba virugu vya kutwanga wenzao{kama mchezo fulani hivi},wazee wanasema vijana wa siku hizi hawajiamini kama kale.Naambiwa vipi kujumuika kuselebuka mimi naulizia hayo mambo,nikajibu ni moja ya kusherekea pia kwani napata nasaha za wazee wa jadi wenye kila aina ya thawabu.Basi unaambiwa kuku wakienyeji wamechinjwa{hakuna kuku wa kisasa huku},mbuzi,ng'ombe na wengine waliwinda sungura na wanyama wengine kwa ajili ya kitoweo,hizi ni nyakati za wanyasa kusahau samaki kidogo na ugali wao wa muhogo lakini lazima samaki awepo ili kukamilisha unyasa wetu.Watu wamejazana wanafurahi sana jumamosi yenyewe kabla ya jumapili.Ni porojo za hapa na pale yaani kila mnyasa ni furaha tupu,mungu awalinde wanyasa wenzangu hawa.ngoja nikomee hapa kwa leo.

December 26, 2007

NYASA;krisimasi,furaha,burudani na uhai wa wanyasa

Naam nilikuwa katika kijiji lundu kujionea burudani na furaha ya kusherehekea krisimasi ambayo bila shaka ni ni wakati wa wazazi,watoto,ndugu,jamaa na marafiki kujumuika katika simu hii ambayo hupatika mara moja kwa mwaka pale wakristo wanapokumbuka siku ya kuzaliwa Yesu krsito.Ni kawaida yangu kutulia katika siku za aina hii lakini nilishindwa kutulia ilibidi nijiulize nitaandika nini nikifika Mbinga asubuhi hii maana wenzenu mambo ya mtandao haya mapaka tusafiri kidogo ndipo tuandika katika blogu namna hii.Naam nimekuwa katika mzunguko mkali wa siku hiyo ya krisimasi ili kujionea burudani,furaha na uhai wa wanyasa katika maisha yao lakini nikaona sisi bina damu tuna kawaida ya kusahau matatizo siku kama hizi maana nikaona hata wale maadui wanakumbatiana kwa wema kuikumbuka siku ya mwokozi wao.Asubuhi hii ikawa balaa maana kuna jamaa alikwenda kuvua samaki hivyo nimemwahidi kwenda kupata japo kitoweo kumbe mwenzie naondoka zangu kusafisha macho mjini Mbinga angalu nione wamjini wanaburudika vipi hata siku kama ya leo.Nimekuta watu wamelewa,wanatapika hovyo,mara mafumanizi na uchafu kibao na nikaambiwa na mwenyeji wangu kuwa kuna mwanamke mmoja kafumaniwa na kijana wa kinyasa mtaa wa Flastoo.Hapo nikaguna huyu mnyasa yuko hai kweli? nikambiwa wanyasa wana mbio katika hatari maana jamaa kachia mbio kuokoa uhai wake....si unajua fumanizi za wenyemali.Sasa badala ya furaha,burudani na uhai wa wanyasa jamaa kasafiri hadi hapa mjini halafu anajiona wa leoleo na vihela mbuzi vyake akakoswakoswa na wenye uchu wa kutanya uhai wa wenzie na bahati yake kwa wanyasa kuwa mbio kali ni sifa moja ya uhai wako nyakati za hatari.Ndiyo wanyasa wa mbio za ajabu mithiri ya swali mbugani.Lakini baada ya kuandika hapa mjini katika blogu hii natarajia niende zangu kijiji maana jamaa akija nadhani ataghadhibika kwani nimeahidi kununua samaki wake ili apate pesa za kuburudika na furaha ya familia maana jana kalewa mipombe halafu kasahau familia lakini kaahidi leo ni burudani ya familia yote sasa watoto wako juu kwelikweli maana wanataka kuonyesha uwezo wao wa kuburudika. mapumziko mema,watu wote wa ughaibuni maana najiuliza hivi Ndesanjo anasoma habari za wanyasa kweli?vipi kaka Jeff,DaMija,Michuzi na kitoto pale London?sijui lakini polepole,KARIBUNI NYASA!